Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Nawewe niwale wale Hebu jiulize Tumefikaje hapa !

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu jibu hoja kwa hoja,na sio hoja kwa mihemko.
Mimi nimekueleza huwa naangalia luninga za wenzetu na huwa wanajitahidi kuzilinda serikali zao ,wewe unaposema na we we in walewale maanake nini?Umejibu hoja gani?
Hapa jf ni sehemu ya kuelimishana ili tusonge mbele kama taiga mkuu.
 
pasco acha hizo mkuu. Maslahi ya nchi yanalindwa na katiba na sheria zilizopo. Katiba ya nchi inaruhusu siasa za vyama vingi. Utawala usiopofuata katiba, matatizo kama haya ndo hujitokeza. Kazi ya upinzani ni kukosoa serikali. Serikali haitaki kukosolewa, what do yu ekspektii?
 
Ukweli ndio unamaslahi kwa Taifa na msema ukweli ndiye mzalendo wa kweli.

Hata mh Rais wetu hilo analitambua ndiomaana anasema kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Kitu cha kusikitisha haohao ndio wanaomtaka mtu kama Lissu awempenzi wa shetani kwa kutokusema ukweli juu ya ukweli wanaouficha.
 
Mkuu, sijui kama nimeielewa vizuri hoja yako kwani umechanganya hoja karibia nne ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja. kuhusu morality, public interest (maslahi ya kitaifa), kusema ukweli na issue sijui za kuandamana na wapinzani kupinga hoja zinazotolewa na serikali...kila hoja hapo juu ni independent na inahitaji forum yake na nikisema nichambue kwa undani...huenda ikanichukua hata page 300. kama umesoma sheria, kuna precedence nyingi tu pale sheria inapokinzana na kitu kinachoitwa morality. kwa bahati mbaya or nzuri, Tanzania tunafuata sheria zilizotungwa na Bunge na siyo maadili( morality).

kwa kifupi, what looks immoral to you...is vice-versa and true on the other side. Kuna rules of the game...kwamba wanasiasa lazima waseme uongo kwa wananchi ili waendelee kuaminiwa etc...practice inaonyesha hivyo na wananchi wanajua kuwa wanaongopewa lakini hawana namna...na hiyo ndiyo moral ya wanasiasa.

kuhusu kupinga kila kitu:
kwa kipindi cha miaka kama 2 siasa za Tanzania zimekuwa ngumu sana kwa upande wa vyama vingine ambavyo havikufanikiwa kushika dola( upinzani). kumekuwepo na siasa za visasi na ustaarabu umetoweka. ingawa upinzani haujaanza leo wala jana (Refer the political parties Act of 1992)...upinzani umekuwa unahujumiwa na kutendewa sivyo ndivyo...kwa hiyo hakuna namna, lazima waendelee kupinga kama retaliation dhidi ya serikali iliyoko madarakani. hilo siyo jambo geni hususani kwenye mazingira ya siasa za Kiafrika...na mimi nasema waendelee kupinga tu...maana hakuna namna sasa!

Sura ya Upinzani na falsafa iliyojificha: kwanza kabisa, vyama vingi (sijui ndo munaita upinzani) ingawa sikubaliani ni definition hiyo....vilianzishwa kwa kushinikizwa (Rejea tume ya nyalali) na wengi kwenye mfumo wa serikali hawakuwa tayari mioyoni mwao kupokea vyama vingi kwani waliaminishwa kuwa kutatokea vita na mengine mengi ya kupotosha. baada ya vyama vingi kuwepo, bado watu walio wengi walibaki walewale...na falsafa ileile...kuwa upinzani ni mbaya na mtoto akienda kwenye chama tofauti na CCM ataitwa msaliti na mengineyo ya kubeza....kutokana na kutokuheshimiana na kujenga siasa za uadui...ndo imezaa taswira ya falsafa ya upinzani wa leo....

Je ni lazima kusema ukweli kila unaousikia?:- hapo nahisi utakuwa umesahau misingi iliyojenga taifa hili...ujamaa na kujitegemea!. kila zuri lina baya pia, hivyo basi ujamaa ulikuwa na side effect kwa watu wake. watanzania siyo watunza siri. na huo msemo upo huku nchi za kusini mwa Afrika. mfumo uliwatengeneza watu kuwa watoa siri, taarifa na mengineyo kama kuna mgeni siyejulikana kijijini na hata suala la kujilimbikizia mali. kila mtu alibaki kuwa watch-dog kwa mwenzake...(ingawa sijui sasa ikoje). ndo maana watanzania wengi hawana siri na ni wambea....@Pascal Mayalla
 
Mayala usiwe msahaulifu.
Hakuna anayejipendekeza kuwakamata wapinzani.

Naomba nikukumbushe kama unajifanya msahaulufu.

Magufuli alisema bila ya kificho mbele ya waandishi wa habari akimuagiza ndugai kuwa awashughulikie wapinzani bungeni tena akaenda mbali kuwa awafukuze ili waje mtaani awashughulikie.

Na leo tunaona ahadi yake iyo ikitimia.

Mayala heshima yako ni kubwa humu ndani, usiache kuendelea kutumia akili yako ya zamani.

Haya yote ya ukamataji na kadhia nyengine zinazowakuta wapinzani ni mkono wa magu na anatimiza ahadi yake.

Haiitaji akili kutambua hilo
 
Mkuu pascal kwenye JD ya Rais hakuna kitu kinaitwa kufanya jambo lolote bàya,aliomba kazi aifanyie Tanzania na watanzania mambo mazuri,kwa hiyo anapofanya mazuri anatekeleza wajibu wake na tunamlipa kwa hilo. Akitenda baya tutamuonya na kwa watu wenye akili zao wanamfukuza kabisa.So kumkosoa rais ni wàjibu wa lazima ila kumsifu si wajibu wala si lazima
 
Ukweli ni ukweli tu na uongo ni uongo tu. Ni sawa na giza na mwanga huwa hakuna middle ground. Kama kweli unaamini katika Ahadi ya Mwana TANU kama ulivyojinasibu nilitarajia uwe na msimamo usioyumba.
 
Ndio sio lazima kusema kila ukweli unaouona ila kuna ukweli mwingine ni lazima usemwe.Kwa hili la TL mimi sidhani kama alivyolisema lingekua na athari yoyote kwa taifa maana ni haki ya wananchi kujua matumizi mabaya ya kodi zao ila tatizo ni kwamba limesemwa awamu ambayo haitaki kusikia ikisemwa kwa lolote.kwani kuna mambo mangapi ya hovyo yaliyofanywa na serikali zilizopita na yakasemwa na vyama vya upinzani waziwazi na mwisho wa siku haikua issue kubwa na yakapita.kwaiyo tatizo hapa sio ukubwa wa kilichosemwa bali wale ambao hawapendi kusikia kilichosemwa.Hawa kwavile hawapendi kusemwa ndo maana hata wakisemwa jambo dogo la kawaida wao wanalikuza kwakutumia nguvu nyingi kulipamba ili waonekane wao hawakoseagi.Mimi nadhani ili jambo wala lisingekua kubwa kama mara baada ya TL kulisema serikali ingekuja na majibu kua ndio ndege imekamatwa na tunashughulikia,baada ya hapo wala tusingesikia hizi kelele zote ila kitendo chakutumia nguvu kubwa kujipamba ayo ndo matokeo yake.ILA LAZIMA UJUE SIKU ZOTE UKWELI NI MFUPI NA UONGO NI MREFU.
 
walishasema kazi yao kuuu ni kupingapinga tu basi lakini nafikiri kuna haja ya kujitafakari sio kila kitu kuropokaropoka kuna issues nyingine ni too classified sio lazima Uzi disclose for political gain hii issue ni national matter against our enemy na wanatushangaa baadhi yetu kuwa upande wao
kama unadai unadaiwa,ufiche usifiche unadaiwa tu.Sisi walipa deni kujua tunadaiwa imemwongezea nini mdai wetu? Acheni kujitoa ufahamu jamani tutaliangamiza taifa letu
 
What is the end product of seeking truth if not telling it. Hahaha going with it to your grave??
Halafu kusema ukweli na kuangalia maslahi ya Taifa haviendi sambamba kila wakati.

Chagua moja kama ni kusema ukweli sema ukweli kama ni maslahi ya taifa ni maslahi ya taifa.

Na tunajua wengi wanafanya maovu in the name of maslahi ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro hua unazunguka sana ila una shindwa kusema ama kujiripua kua wewe ni CCM.Trust me hii haina madhara hata kidogo the moment utakapo declare basi wewe utakua katika pipeline ya kupata wadhifa mkubwa .Tumia fursa usijifiche .

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemwambia ukweli kabisa, awe wazi tu.
Jamaa anajikombakomba mpaka inakera.
Kitu kiko wazi, Magu yeye kila siku ni kuliletea taifa hasara tu lkn mtu anataka tufiche.
Tufiche kwa faida ya nani?

Mficha maradhi kifo humuumbua sasa sijui Pascal Mayalla anataka mpaka kifo kije kituumbue
 
Mi nadhani ukweli lazima usemwe bila kujalisha nini... Kwa maana Rais wetu kila siku anasema MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU.
 
walishasema kazi yao kuuu ni kupingapinga tu basi lakini nafikiri kuna haja ya kujitafakari sio kila kitu kuropokaropoka kuna issues nyingine ni too classified sio lazima Uzi disclose for political gain hii issue ni national matter against our enemy na wanatushangaa baadhi yetu kuwa upande wao
Rubbish,

Takataka kabisa.
Kuliletea hasara taifa ni maslahi ya taifa?
Are u serious?

Tatizo la hii nchi ni kwamba mbumbumbu ndiyo wanaotafuta na kupeana uongozi wenye akili timamu wamekuwa waendesha taxi mitaani
 
Maoni yangu ni kwamba inabidi tuelewe vizuri na tukubaliane, nini hasa maana ya MASLAHI YA TAIFA. shida iko hapo. kwa upande wa watawala wetu, maslahi ya taifa ni maslahi yao. maslahi ya CCM ndiyo maslahi ya taifa. Full Stop. sasa shida inaanzia hapo. Chukulia suala la Lissu na Bombadia iliyokamatwa. Hoja ya Lissu ilikuwa ni kwamba Taifa linapelekwa kwenye hatari kubwa ya kuvunja ovyo mikataba, hali ambayo itapelekea tulipishwe faini kubwa na nyingi, na hii inaathiri kwa kiasi kikubwa MASLAHI YA TAIFA. Lissu alijenga hoja yake katika kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Kabudi, na Waziri wa habari nk., Dr. Mwakyembe, ambaye pia ni mwanasheria nguli. hawa walisema bungeni, baada ya hoja za Lissu kuhusu tahadhari kwa maamuzi ya serikali mintarafu mikataba, kwamba Tanzania ni Sovereign State, na kwa hiyo hatuwezi kuogopa kuvunja mikataba. Lissu alitahadharisha kwamba hii kauli ni Reckless na haina umakini wala weledi, hasa ikitoka kwa wanasheria nguli. kwa hiyo hoja ya Lissu iko wazi sana, kwamba anatetea MASLAHI YA TAIFA. Ilibidi aseme wazi kwa sababu kuna ajenda ya watawala ambayo wanaipigia kelele nyingi sana kwa kutumia vyombo vyao vyenye nguvu. sasa Tundu Lissu ni mtu mmoja tu, tena asiye na nguvu kama Dola. ilibidi apige kelele namna ile ili taifa lisikie.

Watawala katika jitihada za kumzima Lissu, kuwafanya wananchi wasimsikilize, wakampaka rangi ya kukosa uzalendo, kutojali maslahi ya taifa, na kufurahia matatizo ya nchi. hii ni propaganda ambayo wenye akili wanatarajiwa kuiona na kuiweka wazi. Aliyesababisha hasara hii kubwa kwa taifa, ndiyo huyo ambaye sasa hivi ndiye Rais wetu. ameingia kwenye mzozo mkubwa na wapinzani, kutokana na njia zake ambazo siyo za kikatiba, na kinyume cha sheria na kanuni za vyama vingi, na pia anatumia nguvu za Dola kuwabana, kuwatesa na kuwanyanyasa wapinzani. haya yote yanatakiwa kutiliwa maanani, namna nyingine tutakuwa tunacheza ngoma za wapika propaganda.

Kwa hiyo suala la Morality lina nafasi yake, lakini morality hapa ni kuwaumbua watawala, kuwaweka mbali na kile kinachoitwa MASLAHI YA TAIFA. kama kweli maslahi ya taifa yangewekwa mbele, tusingeshuhudia bomoa bomoa inayoendelea hivi sasa katika barabara ya kimara - kiluvya, kwa mtindo huu, tena kinyume na maamuzi ya mahakama.

MASLAHI YA TAIFA ni kujua ni kwa vigezo gani Magufuli alivunja mkataba ule, ukweli uwekwe wazi kabisa, siyo kuficha ficha eti kwa sababu Magufuli ni Rais. inabidi tufanye kama kule Israel, ambapo mtawala anaweza kushitakiwa wakati wowote. kumfanya mtawala kuwa nusu mungu ni kunajisi maslahi ya taifa na siyo moral.
I second this post
 
Tuanze kwa kujiuliza kwanza, Je Ukweli ulifichwa kwa nia njema au mbaya?.
Je Ukweli ulifichwa kisiasa au Kimkakati?, kama ni kisiasa basi hayo ni manufaa ya kisiasa ya watu wachache na Siyo Taifa zima Kwa hivyo ni sahihi kuuibua ili kumpiku mpinzani wako wa kisiasa, lakini kama ulifichwa kimkakati kwa maslahi ya Taifa basi si vyema kuusema huo ukweli, maana hii ni sawasawa na Majambazi wanamtafuta dingi yako aliyejificha chini ya uvungu halafu wanakuuliza mzee yuko wapi then kwa kuwa unajifanya ni mkweli sana unawaonyesha mzee alipo, hapo kweli utakuwa Umezingua.
Lakini Kama Wanamtafuta Mzee ili akajibu Mashitaka yake ya Kutaka kuchoma kijiji moto, tena unajua kweli alishiriki kikamilifu katika hilo halafu usiuseme kuonyesha huyo mhalifu alipojificha basi wewe mficha ukweli utakuwa na wewe huna maana!, kwa sababu katika hatua hii inatakiwa kuokoa kijiji siyo mtu!
 
Back
Top Bottom