Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Mara kadhaa raisi amesema... MSEMAKWELI NI MPENZI WA MUNGU.....

Na moja ya ahadi za TANU (CCM baadaye) ni kusema kweli daima, fitina ni mwiko...

KWENYE HAYO HAPO JUU... the only condition ya kusema kweli ni
1. Ukweli uwe kweli
2. The fact kwamba ni ukweli, hakuna lingine la kuangalia... USEMWE TU
3. Ukweli usemwe wakati wote.... hata mahakamani, ukidanganya, na ikathibitika, WOTE TUNAFAHAMU MATOKEO YAKE
4. Ukweli hauna muda, mahali, wala anayeambiwa ukweli huo ni nani... UKWELI DAIMA

HIVYO TUSEME UKWELI, NA SIKU ZOTE UKWELI UNAUMA....


Mbona issue ya change ya radar ilijadiliwa kwa uwazi sana bila watu kukamatwa? Je haikuwa ya maslahi ya Taifa? je kuna tofauti gani baina ya deni inalodaiwa serikali na ile change ya radar ambayo serikali ilidai? tumekuwaje watanzania? mbona ugonjwa wa unafiki unashika kasi sana jamani?
 
Paskali: hili siyo swali la morality tu, pia ni la kisheria. Kuna madhahidi fulani fulani hawakubaliki kutoa ushahidi - mathalani, Lawyer kuhusu alichoambiwa ns mteja; au Padri aluchoambiwa wakati wa kuungama, au Daktari kuhusu mgonjwa wake. Hizi ni ckear-cut, lakini kuna zingine pia japo zinapita, hutiluwa mashakanashaka: mfano ni mtu na mumewe au baba na mwanaye au nyani na ngedere. Hii ya Tundulissu kutoa siri za nchi na kuwapa maadui ushahidi wa kimahakama miaka nenda rudi, halafu kuwatonya kwamba kuna ndege yetu mahali waende wakaikamate, huu ni uhaini. He us spying on his country for the benefit if uts creditors. Swali pekee tulilonalo ni kama atanyongwa au atapata msamaha wa Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu tusaidie nasisi tuamini kwamba LISU aliwatonya Wadai wetu... maana nahisi hapa kama umekariri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linakuja ambapo kiongozi wa juu haishi kwa Maneo yake 'What Can you do when a Public Figure does not keep his words'
 
Paskali kiukweli Leo nimekuvulia kofia kama mwanahabari mbobezi .Mara nyingi Mimi hupenda kuangalia runinga za wenzetu na hasa kwenye mahojiano .Uandishi Wa wenzetu siku zote akiona serikali inabanwa na ili kulita taiga lake,itakuta mwandishi Hutu in mwepesi kukatiza kipindi kwa kuomba msamaha kuwa muda wake umeisha .Huwezi kuona wenzetu wakiivua nguo serikali yao .
Lakini hapa kwetu naona tunaanza kushabikia kuona serikali inashindwa kufanya Nazi ili sijui iwe vipi.
Naona siku hizi watu wanaomba serikali isisaidiwe kupata misaada kwa sababu za kisiasa.
Huu ni upuuzi uliopitiliza,maana wanaoumia no wengi Wa kipato cha chini na sio watawala Wa kipato cha juu.
 
Tatizo la Paskali ni kumangamanga na kuhamisha magoli kulingana na maslahi yake yako wapi! Kusema ukweli sio Hodhi au haki ya mtu mmoja bali ni amri ya Mungu kwa waja wake wote ndio maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu, hapaitajiki kuuwekea vigezo
zaidi, tuache UKWELI UBAKI KUWA
UKWELI, ILI UTUWEKE HURU. Paskali koma hiyo tabia ya kushift goal posts whenever it suits you.
 
sio kila ukweli unausema aisee utakuja angamiza Taifa

Hivi unasema ukweli ili kulifurahisha taifa? Nijuavyo mimi na rais ni shahidi yangu kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu na huwa anasema atasema ukweli hata kama tutamchukia. Sasa inakuwaje nyie mpange ukweli wa kusemwa wakati hata rais yuko tayari kuchukiwa kwa kusema ukweli!?

Cc: Paskal Mayalla
 
Pascal

Suala la 'morality' halisimami bila viungo vingine na kimoja ni integrity (uaminifu)
Kama hakuna integrity haiwezekani ku maintain moral principles.
Mkokoteni unawekwa nyuma ya farasi si mbele, huwezi kuongelea moral principles bila kuwa integrity

Integrity inaanza kwa mtu, watu, jamii na taifa. Uki compromise integrity kamwe usitegemee ''morality''
Ukivunja integrity unavunja 'morality' na zao lake ni free play siyo fair play kama utanielewa

Tukiamini watu wasaini mikataba tunawapa integrity
Wakichukua 10% na kuweka Uswiss wana-compromise moral principles na hakuna std.
Anayesema tunaibiwa anakiuka 'morality' gani ikiwa tayari waliopewa trust wamevunja?

Mfano wa pili, kukiwa na tatizo bila sisi kuambiwa ni kuvunja trust, wanaofanya hivyo hawana integrity na wana compromise moral principles zao na za Taifa.
Akitokea mtu akasema kuna tatizo kadhaa! mtu huyo anakiuka morality gani?

Eneo la usalama na hasa Jeshi lina integrity na morality ya kiwango cha juu sana
Upo uchaguzi kiongozi wa Jeshi alizungumzia nini kitafanywa na jeshi kukitokea vurugu

Kiongozi yule alivunja integrity ya jeshi kwa kuingiza siasa.

Hata hivyo alifanya hivyo kwa masilahi mapana ya Taifa (public interest) licha ya ku-compromise integrity ya jeshi. Akasema ukweli bila kujali morality akitanguliza masilahi ya nchi

Ndivyo kiongozi mwingine wa siasa ameona kuna ''moral void' katika suala fulani.
Hata kama ame compromise morality, anachofanya ni kwa masilahi ya nchi, kasema ukweli.

Ukiongelea integrity na morality kwa Taifa, kubwa kuliko yote ni public interest
 
Paskali kiukweli Leo nimekuvulia kofia kama mwanahabari mbobezi .Mara nyingi Mimi hupenda kuangalia runinga za wenzetu na hasa kwenye mahojiano .Uandishi Wa wenzetu siku zote akiona serikali inabanwa na ili kulita taiga lake,itakuta mwandishi Hutu in mwepesi kukatiza kipindi kwa kuomba msamaha kuwa muda wake umeisha .Huwezi kuona wenzetu wakiivua nguo serikali yao .
Lakini hapa kwetu naona tunaanza kushabikia kuona serikali inashindwa kufanya Nazi ili sijui iwe vipi.
Naona siku hizi watu wanaomba serikali isisaidiwe kupata misaada kwa sababu za kisiasa.
Huu ni upuuzi uliopitiliza,maana wanaoumia no wengi Wa kipato cha chini na sio watawala Wa kipato cha juu.
Nawewe niwale wale Hebu jiulize Tumefikaje hapa !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maslahi ya taifa ni pamoja na kusema ukweli

"Msema kweli ni mpenzi wa mungu"- John pombe magufuli
 
Paskali kiukweli Leo nimekuvulia kofia kama mwanahabari mbobezi .Mara nyingi Mimi hupenda kuangalia runinga za wenzetu na hasa kwenye mahojiano .Uandishi Wa wenzetu siku zote akiona serikali inabanwa na ili kulita taiga lake,itakuta mwandishi Hutu in mwepesi kukatiza kipindi kwa kuomba msamaha kuwa muda wake umeisha .Huwezi kuona wenzetu wakiivua nguo serikali yao .
Lakini hapa kwetu naona tunaanza kushabikia kuona serikali inashindwa kufanya Nazi ili sijui iwe vipi.
Naona siku hizi watu wanaomba serikali isisaidiwe kupata misaada kwa sababu za kisiasa.
Huu ni upuuzi uliopitiliza,maana wanaoumia no wengi Wa kipato cha chini na sio watawala Wa kipato cha juu.
Kwa wenzetu wapi wewe uswazi kwako?! Huko kwa wenzetu unakokuota vyombo vya habari vinagawanyika kabisa kiitikadi na kisiasa na watasimama hivyo na kuponda au kuunga mkono serikali kutegemea msimamo wao wa kisiasa, leo hii kituo cha TV cha CNBC katu hakiwezi kuunga mkono serikali ya Republican na kule Uingereza gazeti la The Sun haliwezi kuitetea serikali yoyote ya chama cha Lbour, iwe mvua au kiangazi!
 
let people know the truth and the country will be safe by Abraham Lincoln,kuna wakati mnaojiita wanahabari huwa mnawaheshimu sana wa asisi wa demokrasia lakini kunamuda mnajifunga macho kuukata ukweli unaowapa ahueni ya maisha..!!the truth is incontrovertible. Malice may attack it,ignorance may deride it,but in the end,there it is...!!!🙁🙁🙁🙁
 
Njaa hainaga kawaida ya kumuacha mtu salama...sasa unaogopa kusema nini sizonje ndo anaewatuma hao kamata kamata?unafiki mwingine mpaka kero yani...
 
Tatizo lisu na upinzan wote hawajui nini wakiseme na nini kisisemwe kwa maslai ya Taifa. Wao wako for political gain sio public gain.

posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
 
kabla ya kuongea kitu, unatakiwa ku foresee impact yake kwanza. jambo hili limewapita kushoto watu wengi na sidhani kama linatakiwa kutafsiriwa kwenye misingi ya morals (morality), bali uelewa kielimu, kiutandawazi,kiuzoefu wa mahusiano kimataifa na kitaifa, na kisiasa pia. kuna wakati nilibishana na mtu kuwa unaweza kuwa na phd au hata profesa lakini bado mjinga...anabisha hadi leo, lakini ukweli ndio huo. kuna watu wengi akili zao zina mapungufu makubwa sana pamoja na kwamba kwenye vyeti wako vizuri.
 
Paskali unaongelea "Moral principle" gani hasa kwenye swala kama hili? Kuna watu walikosa "morality" wakavunja mkataba kwa ubabe bila kufuata principles! Matokeo yake tukashtakiwa na kushindwa kesi hivyo kupaswa kulipa fidia! "Moral principle" ingetaka hapa mhusika awajibike kwa kulisababishia Taifa hasara! Baada ya kushindwa wahusika serikalini walipaswa kulipa deni/fidia husika ila hawakufanya hivyo mpaka deni likaongezeka mara dufu! "Moral principle" ingetaka wahusika wa hili wawajibishwe kwa kulisababishia Taifa hasara! Lakini hili nalo halikufanyika!

Kusingetokea mwanaume mwenye "moral authority" ya kuthubutu kutaja jambo hili hadharani, bado yangekuwa ni yale yale mambo ya "funika kombe mwana haramu apite"!! Yaani mnaacha kukimbizana na mwewe aliyekula kuku mnahangaika na aliyeona manyoya na kulia kwa sauti "jamani ee, kuku kaliwa"!!!

Huo ni unafiki na uzandiki wa kujipendekeza tu kwa watawala!!!
 
Nitakupinga kama una lengo la kuzuia mimi mlipa kodi:
- Nisipate taarifa za matumizi mabovu ya kodi yangu yanayosababishwa na watawala wabovu
-Nisipate taarifa za udhaifu wa kiongozi ninayemlipa mshahara na masurufu mengi kuliko wote kwa kupitia kodi yangu.
- Nisipate taarifa za namna ya kuwawajibisha viongozi ninawalipa na kuwahudumia wao na familia zao.
- Kama unamsema Tundu Lissu umekosea sana! Huyu ni shujaa wangu anayenisaidia nitimize yote matatu hapo juu.
-----Ningejulia wapi kuwa Huyu Rais niliyemchagua na ninayemlipa kumbe kazi yake ni kuliingizia hasara taifa kwa kutoa maamuzi mabovu?
Tundu lissu GOOOOOOOOOOOOOOOO ma bro you my hero! Deep into Magufuli's heart he appreciate you!!
 
Back
Top Bottom