Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi.

Kama kawaida yangu, kila nikipata muda, nashuka na zile makala zangu elimishi za KMT - "Kwa Maslahi ya Taifa". Mada ya leo ni swali la kitu kinachoitwa "morality": "Je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?.

Na tukija kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli wowote tunaousikia, je ni lazima tuseme tuu kila kitu tunachokisikia au kwanza, tutangulize mbele maslahi ya taifa kwa kujiuliza kwanza, hicho unachotaka kusema kina maslahi kwa taifa?, na unatakiwa kuupima kwanza huo ukweli kwa kujiuliza, je, ukweli huu ukijulikana una matokeo gani kwa taifa?, ndipo tuuseme, au tuendelee tuu na hii tabia ya kusema kila kitu unachokisikia?. Ukisikia jambo lolote, wewe liseme tuu bila kujali jambo hilo linamatokeo gani as long as jambo hilo ni la kweli?.

Na ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, wapoliticise kila kitu?, kila jambo? na kila tukio?.

Declaration of interest.
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya kwanza ya mwana habari, (cardinal rule ni " tell nothing but the truth, no matter what!", lakini before telling the truth, mwandishi anatakiwa kutumia kitu kinachoitwa "objectivity test" yaani kuwa objective kwa kuupima ukweli huo una faida au manufaa gani kwa jamii, taifa na mhusika?.

Hivyo mimi as a journalist ni mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU ya " Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, nasema na kuandika kwa kutumia kitu kinachoitwa responsible journalism kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kabla sijaandika, ninajiuliza kwanza, je ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.

Ukisikia jambo, au ukiona jambo, japo ni ukweli lakini kama ukweli huo, ukijulikana, badala ya kujenga, utabomoa, then ukweli huo, siusemi. Huu ndio uzalendo wa kweli wa taifa lako kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Mfano mzuri ni kwenye issue ya JPM, kuna ukweli fulani niliowahi kuusikia kumhusu JPM, hivyo niliposikia anaweza kuja kuwa rais wa JMT, niliusema kwenye bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
Kwenye bandiko hilo kuna kitu nilisema nitakisema, mwisho wa siku, sikukisema!. Na baada ya JPM kuwa rais wa JMT, kuna siku nilikiulizia, Kauli ya Kakobe "Magufuli atubu", yaibua mambo! Je asili halisi ya Rais Magufuli ni Msukuma, Mhaya au Muha wa Kakonko? nikakuta hakuna anayekijua. Kwa vile sasa tayari JPM ndie rais wetu, ukweli huo ninaoujua ukijulikana, hautasaidia kitu, sio tuu, haujengi bali unabomoa, hivyo siusemi kabisa, lakini ili kuzuia jambo kama hili lisijirudie in future, nilitoa ushauri Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu?
Sometimes ukweli too much unaponza!.

Hii Kamata Kamata ya Kila Waompinga Magufuli, Ni Magufuli Anawatuma au Polisi Wanajipendekeza Tuu?.
My honest opinion, ingawa ni kweli rais Magufuli hapendi critics, mimi nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu toka kwenye kinywa chake na sio kwa kuhadithiwa, alisema anapenda challenge, ila hizo challenge ziwe ni ukosoaji wa kweli wenye nia njema, hivyo naamini hizi kamata kamata zinazoendelea za kuwakamata karibu kila wanasiasa wanaompinga rais Magufuli, siamini kama ni Magufuli anawatuma!, naamini hivyo ni kazi ya polisi wetu ambao wana jikomba komba tuu ili kuonekana wanafanya kazi.

Kwenye siasa za multipartisim duniani kote, kazi ya the opposition ni kupinga, kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.

Nimeishi kidogo UK, US, na Uswiss. Uingereza pale Times Squire karibu kila siku ni maandamano. US ule mtaa jirani na Capitol Hill kuna uwanja unakuwa huru kupinga chochote, Uswiss uwanja huru wa kupinga, ni pale uwanja wa wazi nje ya ukumbi wa Bunge, the The Bundes House. Hivyo sioni mantiki ya sababu zozote wanaompinga rais kubughudhiwa!, this is not democracy, Tanzania sio nchi ya kidikiteta!, tena kiukweli, kama katiba yetu imeruhusu mikutano na maandamano, hakuna any justified reasons at all za rais Magufuli kupiga marufuku, ni ukiukwaji wa wazi wa katiba ya JMT, but to be honest, yeye kama rais wa JMT kwa mujibu wa katiba yetu, hana mamlaka ya kuzuia jambo lililoruhusiwa na katiba, and he gas nothing to loose akiruhusu mikutano na maandamano.

Wito kwa IGP, Kamanda Sirro, controll vijana wako watekeleze majukumu yao kwa sheria taratibu na kanuni na sio kwa kutaka kujipendekeza au kujikomba komba!.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti ...


Jee Wapinzani Kazi yao ni Kupinga Tuu Kila Kitu au Kukosoa Tuu Hakuna Kupongeza Hata kwa Mazuri?.
Japo kazi ya upinzani ni kupinga na kukosoa, lakini tunapokuja kwenye issues muhimu kwa maslahi ya taifa, maslahi yataifa ndio yanatangulizwa mbele, sisi sote kama Watanzania, we stand as one, tunakuwa kitu kimoja, tunakuwa watu wamoja, tunaweka mbembeni tofauti zetu za kisiasa, hakuna tena siasa za vyama, wala siasa za watu, tunaweka pembeni siasa, tunaitanguliza mbele Tanzania, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, we stand as one, na kila kitu kinafuatia baadae.

Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El ...


Mfano mwingine wa kuujua ukweli fulani na kutousema ni ukweli huu nilio uandika kuhusu Bunge letu tukufu. Kwanza niliandika Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi?, kisha nikaandika Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? Bunge likakasirika, nikaitwa Bungeni kuhojiwa na Kamati Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge nilihojiwa Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge na baada ya mahojiano, Bunge walinyamaza kimya, na mimi kuna ukweli niliwaambia ukawaingia wakanyama kimya na mimi sikuwahi kusema kilitokea nini kule , nimenyaza mpaka leo mpaka kesho, kwasababu sio lazima kila ukweli usemwe, ukweli mwingine ukijulikana ni aibu!. Ukweli mwingine una bagaza, na hausaidii chochote!.

Hata lile tukio la Machi 17, kuna watu tunajua lilitokea lini na Jamaa alichomoka kwa ugonjwa gani!, lakini kwa vile tumetangaziwa ni tarehe 17 na ugonjwa ni ule, japo ukweli tunaujua, lakini hatuusemi!. Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?
Conclusion
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini je ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia?. Kwenye medani za siasa, kabla ya kuusema ukweli tunaousikia, je tutangulize kwanza mbele maslahi mapana ya taifa kwa kuupima kwanza, ukweli huo una matokeo gani, ndipo tuuseme, au tuendeleze kusema tuu, kupayuka na kuropoka kila ukisikia lolote, lisema tuu kwa sababu ni la kweli?. Je Ili kupata manufaa ya kisiasa, je ni lazima wanasiasa wetu, tupoliticise kila kitu?.
Wito wangu ni sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni cha kweli!, tujifunze kunyamaza, ukimya nao ni jibu!.

Wasalaam.

Paskali

Rejea.
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Kitendo cha kuita nchi majirani zako kuwa ni "vinchi" ni uungwana ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hoja ya Udikiteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...
 
walishasema kazi yao kuuu ni kupingapinga tu basi lakini nafikiri kuna haja ya kujitafakari sio kila kitu kuropokaropoka kuna issues nyingine ni too classified sio lazima Uzi disclose for political gain hii issue ni national matter against our enemy na wanatushangaa baadhi yetu kuwa upande wao
 
As long as UKWELI utahusiana na KODI ninayolipa basi lazima usemwe.Ukifanya baya lazima lisemwe.Ukifanya zuri litasemwa pia,kama linamakosa litakosolewa ili liwe zuri zaidi.

Hakuna mtu aliyempinga JPM kwenye issue za Madini aka Makinikia lakini onyo lilitolewa na wayfoward ili kuepuka malipo zaidi kama tuliyonayo leo ya madege yetu kutaka kupigwa mnada huko UGHAIBUNI.

Ukiwa kiongozi lazima ukubali kusikiliza hata kama hupendi kuusikiliza ukweli lazima uusikilize.

JPM hapendi kuambiwa ukweli anapenda kusifiwa tu hata anapoharibu.Na ili uapte cheo basi lazima umsifie ufanye anayofanya yeye,Ukinyanyasa wapinzani lazima upewe nafasi kubwa.

Akina Ndugai wanasubiria U-PM ndiyo sababu hata huko Bungeni wanafanya vihoja.Ukienda Mahakamani Mahakama ni Bubu sababu Jaji Mkuu anataka apewe ulaji kamili hivyo anajali tumbo kwanza hakuna haki,haki katafute Mbinguni.

Kama Taifa tumeishakufa tumebaki kama Makaburi yaliyopakwa chokaa.
 

hahahahah..bado mnahangaika tu

Mnafanya maamuzi mabovu na kuingiza gharama nchi halafu mnataka wenye nchi yao wasijue????? uzwazwa huo
 
Nyakati fulani tuwe wa kweli, si kila ukweli ni lazima usemwe upenuni, tatizo linakuja pale ukweli unaposemwa chumbani na msema kweli, bado mtu anayeambiwa kweli hasikii wala kubadilika. Matokeo yake ni ukweli huo au siri hizo kutoka nje. Hasa hasa kama ukweli huo au siri hizo au jambo hilo linaumiza wengine ambao hawakustahili huku likiwaacha wengine wakifaidi kwa majivuno na tambo kubwa kana kwamba ni malaika, kumbe sivyo. Sasa wewe ambae ulipoambiwa ukweli mlipokuwa wawili au chumbani tena sio mara moja au mbili na ukagoma kuupokea, unatarajia mwonyaji au msema ukweli afanye nini zaidi ya kupiga panda hadharani labda utashtuka akifanya hivyo. Na kweli wabishi wengi jambo likitoka nje utawaona reactions zao tu .........! Hawajikiti kwenye kujibu hoja bali hu-deal na mtoa hoja!
 
"Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko" - ahadi ya/za mwanaTANU/CCM ambazo tulifundishwa tangu shule. Ni muhimu sana kukumbushana ahadi hizi hususan kuwakumbusha ahadi zao hizo. Tena siku hizi imeboreshwa zaidi - "MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU", naam Mungu na akawe shahidi wa haya tusemayo.
 
Paskal,
Naamini umetumia muda kuandika waraka huu lakini kuna makosa madogo madogo,ndio ubinadamu.
Andiko lako lote limeshindwa kuleta rejea zenye maana kuhusiana na hasa ulichodhamiria,morality katika kuelezea ukweli!!
Washiriki wakuu wa andiko lako ni serikali iliyoko madarakani na upinzani lakini umeshahu kuwa kashfa zote kubwa ambazo zingine zimetuvua nguo mpaka kumgusa mkuu wa nchi (mgao wa Escrow uliingia Ikulu,Suit za kifahari...) zilizungumzwa na upinzani.
Sijawasikia wapinzani wakiuliza kwa nini tumenunua vifaru vya Urusi kuliko vya Marekani au makombora ya kudungulia ndege yamepitwa na wakati,naamini wanaijua mipaka hayo.
Katika andiko lako hili umeweka rangi (kumpamba) Mkuu kuwa ulimsikia akisema anapenda challenge lakini naomba nikuulize kuwa baada ya kumsikia vipi matendo yake?
Kama kweli napenda challenge na hafurahii yanayotokea mbona hajakemea mpaka leo?Mikutano yake yote inaanza na kuhimiza amani na umoja lakini mwishowe ni vijembe na vittisho.
Twende kazi,ndio kwetu hapa na JPM ndiye Raisi wetu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…