Kaka yangu Paskali, naweza kukupa somo jipya litakalo kusaidia katika maisha yako yaliosalia hapa duniani.
Kamwe hakuna ukweli unaobomoa, maana ukweli ndio asili ya Mungu mwenyewe kwa hiyo unaposema ukweli mahali popote umeufurahisha moyo wa Mungu. Kiroho, Kimwili, na kisaikolojia usiposema ukweli umejiumiza mwenyewe.
Labda jambo ambalo ungesema katika kusema ukweli lazima hekima itumike. Nitamani ni kuwekee mfano mmoja wa kusema ukweli kwa hekima.
Mfalme Daudi alimtamani mke wa mwanajeshi wake, kwa hiyo akamfanyia hila kuhakikisha anauawa vitani, Mungu hakupendezwa na jambo hilo, kwa hiyo alimtuma nabii Nathan kumwambia Daudi uovu wake. Nabii alimwambia Daudi kuwa kuna mtu mmoja tajiri ametembelewa na wageni, ila amechukua kondoo wa maskini akawachinjia wageni wake.
Mfalme Daudi alihamaki na kusema kwamba huyo tajiri lazima auawe, nabii akamwambia Daudi kuwa mtu huyo niwewe Daudi alilia sana na kutubu. Ukweli kwa njia ya hekima, ila ukweli unatakiwa usemwe kila wakati