Kuna kitu naomba kueleweshwa,Siro hajastaafu jesho la polisi ila kapelekwa ubalozini akiwa na cheo chake,Sasa IGP ni Wambura akiwa na cheo hiko hiko...Je nani Senior kati ya Siro na Wambura? na je wote wana cheo kimoja na madaraka tofauti?
IGP ni cheo ingawa Polisi kwa cheo hicho wanakitumia kwa kumuita mkuu wa jeshi la polisi pia.
Ulichokiuliza mantiki yake inaijia hapo, kwanini kuwe na Igp Wambura wakati Igp Siro hajastaafu.
Kwa cheo cha Siro ni Igp ambaye anatumikia nafasi ya Ubalozi na Wambura ana cheo Cha Igp na madaraka ni Igp pia.
U senior au umbele katika majeshi, unahesabika kwa mtu aliyetangulia kuvaa cheo kinacholingana kwa kutangulia hata kwa siku1tu kuvaa.
Hapa kwa kweli kuna mkanganyiko kidogo ukitofautisha na Army(Jwtz).
Jeshi mkuu wao wa jeshi ni Cdf lakini cheo chaweza kuwa General ama vyovyote, ni tofauti na Polisi cheo cha Inspector General of Police kukitumia kama madaraka!
Na ukumbuke pia kuwa ukuu wa Polisi, Jeshi, Magereza na vitengo vinavyofanana nao, madaraka hayo ni ya kisiasa, muda wowote rais anatengua uteuzi wake na kuwekwa pembeni ama kupangiwa kazi nyingine kama walivyofanya kwa Mangu, Siro na Mzee aliyekuwa mkuu wa Jeshi la magereza.