Swali la Siku: Jambo gani uliloambiwa utotoni unalohisi ni Upotoshaji ungehitaji kujua Uhalisia wake?

Swali la Siku: Jambo gani uliloambiwa utotoni unalohisi ni Upotoshaji ungehitaji kujua Uhalisia wake?

mimi nataka kujua kama ni kweli jogoo akizeeka sana anataga kiyai kidogo JamiiCheck

niliambiwa nikiwa mdogo mpaka leo naamini amini

na pia je mbwa kichaa akikung'ata unakuwa kichaa na wewe?
 
Nilipokuwa form one tuliambiwa mtu yeyote akitaka kuadhibiwa na mwalimu asikatae adhabu hata kama hana kosa, baada ya kuadhibiwa ndipo ajitetea kuwa hana kosa. Hii nilikuja kugundua kuwa ni uwongo baada ya mwanafunzi mmoja kupigwa hadi akapoteza maisha kwani maiti haikuweza kujitetea.

Nilibadili mindset.
 
Pia nilishaambiwa kuwa mshamba anatakiwa achekwe na kubezwa lakini baada ya kukua nikagundua kuwa mshamba_hachekwi bali anaonewa huruma na kusaidiwa.
Halafu niliambiwa ukifa mke na watoto wako hawatapata tabu kwani atarithiwa na kaka au mdogo wako au kuolewa kwingine lakini kwa wivu nilionao naomba Nikifa MkeWangu Asiolewe.
BRAZA CHOGO sijui we unalitazamaje hili la mkeo kuolewa.
 
Niliambiwa mwanamke sio ndg Yako=>Kweli
Niliambiwa na mama "Mwanangu kile kidogo ulicho nacho (Cha kwako) Cha faa sana kuliko kingi Cha ndugu Yako kisichokusaidia kitu!!

Mama alinipa mfano ......fikiria jirani Yako (ndg) ana maisha mazuri hata kama ana Mali haziwezi kukusaodia kitu lkn kama wewe una kitu chako Cha kwako hata kama ni kidogo kitakufaa sana.

Haya maneno na mengine mengi aliniambia baada ya Mimi kwenda kuishi Kwa dada(shemeji) yangu na kugoma kurudi kijiji. Yaliniumiza sana maneno hayo. Hata Leo hii siwezi shobokea maisha ya mtu mwingine yasiyo nisaidia kitu.

Uongo niliowahi ambiwa

Babu aliniambia ukila nyama kubwa utaangukia mlangoni

Kuna baadhi ya wanyama kwenye ukoo wetu tulizuiliwa kuwala mfano paa, digidigi nk eti ukila unababuka ngozi nk.
 
Pia nilishaambiwa kuwa mshamba anatakiwa achekwe na kubezwa lakini baada ya kukua nikagundua kuwa mshamba_hachekwi bali anaonewa huruma na kusaidiwa.
Halafu niliambiwa ukifa mke na watoto wako hawatapata tabu kwani atarithiwa na kaka au mdogo wako au kuolewa kwingine lakini kwa wivu nilionao naomba Nikifa MkeWangu Asiolewe.
BRAZA CHOGO sijui we unalitazamaje hili la mkeo kuolewa.
Mkuu hufai😹
 
Radi ( Ladu ) Lina mapembe na linapigana na Kondoo kweli kweli.

Linaunguza mti eti ila linashindwa Kichwa Cha Kondoo.
 
Mjamzito akila mayai atazaa mtoto asie na nywele.
 
1. Kwamba.... Elimu ni ufunguo wa maisha.
Sasa swali langu ni kwamba vipi wale ambao hawaja ipata elimu, huo ufunguo ndio wanakua wameukosa??
Je wale wanaipata elimu, wanauhakika wa kufanikiwa kwasababu tayari wanamiliki ufunguo wa maisha??
Hii debate ilikuwa haipiti wiki mbili tunarudia
 
Niliambiwa ukiona mtu amekonda/ mwembamba mabega yamepanda juu, basi ana HIV.
Ukijiangalia kwenye kioo usiku, utaota ndoto za kutisha.
Wasukuma ni wachawi.
Ukiona mahali pameandikwa Made in China/Kenya jua ni nyuma ya mlima tu hapo.
 
Back
Top Bottom