Swali la sikukuu: Ununuzi wa magari ya kifahari kwenye halmashauri kosa ni la Wakurugenzi au Madiwani wa CCM?

Wakurugenzi na madiwani wote ni zao la uchaguzi feki ulioharibiwa na serikali ya CCM.

Hata wewe baptist ni sehemu ya huo uozo sababu ulishangilia ule ushindi hewa.
Ahadi za ushindi wa kishindo. Wametumika kama kondom wameshatupwa. Haiwezekani waraka wa aina ya magari wanayostahiri wakati waraka upo mezani. Wasiwadanganye watanzania. Watanzania siyo wajinga. Kama kweli ni kosa Waziri Mkuu ajiuzuru kwa kuwa ofisi yake imeshiriki katika kuvunja kanuni na taratibu za serikali huku yeye akiwa mtendaji Mkuu wa serikali. Ajiuzuru tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Madiwani wa ccm wanadumisha ileile jadi yao ya bungeni ya; ndiooooooooooooooooooooooooooo.
hata bila kusoma kwao sio tatizo bali kauli mbiu yao ni ndiooooooooooooooooooooooo😀
 
.
 
Hawa wakurugenzi mbona wanakuwa na matumizi makubwa hivi? VP wakuu wa mikoa na wilaya nao wananunua magari ya thamani kubwa hivi?
 
Kaka johnthebaptist wewe ndio wa kukipiga chama mkuki leo kweli
Just ungesema madiwani sio Lazima useme madiwani wa ccm
 
Hayo magari mbona hata huko CCM mmeyanunua? CCM ukoo wa panya baba mwizi,mama mwizi na watoto waizi.
Wamewashupalia Wakurugenzi wa Halmashauri,wameshasahau kazi kubwa waliyofanya Uchaguzi wa SM na huu wa juzi.Ukizoea kula nyama ya binadamu...
MaDED wanatumika kuwaondoa Wananchi kwenye kuhoji kilichotokea October 27&28.Uporaji wa kura na mauaji ya Demokrasia pamoja na issue ya wabunge wa Viti maalum CDM visijadiliwe.
Uhuni unaofanywa nchi hii ni aibu tupu.Vyombo vya kusimamia sheria/usalama wa RAIA na Mali zao ndiyo wanatumika kuivuruga misingi ya Taifa kwa kasi kubwa.
 
kosa la CCM nzima, lazima iwajibike kwa ubadhilifu huu na mwingine mwingi tu unaeondelea kuteketeza hela za walipa kodi maskini
 
Naona umeanza kupata akili kweli Yesu kazaliwa haleluya, kosa ni la PM ambaye anatoa vibali vya kununua hayo mashangingi
 
MaDED washughulikiwe haswa maana walisaidia sn wizi wa kura za wananchi
 
Ni Rais pekee ambaye ameshindwa kutoa mwongozo, kama Mkuu wa Serikali na Nchi, ni magari aina gani Mawaziri, Makatibu Wakuu, MaRC, MaDC/MaDED watatumia katika kazi zao za kila siku. Hawa wote na wengine ni Wafanyakazi wa Serikali na magari pia ni ya Serikali kwa hiyo yalitakiwa yanunuliwe na Serikali badala ya kila kiongozi anunue analotaka. Baada ya Uhuru, Mawaziri wote walipewa magari aina ya Humber, watumishi wengine wote walipewa Land Rover tofauti ya hadhi ikawa ni Station Wagon kwa Wakubwa, Pick-ups kwa wadogo na pikipiki na Baiskeli kwa wadogo zaidi. Magari ya kifahari wanayotumia Wafanyakazi wa Serikali yana injini kubwa bure kwa hiyo zinatumia mafuta mengi bure, pili ni 4WD ambayo haitumiki kabisa na zina viyoyozi, nyumba zao zina viyoyozi hata ofisi zao, vyote vikigharimiwa na Serikali inayobana matumizi. Ng'ombe ukimpa uhuru atakula mahindi, mchele, kahawa hata unga wa chakula cha watoto!
 
Si suala la kuuliza, BINADAMU yeyote anaweza kuwa RAISI wa Tanzania.
Ni nchi pekee duniani isiyo angalia uwezo na kipaji ili kuwa mkuu wa nchi
 
Mkurugenzi ni bwege zaidi. Kwa nafasi hiyo na elimu hiyo hastahili kuwa mtu anayelilia gari la aina hiyo. Hiyo ni hatua ya kitoto kabisa! Tulio na uelewa hatuhitaji tena kujionesha. Nafasi hiyo inamtosha kabisa kufahamika ubora wake na siyo kwa gari lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…