MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Tokea mwaka 1944, baada ya kutengeneza mfumo wa Bretton-Woods hakuna taifa ambalo limewahi kuwa na uchumi mkubwa kama Marekani. Kufika mwaka 1945, Marekani ilikuwa inamiliki nusu nzima ya uchumi wa dunia. Fedha ya Marekani ikishikiliwa na dhahabu (Gold-Backed) ilikuwa ndiyo inatumiwa kwa kiwango kikubwa kwenye biashara zote za kimataifa.
Mwaka 1957, baada ya Raisi Gamal Abdel Nasser wa Misri kutaifisha mfereji wa Suez, Uingereza, Ufaransa na Israel waliunda mkakati wa kuvamia Misri ili kumtoa Nasser. Mkakati huu ulikufa kibudu baada ya Raisi wa Marekani General Dwight Eisenhower kuwachimba mkwara mzito Waingereza kwamba wangeacha kununua hati-fungani (Sovereign Bonds) za Uingereza na nyingine wangeziuza, jambo ambalo lingeangusha uchumi wa Uingereza.
Kiufupi, baada ya hili kutokea Raisi wa Ufaransa General Charles De Gaulle alilalamika na kusema kwamba "The dollar gives America an exorbitant privilege in international financial system". Akimaanisha kwamba dola inampa Marekani nguvu iliyomithirika kwenye uchumi wa dunia dhidi ya mataifa mengine. Kiufupi Marekani akikutoa kwenye mfumo wake wa kifedha, lazima uumie.
Wataalamu wanatumia vipimo (Metrics) kama GDP na PPP kupima uchumi wa dunia. Ukitumia kipimo cha GDP, nadhani Marekani ndiyo taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani likifuatiwa na Uchina. Uchumi wa Marekani peke yake ni asilimia 24% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Kiufupi ni kwamba, all financial roads lead to America.
Marekani hayuko peke yake, anashirikiana na wenzake wa kule Ulaya (European Union) na wenzake wa chama cha mabwanyenye wa dunia almaarufu kama G7. Ukichanganya uchumi wa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia, Canada na Japan, ambao ndiyo nchi tajiri zaidi duniani unapata asilimia 30.7% ya uchumi wa dunia (Global GDP).
Kiuhalisia, haya mataifa saba ndiyo yanayoendesha uchumi wa dunia kupitia mifumo waliyoitengeneza baada ya mwaka 1945. Viwanda vikubwa duniani ni vyao, masoko makubwa ya hisa ni yao, mabenki makubwa duniani ni yao, wao ndiyo wanaongoza katika kuzikopesha fedha nchi nyingine na wao ndiyo wanaongoza kwa kuuza huduma zaidi hapa duniani.
Maswali yangu ya kiuchumi ni haya yafuatayo:
Mosi, kwanini Urusi ambayo ni asilimia 4% tu ya uchumi wa dunia (Share in Global GDP) bado haijaanguka baada ya mataifa makubwa yanayomilikia asilimia 30.7% ya uchumiwa dunia kuwawekea vikwazo vikali ?
Pili, kwanini makampuni ya Urusi ya nishati ndiyo yameongoza duniani kwa kuuza zaidi nishati, ilhali yamewekewa vikwazi baada vikali ? Takwimu zilizotolewa na Marekani yenyewe zinasema kiujumla mashirika ya nishati ya Urusi yameuza zaidi na kupata faida kipindi hiki cha vita na vikwazo kuliko kipindi kingine chochote. Tatizo liko wapi hapa ?
Tatu, Je, tutegemee kwamba kuna siku hivi vikwazo vitafanya kazi na vitauangusha uchumi wa Urusi kama ambavyo Raisi Biden alisema mwaka 2022 kabla ya uvamizi kuanza ? Alisema kwamba uchumi wa Urusi ungeanguka ndani ya wiki chache tu, sasa ni mwaka na zaidi. Mataifa ya Magharibi yamefanikiwa au tuendelee kusubiri ?