Kwahiyo unataka kusema kwamba G7 wangeiwekea vikwazo Urusi kwenye mashine, basi uchumi wa Urusi ungeanguka na wao wenyewe wasingekutwa na madhara yoyote yale, si ndiyo ?
Hakuna niliposema hawatoumia ila nani ataumia zaidi.
Kwani Boeing na Airbus zilipoweka sanctions kwa Russia nani anaumia zaidi, Russia ina zaidi ya Boeing 70, umeona Boeing inapata hasara kisa imefunga biashara pale Russia? Je umefuatilia hali ilivyo kwenye Russian airlinesz service wanazitafuta hadi Iran. Au DGM Mori ya Japan & Germany ikigoma kuuza CNC lathes kwa Kalashnikov Concern nani atafanya cuttings za silaha na zile precision ngumu ambazo Warusi hawana.
Au vipi Thales ya Ufaransa ilipositisha kuuza imaging devices kwa Uralvagonzavod kutengenezea sensors za T-90 main battle tanks nani aliumia zaidi. Huyu kakosa hela na hajatetereka kwa lolote, huyu kakosa thermal imaging katumia za makampuni yake hafifu.
Umeona McDonald's inafirisika baada ya kuondoka Russia na mali zake kutaifishwa na serikali? Hata shares zao umeona zimeshuka?
Siemens ikiamua kutofanya service ya gas turbines za Gazprom, pipeline zikaharibika na zilivyo very expensive nani ataumia zaidi. Urusi ikisitisha gesi kwa Ulaya wanaingia gharama kubwa kutafuta mbadala kwingine, Urusi inabaki na mabomba yake ya gesi na miundombinu inakufa na hela ya mauzo wanakosa.
Ukiwa na biashara ya kuuza unga mjini, nina mashine za kusaga nauza mjini na nikagoma kukuuzia wewe tu na ndio mimi the best kwenye quality na serviceability nani ataumia zaidi kati yetu?
Hii hoja sijaielewa hata kidogo, labda unifafanulie kwa zaidi. Kwamba unataka kusema, Urusi ya kisovieti ilikuwa lilikuwa taifa imara kwasababu ya teknolojia ya Marekani iliyotolewa kule Volgograd? Hivi kuna nchi hapa duniani ambayo imetumia teknolojia yake peke yake kukua ?
Nimekupa mfano kwamba Marekani ilichangia ukuaji wa kiuchumi wa Urusi. Tena sio hapo tu, Marekani kwenye WW2 ilitoa zaidi ya ndege 10,000 vifaru maelfu na trucks zaidi ya elfu mia tatu. That time Soviet Union hawana uwezo kabisa wa kutengeneza heavy trucks na nchi yao ikija winter na udongo wao ule inajaa matope. Hapohapo wana vifaru kina T-34 vina uzito tani kadhaa, namna ya kuvipeleka frontline hawana ndipo usiyemtaka akaja na hizo trucks.
Kazi za kina Ford, tena nimekumbuka Ford mwenyewe kahusika kuiendeleza Soviet Union. Ford kahusika pakubwa kufanya establishment ya Soviet automobile industry, kiwanda alijenga mji wa Gorky. Marekani hakimbiwi!
Ila nachokishangaa kwenu ni kushindwa kufahamu kwamba, teknolojia zote muhimu ambazo Marekani anazitumia karne ya ishirini na moja siyo zake bali za Ujerumani. Wanasayansi 1500 wa Ujerumani waliopelekwa Marekani na Bwana Allen Dulles kupitia Operation Paperclip, ndiyo walilipa Marekani teknolojia kama Fission-Technology (Atomic), Sonar, Rocket-Science, Genetic-Engineering, Satellite Engineering, n.k
Nani kaizuia Urusi kupeleka wanasayansi kwake?
Kwani unajifanya hujui kwamba Marekani haina watu maalum, nchi huru ile hata wewe unatamani kwenda.
Ni kwamba hujui kwamba Marekani ina mazingira mazuri ya wanasayansi? Elon Musk angebaki South Africa usikute angekuwa anauza simu. Nawewe leta wageni waliohamia Urusi wakafanikiwa, au huwa wanaenda walevi tu kule.
Na kama Marekani imeendelea sababu ya wanasayansi 1500 wa Ujerumani, Ujerumani ina wanasayansi laki ngapi waliobaki kipindi kile mpaka sasa mbona haijaizidi Marekani? Vyuo vilevile vilivyowatoa si bado vipo, jamii, asili ya kizazi, nchi. Kila kitu ni kilekile, waizidi Marekani basi ambayo hao 1500 walishafariki kabla hajazaliwa.
Na kwanini utaje Wajerumani si ungeanza na Warusi. Baba yake Sergei Blin alikuwa lecturer chuo kimoja Urusi, maisha ya kipuuzi akaondoka nchini kwao akaenda Marekani na mke wake kufundisha chuo na kujiendeleza. Mtoto Sergei Blin akajifunza kwenye shule za Kimarekani akasoma chuo na kukutana na Larry Page, mambo mengi yakatokea na sasa tuna Google na Alphabet Inc. Blin angekuwa Urusi angeambulia njaa, sasa ni bilionea hakuna Mrusi anamzidi hela.
Leonardo DiCaprio ana asili ya Kirusi upande wa bibi yake, nani mwigizaji Mrusi wa Urusi anamzidi?
Steven Seagal ni asili ya Urusi anafanyia uigizaji Marekani, nani mwigizaji wa Urusi anamzidi? Pamoja na Seagal kuwa wa kawaida sana pale Hollywood na kutoipenda Marekani ila hawezi acha maisha pale eti aende sijui uko Vladivostok vichochoroni mwa dunia uko ukitoa movie unatazama na jirani zako.
Au Sikorsky asingeamia Marekani helicopter nzuri duniani tungepataje, maana kule Urusi alikosa funding sababu za kishamba za ujamaa.
Sasa turudi kwenye uchumi. Tutumia mawazo ya baba wa uchumi wa kibeberu, Bwana Adam Smith. Hivi kuna taifa ambalo lina ABSOLUTE ADVANTAGE kwenye kila kitu hapa duniani ? Kwamba leo hii Marekani anaweza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi mataifa makubwa bila yeye kupata hasara ? Hebu tueleweshane
Unaandika mambo mengi sana. Hapa napo nayaweka mawazo yako katika kurunzi ya kiuchumi. Hivi unahisi taifa la Marekani lina Absolute-Advantage in every sphere of the
economy?
Marekani haina absolute advantage kwenye kila kitu ndio maana inaishi vizuri na washirika wake. Urusi mshirika wake mkuu ni China, miaka ya 1960s waligombania mipaka.
Na kwanini Marekani iwekee vikwazo washirika, kwanini China iiwekee vikwazo Urusi.
Hii mifano yako inanishangaza kidogo, nadhani hujafanya utafiti wa kutosha kwenye historia ya uchumi wa dunia.
Wasomi wakubwa duniani kama Professor Joseph Nye wanasema kwamba Ujerumani lilikuwa ndiyo taifa tajiri kwenye uzalishaji (World's Largest Manufacturer) kuliko hata Uingereza mnamo mwaka 1900. Kipindi hiki Marekani alikuwa ni taifa tajiri zaidi duniani katika ulinganisho wa manunuzi (Purchasing Power Parity).
Tunarudi palepale, Urusi hayupo kwenye kuongoza lolote kiuchumi. Taja hao Ujerumani sijui Japan ila Urusi hayupo, atakuja kwenye list ya nchi ambazo walizaliwa wakajikuta wanakalia gesi na mafuta ndio hapo utawakuta Urusi, Nigeria, Angola, Venezuela na wanachama wa OPEC.
Kingine ambacho kinanishangaza ni kwamba unasahau kwamba kabla ya vita ya pili ya dunia, taifa la Japan lilikuwa ni moja kati ya mataifa tajiri duniani. Hizi hoja za kusema kwamba Marekani ndiyo aliwashawishi wajerumani na wajapan wastaarabike ndiyo wakawa matajiri umezitoa wapi ?
Unajua madhara iliyopata Ujerumani baada ya vita? Unajua allied concentrated bombing runs za Ruhr industrial city, Dresden na miji yote ya viwanda ilivyofanya uharibifu kwa kutumia bombers kama B-29, Lancaster, Mosquito. Unajua jinsi Red Army ilivyokuwa inatumia artillery kubomoa miji yote ililosimama njiani kuelekea Berlin?
Sasa baada ya vita kuisha Ujerumani ilikuwa imechakaa vibaya. Na sio Ujerumani pekee, Marekani ilitoa Marshall Plan kwa nchi za Ulaya.
Japan yenyewe Marekani alikaa miaka kadhaa akisaidia kujenga nchi, chini ya General Douglas MacArthur. Kutoka hapo mpaka 1950s Korean wars bado Marekani ilikuwepo Japan haijamaliza mission.
Aidha unayaangalia mambo kisiasa, au hujasoma uchumi. Kitaalamu, Marekani lilikuwa taifa tajiri zaidi duniani mwaka 1872 (Gilded Age), lakini siyo katika kipimo cha Gross Domestic Product (GDP). Ukitumia kipimo (Metric) cha GDP, kutoka mwaka 1872 Marekani alikuwa na uchumi mdogo mno kulinganisha na mataifa kama Ufalme wa Uingereza na Ufalme wa Ujerumani.
Kipimo kilichotumika kusema Marekani ndiyo tajiri ni kile cha manunuzi, Purchasing Power Parity (PPP). Nakubaliana na baadhi ya wachumi kwamba GDP ni kipimo sahihi, lakini ukizingatia vipimo vingine kama GNP na PPP utafahamu kwamba kwanini mataifa yenye GDP ndogo kuliko yale ya G7 bado yanafanya vizuri.
Sasa mtaalamu, hebu tufahamishane. Kwamba Marekani na chama chake cha G7 leo hii wanaweza kupambana vita ya kiuchumi na mataifa kama Urusi, OPEC au Uchina bila wao kukumbwa na madhara makubwa kiuchumi ?
Kutosoma kwangu uchumi hakuifanyi Urusi iwe giant kiuchumi, au kusoma kwako uchumi hakuifanyi Urusi kuwa angalau ya tano kiuchumi duniani. Facts ni zilezile, hayo yote uliyotaja Gilded Age, PPP, GDP, G7 kote Russia anabaki palepale kwamba hana maajabu kiuchumi. Na hapo sanctions zimeanza 2014 kuja sasa