HAWAJAKOSEA
1. Hakuna imaginary wealth, kumbuka Hela inapima thamani ya bidhaa zilizopo na sio kwamba pesa zenyewe Zina thamani zikisimama zenyewe. Mfano South Sudan pesa yake ilikua na thamani almost 30 times kuliko yetu ila kama hakuna uzalishaji thamani ikaporomoka kwa spidi ya juu. So hata hizo currency printing na stock markets ziko backed na actual value ya kampuni ambazo zinauza hisa.
Nakupata mkuu, lakini naomba niulize tu. Fiat Currency kama dola ya Marekani inapima thamani gani ya ya bidhaa zilizopo ilhali leo hii inaweza ikachapishwa na kushushwa thamani na benki kuu ya Marekani wanapotaka wao kutimiza malengo fulani ya kiuchumi au kisiasa (Currency Debasement), mfano kuhimili deni la taifa (Avoiding default) na kuchangia bejeti hafifu (To cover deficit), ???
Hivi ndugu yangu, nchi yenye Budget Deficit na Large Debt surpasing the 70% GDP threshold, fedha zake na masoko ya mitaji yanaweza kweli kuakisi uhalisia wa uchumi wa nchi hiyo, ???
2. Dunia imebadilika tunahama kutoka kuwa Labor intensive tumekua capital intensive so nchi zenye mitaji ndio tajiri kuliko zenye rasilimali watu au rasilimali ghafi. Mfano bandari inaweza kuwa operated na mtu mmoja akiwa nyuma ya computer so hapo you only need capital. Same to kuzalisha mafuta au gesi watu Sasa Wana renewable energy kama umeme wa upepo au joto ardhi tofauti na zamani kwamba kama hauna mabwawa au mafuta huwezi zalisha umeme n.k. so rasilimali haziwezi kuwa kipimo Cha uchumi imara however uwepo wa mitaji, ubunifu, teknolojia vinaweza chochea uchumi zaidi na kuongeza thamani hata kama nchi Haina rasilimali husika.
Mitaji, Ubunifu na Teknolojia haviwezi kulifanya taifa likawa tajiri bila kuwa na bidhaa muhimu kama dhahabu, nishati na chakula. Hizi ndizo bidhaa muhimu zinazoufanya uchumi wa nchi uhimili mfumuko wa bei usio na mpangilio. Masoko ya huduma, mitaji na bidhaa nyingine ni muhimu, lakini hayawezi kuzudi umuhimu wa nishati, chakula na dhahabu kwenye uchumi wa nchi.
Kiufupi, hata Marekani na Uingereza waliweza kuwa mataifa tajiri zaidi duniani kwasababu yalikuwa yanamiliki rasilimali nyingi zaidi duniani kama nishati, chakula na dhahabu kuliko mataifa mengine. Uingereza baada ya kupoteza makoloni yake mitaji, teknolojia na ubunifu, wake haujamsaidia sana kwasababu hana rasilimali muhimu kama ilivyokuwa hapo mwanzo. Huu ndiyo ukweli mchungu ambao wengi hampendi kuusikia.
3. Tangible assets say Tanzania tuna dhahabu au mafuta. Ni muhimu tufahamu commodity markets are highly volatile, yaani price shocks kidogo tu uchumi unaporomoka kama wa Venezuela. So ukitegemea extractive industries ni hatari maana uchumi unapaa na kushuka based on soko la mazao duniani. However money stores value kuliko mazao maana hata ikishuka thamani Bado unaweza stabilize kwa macro economic policies kama Open Market operations, currency pegging, denomination, interest rates, Broad money reforms n.k
Supply Chain Shock ni tatizo zaidi kwa nchi ambazo zinategemea uchumi wa masoko ya mitaji peke yake bila kuwa na rasilimali (Tangible Assets) kama dhahabu, chakula na nishati. Mwaka jana mchumi Prof Joseph Stiglitz alisema kauli ambayo ilikera wengi nchini Marekani. Kwamba kupandisha riba juu au kutumia mbinu mbalimbali za kiuchumi bila kuingiza bidhaa muhimu hakuwezi saidia uchumi wa nchi kama inavyotarajiwa.
Lakini unasahau kwamba, riba zikipandishwa juu, thamani za hati-fungani (Bonds) huwa zinashuka jambo ambalo hupelekea taasisi mbalimbali za kifedha kushindwa kutoa huduma ipasavyo. Mfano halisi, wachumi wa Marekani walikuja na mbinu ha kupunguza riba hadi kufika 0.5%, hivyo kufanya watu wakope sana kwasababu mikopo ni bei nafuu.
Watu wakichukua mikopo kwa gharama ndogo hawaendi kujenge nyumba, ila wanazichukua na kwenda kuwekeza kwenye masoko ya mitaji tena. Hivyo mara nyingi hawa watu wanatajirika kupitia masoko ya mitaji tu, bila kuwa na vitu (Tangible Assets). Aidha sasa, unapotokea mkwamo fulani kwenye uchumi na kupelekea mfumuko wa bei kuwa mkubwa, benki kuu inapopandisha riba juu basi fahamu kabisa kuna watu wanaumia.
Marekani imepandisha riba hadi kufika 6%, jambo ambalo siyo la kawaida. Madhara ya hizi sera za kiuchumi zimeyakuta mabenki ambayo yamewekeza sana kwenye soko la hati-fungani. Riba zikiwa juu, thamani ya hati fungani hushuka chini hivyo mabenki hayawezi kupata fedha za kuweza kuwapa wateja wake. Mwishowe yanaanguka.
Mkuu, kubwa zaidi ni kwamba riba zikipanda juu, akiba za watu (Savings) hushuka thamani na kufanya maisha ya watu kuwa magumu. Majanga yote haya yanaweza kusababishwa na jambo dogo tu kama SPECULATION OF PRICES hasahasa kwenye masoko ya teknolojia (Start-Ups) au ardhi (Real-Estate).
Ndiyo maana wachumi wengi hushauri kwamba watu wawekeze zaidi kwenye vito vya thamani (Gold Bars, Bullions and Coins) kuliko kuweka hela kule benki ambako mtu mmoja anaweza kuamua tu kuvuruga uchumi, hela zikashuka thamani ukaishia kuwa masikini. Hili lipo hata kwenye mataifa makubwa.
Umesema Money Stores Value kuliko rasilimali kama chakula. lla ukweli wa hii kauli kwenye vitendo ni upi ? Kwamba, fedha inaweza kukaa na thamani kupita rasilimali kama dhahabu, hebu tuelezane mwamba.
Mwisho kabisa, nimesoma kidogo kuhusu historia ya mitikisiko mikubwa ya uchumi duniani. Nikiri na kusema kwamba Open Markets Operations, Currency Pegging, Broad Money Reforms na Interest Rates siyo njia pekee na sahihi za kudhibiti uchumi. Kuna njia zimetumiwa na mataifa kudhibiti uchumi moja kwa moja kwa kushughulika na bidhaa na matokeo yalikuwa ni chanya. Hii ilitumika Marekani mwaka 1971 (The Nixon Shock) na mfumuko wa bei uliisha ndani ya mwezi mmoja tu.
Mbinu hii wachumi wengi duniani haswa wale waliberali wanaichukia, lakini wachumi wakihafidhina kama Prof Richard Wolff wanasema ndiyo sahihi zaidi kuliko kutumia Fiscal & Monetary Policies ambazo tumezoea kuzitumia.
So hoja yangu hapa ni kwamba, uchumi wa makaratasi (hard currency, exchange rates, interest rates, bonds, stock markets) una reflect uhalisia wa uchumi kuliko kuwa na bidhaa tu za kushikika.
Wewe kama mchumi ulitakiwa utoe takwimu kuthibitisha hii kauli. Unachokisema mimi sikubaliani nacho kwasababu za kiuchumi kabisa. Hebu nikupe mfano halisi tu. Marekani anatumia FIAT CURRENCY (Currency not pegged to the price of Gold).
Tukisema mbinu kama Currency Pegging inafanya kazi nadhani tutakuwa waongo kabisa. BENKI KUU YA MAREKANI inasema kwamba serikali ya Marekani inamiliki dhahabu nyingi zaidi duniani kule Fort-Knox kiasi cha tani 1833, kiasi ambacho hata uunanishe dhahabu ya Ujerumani, Urusi na Ufarasa hawawezi kukifikia.
Kasheshe la kiuchumi linakuja hapa: Mpaka kufika mwezi February 2023, takwimu zinasema MONEY-BASE (Phyasical Money in Circulation) ya Marekani ni Dola Trilioni 5.3 ilhali dhahabu ambayo inategemewa ishikilie dola ya Kimarekani thamani yake ni milioni 261 OZ (Troy Ounce).
Sasa tukifanya mahesabu rahisi ya Currency Pegging (5.3 Trillion / 261 Million Troy Ounce = $ 20,306 Per Ounce). Hapo inamaanisha kwamba OZ moja inanunuliwa kwa dola za kimarekani 20,306. Zamani Ounce moja ya dhahabu iliuzwa dola za kimarekani 2000 tu.
Hapa inamaanisha kwamba kama ulikuwa na fedha za kimarekani dola 400,000 ili kununua nyumba yenye hiyo thamani halafu ukafanya Currency Pegging inakula kwako. Kumbuka dola 400,000 ni sawa na Ounce 200 za dhahabu. Ukifanya Currency Pegging through Gold, kwa kanuni ya hapo juu basi utakuta dhahabu imepanda bei huku dola ikishuka thamani.
Hizo Ounce 200 za dhahabu zitapanda bei na kutoka dola 400,000 hadi dola 4,000,000 za kimarekani. Kumbuka katika yake mahesabu dola itanunua dhahabu kwa gharama ya $ 20,306 kwa Ounce. Sasa Money Base (MO) ni trillioni 5.3, hilo la kusema kwamba utajiri wa makaratasi unaakisi uhalisia wa uchumi linatoka wapi ndugu yangu, ???
Hela zimekuwa nyingi kwenye mzunguko kwasababu Marekani anachapisha fedha hovyo ili kuhimili deni lake kubwa ambalo haliwezi kulipika, lakini pia kwasababu Marekani ana BUDGET-DEFICIT. Hivyo anatumia nguvu za fedha yake kuzifanya nchi za dunia nzima ziupe ruzuku uchumi wa Marekani (The Entire world is subsidizing American Economy through the dollar and capital markets)
Huoni hapa kuna tatizo, kama nakosea hebu nipe mahesabu sahihi! Nasubiri mkuu...