Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Ha ha haa.
Mie Sina la kusema .
Ila Putin aliulizwa kwa Nini mlikimbia Kiev akajibu hatukukimbia Bali tuliondoka kuheshimu makubaliano ya amani yaliyokua yakisimamamiwa na Ututuki.
Putin akamuuliza mwandishi au unataka turudi?

Basi majibu yote yalikua hapo.

Hata hivyo hivi kweli mtu msomi na mwenye akili timamu unaweza kusema Ukraine anashinda vita?
Au Urusi anashindwa vita?
 
Umesema Money Stores Value kuliko rasilimali kama chakula. lla ukweli wa hii kauli kwenye vitendo ni upi ? Kwamba, fedha inaweza kukaa na thamani kupita rasilimali kama dhahabu, hebu tuelezane mwamba.
Nilivyoisoma hii sentensi kule kwake nikarudia tena, na tena halafu nikawazaa🤔

Ivi mwamba yupo siriazi. Pesa ni kitu tumekubaliana tu kiwakilishe thamani ilihali chenyewe kama chenyewe hakina hiyo thamani. Sasa kitu cha makubaliano ndo kiwe madhubuti kuliko vitu vyenyewe😳. Akat tunaweza kuamua kutokubaliana, kutoiamini na hapohapo inageuka nothing.

Kidogo niseme wachumi nao wanafundishwa ujinga. Ila afadhali we mchumi mwenzake umelipoint out. Ngoja ntasoma majibu yake.

Asante kwa mada na majibu, tunajifunza sana page by page, comment by comment. Inafariji hata tu kuona kuna watu wanaofikiria sense. Big up👊
 
Boy,


Kwa nin west wanafata kibubusa sera za us ambazo zinapelekea chumi zao kutetereka kinomanoma
 
Kweli kabisa Mkuu Mwana Taaluma.
Ni tofauti kubwa sana kujua mambo Kwa ukamulifu na kujua mambo Kwa ujanjaujanja.
Hii ndio inawakumba Baadhi ya Pro USA.anaulizwa swali anatoa maelezo meeeengi nje ya mada ili aonekane anajua mambo.
Sasa bahati sio Yao tena, Wanakula spana za hatari. Kila sekta wanakutana na kichwa kimoja hatari sana kina watuliza.


Yaani hii special operation wajamaa walijipanga haswa.
 
Contradictory!! Umesema Dollar ya Marekani ilichapishwa nyingi kuliko mahitaji Cha ajabu unasema circulation volume imepungua?

If at all it was surplus to requirements how on earth is the volume staggering? In fact low volume or velocity of currency in circulation requires more pumping of dollars in the economy to stimulate multiplier effects.

Can you please clarify your contradicting statements?
 
Nikawauliza hivi ni sahihi kusema kwamba taifa ni dhaifu kiuchumi kwa kuzingatia tu, uchumi wa kifedha, Finance Economy. Bila kuzingatia uwezo wa nchi kwenye uchumi wa bidhaa, Commodity Economy, ???
Tulikujibu tunapima ubora wa kiuchumi kupitia GDP or GNP, GNI, HDI n.k ambazo Zina encompass both commodity, finance and service sectors.

Sielewi kwanini una assumption kwamba capital markets ni uchumi hewa? AZAM inauza real commodities ila ikitaka wawekezaji inaenda pale DAE ku trade meaning watu wananunua hisa za Real products Sasa kivipi Tena inakua uchumi hewa?
Mfano kampuni ya Apple pekee ni almost sawa na GDP ya Afrika nzima Sasa kampuni kama hiyo ikiwa Ina trade hisa zake kwenye stock markets kivipi inakua "finance economy" ilihali inauza actual commodities kama simu, tablets, technology, cloud storage n.k??

Why do you assume Finance markets ni uchumi hewa ilihali kampuni Zinazouza hisa zinauza real products?
 
Sasa bahati sio Yao tena, Wanakula spana za hatari. Kila sekta wanakutana na kichwa kimoja hatari sana kina watuliza.


Yaani hii special operation wajamaa walijipanga haswa.
Ha ha haa.
Na Siri kubwa ya wapiga spana wa upande wa wajamaa katika mada hizi za haya yanayotokea ulimwenguni Leo hii ni "ukweli na haki TU".
Daima ukisema ukweli na ukitetea haki unakua unahoja za msingi.
Lakini zaidi ukiseam kweli unakua huru.hawa wanaopingana na ukweli huishi kwa hoja za kubabaisha babaiaha TU.
Na haya ndio yanayowapata pro NATO wengi humu.
 
Natamani Sana kwenye mada hii ya uchumi angeonzeka mchumi daraja lakwanza, mwenye data na fact kaka yangu Chige bila kumsahau kaka yangu Mchambuzi ili wengine tuendelee kujifunza namna uchumi na siasa za kimataifa zilivyo katka uhalisia. Pia nitoe shukran Kwa ndugu yangu zitto junior michango yake nimizuri Sana hongera Sana mkuu, bila kumsahau mchumi na mwanasheria wetu wa mjadala huu The Boy Wonder . Lakini pia natamani kuona michango ya Kichuguu ingawa nimtu ambae Huwa simkubali katika maoni yake katika siasa za ndani na zile za kimataifa..
 
Uchumi wa Urusi hauko Imara kama watu wengi wanavyoaminishwa. Putin alikuwa ametunza akiba kubwa sana akijiandaa na vikwazo baada ya vile vya mwa 2014. Kwa sasa hivi Urusi inatumia zaidi akiba hiyo kuliko income mpya. Pamoja na kwamba Urusi ina raslimali nyingi sana mabazo ndiyo uti wa mgongo wa nchi hiyo; hawana industrial goods zaidi ya silaha. Mauzo yao nchi za nje yamekuwa ni ya hasara sana. Kwa mfano mauzo ya mafuta India na China yanakwenda kwa bei ya karibu na bure; wanalazimika kuuza mafuta mengi sana kupata kiasi wanachohitaji. Faida yote inakwenda India na China kwani wao ndio wanaouza products za mafuta hayo nje kwa faida.
 
Mchumi na hili nalo nikuelekeze tena, ilhali ulitakuwa uwe unalifahamu, ???

Mosi, Marekani ilivyopandisha riba juu (Hiking Interest Rates) imepelekea doka kuimarika kitendo ambacho kimesababisha madhara makubwa kwa masoko yanayokuwa (Emerging Markets), kwasababu nchi nyingi zilipunguza thamani ya fedha zao hadi kwa asilimia 10% hadi 20% dhidi ya dola ya Marekani ili kuweza kumudu kuingiza (Imports) bidhaa kutoka soko la kimataifa.

Maana yake sasa, fedha za nchi zikipungua thamani, nchi inapata mfumuko wa bei, unaopelekea nchi kutumia fedha nyingi za kununua bidhaa muhimu kama mafuta na chakula. UNCTAD wametoa takwimu na zinaonyesha nchi zinazoendelea (Deloping Economies) zimekumbwa na DOUBLE-BURDEN (High Flood Prices Vs Strong Dollar).

Pili, Dollar Liquidity Swap Lines hazipo kwa kila nchi duniani, ndiyo maana uhaba wa dola umekuwa mkubwa. Siyo kila nchi inaweza kwenda kuchukua dola inavyotaka. Mpaka sasa, July 2023, mataifa ambayo yamepewa Unlimited Liquidity Swap Provisions na Marekani ni (Canada, United Kingdom, European Union, Japan and Switzerland).

Anafuatiwa (Australia, Brazil, South-Korea, Mexico, Singapore na Sweden) ambao Liquidity Swap Line yao ni dola za kimarekani Bilioni 60. Baada ya hapo kuna ( Dernmark, Norway, Newzeland) ambao Liquidity Swap Line yao ni dola za kimarekani Bilioni 30.

NB: Welcome to global economics my friend.....
 
Russia ana eneo kubwa Ila eneo kubwa la ardhi na bahari sio potential Kwa sababu ya Hali ya hewa.
 
Ndugu Zitto Jr, nadhani mimi na wewe tunapishana pahala padogo mno. Hebu twende sawa:

Mosi, napozungumzia Commodity Economy, nazungumzia uchumi ambao unaendeshwa na bidhaa ambazo zimeshikilia au zinatumika kwenye uzalishaji (Base Material). Kiuchumi, vitu kama dhahabu, nafaka, makaa ya mawe na madini mbalimbali, huitwa Commodities. Hizo Iphones, Gucci zinazouzwa, kiuchumi siyo (Commodities/Base Materials) bali huitwa, Finished Products. Wachumi huita otofati uliopo baina ya Base Material na Finished Products kama, Product Differentiation.

Ukienda kule World Trade Organisation (WTO) na kupitia baadhi ya mikataba yake, hasahasa ile ya miaka ya 90's haya yamewekwa wazi kabisa, kwamba ipi kisheria inachukuliwa kama Commodity na ipi inachukuliwa Finished Product. Ila pia hata kanuni za masoko yao ni tofauti. The Economics of Commodities is totally different from the economics of Finished Products. Ukisoma biashara ya kimataifa (International Trade and Commerce) na kupitia hii mikataba mikubwa kama GATT na GATS utaona utofauti wake ni mkubwa mno.

Pili, unaposema kwamba kampuni la Apple linatengeneza Iphone inauza Commodities, hii kibiashara na kisheria haiko sawa. An Iphone is not a commodity but a finished product. Wewe mchumi unatakiwa ulifahamu hili vizuri kabisa. Ukishafahamu hili, basi utatambua kwamba kibiashara, International Standards require that commities be produced in a uniform way worldwide. Masharti ambayo mkulima wa mchele wa Marekani amewekewa ili auze mchele kwenye soko la dunia, ndiyo hayohayo mkulima wa mchele wa Mbalali amewekewa ili auze mchele kwenye soko la dunia. Hili kitaalamu linaitwa, Fungibility.

Masharti ambayo, APPLE amewekewa ili atengeneze na auze bidhaa yake, ni tofauti kabisa na masharti ambayo XIAOMI amewekewa ili atengeneze na auze bidhaa yake. Finished Products zinatofautiana viwango kwasababu mbalimbali, muhimu ni kama gharama za tafiti (Research and Development), gharama za soko la ajira (The Cost of Labour Markets) na gharama za haki miliki (Intellectual Property Rights). Haya hufanya bei za Finished Products ziwe tofauti.

Huu mchakato mzima wa kutengeneza bidhaa, kuipa thamani na kuiuza kwenye soko la hisa, ndiyo Finance Economy yenyewe. Hata kwenye soko la huduma huwa hivihivi. Kinachotofautisha baina Finance Economy, ni kwamba wahusika wanaweza kucheza na bei za masoko kwa kufanya mambo kama: Overvaluation of Product and Speculation. Hili halipo kwenye Commodity Markets, because commodities are usually sold at their marginal cost of production.


Tatu, kwenye Commodity Markets mara nyingine huwepo na bei ya pamoja ya soko la kimataifa (Benchmark Price). Kubwa zaidi masoko yao ni maalumu, na hayauzi kwenye soko la hisa. Ukienda kwenye masoko ya makubwa ya vito vya thamani kama London Bullion Market Association (LBMA) utakuta bei ya dhahabu iko sawa na masoko mengine duniani kote. AU kama kibaba kimoja (Bushel) cha ngano ni senti 600, basi ndiyo huwa hivyo sehemu nyingi. AU kama mafuta (Brent Crude Price) ni dola 60% kwa pipa basi sehemu nyingi itakuwa hivyo.

Ila huku kwingine, Iphone huwa na bei yake na Xiaomi huwa na bei yake, japo zote mbili ni simu. Hili huathiri hadi thamani zao za hisa.

Nne, kiuchumi bei za Commodities haziwaathiri wanunuaji na wauzaji(Buyers and Sellers), bali hata watumiaji (Consumers). Bei ya mafuta au chakula zikipanda, tunaumia wote duniani. Hata wale wazalishaji wa simu kama APPLE huathirika. Ila bei za Iphone au Xiaomi zikipanda, nani anaathirika, ilhali hata Iphone sijawahi kumiliki mimi, ???

Tano, kisheria kampuni kama APPLE linavyouza hisa kuna au kampuni jingine ambalo limeamua kufanya Initial Public Offering (IPO) kuna mambo ambayo yanazingatiwa. Mengi kati ya hayo mambo hutokana na makadirio au makisio. Mfano, mabenki yanavyoyasaidia makampuni kupanga bei za hisa kuna kitu kiitwacho, HERD INSTINCT hutumika kama mbinu ya kupanga bei za hisa. Hapa kampuni hufanya makasio ya jinsi watu kama wewe Zitto Jr na wengine mnaopenda jina la APPLE mtashoboka na kukimbilia kununua hisa.

Mimi niliyesoma Intellectual Property & Entertainment navyosema Imaginary Wealth niko sahihi kabisa kisheria. Ukweli ni kwamba Intellectual Property Law protects and rewards expressed novel ideas that cannot be easily or uniformly quantified. Nikupe mfano rahisi tu, mradi wa ndege za Marekani wa F-35 Lock-Heed Martins umegharimu Marekani zaidi ya dola Trilioni 1 kwenye kufanya tafiti (Research & Development). Kasome mikataba kama TRIPS 1995, haya yako wazi kabisa mzee.

Ndege moja inaizwa hadi dola milioni 9, na Sheria (Intellectual Property Law) inamruhusu mtafiti kupanga bei yake kufidia gharama zake za tafiti. Hili jambo zima huathiri hata bei za hisa na thamani ya kampuni. Kisheria ni kwamba bidhaa (Finished Product), inapokuwa sokoni gharama yake hutokana haki ambazo ni za kifedha na zisizo za kifedha (Moral & Economic Rights of producers)

NB 1: Nashukuru umeuliza hili swali ili tuwekane sawa hasa kwenye suala zima la Finance Economy vs Commodity Economy, tukizingatia mambo muhimu kama International Trade and Commerce.

NB 2: Nakubaliana kabisa na wewe kwamba bidhaa (Products) lazima ziwe zina bei yake ambayo kiuchumi ni mihimu mno. Hili ni muhimu sana kiuchumi. Vipimo vya GDP, PPP, NG ni muhimu. Japo hivi vipimo mara nyingi huangalia uchumi peke yake kwa taswira ya jumla, bila kuangalia kwa ukaribu utendaji wa mambo kama biashara ya kimataifa (The Inner Workings of International Trade & Commerce) yanavyoathiri uchumi wa mataifa kiujumla hasa kwenye Finance Economy vs Commodity Economy.

NB 3: Niliweke na hili sawa ili usije ukazuka mjadala mwingine tena huko mbele, Not every natural resource is a commodity.

 
Sasa kumbe ulitaka mjadala ujibiwe na wanauchumi waliosomea. Si ungeweka dokezo tangu mwanzo badala ya kuchoshana.
Na kilichofanya uulize maswali na unajua sio mchumi niliyesomea ni nini, mpaka pale nilipotaka unijibu ndio ukajua mimi sio mchumi
 
Sasa kumbe ulitaka mjadala ujibiwe na wanauchumi waliosomea. Si ungeweka dokezo tangu mwanzo badala ya kuchoshana.
Na kilichofanya uulize maswali na unajua sio mchumi niliyesomea ni nini, mpaka pale nilipotaka unijibu ndio ukajua mimi sio mchumi
Kwanini wewe ulikimbilia kujibu swali la kiuchumi ilhali unafahamu wewe siyo mchumi, ???
Tatizo ni kimbelembele au ujuaji tu mazee ???
 
Chakula, gesi, mafuta na zana za kijeshi sio vipimo vya uchumi. Hapo Urusi inajitosheleza kwa soko la ndani ila inahitaji pia kuuza nje na kununua nje, mambo inayofanya.
Uwezo wa kiuchumi na ukuaji wake una vipimo vyake. Wanauchumi wangetaja vitu kama GDP, PPP, investments, exports, imports, government expenditure, public consumption na kadhalika.
 
Kwanini wewe ulikimbilia kujibu swali la kiuchumi ilhali unafahamu wewe siyo mchumi, ???
Tatizo ni kimbelembele au ujuaji tu mazee ???
Umeanza kuniquote wewe, sikuanza kukujibu mimi. Na nimekuwa tagged kwenye uzi wako. Na hujaweka dokezo kwamba unastahili kujibiwa na wasomi wa uchumi.
 
Umeanza kuniquote wewe, sikuanza kukujibu mimi. Na nimekuwa tagged kwenye uzi wako. Na hujaweka dokezo kwamba unastahili kujibiwa na wasomi wa uchumi.
Ndugu Armata, mambo yako bayana kwenye kichwa cha habari na uzi mzima, kwamba maarifa ya uchumi yanahitajika kwenye huu uzi. Mbona wengine walielewa vizuri tu!
 
Kimweri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…