USA na West hawajawahi tarajia uchumi wa Urusi uanguke. Lengo lao kwenye sanctions ni kuilazimisha Urusi iwe na options kwenye harakati zake za expansionism. Ijue wakati inaendelea kufanya uvamizi itaendelea kupoteza mazingira ya kiuchumi na hao wanaoweka vikwazo, isiwe na uhuru wa kuvamia ikijisikia.
Kama West na US zingetaka kuiua kiuchumi Urusi basi zingeanzia kwenye machine tools na precision machinery ambako Urusi haijiwezi
View attachment 2698026View attachment 2698027
Importation ya mitambo muhimu ya uzalishaji ingesitishwa yote na Urusi wangeishia kutegemea black market au kutegemea machine tools za China ambazo huwa haizipendelei.
Kwanza Marekani inahusika kwenye kuisaidia Soviet Union kukua kiviwanda mwanzoni mwa utawala wao, Volgograd tractor plant ilijengwa na Wamarekani pale Soviet Union iko busy kukua kwenye kilimo. Walikuja kupishana na Marekani walivyoanza kujitutumua na kujishindanisha na Marekani. Na technology transfer wakawa wanaitumia kutengeneza silaha, mfano hiyo Volgograd plant ilitengeneza vifaru, infantry fighting vehicles na artillery.
Sasa nchi gani itakubali ikupe teknolojia uunde silaha alafu uitunishie misuli, wakaachana nayo.
Hata China wanamfanyia hivi Warusi na Wamarekani, unamuuzia licence ya helicopter kutoka Sikosrky ya Marekani yeye anatumia kutengeneza attack helicopter. Sasa unaamua kumpa teknolojia chache zisizo na dual use na sometimes unagoma kumuuzia baadhi ya vitu asiige.
Marekani iliwahi kuwashawishi Germany na Japan baada ya WW2 kustaariba na kuishi kama waungwana duniani wakati kwenye vita walipigana. Leo hizo ni nchi za tatu ya nne kiuchumi duniani, South Korea waliopambaniwa na Marekani ni nchi inazidi Urusi kiuchumi. Hizo nchi tatu ni almost hazina kitu kwenye rasilimali wala ukubwa wa ardhi kama Urusi. Kama Urusi wangekuwa serious na vitu vya msingi hizo nchi tatu hazikutakiwa ziikaribie kiuchumi.
Una rasilimali za kutosha madini mengi kuanzia aluminium, gold, bauxite, iron ore, copper, diamond hadi rare earth metals, gesi ni wa kwanza duniani, mafuta ya kutosha mpaka unaitwa OPEC wakati sio mwanachama, unalima ngano, una mbao, una ardhi kubwa sana wakati idadi ya watu milioni 144 ukitaka kutenga eneo kubwa la kilimo unaweza, una uvuvi. Bado unazidiwa na Italy kwa GDP. Sasa wewe upewe nini hapa duniani?
Urusi sio kwamba hawaipendi, ni yenyewe inalazimisha kujipanbanisha na kuishi kama karne ya 20. Marekani haina haja ya kupambana na Urusi, na inachofanya ni kilekile tena pungufu ya ambacho superpower yeyote kwa timeline yoyote hapa duniani huwa anafanya.