Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Ndugu mhandisi,
Niseme tu, tangu nianze huu mjadala wewe umeonesha kwamba ni mtu makini sana. Unafuatilia mambo, unasoma kwelikweli na una uelewa wa haraka. Katika hili nakupa nyota zako kibao. Hivi ndivyo mijadala ya wasomi inatakiwa kuwa. Sasa naomba nirudi kwenye mada, na ntajikita kwenye suala muhimu sana la kiuchumi, hasahasa tunapozungumzia DATA INTEGRITY:

Umesema hatuwezi kupata taswira sahihi ya uchumi wa Urusi kwasababu serikali imeficha takwimu muhimu. Ukaleta na mifano ya kutosha ili kuwekea mashaka takwimu za shirika la fedha duniani (IMF) kuhusu uchumi wa Urusi kukua. Hivyo basi, kama hakuna takwimu sahihi na za kutosha, hatuwezi kuwa na taswira sahihi. Mimi hapa maswali yangu ni machache tu:

Mosi, wewe unasoma historia ya maendeleo ya dunia na uchumi wake tangu kipindi cha dola la Mrumi (The Roma Empire) hadi kufika leo hii. Katika kusoma kwetu, huwa tunapewa hadi takwimu za idadi ya watu na uchumi wa nchi za kale kama Rumi. Mfano, halisi wanahistoria kutoka CAMBRIDGE UNIVERSITY wanasema kwamba kipindi cha Kaisari Trajan (Emperor Trajan) dola la Rumi, lilikuwa ni asilimia 20% hadi 26% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Hizi takwimu za uchumi za miaka zaidi ya 2000 iliyopita wachumi na wanahistoria wanazitoa wapi, ilhali Warumi wenyewe hawakuwapa, ???

Je, tutakuwa sahihi kusema kwamba takwimu hizi zina walakini (The Lack Integrity) kwasababu Warumi wenyewe hawakutupa, na mambo mengi ya uchumi wa Rumi hatuyafahamu. AU kwasababu wanahistoria hawakuishi kipindi hicho, ???

Mnamo Karne ya 19 wakati Uingereza inaenda kuanzisha utawala nchini India (The British Raj), wachumi wanasema India ilikuwa na uchumi asilimia 24% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Huku Uchina ikiwa na asilimia 34% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Hizi takwimu wahindi wala wachina hawakuzitoa, ila wanahostoria wameweza kutambua. Hapa napo tutakuwa sahihi, kusema tusizitegemee takwimu ambazo hatukuwahi kupewa na serikali ya nchi hizi mbili, ???

Pili, wachumi huweza hadi kutabiri uchumi wa miaka 50 ijayo ilhali wao wako leo. Mfano, hai The Peter G. Peterson Foundation, hivi karibuni wametoa takwimu za deni la Marekani kwa mwaka 2053, na kusema kwamba Marekani itakuwa inalipa asilimia 40% ya bajeti yake katika kulipa deni. Maana yake katika kila dola 10, Marekani atakuwa analipa dola 4 kwenye madeni. Hawa wametumia mbinu gani (Model)za kiuchumi katika kuweza kutabiri hivi, ilhali hata mwaka 2030 bado hatujafika, ???

Tatu, kama unasema tusiwaamini IMF kwasababu Urusi hawajatoa takwimu zotem basi utakuwa umesahau kilichotokea miaka miwili iliyopita. Duniani yote na taasisi kubwa zilikumbwa na uhaba wa takwimu sahihi za kiuchumi kutokana na nchi kufungwa na shughuli za kiuchumi kusimamishwa (Lockdowns). Nchi kama Uchina na Marekani hazikuweza kutoa baadhi ya takwimu muhimu kwasababu raia hawakuwepo katika maeneo yao ya kiuchumi. THE HARVARD BUSINESS REVIEW, kwenye makala yao ya tarehe 10 November 2020, iliyoandikwa na Demitry Estrin walilizungumzia hili.

Mbali na hizi changamoto zote za uhaba wa takwimu, taasisi kama IMF waliweza kutoa takwimu zao zilizotoa taswira sahihi kabisa za uchumi wa mataifa mbalimbali duniani. Kwenye hoja hii, maswali yangu ni haya yafuatayo:

A. Kama IMF waliweza kutoa taswira sahihi za uchumi wa nchi mbalimbali kipindi cha (Lockdown), na tukaziamini hata pale ambapo mataifa mengi yalishindwa kutoa takwimu, kwanini tushindwe kuziamini hizi takwimu zao za kipindi hiki, ???

B. Mbali na uhaba wa takwimu, taaisi za kiuchumi kama The International Monetary Fund (IMF), The World Bank (WB), The Economist Intelligence Unit, walitoa takwimu sahihi sana ambazo zilielezea kwamba dunia itaingia kwenye kipindi cha mdororo wa kiuchumi wa kimkakati (Technical Recession) kuanzia mwaka 2021, na kweli yalitokea na tukayashuhudia. Walitumia mbinu gani za kiuchumi kuweza kufanya utabiri kwa usahihi, ???

Nne na wisho, ndugu mhandishi, taasisi za kifedha kama The International Monetary Fund (IMF) na World Bank (WB) huwa zinategemea chanzo kimoja tu cha takwimu, ambacho ni takwimu kutoka kwa nchi. IMF katika kutoa taarifa zao, huwa na vyanzo mbalimbali (Primary Data Sources, Secondary Data Sources). Taarifa zote za kiuchumi huwa zinaeleza kuwa wametumia vyanzo gani vya taarifa na mbinu za zipi za kiuchumi ili kutoa taswira ya uchumi.

Mbali na nchi kuwa ndiyo chanzo kikubwa, taasisi kama World Trade Organization (WTO) na mashirika mengine ya kimataifa yanayohusika na biashara hutoa takwimu muhimu mno, hata kama nchi itajaribu kuficha. Taifa lolote lile ambalo linategemea biashara za kimataifa (International Trade) kama chanzo cha mapato, haliwezi kabisa kuficha taarifa zake zote muhimu. Hebu nieleweshe hapa ndugu yangu, kama Urusi wameficha takwimu, taasisi za kiuchumi zitashindwa hata kufanya makadirio ya uchumi (Economic Estimation) kwa kutumia mbinu mbalimbali, ???

Hebu nisaidie kuelewa ndugu yangu.....
 
Nimeipata mkuu [emoji1780]
 
Jarida la THE FINANCIAL TIMES, tarehe 9 August 2024, limeanza kuzungumzia uwezekano wa kuwepo na mataifa yenye nguvu katika uzalishaji, katika lugha ya kiingereza mataifa haya yamepewa jina la "COMMODITY SUPERPOWERS". Tena jarida hili limeenda mbali na kusema kwamba mataifa kama Uingereza na Marekani yalifika hapo yalipo kiuchumi kutokana na uwepo mkubwa wa rasilimali ndani ya madola yao karne zilizopita.

Nilipoanza huu mjadala niliwauliza wachumi kwamba: Je, mataifa ya Magharibi yalikosea kuangalia uchumi wa Urusi katika nyanja ya uchumi wa masoko ya mitaji na fedha (FINANCE ECONOMY) peke yake bila kuzingatia uchumi katika nyanja ya kuzalisha na kuuza rasilimali (COMMODITY ECONOMY), ???

Baadhi yetu walisema uchumi wa masoko ya mitaji na fedha ndiyo uchumi wenyewe, na tuendelee kutumia vipimo hivyo kwasababu ndiyo vinaakisi utajiri wa nchi. Binafsi najiuliza maswali mengi, ambayo sijapata majibu bado. Hivi haya mataifa matajiri hapa duniani, yangeweza kufika hapo yalipo bila kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuliko mataifa mengine, ???

Ila nafurahi kuona wachumi hasahasa wa Magharibi, wameanza kuona uwezekano kwamba uchumi wa rasilimali (COMMODITY ECONOMY) una sehemu kubwa mno katika kupima nguvu ya uchumi kwa baadhi ya nchi. Naamini, kadri siku zinavyoenda wachumi watajipima upya na kuanza kufanya marekebisho makubwa kwenye kanuni za uchumi wa dunia. Uchumi ambao utafundishwa miaka 10 ijayo utakuwa tofauti kabisa na huu ambao sisi tunausoma leo hii.

Nitoe mifano ya mwisho: Gideon Rachman, mhariri wa majarida makubwa ya THE FINANCIAL TIMES na THE ECONOMIST anasema kwamba, miaka kabla ya 2008 wachumi wengi walikuwa kwenye mjadala mkubwa kuthibitisha kwamba gharama ndogo za uzalishaji (Low-Cost Production) na soko la ajira lenye gharama ndogo (Cheap-Labour), vimechangia mno anguko la uchumi la mataifa ya Ulaya. Wachumi wengi walipinga, lakini baada ya mwaka 2008, wakaanza kukubaliana na huu ukweli mchungu.

Upande mwingine, uchumi huwa hautegemei kabisa hisia wala mihemko (Psychology). Ila matatizo yaliyoikumba dunia kama UVIKO kuanzia mwaka 2019-2022 yamethibitisha kuwa PSYCHOLOGY ni moja ya kiashiria muhimu sana kinachotumika kufanya utabiri wa uchumi wa mataifa husika. Jarida la THE HARVARD BUSINESS REWIEW, lililochapishwa, November 10, 2020 lilipendekeza mbinu mpya (A Model) ambayo ingewasaidia wachumi kuweza kutabiri uchumi wa nchi mbalimbali, hasahasa kwenye kipindi ambacho kuna uhaba wa takwimu kutokana na nchi nyingi kufunga (Lock-Downs).

Katika mbinu hii, viashiria vya PSYCHOLOGY na HISTORY vimekuwa na umuhimu mkubwa sana wa kutabiri uchumi wa nchi mbalimbali. Mbinu mpya (A Model) ilitumika na wachumi, na imeonesha usahihi mkubwa mno kwenye baadhi ya maeneo. Hili linanifanya nikumbuke Novel ya FOUNDATION ilizoandika na Professor Isaac Asimov mwaka 1951, ambapo kwenye kitabu kuna mhusika aliweza kutengeza mbinu iitwayo "PYSCHO-HISTORY" kuweza kutabiri kila kitu kuanzia siasa, uchumi na utamaduni. Andiko la THE HARVAD BUSINESS REVIEW limezungumzia PSYCHO-HISTORY kwenye kutabiri uchumi.

NB 1: Naamini Bwana Yesu akiendelea kutujalia uzima tutakuja kuona mengi ambayo yatafanya wachumi na wanasiasa turekebishe na kujikosoa kwenye baadhi ya mitazamo.

NB 2: Hii ifuatayo ndiyo nukuu ya jarida la, THE FINANCIAL TIMES, August 9, 2023


 
Kwanza kabisa, ukizungumzia takwimu za uchumi wa dunia katika vipindi vya miaka mingi iliyopita, huwezi kusahau kumtaja mchumi mmoja anayefahamika kama Angus Maddison.

Angus Maddison alikuwa mwanahistoria wa uchumi, mtaalamu wa masuala ya uchumi wa dunia katika historia (kikiwemo kipindi ulichokitaja cha Roman Empire). Kazi zake za miaka mingi iliyopita zimepelekea kuanzishwa kwa kitu kinachofahamika kama The Maddison Project mwaka 2010 na pia The Maddison Project Database, yenye takwimu za uchumi za tangu mwaka 1 (AD 1) ambazo zimekuwa zikifanyiwa marekebisho mara kwa mara.

The Maddison Project inatajwa na wachumi mbalimbali duniani kama chanzo kimoja muhimu zaidi cha takwimu za uchumi wa dunia kihistoria.

Angus Maddison:
The Maddison Project:

Kwa ufahamu wangu kuhusiana na mbinu na nyenzo (methods) zinazotumika na hawa wachumi wanaosimamia hiyo project, takwimu za uchumi wa dunia za miaka au karne nyingi zilizopita zimekuwa zikifanyiwa makisio au zikikadiriwa kwa kutumia data za uchumi wa mwaka 1990 kama reference point kurudi nyuma na kuelekea mbele. Takwimu zao zote mpaka sasa zimekuwa zikizingatia 1990 benchmark iliyokwisha kuwekwa na Angus Maddison mwenyewe.

Hii mbinu ya makadirio kihisabati/kitakwimu inafahamika kama Extrapolation Method; ambayo ndio namna au mbinu kuu zaidi inayotumika na wachumi duniani kutoa makadirio ya uchumi wa karne nyingi zilizopita ama zile zitakazokuja baadaye. Hapa nimejibu swali lako la pili.

Extrapolation Method:

Sasa, pamoja na kuwa hawa jamaa wako makini na ripoti zao zinasifika na wachumi nguli na taasisi mbalimbali za kiuchumi duniani, hilo halimaanishi kuwa tunapaswa kuziamini takwimu zao kwa asilimia 100 kwamba ni sahihi. Kwa sababu, takwimu zao sio vitabu vya dini; nikiwa na maana ya kwamba, huwa zinafanyiwa marekebisho (revisions) kila wakati au mara kwa mara kutokana na mabadiliko mbalimbali ya uchumi wa dunia baada ya kufanyika kwa tafiti mpya, ukizingatia kuwa takwimu zinazotolewa kwa kiasi kikubwa zinahusu uchumi wa vipindi ambavyo kwa sasa hakuna aliyekuwepo.

Hebu fikiria: Kama takwimu za uchumi wa sasa, kipindi ambacho tumo ndani yake tukishuhudia, huwa zinafanyiwa revisions mara kwa mara, itakuwaje kwa takwimu za uchumi za kipindi ambacho hatukuwepo kukokotoa?

Hayo ndiyo majibu yangu kuhusiana na swali la kwanza na la pili.

Kuhusu swali la tatu:
Ili kutoa makadirio ya uchumi wa dunia, IMF hufuata utaratibu unaofahamika kama "bottom-up approach". Maana yake ni kwamba, mchakato mzima wa kufanikisha ripoti za uchumi wa dunia huwa unaanzia katika ngazi ya chini kabisa ambayo ni ndani ya nchi mojamoja kabla ya kufikia ngazi za juu za maamuzi.

IMF kama taasisi ya kimataifa ina ofisi ndogo na mwakilishi [au balozi] wake katika kila nchi mwanachama wa IMF; kwa kiingereza wanamuita country desk officer.

Huyu mwakilishi pamoja na timu yake ndiye anayekusanya taarifa zote muhimu za uchumi wa nchi anayofanyia kazi na kisha kukokotoa na kuandaa makisio au makadirio kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa na kuridhiwa na IMF pamoja na nchi wanachama, wakati huo mamlaka au serikali ya nchi husika inakuwa na jukumu kama mwanachama wa IMF la kukabidhi taarifa ambazo ni most current kuhusiana na uchumi wa nchi.

Kwa mujibu wa IMF, taasisi za ndani za nchi ndizo "ultimate providers" wa takwimu ama data za uchumi wa nchi husika.

Kupitia hizo taarifa kutoka taasisi za ndani [ama serikali], timu ya wataalamu kutoka IMF ndani ya nchi husika ikiongozwa na country desk officer hutoa makadirio ambayo baadaye hupitia mfululizo wa marudio, kisha hutolewa rasmi na IMF kupitia machapisho maalumu ambayo huwa tunayapata mara kwa mara. Hizi timu za wataalamu katika kila nchi huwa zinafanya kazi kwa kujitegemea, kwa maana ya kutokuwa na muingiliano wa kimajukumu kati ya timu ya nchi moja na nyingine, hivyo mbinu za utendaji kazi (methodologies) zinaweza kutofautiana kati ya timu ya nchi moja na ile ya nchi nyingine.

Ukitaka kufahamu zaidi kuhusu hilo, tembelea website ya IMF. Kuna kurasa za nchi zote wanachama wa IMF. Pia, kuna contacts ambazo unaweza kuwasiliana moja kwa moja na mwakilishi wa IMF aliyeko katika nchi yako kama ukihitaji kufanya hivyo.

Link:

Ili kujibu swali lako sasa:
As long as ofisi ya mwakilishi wa IMF inaendelea na majukumu yake kama kawaida, na serikali inatoa ushirikiano kama mwanachama hai, IMF inaweza kukusanya taarifa zote muhimu na kutoa ripoti za kiuchumi zinazohusu nchi husika. Kwahiyo, hata kipindi cha lockdowns kutokana na COVID-19, wawakilishi wa IMF na timu zao bado waliendelea na majukumu yao kama kawaida katika nchi walizopo bila ya kukiuka taratibu zingine za kujikinga na COVID-19.

Kwa sababu taasisi za nchi mwanachama wa IMF ndizo "ultimate providers" wa taarifa zinazotumiwa na IMF, tatizo kubwa linaibuka pale ambapo serikali ya nchi husika kwa makusudi inakataa kutoa ushirikiano kikamilifu katika kukabidhi data na pia kutoa hadharani taarifa za kisera na maendeleo ya kifedha na kiuchumi kwa ujumla kutoka katika taasisi na sekta zote muhimu za uchumi wa nchi. Matokeo yake ndiyo kile ambacho wamekisema kina Jeffrey Sonnenfeld.

Na uzuri zaidi, wataalamu wa IMF wamekiri wenyewe kwamba kuna massive uncertainty kuhusiana na mustakabali wa uchumi wa Urusi.

Swali la nne nililigusia kwa kiasi fulani katika post yangu iliyopita nikizungumzia kuhusu takwimu za mafuta na gesi kuzuiliwa.

Watafiti mbalimbali wanaolenga kubaini mauzo halisi ya mafuta na gesi ya Urusi wamekuwa wakitegemea zaidi takwimu za wanunuzi ama wateja wa mafuta na gesi kutoka Urusi. Vilevile, makisio mengi yamekuwa yakifanyika kupitia takwimu za mataifa ambayo yamekuwa yakinunua nishati kutoka Urusi (international trade partners). The same applies kwenye bidhaa nyinginezo.

Ni kweli kwamba taasisi kama IMF huwa inashirikisha vyanzo ama taasisi zingine za kimataifa katika kukusanya taarifa za kiuchumi ili kuandaa ripoti zao za makadirio ya uchumi, lakini vyanzo hivyo navyo hutegemea vyanzo vyao vya taarifa ili kutoa takwimu zao. Vilevile, miongoni mwa taasisi zinazoshirikiana na IMF, nazo pia hutegemea taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya nchi ili kutoa ripoti zao kuhusu uchumi wa nchi husika. Maana yake ni kwamba, changamoto ya kutopata taarifa zinazoridhisha iko palepale endapo kukiwa na zuio la serikali ya nchi husika.

Ndio maana katika michango yangu ya awali, nilijikita zaidi kunukuu takwimu za mauzo ya Urusi (exports) zilizokusanywa kutoka kwa international trade partners.

Shukrani!
 
Mkuu nimekusoma,

Kuhusu hili la takwimu hata Harvard Business School walitengeneza mbinu yao ya kutabiri (Forecasting Model) uchumi mwaka 2020. Mbinu inatumia Historia na Uchumi, kama Madisson ila inaongezea mambo mengine muhimu tu ambayo yanatoa taswira nzuri kabisa ya uchumi, hata kama nchi haitatoa takwimu. Binafsi nadhani, uchumi ni kama mimba, huwezi kuuficha hata siku.

Tujipe muda na tuombe uzima, tutarudi tena kwenye huu mjadala kufahamu mbivu na mbichi....
 
Ndugu mchumi unadhani mimi napingana na wewe kwamba matatizo ya uchumi wa dunia yanavisababishi vingi (Macro-Economic Variables). Hili nalifahamu vizuri tu, na nadhani hakuna muungwana anayeweza kulipinga. Hakuna ambaye anakataa kwamba mataifa kama Marekani na chama chake cha G7 wana uchumi mkubwa duniani. Ambapo mimi na wewe tunapishana ni hapa tu:

Biashara ya kimataifa (International Trade) inaathiri Macro-Economic factors kama, Interest Rates, Inflation and Currency Exchange. Ukizingatia dunia ya utawandawazi ilivyo, taifa ambalo linaongoza na kutegemewa kwa kuuza bidhaa za muhimu kama nishati na chakula ambazo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa viwanda duniani, huwa na nafasi ya kipekee kwenye uchumi wa dunia hata kama litakuwa na uchumi wa kawaida.

Ndiyo maana mara zaidi ya 5 nimekuuliza kuhusu AUSTRALIA kama mfano hai wa hili nalolizungumza ila maza zote umekwepa kunijibu. Natumai tutakuwa tumeelewana.
 
Nimefurai na uzi huu upo kisomi na evidence toka kwa mtaalam google
 
Urusi sio socialist country, ujamaa ulishakufa muda mrefu sana Urusi. Ukiacha kampuni chache za gesi na sila sehemu kubwa ya uchumi wa Urusi inamilikiwa na mabwenyenye wa kirusi "Oligarchs" kama Vladmir Lisin, Vladmir Potanin, Prighozin, Roman Abromovich n.k
 
Naeka kituo hapa
 
Mitaji, Ubunifu na Teknolojia ndio kila kitu karne hii na ndivyo vinayafanya mataifa kuwa tajiri na yenye nguvu bila hata kuwa na bidhaa kama dhahabu, mafuta/gesi na chakula. Mitaji, ubunifu na Teknolojia ndizo nyenzo muhimu zinazoufanya uchumi wa nchi uhimili mfumuko wa bei usio na mpangilio. Masoko ya huduma, mitaji na teknolojia nyingine ni muhimu na ndio yanaendesha sekta za nishati, chakula na dhahabu katika karne hii.
Mfano mzuri ni
Singapore,
Taiwan,
Japan,
Korea Kusini,
Switzerland.

Pia sijui kwa nini watu wengi huwa wanafikiria Marekani haina rasilimali nyingi, haizalishi chakula na nishati, inawezekana ni kukosa exposure tu. Kwa taarifa yako Marekani ni mojawapo ya mataifa matano duniani yenye rasilimali nyingi zaidi na pia ndiye exporter/muuzaji wa chakula kwa mataifa mengine ya nje namba 1 duniani.
Ndiyo nchi yenye hifadhi ya dhahabu kubwa zaidi duniani.
 
Ivi ile pesa yao inakuja lini tuachane na dollar? Ebu nikumbushe inaitwaje?
 
Mataifa yote duniani kwa sasa yanatumia fiat currency. Hata hiyo ruble kuwa pegged kwa gold imefanyika mwaka jana tu Urusi wakati ikitafuta njia za kukimbia vikwazo vya uchumi vya West na bado hata haijawaha na manufaa yoyote ya kiuchumi kushinda nchi zote kama China zilizoko kwenye fiat currency. Ruble mwezi huu imeanguka vibaya kiasi karibia na wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake Ukraine mwaka jana.
 
Huelewei kabisa masoko ya mitaji ya West yanvoyofanya kazi na jinsi gani raia wa West wanavyonufaika nayo. Ni vyema ukafahamu Multinationals companies kubwa duniani kama sio state owned basi zinapata mitaji yake katika masoko ya mitaji ya West au benki za West, faida wanayopata nyingi zaidi inaenda kwa raia wa huko West,

Hizi kampuni Multinationals au kubwa kama
Barrick Gold,
VISA
Coca-Cola,
Pepsi,
Boeing,
BMW, Scania, Ford
Microsoft,
HP, DELL, ASUS, Apple,
META( Facebook, Instagram), YouTube, Twitter/X, Snapchat, Google, WhatsApp
kampuni za silaha,
Hoteli kama Hyatt, Sheraton
Makampuni ya tumbaku, pombe
Exim bank,
Benki kama Standard Chartered ya Uingereza faida yake kwa 90% inatoka Africa na Asia.

Mitaji ya haya Makampuni na mengine mengi ni kupitia masoko ya mitaji huko US na Ulaya na pia faida inayopatakina kiasi kikubwa zaidi kinarudi kwa hao raia wanaonunua hizo hisa zao.
 
Kusema Marekani wanachapisha fedha hovyo ni conspiracy tu, ni sawa na kuifananisha na Zimbabwe ambapo huo ni ujuha. Federal reserves wanachapisha fedha pale inapohitajika kuchapisha fedha, pia fahamu hakuna benki kuu iliyo huru kama Federal Reserve ya Marekani. Kuanzia uongozi hadi ufanyaji kazi wake ni wa uhuru wa hali ya juu usiongiliwa na Rais au serikali ya Marekani. Biden hawezi kumwambia Jerome Powell achapishe fedha tu naye akazichapisha, Senate ya Marekani itamu impeach akifanya hivyo.
 
Dhahabu kwa sasa haina umuhimu mkubwa sana wa kipekee katika uchumi wa dunia kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 1971 ambapo Marekani iliondokana na gold standard system.

Kwa sasa dhahabu ukiachana na matumizi ya urembo na mengineyo katika uchumi wa dunia benki na matajiri wanahifadhi dhahabu kama insurance policy tu siku mambo duniani yakiharibika kabisa waweze kupata pa kutokea.
 
Nafasi ya kipekee YES, lakini Yuko peke yake? NO. Ni vizuri tuelewe hata utegemezi kwenye gesi ya Urusi umepungua sana kwa mataifa ya EU na niliweka takwimu hapo nyuma so unless ingekua monopoly ila zaidi ya hapo relevance ya Urusi itashuka na uchumi utaonyesha madhara.

2. Currently ruble Ina perform vibaya sana kama ingekua Russia ndio kimbilio la Kila mtu why sarafu Yao iporomoke kiasi kile. Maadam ulisema madhara ya vikwazo vya uchumi vinaipiga G7 na sio Russia je una maoni Gani kwa pesa ya ruble kuporomoka na uchumi wa china kupata mtikisiko?

3. Hii hapa article ya BBC inaonyesha data za Sasa huko China kwamba unemployment rate imevunja rekodi kiasi wamezuia zisichapishwe tena. Je china ni west economy? Je china haifanyi biashara na China? Jibu ni HAPANA. Sasa kwanini imeathirika kiuchumi? Mpaka hapo ma

https://www.google.com/url?sa=t&sou...DKAB6BAgOEAE&usg=AOvVaw2WdIr8xiDG-BuBgM7WjlS4

4. Takwimu za juzi zinaonyesha uchumi wa Japan umepaa kwa kukua by 6% tofauti na matarajio kuwa ungekua kwa 3%. Since mada Yako ilisema madhara ni kwa west nations kisa zinaipinga Russia inakuaje Japan ipae kiuchumi ilihali Russia na China zinapumulia mashine kwa Sasa?

Ndio tunarudi kule kule mwanzo kuwa;
1. matatizo ya uchumi wa kidunia yangetokea with or without vita ya Russia na Ukraine or Vikwazo vya Russia.
2. Kingine madhara ya vikwazo vya uchumi haviwezi onekana siku Moja ila baada ya muda mrefu kama Sasa ambapo majibu yanaanza kupatikana taratibu.
3. Ulisema pia currency kuwa backed na gold ndio true value kuliko Fiat currency. Nilisema hata commodities are open to price shocks and volatility na umeona licha ya kuwa backed na gold bado Ruble inaporomoka mnoo.

So nachoweza conclude ni kwamba uchumi hauwi determined na factor moja tu ila multiple factors zikitokea kwa pamoja so cherry picking won't save Russia from the impending doom.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…