Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Australia???

Ngoja niende gugo
1690644586823.png
 
Swali langu kuhusu Australia, mbona hunipi majibu mchumi ???
Kama ambavyo hujanipa Jibu la swali langu kwamba wakati una conclude kuwa vita ya Ukraine imechangia inflation au matatizo ya kiuchumi huko western Bloc (G7) je ume control for other macroeconomic variables??

Maana tukihamia kwa Australia tukaachana na Russia mada itageuka tena muelekeo.
 
Mchumi, hebu nisaidie: Hivi leo BOT ikaamua kufanya QE ili kuingiza fedha kwenye mzunguko, au tukachapisha fedha nyingi ambazo zikapelekea kuwa na Money Base (MO) kubwa ambayo inazidi bidhaa na rasilimali zilizoko sokoni na upatikanaji wa rasilimali, nini kitatokea, ???
Hili nimeshajibu kwamba thamani ya bidhaa huwa inakua at par na machapisho ya fedha maana fedha kama fedha Haina thamani unless iwe na attached value ya bidhaa.

Mfano kama Tanzania tuna GDP ya trillion 100 kutokana na thamani ya bidhaa zinazouzwa au kuzalishwa (Govt expenditure, net exports, investments n.k) Ina maana hata machapisho ya pesa yataendana na thamani ya bidhaa zilizopo not otherwise.

So hayo mambo yanafanyika kwa utaalamu wa hali ya juu, na sio kwamba zinachapishwa tu basi zinaachwa kusambaa tu nope huwa zipo monitored kuona the number of times the money actually changes hands (velocity), na pia zinavyochochea uzalishaji (Net investments, multiplier effects) Sasa wakiona watu wanaanza kuvuna actual goods kupitia hizo pesa ndio serikali hiyo hiyo inaondoa fedha Tena kwa mzunguko kupitia Kodi, Hati fungani n.k

Na hivo vyote vinatokea based on DEMAND and SUPPLY. Ndio maana hata mafuta licha ya umuhimu wake Kuna wakati yanaporomoka bei, au hata dhahabu Kuna miaka kuanzia 2014 hivi iliporomoka bei ikaja tengemaa 2018 through 2019. Maana dhahabu ikizalishwa nyingi obvious soko linashuka au dhahabu ikipata mbadala obvious soko linaporomoka na ndio maana pesa inaweka shikilia thamani ya bidhaa kuliko dhahabu au any other commodity ambayo ipo prone to volatile price shocks.
 
Kama ambavyo hujanipa Jibu la swali langu kwamba wakati una conclude kuwa vita ya Ukraine imechangia inflation au matatizo ya kiuchumi huko western Bloc (G7) je ume control for other macroeconomic variables??

Maana tukihamia kwa Australia tukaachana na Russia mada itageuka tena muelekeo.
Ndugu yangu unataka kusema bila vita ya Ukraine mataifa ya G7 bado yangeingia kwenye matatizo makubwa ya uchumi kwa haraka kama ambayo inatokea leo, ???
 
Mfano kama Tanzania tuna GDP ya trillion 100 kutokana na thamani ya bidhaa zinazouzwa au kuzalishwa (Govt expenditure, net exports, investments n.k) Ina maana hata machapisho ya pesa yataendana na thamani ya bidhaa zilizopo not otherwise.
Hebu nisaidie mkuu, hii kanuni inafanya kazi hadi kwa taifa kama Marekani, ???
Kwanini fedha ya Marekani ni nyingi kuliko bidhaa zilizopo sokoni, ???
 
Kipimo kipi kinatumika kupima utajiri wa mataifa, ???
Of course most use GDP kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazozalishwa au kuuzwa (Production and expenditure Approach) kwenye nchi katika wakati husika. Na bidhaa hizi sio tu Mchele na unga Bali mpaka intangible assets kama services kama huduma za kisheria, teknolojia, utabibu, utalii, na financial markets.

Na ndio maana Marekani ina madeni almost 100% ya GDP lakini ndio taifa kubwa kiuchumi, ila pia Ina trade deficit maana inanunua kuliko kuuza but ipo juu bado? Sababu gani?? Stable financial sector. Hayo unayoita makaratasi au thamani hewa ndio actual inayoifanya US kuwa juu otherwise Ina madeni pengine kuliko nchi yoyote duniani na Ina negative trade balance kuliko nchi nyingi ila Bado inazikopesha na kuzipa msaada Kila siku.

As much as we agreed uchumi sio zero sum game then tukubaliane kwamba BIDHAA na FIAT MONEY Zina complement each other ila Moja peke yake haiwezi kuwa sustainable
 
Hebu nisaidie mkuu, hii kanuni inafanya kazi hadi kwa taifa kama Marekani, ???
Kwanini fedha ya Marekani ni nyingi kuliko bidhaa zilizopo sokoni, ???
No it's not true, ingekua pesa ni nyingi kuliko bidhaa basi kungetokea hyperinflation kama iliyotokea kipindi cha Great Economic Depression.

I would request actual data to back this fact.
 
Sawa mchumi, hivyo mfumuko wa bei na riba kufika 6% ilikuwa ni lazima itokee.
Eeh mkuu we can a conduct a panel regression kwa nchi za G7 vis a vis na Russia tutaweza ona jinsi Gani uchumi tu ungeleekea huko bila hata Ukraine na Russia kupambana.

Mfano wakati wa COVID-19 watu hawakuwa na ajira kabisa so bei za bidhaa zilishuka maana hakuna purchasing power Sasa baada ya crisis watu wengi sana wakaajiriwa kwa mkupuo so obvious purchasing power ilikua kwa spidi sana mwishowe Kila mtu anakua na pesa so lazima mfumuko wa bei.

Hiyo ni mfano tu, so sudden change in the unemployment rate can lead to inflation other factor remaining constant

Nikipata huo muda nitafanya hizo test then nitakuja kurudi humu na majibu yenye statistical evidence to show the actual variables zilizochangia hili tatizo ni ipi.
 
Of course most use GDP kwa kuangalia thamani ya bidhaa zinazozalishwa au kuuzwa (Production and expenditure Approach) kwenye nchi katika wakati husika. Na bidhaa hizi sio tu Mchele na unga Bali mpaka intangible assets kama services kama huduma za kisheria, teknolojia, utabibu, utalii, na financial markets.
Anhaaa, unaeleweka mchumi.
Na ndio maana Marekani ina madeni almost 100% ya GDP lakini ndio taifa kubwa kiuchumi, ila pia Ina trade deficit maana inanunua kuliko kuuza but ipo juu bado? Sababu gani?? Stable financial sector. Hayo unayoita makaratasi au thamani hewa ndio actual inayoifanya US kuwa juu otherwise Ina madeni pengine kuliko nchi yoyote duniani na Ina negative trade balance kuliko nchi nyingi ila Bado inazikopesha na kuzipa msaada Kila siku.
Suala hapa ni Marekani kuwa na Stable Financial Sector au The US Dollar being the world's reserve currency which gives American a way out, an Exorbitant Privilege of avoiding Balance of Payment Crisis, ???
 
Kweli kuna propaganda nyingi mno kwenye hii vita. Japo nachofahamu mimi ni kwamba hii vita imekuwa mbaya zaidi kiuchumi kuliko kijeshi. Mpaka sasa hakuna taifa kubwa barani Ulaya ambalo halijaumizwa na mfumuko wa bei au mdororo wa uchumi.

Ila kubwa ni kwamba mwaka 2022 taasisi kubwa za kifedha zilitoa utabiri kwamba uchumi wa Urusi (GDP) ungenguka kwa asilimia 12%, lakini baadaye wakabadilishwa takwimu za makadirio na kusema kwamba uchumi wa Urusi utaanguka kwa asilimia 2% hadi 3%.

Nachojiuliza nini kilitohea hadi wakaandika makadirio makubwa hivi lakini ghafla wakabadilisha takwimu. Wangebadilisha kutoka 12% hadi 10% ningeelewa, maana uchumi hupimwa kwa makadirio (Estimates), ila kutoka 12% hadi 3% ni parefu sana.

Hebu tujuzane zaidi.....
Walitumia makadirio ya matukio yaliyopita ya Nchi ambazo ziliwekewa vikwazo,vilevile wali project Nchi nyingi zikiwemo za Europe zitafuata maagizo ya USA za kutaka Nchi kusitisha biashara na Russio jambo ambalo limekuwa against.
 
No it's not true, ingekua pesa ni nyingi kuliko bidhaa basi kungetokea hyperinflation kama iliyotokea kipindi cha Great Economic Depression.

I would request actual data to back this fact.
Unasahau mambo ya msingi mchumi:
1. The US Dollar is the world's reserve currency.
2. The entire world needs the dollar to do international trade.
3. Unlike any other country in the world, American debt is owned in US Dollars.
4. The USD as Reserve Currency can make America avoid Balance of Payment Crisis.

NB: American can print lots of money to finance budget, fulfill its debt obligations, and still not fall into a pit of hyper-inflation. This is because the money printed will eventually end at the hands of foreign powers who will buy it as a commodity, and again reinvesting it in America by buying US Treasury Bills, other bonds, stocks or investing in tech start-ups etc

It's a ponzi scheme, some of you economists fail to see....

Walitumia makadirio ya matukio yaliyopita ya Nchi ambazo ziliwekewa vikwazo,vilevile wali project Nchi nyingi zikiwemo za Europe zitafuata maagizo ya USA za kutaka Nchi kusitisha biashara na Russio jambo ambalo limekuwa against.
Kwanini Ulaya hawakutaka kusitisha biashara na Urusi ilhali bidhaa wangeweza kuzipata kwingineko, ???
 
Nitajibu bila takwimu labda badaye nikipata muda nitaweka.
Vikwazo vya magharibi za Nchi 30 tajiri zaidi dunini hazijafua dafu dhidi ya Russia masikini kwa sababau hizi.inasemwa kwamba uchumi wa dunia unaendeshwa kwa capital markets,but tukumbuke kuwa 100% hii capita market inategemea product markets/resources.

Karne ya 19 & 20 mataifa hayo tajiri yalizunguka dunia nzima yakipigana na wenyeji wa Nchi nyingine kutafuta rasilimali kwa ajili ya viwanda vyao.Leo katika karne hii bado wanazitafuta hizo rasilimali kwa njia tofauti tofauti na kwa ugumu zaidi kuliko wakati ule.Tukumbuke kuwa Russia pekee ki eneo ni zaidi ya mara 4 ya Nchi zote za Ulaya.

Na kitu kikubwa ukubwa huo wa kieneo wa Russia umeambatana na rasilimali zote muhimu unazozijua hapa Duniani.Russia ndio Nchi pekee Duniani tajiri kuliko Nchi yoyote chini ya jua.viwanda vya ulaya vyote vinategemea resources kutoka huko-kwa hali hiyo hata uweke vikwazo milioni lazima vitakurudia na ndicho kilicho tokea kwa Nchi zote za ulaya na USA.Ukisema uachane na Urusi utakwenda Nchi ipi kipata hizo resource and at what cost???.

Kuna watu hadi Leo wanadhani Adolf Hitler alikuwa fara kutaka kuiweka Urusi chini yake-jamaa alikuwa na akili aliona mbali miaka 100.

**Ukitaka kuitawala Dunia hakikisha kwanza unaitawala Russia.
 
"Ukitaka kuitawala Dunia hakikisha kwanza unaitawala Russia."

maneno haya yamenikumbusha kauli ya mwanadiplomasia wa kimarekani, alipata kusema maneno flani yakufurahisha sana,

alisema, "Who controls the Rimland rules Eurasia, who rules Eurasia controls the destinies of the world."

Rimland hapa ina maana ya zile nchi zinazoinguka USSR (kuanzia turkey-cyprus-greece, arab land, india, china hadi korea zote 2), and this was the basis of american policy post ww2 (cold war era),....
 
Hayo maneno yalisema na Prof Halford Mackinder (The Father of Geopolitics) kwenye chapisho lake la mwaka 1904 liitwalo The Geographical Pivot of History. Mle ndani alianzisha kitu kiitwacho The Heartland Theory, na kusema taifa lolote litakalofanikiwa kuitawala Urusi (The Heartland) ndiyo litaitawala dunia.

Kiufupi, hata Adolf Hitler anapovamia Urusi mwaka 1931 ilikuwa kwasababu aliamini katika hii falsafa, ambayo wanafalsafa wengine kama Henry Kissinger, George Kenan na Zbigniew Brezinsky waliifuata.
1690653168749.png

NB: Ila je, hili lina ukweli wowote au yalikuwa ni mawazo tu ya wasomi wa Ulaya ???
 
Nitajibu bila takwimu labda badaye nikipata muda nitaweka.
Vikwazo vya magharibi za Nchi 30 tajiri zaidi dunini hazijafua dafu dhidi ya Russia masikini kwa sababau hizi.inasemwa kwamba uchumi wa dunia unaendeshwa kwa capital markets,but tukumbuke kuwa 100% hii capita market inategemea product markets/resources.

Karne ya 19 & 20 mataifa hayo tajiri yalizunguka dunia nzima yakipigana na wenyeji wa Nchi nyingine kutafuta rasilimali kwa ajili ya viwanda vyao.Leo katika karne hii bado wanazitafuta hizo rasilimali kwa njia tofauti tofauti na kwa ugumu zaidi kuliko wakati ule.Tukumbuke kuwa Russia pekee ki eneo ni zaidi ya mara 4 ya Nchi zote za Ulaya.

Na kitu kikubwa ukubwa huo wa kieneo wa Russia umeambatana na rasilimali zote muhimu unazozijua hapa Duniani.Russia ndio Nchi pekee Duniani tajiri kuliko Nchi yoyote chini ya jua.viwanda vya ulaya vyote vinategemea resources kutoka huko-kwa hali hiyo hata uweke vikwazo milioni lazima vitakurudia na ndicho kilicho tokea kwa Nchi zote za ulaya na USA.Ukisema uachane na Urusi utakwenda Nchi ipi kipata hizo resource and at what cost???.

Kuna watu hadi Leo wanadhani Adolf Hitler alikuwa fara kutaka kuiweka Urusi chini yake-jamaa alikuwa na akili aliona mbali miaka 100.

**Ukitaka kuitawala Dunia hakikisha kwanza unaitawala Russia.
Ndugu mchumi, mtaalamu mwenzako Zitto Jr anasema haipo hivyo, ulivyosema wewe hapa. Anasema kwamba miaka mitano ijayo G7 watapata mbadala wa nishati ya Urusi. Ila takwimu za kihistoria zinasema kwamba Ujerumani amekuwa akitegemea gesi, mafuta, chuma na mpira kutoka Urusi ili kuendesha uchumi wake wa viwanda tokea miaka ya 1930's na mpaka leo imepita miaka 93 bado hajapata mbadala.

Hivi inawezekana kabisa kwamba kuna siku mataifa ya magharibi hasahasa Ulaya, yataacha kutegemea rasilimali kutoka Urusi, na ile nchi ianguke kutokana na kuwa dhaifu kiuchumi, ??? Haya hapa chini ni maneno ya mchumi na mwanahistoria kutoka Yale University na Cambridge University.

1690653847414.png
 
Kwanini Ulaya hawakutaka kusitisha biashara na Urusi ilhali bidhaa wangeweza kuzipata kwingineko, ???
Gharama za kuzifata huko zilipo mpaka kuzifikisha kwao ni kubwa kuliko kuzifata za Urusi....Sana Sana wameziwekea baadhi ya 'vigingi' kama adhabu mfano 'price cap' kwenye mafuta ya Urusi pekee.
 
Back
Top Bottom