Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Waivamie ya Nini wakati imeshindwa vita? Hivi Russia kuiteka Kiev imeshindikana kwa zaidi ya mwaka Sasa ndio sembuse wapambane na NATO?

Hivi Kuna Taifa lilikua na nguvu kuliko USSR? ila iliporomoka kirahisi tu ndio sembuse a weakened Russia?

Wanachohofia ni madhara ya vita tu yatakua makubwa ila sio kwamba wanaogopa kushindwa vita.
Aione lee van cliff
 
Ruble against $ currently .
86B467A7-5521-4564-80A7-AFB7C26F8D37.jpeg
Ebu jaribu kuniwekea ruble kwenye vipande vya dhahabu...maana tunaelekea huko. Hesabu zinakaaje?
 
Nimeenjoy sana somo la Uchumi wa kimataifa hapa. Nina swali;
Vita yoyote inayowahusisha wakubwa, lazima huleta mabadiliko ya sera za kiuchumi kimataifa. Ndicho kinachotokea sasa. Mfano China ana mkono usioonekana kwenye huu mgogoro, kwani yeye ni mnufaika mkubwa wa matokeo ya vita hii kiuchumi hasa kwenye hiki kiitwacho Multipolar world kwa lugha nyingine ni anguko la US. Swali langu, katika sense ya kiuchumi, hii multipolar world(i.e Vs US Hegemony) itafanikiwa?
 
Bwana Armata nimeuliza maswali rahisi sana ambaya hata mtoto anayesoma shahada ya uchumi, sheria au siasa angeweza kuyajibu. Nilihitaji uchambuzi wa kiuchumi uliojaa takwimu, mahesabu na kanuni za kiuchumi. Bahati mbaya mno nimeona maelezo na maoni yako binafsi. Haina shida twende taratibu hivyohivyo.

Nashangaa mno kuona kwamba msomi kama wewe kutofahamu kwamba The Oil Embargo ni moja ya sababu kubwa iliyosababisha kutengeneza mfumo mpya wa uchumi wa dunia Bretton Woods II na kusababisha American-Asia Corporate Inversion mambo makuu yanayoigharimu Marekani mpaka leo.

Kama vitu rahisi hivi vimekupita wewe mchambuzi wa mambo ya siasa basi kuna tatizo kubwa pahala. Ila tuendelee taratibu hivihivi naamini tutaelewana huko mbele.

Bwana Armata nimeuliza swali rahisi sana. Nini kimepelekea mataifa ya G7 kupandisha riba za mabenki juu (Hiking Interest Rates). Unaweza pia hata kunitajia sababu za kwanini Urusi naye alipandisha riba za mabenki juu. Ntakushukuru kama utanipa majibu.

Umejibu vyema kabisa, lakini hapa napata maswali mengine matatu;

Swali la kwanza, hao Ulaya wanavyotafuta mbadala wa nishati ya Urusi watapambanaje na tatizo la mdororo wa uchumi ambalo limewakumbuka au hili tatizo litaondoka ndani ya usiku mmoja ?

Ifahamike takwimu za International Energy Agency (IEA) zinasema itachukua miaka isiyopungua kumi kwa Ulaya kuweza kupata mbadala wa nishati ya bei rahisi kama ya Urusi.

Swali la pili, gharama za uzalishaji zikipanda juu kwasababu ya ghaarama za nishati mbadala unadhani viwanda vitaendelea kufanya uzalishaji katika kiwango ambacho kilikuwepo kabla ya mwaka 2022, ???

Kumbuka kanuni za uchumi wa kibepari zinasema hivi, ili uweze kupata faida kwenye uzalishaji ni lazima uwe na nishati ya bei ndogo na malighafi za bei ndogo. Wanavyotafuta mbadala wa nishati ya Urusi wataendelea kuwa na nguvu kubwa ya uzalishaji ???

Swali la tatu, wanavyotumia gharama kubwa kutafuta mbadala wa nishati ya Urusi, bara la Ulaya watakabilianaje na tatizo la mfumuko wa bei (Energy Inflation), ???

Mwisho kabisa, ndiyo Urusi imeingia kwenye mdororo wa uchumi kwasababu ya vikwazo vikubwa kutoka mataifa ya G7 ambayo ndiyo yenye uchumi mkubwa duniani. Ila ambacho kinanishangaza ni kwanini mataifa yanayomiliki asilimia 30.7% ya uchumi wa dunia nayo yawe kwenye kundi moja na Urusi taifa ambalo ni asilimia 4% ya uchumi wa dunia. Huoni hapa kuna walakini ???


Bwana Armata majawabu yako yanazidi kunishangaza mno. Urusi siyo taifa lenye uchumi wa mitaji (Capital Market Driven Economy) kama Marekani. Marekani ndiyo taifa tajiri duniani kwasababu asilimia 34% ya soko la mitaji (Capital Markets) duniani linashikiliwa kwa fedha za kimarekani (Denominated in US Dollars). Hivyo Marekani ndiyo makao makuu ya masoko ya mitaji duniani.

Mabenki ya Urusi yakiwa mufilisi haileti madhara kwa dunia hata kidogo, lakini mabenki ya Marekani yakiwa mufilisi dunia nzima itaona madhara kwasababu yeye peke yake ndiyo mwenye soko kubwa la mitaji duniani ambalo karibia benki kuu (Central Banks) zote zinanunua bidhaa na huduma.

Deni la Marekani linamilikiwa (US Treasury Bills are held by foreign states) na mataifa ya nje kama Uchina kama mbinu ya kuyawezesha mataifa hayo yapate fedha za kimarekani kwa wingi kama mbinu ya uwekezaji, lakini pia kupunguza thamani ya fedha zao , jambo ambalo kiuchumi ni muhimu mno kwenye kufanikisha biashara ya kimataifa (China uses this economic technique of devaluating her local currency against the dollar in-order to boost exports)

Nilitegemea haya unayafahamu hivyo usingeleta mfano wa mabenki ya Urusi. lakini kwasababu hukuyafahamu basi nimekupa takwimu na sababu za kiuchumi kwanini umufilisi wa mabenki ya Urusi na Marekani uko tofauti. Mtu yoyote aliyesoma uchumi na kufahamu vizuri siasa za dunia hawezi kufanya huu ulinganifu.

Turudi kwenye swali letu la msingi: Nini kimepelekea mabenki 1000 ya Marekani yanayouza mitaji duniani kote kuwa mufilisi (Insolvent), ???

Uko sawa kabisa, Urusi hauzi nishati ya bure, lakini ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza nishati ya bei nafuu kwa nchi za Ulaya, Uchina na India. Uchumi wa viwanda wa Ujerumani una thamani ya dola za Kimarekani Trilioni 1, lakini unaendeshwa na nishati kutoka Urusi yenye thamani ya dola za kimarekani Bilioni 60 tu. Huo mbadala watakoupata hapa ni upi ndugu yangu ?

Kuhusu mkataba baina ya Uchina na Saudi Arabia nilitegemea ufahamu kwamba nishati inayotoka ghuba ya Uajemi kwenda Uchina husafirishwa kupita bahari hivyo ni gharama kwasababu ya muda, bima (Maritime Insurance) na upakiaji (Packaging). Gesi inayokuja kutoka Saudi Arabia kwenda Uchina ni LNG, ambayo ni gharama mno kuitengeneza. Ila pia kumbuka kampuni la bima kama LLYODS OF LONDON la Uingereza linachaji dola za kimarekani milioni 50 kwa mzigo mmoja wa majini.

Unadhani kuliko kutumia Trans-Siberian Pipeline ambayo husafirisha gesi kwa haraka bila ukomo, Uchina atajikita kabisa kwenye kutegemea mkataba wake na Saudi-Arabia ???

Bwana Armata nakushauri kama kaka, usijibu hivi tena mbele za watu. Yaani unapima soko la nchi husika kwa kuangalia manunuzi ya magari kweli. Unataka kusema leo hii Tanzania ikununua magari mengi kuliko Kenya basi soko letu ndiyo kubwa ???

Halafu kuichumi huwezi kulinganisha nguvu ya manunuzi (Purchasing Power) ya nchi mbili moja kwa moja. Inabidi uzingatie mambo kadhaa wa kadhaa, ndani ya nchi unazozifanyia uwiano. Wachumi wengi hutumia kipimo kiitwacho THE BIG MAC INDEX, kupima nguvu ya manunuzi baina ya nchi mbili (Purchasing Power Parity). Hili linafanyika kwasababu bei za vitu kwenye nchi mbalimbali zinatofautiana.

Bwana Armata wewe mwenzangu ulisomea wapi uchumi, mbona mambo unauliza mambo ambayo yanatutia wenzako ukakasi ? Tunarudi kulekule kama nilivyosema.

Marekani ana mengi ya kupoteza kuliko Urusi kwasababu yeye nchi yake ndiyo makao makuu ya soko la mtaji hapa duniani (The Epicenter of World's Capital Market). Uchumi wa Marekani unaendeshwa na udhibiti wa masoko ya hisa, riba, hati-fungani na uchapishwaji wa fedha. Urusi ana sehemu ndogo mno kwenye uchumi wa mitaji.

Riba zinapopandishwa juu bila mpangilio, wawekezaji wengi zikiwemo benki kuu za (Central Banks) duniani kote, na mashirika mengine hupoteza imani kwenye mfumo jambo ambalo linaweza kusababisha mtafaruku kwenye masoko (Market Volatility), kuanguka kwa mabenki, hata mitaji kuondoka nchini (Capital Flight) au hata mtikisiko wa uchumi wa dunia kama ilivyokuwa mwaka 2008.

Ewaah, swali langu liko hapa. Kwanini matajiri wa G7 hawajawekea vikwazo makampuni ya nishati ya nchi masikini kama Urusi, na kuamua kutumia fedha zao kupata nishati mbadala ???

Kama uchumi wa Urusi unaendeshwa kupitia gesi na mafuta, kwanini uweke vikwazo kwingineko kwenye sekta ambazo hazina madhara makubwa, lakini uache kuweka vikwazo kwenye sekta ambazo zinaipa Urusi nguvu ya kuendesha vita yake ya kivamizi na uchumi wake, ???

Aidha unachanganya watu makusudi, unakwepa swali au hufahamu kitu. Binafsi nimeuliza kuhusu soko la hati-fungani (Bond Market) na siyo soko la hisa (Stock Market). Wewe umejibu kana kwamba hivi vitu viwili ni kitu kimoja, jambo ambalo limenishangaza sana.

Ungefahamu utofauti uliopo baina ya haya masoko mawili, na jinsi yanavyofanya kazi kwenye uchumi wa dunia sidhani kama ungetoa hata mfano wa Urusi. Nimekuuliza kwanini soko la hati-fungani, ambao ndiyo uwekezaji unaoaminika zaidi kule Ulaya limeanguka ???

Hujanijibu kitaalamu, umezunguka mbuyu na kuleta siasa.


Mkuu, unafahamu nini maana ya Quantitative Easing (QE), ???

Mkuu, unazidi kuchanganya mambo. Binafsi sijazungumzia fedha ya Marekani kutumika kama EXCHANGE peke yake. Hayo umeyasema wewe. Binafsi nimeuliza kuhusu asilimia 55%-59% ya matumizi ya fedha ya Marekani as COMMODITY, STOREHOLDE OF WEALTH and A BEBT-INSTRUMENT not only as a MEANS OF EXCHANGE.

Ikumbukwe kiuchumi, mbali na kabla ya kufanya manunuzi dola ya Marekani ni bidhaa kama bidhaa nyingine ambazo Marekani inauza kwa nchi mbalimbali. Hivyo nilivyozungumzia asilimia 55% nilizungumzia hili.

Nadhani hili tuliache, kwasababu ulilijibu bila kulielewa vizuri.

NB: Binafsi naendelea kusubiri majawabu yako nijifunze zaidi mkuu....
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍👍
 
Tokea mwaka 1944, baada ya kutengeneza mfumo wa Bretton-Woods hakuna taifa ambalo limewahi kuwa na uchumi mkubwa kama Marekani. Kufika mwaka 1945, Marekani ilikuwa inamiliki nusu nzima ya uchumi wa dunia. Fedha ya Marekani ikishikiliwa na dhahabu (Gold-Backed) ilikuwa ndiyo inatumiwa kwa kiwango kikubwa kwenye biashara zote za kimataifa.

Mwaka 1957, baada ya Raisi Gamal Abdel Nasser wa Misri kutaifisha mfereji wa Suez, Uingereza, Ufaransa na Israel waliunda mkakati wa kuvamia Misri ili kumtoa Nasser. Mkakati huu ulikufa kibudu baada ya Raisi wa Marekani General Dwight Eisenhower kuwachimba mkwara mzito Waingereza kwamba wangeacha kununua hati-fungani (Sovereign Bonds) za Uingereza na nyingine wangeziuza, jambo ambalo lingeangusha uchumi wa Uingereza.

Kiufupi, baada ya hili kutokea Raisi wa Ufaransa General Charles De Gaulle alilalamika na kusema kwamba "The dollar gives America an exorbitant privilege in international financial system". Akimaanisha kwamba dola inampa Marekani nguvu iliyomithirika kwenye uchumi wa dunia dhidi ya mataifa mengine. Kiufupi Marekani akikutoa kwenye mfumo wake wa kifedha, lazima uumie.

Wataalamu wanatumia vipimo (Metrics) kama GDP na PPP kupima uchumi wa dunia. Ukitumia kipimo cha GDP, nadhani Marekani ndiyo taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani likifuatiwa na Uchina. Uchumi wa Marekani peke yake ni asilimia 24% ya uchumi wa dunia (Global GDP). Kiufupi ni kwamba, all financial roads lead to America.

Marekani hayuko peke yake, anashirikiana na wenzake wa kule Ulaya (European Union) na wenzake wa chama cha mabwanyenye wa dunia almaarufu kama G7. Ukichanganya uchumi wa Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Italia, Canada na Japan, ambao ndiyo nchi tajiri zaidi duniani unapata asilimia 30.7% ya uchumi wa dunia (Global GDP).

Kiuhalisia, haya mataifa saba ndiyo yanayoendesha uchumi wa dunia kupitia mifumo waliyoitengeneza baada ya mwaka 1945. Viwanda vikubwa duniani ni vyao, masoko makubwa ya hisa ni yao, mabenki makubwa duniani ni yao, wao ndiyo wanaongoza katika kuzikopesha fedha nchi nyingine na wao ndiyo wanaongoza kwa kuuza huduma zaidi hapa duniani.

Maswali yangu ya kiuchumi ni haya yafuatayo:
Mosi, kwanini Urusi ambayo ni asilimia 4% tu ya uchumi wa dunia (Share in Global GDP) bado haijaanguka baada ya mataifa makubwa yanayomilikia asilimia 30.7% ya uchumiwa dunia kuwawekea vikwazo vikali ?

Pili, kwanini makampuni ya Urusi ya nishati ndiyo yameongoza duniani kwa kuuza zaidi nishati, ilhali yamewekewa vikwazi baada vikali ? Takwimu zilizotolewa na Marekani yenyewe zinasema kiujumla mashirika ya nishati ya Urusi yameuza zaidi na kupata faida kipindi hiki cha vita na vikwazo kuliko kipindi kingine chochote. Tatizo liko wapi hapa ?

Tatu, Je, tutegemee kwamba kuna siku hivi vikwazo vitafanya kazi na vitauangusha uchumi wa Urusi kama ambavyo Raisi Biden alisema mwaka 2022 kabla ya uvamizi kuanza ? Alisema kwamba uchumi wa Urusi ungeanguka ndani ya wiki chache tu, sasa ni mwaka na zaidi. Mataifa ya Magharibi yamefanikiwa au tuendelee kusubiri ?
Mrusi akili mingi mingi 😂
 
Ndugu Eliakeem nimefurahi kukuona hapa ndugu yangu, maana ni siku nyingi tangu tuachane kwenye ule mjadala wetu kuhusu kukwama kwa mradi wa bwawa la Nyerere.

Nurudi kwenye mada, binafsi najaribu kuuliza hili maswali ambayo yamenitatiza lakini naona sipati majawabu yanayoeleweka. Ukilinganisha uchumi wa Urusi na mataifa ya G7 katika kiwango cha GDP, utaona jinsi ulivyo mdogo. Ila ukiangalia katika kwenye masoko ya kimataifa, na bidhaa anazoziuza unapata taswira nyingine kabisa.


===============================================================
Hebu tuachane na Urusi, tuzungumzie taifa la AUSTRALIA. Ambapo mwaka 2008 wakati wa mtikisiko wa uchumi ulioathiri dunia yote, taifa la Australia peke yake ndiyo halikuathirika na lilipata utajiri mkubwa mno kipindi kile kuliko wakati mwingine wowote ule. Nini, kilichangia hili taifa kutoathirika na mtikisiko, ???

Hebu ndugu zangu wa muda mrefu naowaheshimu sana hapa jukwaani, Chamoto , Drifter, Wyatt Mathewson , na TUJITEGEMEE watusaidie kujibu hii hoja kuhusu AUSTRALIA.

Salama kabisa mkulu. Pia nimefurahi kukuona hapa jukwaani.
Kuhusu suala la Urusi, binafsi naona dunia imeingia kwenye mtego wa marekani na ulimwengu wa magharibi kwa ujumla wa kuamini sana taarifa, tafiti, habari nk kutoka kwao. Magharibi wana uwezo mkubwa sana wa kuiaminisha dunia kwa chochote wanachosema na dunia ikaamini. Mfano, kipindi cha Gulf War miaka ya 2000 mwanzoni kabisa, waliiaminisha dunia kwamba Iraq 🇮🇶 chini ya Saddam wakasema ana biological weapons, sijui nuclear bombs. Kumbe ulikuwa uongo. Vivyo hivyo kwa Syria na Libya. Alisingizia uongo, akaharibu nchi za watu. Leo hii nchi hizo zimebaki mahame. Hazijadhibitiwa mpaka leo. Libya imekuwa pango la wanyang'anyi. Haitawaliki. Lakini hayo yote huwezi yaona kwenye media zao. Wao watawaonesha kitu chenye manufaa kwao. Vilivyo dhidi yao hutaviona. Mfano kwenye mkutano wa Russia - Afrika kina mengi yameongelewa. Kutia ndani uongo wa magharibi wa kutoroshea kwao nafaka zilizokusudiwa ziende sehemu zingine za dunia kutia ndani Afrika. Hilo huwezi kuta likitangazwa na media House zao. Pia cheche walizotema viongozi wa Afrika dhidi ya USA, hutawahi ziona zikitangazwa. Wenyewe wana uwezo mkubwa sana wa kutangaza na kuaminisha mitazamo yao na watu wakaamini.
Ukitaka uwe na balanced view, nenda kaangalie na media stream zingine uone wanongeleaje mambo.
Sijui kama nimejibu swali lako, lkn huo ndiyo mtazamo wangu kuhusu propaganda za ulimwengu wa magharibi.
 
Umeandika mambo mengi sana, lakini jambo muhimu zaidi ni lile la kiuchumi. Wewe kukubali kwamba Marekani hana ABSOLUTE ADVANTAGE. Kiufupi hakuna taifa ambalo ni kisiwa. Hii ndiyo kanuni ya Uchumi, kwamba kuna vitu utaweza, lakini vingine hutaweza. Urusi kutegemea teknolojia ya Magharibi ndiyo uchumi wenyewe, kama alivyosema mchumi nguli David Ricardo, kwenye COMPARATIVE ADVANTAGE THEORY.

Mifano mingi uliyoitoa ni ya kisiasa, hivyo sintaijibu, labda tuanzishe mada yake. Ninachotaka ni tujikite kwenye uchumi, maana uchumi ni sayansi na kama wazungu wasemavyo, MEN LIE BUT NUMBERS DO NOT LIE. Hebu tusaidiane kujibu maswali yafuatayo ambayo yako kwenye uti wa mgongo wa huu mgogoro....

Mosi, nini kimesababisha mfumuko mkubwa wa bei (Inflation) nchi za Magharibi. Unadhani hili tatizo mataifa ya G7 yatalimaliza kwa kupandisha tu thamani ya riba (Hiking Interest Rates) peke yake, bila kutegemea rasilimali za kimkakati kutoka nchi kama Urusi na zile za OPEC, ???

Pili, kwanini nchi za Ulaya kama Ujerumani zimeingia kwenye mdororo mkubwa wa wa Uchumi (Economic Recession) mwaka 2023. Unadhani huu mdororo utaisha hivi karibuni, ???

Tatu, kwanini mabenki ya nchi za Magharibi yameanguka sana mwaka huu, Mabenki zaidi ya 1000 ya Marekani peke yake yako mufilisi (Insolvent). Mara ya mwisho matatizo kama haya yalitokea mwaka 2008. Nini kimepelekea haya mwaka huu, ???

Nne, unadhani G7 wanaweza kupata mbadala wa Urusi kwenye rasilimali na masoko. Kwamba wanaweza kabisa kulitenga soko la Urusi lenye rasilimali za bei rahisi na soko la watu zaidi ya milioni 100, ???

Tano, kwanini Federal Reserve imepandisha riba kutoka 1% hadi 6% ndani ya mwaka, kitu ambacho mara ya mwisho kilifanyika miaka ya 90's, ???

Sita, kwanini mashirika ya nishati ya Urusi yamepata faida kubwa mno mwaka 2022, hadi mengine kutoa gawio (Dividend) mara tatu, ilhali kuna vikwazo vya uchumi dhidi ya Urusi visivyopungua 12,000, ???

Saba, Kwanini Uchumi wa India haujaathirika na mfumuko wa bei kama Ulaya na Marekani, hadi kupelekea IMF kufanya makadirio kwamba uchumi wake utakua kwa asilimia 7% (India has a trade surplus), ???

Nane, kikawaida hakuna uwekezaji unaoaminika kama kwenye masoko ya mitaji na dhamana (Capital Markets) kama ule wa hati-fungani (Bonds). Lakini kwanini kule Ulaya soko la hati-fungani lilianguka vibaya katikati ya mwaka 2022 hadi kufika sasa 2023, ???

Tisa, kwanini serikali nyingi za duniani zikiwemo Marekani na Japani, zimeingia kwenye uchapishaji mkubwa pesa (Money Printing) kupitia mbinu za kibenki kama Quantitative Easing (QE), ili kuweza kukudhi mahitaji ya bajeti zao, ???

Kumi, dola ya Marekani ndiyo fedha ya akiba ya kigeni ya dunia (World's Reserve Currency), ambayo hutumika kwenye mikopo mikubwa, biashara ya kimataifa na uwekezaji. Kwanini tangu mwaka 2022 imapungua thamani ya mzunguko (Dollar's Circulation Volume) kutoka asilimia 75% hadi 55%, jambo ambalo mara ya mwisho kutokea ni mwaka 2001. Hapa namaanisha mpaka sasa, dola ya Marekani inatumika kwa asilimia 55% duniani kote. Nini chanzo cha hali hii kutokea, ???

Nadhani tukiyajibu haya maswali, ndiyo tutaweza kuzungumza hali ya kisiasa na kiulinzi ya duniani kote. Maana uchumi ndiyo uti wa mgongo wa kila kitu duniani. Uchumi umeshikilia na kuathiri moja kwa moja mambo diplomasia, ulinzi, tamaduni na siasa za mataifa. Hebu tujuzane zaidi, nasubiri majawabu ili nijifunze zaidi..

Mkuu umetisha ebu siku Moja tia neno kwenye mkataba wa DPW
 
Ungeanza kunijibu maswali yangu mwanzo kabisa na kitaalamu kama anavyofanya bwana zitto junior ningetoa majawabu ya kila swali ulilouliza. Ila bahati mbaya hujafanya hivyo zaidi ya kuzunguka mbuyu na kuchanganya mambo. Nadhani mimi na wewe tuishie hapa, niendelea kufanya mjadala na Zitto Jr ambaye ni mchomi aliyesomea.
Ha ha haa..

Umenikumbusha kisa Cha Regan,Moi na Auko.
 
Ukweli wa hiyo theory unapimwa kwa impact ya yankiuchumu wa Russia duniani.Mgogoro wa Uchumi unayoikumba Ulaya nzima na USA imetokana na vikwazo vilivyowekwa na wao wenyewe dhidi ya Russia.

Issue ya vikwazo kwa Russia imepelekea kuyumba kwa uchumi wote wa Dunia,hii ni kutokana na ukweli kuwa Russia amesababisha Currency ya USA ($) kuyumba vilevile masoko ya mitaji na dhamana kwenye masoko ya USA na Europe kuyumba-hali iliyopelekea Nchi zote kuyumba kiuchumi.

Asiyelijua hili hana akili na asiyetaka kulikubali basi ubongo wake una kamasi.
👏👏👏👏👏👏👏👏👏🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🙏🙏
 
Watu wanaendeshwa na mihemko kiasi kwamba hata ueezo wa kufikiri unapungua.
Kweli kabisa Mkuu Mwana Taaluma.
Ni tofauti kubwa sana kujua mambo Kwa ukamulifu na kujua mambo Kwa ujanjaujanja.
Hii ndio inawakumba Baadhi ya Pro USA.anaulizwa swali anatoa maelezo meeeengi nje ya mada ili aonekane anajua mambo.
 
Back
Top Bottom