Ha ha haa.
Na Siri kubwa ya wapiga spana wa upande wa wajamaa katika mada hizi za haya yanayotokea ulimwenguni Leo hii ni "ukweli na haki TU".
Daima ukisema ukweli na ukitetea haki unakua unahoja za msingi.
Lakini zaidi ukiseam kweli unakua huru.hawa wanaopingana na ukweli huishi kwa hoja za kubabaisha babaiaha TU.
Na haya ndio yanayowapata pro NATO wengi humu.
Kwahiyo unataka kusema kwamba G7 wangeiwekea vikwazo Urusi kwenye mashine, basi uchumi wa Urusi ungeanguka na wao wenyewe wasingekutwa na madhara yoyote yale, si ndiyo ?
Hii hoja sijaielewa hata kidogo, labda unifafanulie kwa zaidi. Kwamba unataka kusema, Urusi ya kisovieti ilikuwa lilikuwa taifa imara kwasababu ya teknolojia ya Marekani iliyotolewa kule Volgograd? Hivi kuna nchi hapa duniani ambayo imetumia teknolojia yake peke yake kukua ?
Ila nachokishangaa kwenu ni kushindwa kufahamu kwamba, teknolojia zote muhimu ambazo Marekani anazitumia karne ya ishirini na moja siyo zake bali za Ujerumani. Wanasayansi 1500 wa Ujerumani waliopelekwa Marekani na Bwana Allen Dulles kupitia Operation Paperclip, ndiyo walilipa Marekani teknolojia kama Fission-Technology (Atomic), Sonar, Rocket-Science, Genetic-Engineering, Satellite Engineering, n.k
Sasa turudi kwenye uchumi. Tutumia mawazo ya baba wa uchumi wa kibeberu, Bwana Adam Smith. Hivi kuna taifa ambalo lina ABSOLUTE ADVANTAGE kwenye kila kitu hapa duniani ? Kwamba leo hii Marekani anaweza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi mataifa makubwa bila yeye kupata hasara ? Hebu tueleweshane
Unaandika mambo mengi sana. Hapa napo nayaweka mawazo yako katika kurunzi ya kiuchumi. Hivi unahisi taifa la Marekani lina Absolute-Advantage in every sphere of the
economy?
Hii mifano yako inanishangaza kidogo, nadhani hujafanya utafiti wa kutosha kwenye historia ya uchumi wa dunia.
Wasomi wakubwa duniani kama Professor Joseph Nye wanasema kwamba Ujerumani lilikuwa ndiyo taifa tajiri kwenye uzalishaji (World's Largest Manufacturer) kuliko hata Uingereza mnamo mwaka 1900. Kipindi hiki Marekani alikuwa ni taifa tajiri zaidi duniani katika ulinganisho wa manunuzi (Purchasing Power Parity).
Kingine ambacho kinanishangaza ni kwamba unasahau kwamba kabla ya vita ya pili ya dunia, taifa la Japan lilikuwa ni moja kati ya mataifa tajiri duniani. Hizi hoja za kusema kwamba Marekani ndiyo aliwashawishi wajerumani na wajapan wastaarabike ndiyo wakawa matajiri umezitoa wapi ?
Aidha unayaangalia mambo kisiasa, au hujasoma uchumi. Kitaalamu, Marekani lilikuwa taifa tajiri zaidi duniani mwaka 1872 (Gilded Age), lakini siyo katika kipimo cha Gross Domestic Product (GDP). Ukitumia kipimo (Metric) cha GDP, kutoka mwaka 1872 Marekani alikuwa na uchumi mdogo mno kulinganisha na mataifa kama Ufalme wa Uingereza na Ufalme wa Ujerumani.
Kipimo kilichotumika kusema Marekani ndiyo tajiri ni kile cha manunuzi, Purchasing Power Parity (PPP). Nakubaliana na baadhi ya wachumi kwamba GDP ni kipimo sahihi, lakini ukizingatia vipimo vingine kama GNP na PPP utafahamu kwamba kwanini mataifa yenye GDP ndogo kuliko yale ya G7 bado yanafanya vizuri.
Sasa mtaalamu, hebu tufahamishane. Kwamba Marekani na chama chake cha G7 leo hii wanaweza kupambana vita ya kiuchumi na mataifa kama Urusi, OPEC au Uchina bila wao kukumbwa na madhara makubwa kiuchumi ?
Hiyo ni lugha tu ya kiuchumi ila ni mikopo kama mikopo mingine tu ya dollar hasa wakati ambapo Kuna crisis na hizo swap lines hazipo fixed Kuna wakati zinapandishwa or in other cases kuwa limitless kwa mataifa kama Japan au UK.
Na kama ambavyo benki haikopeshi tu Kila mtu hata US haiwezi weka dollar available kwa Kila nchi maana mwisho wa siku default rate inaweza kuwa kubwa hivyo dollar isirudi na interest ama ikaishia mikono mibaya ya competitors.
Pia ni regulations tu maana ukiwa na few people holding more dollars it's easy to monitor kuliko ikiuzwa kiholela huwezi regulate mwisho wa siku Ina back fire.
On the other hand, volume or whatever can be affected by the actual availability ya hizo dollar maana kama nyie mnadai sijui dollar zilichapishwa nyingi kuliko mahitaji kivipi Tena recently kulitokea scarcity ya dollar hapa Tanzania na nchi nyingi duniani kiasi dollar ikawa inauzwa na walanguzi kwa bei ya juu sana cha ajabu mnadai imezidi mahitaji.
Huko duniani kwenye masoko ya mitaji kumekuwa na sintofahamu kubwa sana baada ya shirika la FITCH, linalohusika na CREDIT RATING kulishusha taifa la Marekani kiwango, na kusema kwamba siyo sehemu salama tena kufanya uwekezaji wa mitaji. Serikali ya Marekani imeng'aka na kusema kwamba hizo ni takwimu za uongo na zinalenga kuichafua Marekani.
Janet Yellen kalalama sana na kusema kwamba FITCH wametumia kikokotoo chenye hililfu na kusahau kwamba Marekani ina uchumi imara (A Resilient Economic System). Endapo, FITCH wametoa taarifa ya kweli, basi Marekani itaingia kwenye mtafaruku mkubwa na hata thamani ya hati-fungani zake ishuka, kwasababu mataifa mengi yataacha kuzinunua na kwenda kuwekeza kwingineko. Sababu kubwa ambazo FITCH wamezitoa ni hizi hapa:
1. Bad Governance over the past 20 years.
2. Rising Deficit (Kumbuka US inakusanya Trilioni 4 kwa mwaka, lakini inatumia zaidi ya Trilioni 4)
3. Debt Ceiling (Deni la Marekani ni kubwa na mpaka sasa hakuna makubaliano)
Naamini tulilizungumzia vizuri hili suala majuzi, mimi pamoja na Econometrician tukasema huu mchezo ambao Marekani anaucheza utakuja kumpasukia usoni. Janet Yellen amesema kile ambacho hata wewe ulikisema juzi, American Economic System is still resilient and robust. FITCH wameenda mbali na kusema kwamba ndani ya miaka mitatu ijayo uchumi wa Marekani utaingia kwenye mdororo mkubwa, na kuathiri utekelezwaji wa sera za kiuchumi (Fiscal Policies).
Hapa inamaanisha hivi:
Uchumi ukidorora, wawekezaji watauza madeni ya Marekani ambayo wanayashikilia.
Marekani itabidi ajifunge mkanda na kuanza kulipa riba za madeni yake (To avoid default)
Uchumi ukidorora inamanisha atapunguza matumizi kwenye ulinzi, afya na huduma jamii.
Kiuhalisia, picha imekaa vibaya mno. Wachumi wengi kama Dr Nouriel Roubin a.k.a Dr Doom aliyetabiri anguko la uchumi la mwaka 2008 akiwa kwenye kikao cha IMF lakini akachekwa na wachumi wenzake, alitoa utabiri mwingine mwezi wa February 2023 kuhusu mdororo wa uchumi (Recession) ambao FITCH nao wametabiri kupitia takwimu zao. Kasema hali itakuwa mbaya mno. Haya yote yanaweza kuwa kweli au siyo kweli, maana kitu ambacho nimejifunza ni kwamba uchumi ni kama kiumbe hai unaweza ukageuka muda wowote ule.
Mwisho kabisa, inasemekana mbali na deni la dola za kimarekani Trilioni 31, Marekani ina deni jingine ambalo halijaandikwa (Unfunded Liability) ambalo linafika kiasi cha dola za kimarekani Trilioni 128. Hili deni linatoka kwenye sekta ya Afya (Medicare), Mifuko ya hifadhi (Social Security) na Madawa (Medicare Drugs). Hivi unadhani, hali hii ilivyo, Marekani anaweza kuchomoka, ukizingatia uchumi wa dunia umeingia kwenye korongo ukisababishwa na UVIKO na UVAMIZI WA UKRAINE, ???
1. Kupandisha sana riba (Hiking Interest Rates) hadi kufika 5% na zaidi.
2. Uhaba wa bajeti ya Marekani (Rising Government Deficits)
3. Fedha ya Marekani kuwa ndiyo fedha ya akiba ya dunia (World's Reserve Currency)
4. Mashirika ya Marekani kuanguka na kusababisha matatizo.

Wametabir baada ya miaka mitat us itaingia kwenye mdororo mkubwa
Na us akiingiaga kwenye mdororo benki lazima zifirisike
Sasa najiuliza mim ambae kaamshahara kangu huwa napokea kupitia NMB na huwa sitoi zote nyingine naweka akiba napaswa kuwaamin hawa au nijiongeze nikwanyue zote nianze kuficha mchagon???
Lkn boy hv unajua km dola imeshakuwa adim hapa dar???

Mazee, mambo ni mengi sana. Mdororo ukitokea hata kodi hutakusanya vizuri, hapa kama nchi ina madeni mengi makubwa lazima mtatia akili. Hili la dola nimeliona, ila ngoja nisiliseme, lakini kuna wadau wameshalizungumzia leo kwenye jukwaa la siasa.
Nadharia ya vikwazo vya Uchumi kwa Nchi zinazoitumia zinadhani kwamba Nchi zenye utata nao na wenye nguvu kama Putin watabadilisha sera zao ikiwa watasababishiwa maumivu makali na maumivu ya kutosha yatasababishwa juu ya uchumi wao, na Wananchi wao.
Hata hivyo, historia ya vikwazo vya kiuchumi Duniani inaonyesha kuwa hiili haliwezekani kabisa. Kwa kawaida, nchi zenye nguvu za kiuchumi kama Wananchi wa Urusi hawapigi kelele (they do not protest)kuhusu vikwazo hivyo.
Nchi za Magharibi na vikwazo vyao vya kiuchumi walidhani vikwazo vitaweza kusababisha maumivu dhidi ya uchumi wa Urusi, na watu wake, hatahivyo hawajafanikiwa katika kuwashawishi Wakuu wa Urusi kubadilisha sera zake kutokana na sababu mbalimbali kama vile Urusi kutafuta njia mbadala na udhaifu wa mataifa mengine nyuma ya vikwazo.
Chakula, gesi, mafuta na zana za kijeshi sio vipimo vya uchumi. Hapo Urusi inajitosheleza kwa soko la ndani ila inahitaji pia kuuza nje na kununua nje, mambo inayofanya.
Uwezo wa kiuchumi na ukuaji wake una vipimo vyake. Wanauchumi wangetaja vitu kama GDP, PPP, investments, exports, imports, government expenditure, public consumption na kadhalika.
Mkuu mambo uliyoyataja hayana uhalisia , mtu anaweza KUINGIA kwenye mtandao akaandika chochote na huna namna ya kumpinga. Kama hao Wana GDP. PPP kubwa Kwa nini mafuta yakipunguzwa uzalishaji wanapiga kelele kama nini au kama chakula kikizuiwa kuuzwa wanapiga kelele kama nini! Kama Russia au Ukraine ikigoma kukuuzia chakula utakula hiyo GDP ,PPP au fedha zako? au utatumia hiyo fedha Yako kuendesha gari au ndege Yako badala ya mafuta ? Achana na uchumi hewa wa makaratasi angalia uchumi halisia.
Nimepitia michango mbalimbali ya wachangiaji wengine katika mjadala huu hivyo kwa maoni yangu, nitajikita zaidi katika masuala ambayo hayajaguswa sana ili kuepusha marudio ya michango ya wengine.
Kwanza kabisa, sikubaliani na hoja ya mleta mada kwamba vikwazo havifanyi kazi dhidi ya Urusi. Nitazungumza kwa data na facts!
Kwa mtu ambaye hajasoma uchumi kabisa, kitendo cha Rais Putin wa Urusi kuonekana hadharani ama kwenye vyombo vya habari mara kwa mara akilaani vikwazo ambavyo Urusi imewekewa na nchi za magharibi kinaweza kuwa ni ishara mojawapo kuwa vikwazo vinafanya kazi dhidi ya Urusi.
Kuna wakati yeye mwenyewe amewahi kukiri mbele ya waandishi wa habari kuwepo kwa hatari kutokana na athari za vikwazo vya kiuchumi kwa nchi yake. Kwa anayehitaji ushahidi, huu hapa:
It is noted that now there are new tools to support innovative industries
tass.com
Tuachane na hilo, tuzungumze kiuchumi zaidi!
Suala la kwanza ambayo nitalijadili ni usahihi na kuaminika kwa taarifa zilizopo (Data Integrity):
Kumekuwa na ugumu au changamoto katika upatikanaji wa takwimu sahihi zaidi za kiuchumi kuhusu Urusi hususani mara baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.
Takwimu muhimu za kiuchumi kuhusiana na Urusi zilisitishwa kutolewa hadharani na Urusi yenyewe (serikali) mara tu baada ya uvamizi. Hivyo, makisio mbalimbali ya kiuchumi ambayo yamekuwa yakitolewa baada ya hapo na watafiti ama taasisi mbalimbali duniani kuhusiana na mwenendo wa uchumi wa Urusi yamekuwa yakitegemea data ama taarifa finyu moja kwa moja kutoka the Kremlin ama serikali ya Urusi yenyewe.
Miongoni mwa ripoti ama taarifa za kiuchumi zilizowahi kuzuiliwa na Urusi mara tu baada ya uvamizi wake nchini Ukraine ni pamoja na zifuatazo:
a) Taarifa za biashara za nje/kigeni (all foreign trade statistics) zikiwemo takwimu za manunuzi yote kutoka nje (import) pamoja na zile za mauzo (export).
Miongoni mwa sababu zilizotolewa kwenye vyombo vya habari na Federal Customs Service of Russia, chini ya Wizara ya Fedha ya Urusi, kuhusiana na usitishwaji wa utoaji wa takwimu hizo ni "to exclude errors and speculation". Anayefahamu kiswahili fasaha cha "speculation" anisaidie hapo.
Russia's customs service has decided to temporarily suspend publication of import and export data in order to exclude errors and "speculation", the head of the service said on Thursday.
www.reuters.com
Tunaweza kuziamini hizi sababu ama tunaweza kukataa kukubaliana nazo, ila kwa kifupi tu, hii siyo mara ya kwanza kwa nchi kama Urusi kutoa sababu zenye mashaka-mashaka pale ambapo imeamua kufanya jambo lenye utata. Wakosoaji wengi (wakiwemo wachumi) wameitaja hiyo kama hatua ya makusudi na ya kimkakati yenye lengo la kuficha madhara ya awali ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya Urusi.
Mmoja wa wakosoaji ni mchumi huyu (link hapo chini) kupitia taasisi ya wataalamu (think tank) wa masuala ya kimataifa inayofahamika kama Carnegie Endowment for International Peace. Anasema;
In the four months since it went to war with Ukraine, the Kremlin has blocked public access to an unprecedented volume of economic statistics. Those operating outside the government machine have been left working in the dark, with the quality of independent evaluations and predictions suffering accordingly.
Officially, the statistical blackout is aimed at protecting Russian companies and individuals from Western sanctions. It's more likely, however, that the Kremlin is afraid of publishing data that reveal the full scale of the economy's collapse or the extent of monthly spending on the war. Similarly, it may be concealing the formation of new channels for shadow imports that could be tracked.
b) Takwimu zingine ni za mapato ya mafuta na gesi za kila mwezi.
Suala hili limelazimu tafiti mbalimbali zinazolenga kubaini mauzo halisi ya mafuta na gesi ya Urusi kutegemea zaidi takwimu za wanunuzi ama wateja wa mafuta na gesi kutoka Urusi. Vilevile, makisio mengi yamekuwa yakifanyika kupitia takwimu za mataifa ambayo yamekuwa yakinunua nishati kutoka Urusi (international trade partners).
Nijikite sasa moja kwa moja kwenye hoja/maswali yaliyowasilishwa kama mjadala!
Mosi: Maswali mawili ya kwanza ya mjadala yameambatana na madai kuwa vikwazo havifanyi kazi huku swali la pili likienda mbali zaidi na kudai kuwa mauzo ya nishati ya Urusi yameongezeka zaidi kimapato kuliko kipindi kingine chochote.
Kwa mujibu wa mleta mada, makampuni ya Urusi ya nishati ndiyo yameongoza duniani kwa kuuza na kupata faida zaidi kwenye nishati huku chanzo cha "takwimu" kikitajwa kuwa ni Marekani in general bila hata ya kutaja chanzo mahususi wala ambatanisho lolote lile lenye takwimu husika.
Nitaweka takwimu na vyanzo vyangu kadhaa ili kuipinga hoja hizo!
Bidhaa ama commodity inayoongoza kwa kuipatia Urusi mapato mengi zaidi kuliko bidhaa nyingine yoyote ile ni mafuta kwa maana ya crude oil and petroleum products. Kwa mujibu wa takwimu za Trading Economics na Benki Kuu ya Urusi, mauzo makuu ya nje ya Urusi ni mafuta na bidhaa za nishati ambazo ni asilimia takribani 63 ya mauzo yote ya nje, ambapo kwa mafuta pekee ni asilimia 26 ya bajeti ya Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine.
Exports in Russia decreased to 31291 USD Million in December from 31956 USD Million in November of 2024. This page provides - Russia Exports - actual values, historical data, forecast, chart, statistics, economic calendar and news.
tradingeconomics.com
Tukiachana na hilo, nitajikita kwenye uthabiti ama validity ya hoja zilizowasilishwa, kitu ambacho niligusia kidogo katika post yangu iliyopita.
Moja ya taasisi mashuhuri duniani za masuala ya utafiti katika sekta ya nishati inayofahamika kama International Energy Agency (IEA) hutoa mara kwa mara ripoti mbalimbali zinazohusu soko la nishati la kimataifa ikiwemo Urusi.
Ukifuatilia ripoti za IEA za baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kiasi cha mauzo ya Urusi ya mafuta (quantity) kimekuwa kikiongezeka katika miezi ya hivi karibuni na kufikia kiwango cha juu zaidi kuliko miezi ya mwanzoni baada ya uvamizi. Lakini, ongezeko hilo haliakisi mapato yanayopatikana ukilinganisha na mapato yaliyokuwa yakipatikana kila mwezi kabla ya uvamizi. Kuna mambo mawili tofauti hapo:
a) Kiasi cha mauzo (volume/quantity).
b) Mapato yatokanayo na mauzo yenyewe (revenue).
Kabla ya kwenda mbali zaidi, hii hapa chini ni ripoti ya kiasi cha mauzo ukilinganisha na mapato yaliyopatikana kuanzia mwezi Mei mwaka 2022 hadi Aprili 2023:
Chanzo: Euronews, IEA.
Ukiachana na hiyo, nimeambatanisha link yenye ripoti nyingine ya soko la mafuta duniani. Hii ni mpya ama ya kipindi cha karibuni zaidi (Julai 2023).
Oil Market Report - July 2023 - Analysis and key findings. A report by the International Energy Agency.
www.iea.org
Kwa ambao hawawezi kuingia katika hiyo link, taarifa fupi ya mauzo ya Urusi ya mwezi Juni inasema hivi, nanukuu;
Russian oil exports fell 600 kb/d to 7.3 mb/d in June, their lowest since March 2021. Estimated export revenues plunged by $1.5 bn to $11.8 bn – nearly half the levels of a year ago.
Kwa kiswahili:
Mauzo ya mafuta ya Urusi yalishuka kwa kiasi cha mapipa laki sita kwa siku, hivyo kufikia mapipa milioni 7.3 kwa siku mwezi Juni, kikiwa ni kiwango cha chini zaidi tangu mwezi Machi 2021. Makadirio ya mapato ya mauzo ya nje yalishuka kwa kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.5, hivyo kufikia dola za kimarekani bilioni 11.8 - ambayo ni karibu nusu ya viwango vya mwaka mmoja uliopita.
Mwisho wa kunukuu!
Ukizisoma ripoti hizo za IEA, moja ya sababu za kupungua kwa mapato ya mafuta ukilinganisha na kiasi cha mauzo ni kutokana na kwamba Urusi imekuwa ikiuza nishati hiyo kwa punguzo kubwa la bei ama discount kwenda kwa nchi kama China na India mara baada ya lililokuwa soko lao kubwa la mafuta (EU) kupunguza manunuzi kwa kiasi kikubwa. Hivyo, Urusi imekuwa ikizidisha uzalishaji wa mafuta ili iyauze kufidia upungufu wa mapato ambayo ilikuwa ikiyapata kabla ya uvamizi.
Tukiachana na IEA, kuna taasisi nyingine maarufu ya utafiti wa nishati inayofahamika kama Centre for Research on Energy and Clean Air (CREA) ambayo nayo pia hutoa ripoti za mara kwa mara za masuala ya nishati duniani.
Nimeambatanisha hapo chini ripoti yao ya mwezi June mwaka 2023 yenye takwimu za mauzo ya kuanzia Januari 2022, ambazo zinaonesha kushuka kwa mapato ya mauzo ya nje ya nishati ya Urusi ambapo mauzo yalifikia bei ya chini zaidi ya kila mwezi tangu mwanzo wa uvamizi.
Mpaka hapo, sijafahamu bado mahali ambapo mleta mada umetolea takwimu zako. Kama ni Marekani, hata ukipitia takwimu za watoa takwimu wengine maarufu na wa kuaminika kama S&P Global kutoka Marekani hiyohiyo, hawakubaliani na wewe.
Hivyo basi, kwa mujibu wa takwimu zote ambazo nimezileta hapa, naweza kusema kwamba, maswali mawili ya kwanza ya mleta mada wetu (hasa lile la pili) hayako sahihi hata kidogo.
Pili: Swali la mwisho linazungumzia mustakabali wa uchumi wa Urusi baada ya vikwazo. Swali hilo vilevile limejengwa katika msingi wa hoja ileile yenye makosa, kwamba kwa sasa "vikwazo havifanyi kazi". Mwishoni kabisa kuna swali dogo ama la nyongeza linalouliza kwamba: "Mataifa ya magharibi yamefanikiwa au tuendelee kusubiri?".
Maoni yangu juu ya swali hilo fupi ni kama yafuatavyo:
Ili tujue kama mataifa ya magharibi yamefanikiwa ama kinyume chake, inatupasa tujue malengo ya vikwazo hivyo yalikuwa nini. Tatizo kubwa lililopo ni kuwa, aliyeweka hivyo vikwazo ndiye pekee anayejua zaidi malengo ya kufanya hivyo, sisi wengine tunabaki kufanya speculations tu. Aisee, anayefahamu kiswahili fasaha cha "speculation" anisaidie na hapo kwa mara nyingine!
Vilevile, hapa kuna mambo mawili:
a) Kufanikiwa
b) Kufanya kazi
Kidokezo:
Dozi ya dawa ya siku 10 inaweza kuanza kufanya kazi dhidi ya ugonjwa siku ya kwanza kabisa ila ikafanikiwa kutibu ugonjwa kikamilifu siku ya mwisho wa dozi.
Sasa, kwa mujibu wa Baraza la Umoja wa Ulaya kupitia website yao rasmi (Council of the EU and the European Council):
The aim of the economic sanctions is to impose severe consequences on Russia for its actions and to effectively thwart Russian abilities to continue the aggression.
Ukiendelea kusoma hayo maelezo yaliyomo kwenye website yao, kuna masuala kama:
a) Aina za vikwazo vilivyowekwa na vitakavyowekwa.
b) Walengwa na wasio walengwa wa vikwazo (hapa kuna vikwazo dhidi ya sekta, taasisi pamoja na watu binafsi akiwemo Putin).
c) Maana ya vikwazo vilivyowekwa na namna vikwazo vinatekelezwa.
d) Masuala ya kisheria (uhalali ama legality ya vikwazo).
e) Namna za kudhibiti ama kukabiliana na ukiukwaji wa vikwazo.
Na mengine mengi!
Tukirudi katika lengo au malengo ya vikwazo kwa mujibu wa EU, masuala makubwa yanayozungumziwa ni mawili, ambayo ni: "to impose severe consequences" pamoja na "to effectively thwart Russian abilities to continue the aggression".
Kwa kuchunguza kwangu, sijaona mahali panaposema kwamba lengo ni "kuhakikisha uchumi wa Urusi unaanguka ndani ya wiki chache". Nilichokiona ni mpango mkakati ambao ni endelevu wenye lengo la kutoa adhabu kali yenye madhara makubwa na pia kuzuia kwa ufanisi uwezo wa Urusi kuendelea na uvamizi wake.
Tukirejea katika takwimu za kiuchumi ambazo nimezileta hapa, tayari madhara yameshaonekana katika mapato ya bidhaa muhimu zaidi ama bidhaa kubwa zaidi inayosimamia ama inayoendesha uchumi wa Urusi. Hapo nimezungumzia mafuta pekee, bado kuna sekta nyingine nyingi za kiuchumi ambazo zimeshapata madhara yatokanayo na vikwazo. Madhara ambayo wachangiaji wengine wameshaeleza vizuri kabisa.
Hivyo, siyo suala la kusubiri matokeo ama utendaji kazi wa vikwazo mpaka hapo baadaye bali tayari hivi sasa matokeo au madhara ya vikwazo yameshaanza kuonekana ingawa lengo la kuzuia kwa ufanisi uwezo wa Urusi kuendelea na uvamizi wake bado halijatimia.
Huo ndio mchango wangu kwa sasa. Nitachangia zaidi baadaye pale ambapo nitapata muda wa kufanya hivyo. Asante!
CC: @Proved, @The Boy Wonder, @zitto junior, @T14 Armata, @dong yi, @Chenchele, @Econometrician, pamoja na wengine katika mjadala wakiwemo wasiochangia chochote

Kabla ya kwenda mbali zaidi, hii hapa chini ni ripoti ya kiasi cha mauzo ukilinganisha na mapato yaliyopatikana kuanzia mwezi Mei mwaka 2022 hadi Aprili 2023: View attachment 2708547
Chanzo: Euronews, IEA.
Ukiachana na hiyo, nimeambatanisha link yenye ripoti nyingine ya soko la mafuta duniani. Hii ni mpya ama ya kipindi cha karibuni zaidi (Julai 2023).
Oil Market Report - July 2023 - Analysis and key findings. A report by the International Energy Agency.
www.iea.org
Kwa ambao hawawezi kuingia katika hiyo link, taarifa fupi ya mauzo ya Urusi ya mwezi Juni inasema hivi, nanukuu;
Russian oil exports fell 600 kb/d to 7.3 mb/d in June, their lowest since March 2021. Estimated export revenues plunged by $1.5 bn to $11.8 bn – nearly half the levels of a year ago.
Kwa kiswahili:
Mauzo ya mafuta ya Urusi yalishuka kwa kiasi cha mapipa laki sita kwa siku, hivyo kufikia mapipa milioni 7.3 kwa siku mwezi Juni, kikiwa ni kiwango cha chini zaidi tangu mwezi Machi 2021. Makadirio ya mapato ya mauzo ya nje yalishuka kwa kiasi cha dola za kimarekani bilioni 1.5, hivyo kufikia dola za kimarekani bilioni 11.8 - ambayo ni karibu nusu ya viwango vya mwaka mmoja uliopita.
Mwisho wa kunukuu!
Ukizisoma ripoti hizo za IEA, moja ya sababu za kupungua kwa mapato ya mafuta ukilinganisha na kiasi cha mauzo ni kutokana na kwamba Urusi imekuwa ikiuza nishati hiyo kwa punguzo kubwa la bei ama discount kwenda kwa nchi kama China na India mara baada ya lililokuwa soko lao kubwa la mafuta (EU) kupunguza manunuzi kwa kiasi kikubwa. Hivyo, Urusi imekuwa ikizidisha uzalishaji wa mafuta ili iyauze kufidia upungufu wa mapato ambayo ilikuwa ikiyapata kabla ya uvamizi.
Tukiachana na IEA, kuna taasisi nyingine maarufu ya utafiti wa nishati inayofahamika kama Centre for Research on Energy and Clean Air (CREA) ambayo nayo pia hutoa ripoti za mara kwa mara za masuala ya nishati duniani.
Nimeambatanisha hapo chini ripoti yao ya mwezi June mwaka 2023 yenye takwimu za mauzo ya kuanzia Januari 2022, ambazo zinaonesha kushuka kwa mapato ya mauzo ya nje ya nishati ya Urusi ambapo mauzo yalifikia bei ya chini zaidi ya kila mwezi tangu mwanzo wa uvamizi.
Mpaka hapo, sijafahamu bado mahali ambapo mleta mada umetolea takwimu zako. Kama ni Marekani, hata ukipitia takwimu za watoa takwimu wengine maarufu na wa kuaminika kama S&P Global kutoka Marekani hiyohiyo, hawakubaliani na wewe.
Hivyo basi, kwa mujibu wa takwimu zote ambazo nimezileta hapa, naweza kusema kwamba, maswali mawili ya kwanza ya mleta mada wetu (hasa lile la pili) hayako sahihi hata kidogo.
Pili: Swali la mwisho linazungumzia mustakabali wa uchumi wa Urusi baada ya vikwazo. Swali hilo vilevile limejengwa katika msingi wa hoja ileile yenye makosa, kwamba kwa sasa "vikwazo havifanyi kazi". Mwishoni kabisa kuna swali dogo ama la nyongeza linalouliza kwamba: "Mataifa ya magharibi yamefanikiwa au tuendelee kusubiri?".
Maoni yangu juu ya swali hilo fupi ni kama yafuatavyo:
Ili tujue kama mataifa ya magharibi yamefanikiwa ama kinyume chake, inatupasa tujue malengo ya vikwazo hivyo yalikuwa nini. Tatizo kubwa lililopo ni kuwa, aliyeweka hivyo vikwazo ndiye pekee anayejua zaidi malengo ya kufanya hivyo, sisi wengine tunabaki kufanya speculations tu. Aisee, anayefahamu kiswahili fasaha cha "speculation" anisaidie na hapo kwa mara nyingine!
Vilevile, hapa kuna mambo mawili:
a) Kufanikiwa
b) Kufanya kazi
Kidokezo:
Dozi ya dawa ya siku 10 inaweza kuanza kufanya kazi dhidi ya ugonjwa siku ya kwanza kabisa ila ikafanikiwa kutibu ugonjwa kikamilifu siku ya mwisho wa dozi.
Sasa, kwa mujibu wa Baraza la Umoja wa Ulaya kupitia website yao rasmi (Council of the EU and the European Council):
The aim of the economic sanctions is to impose severe consequences on Russia for its actions and to effectively thwart Russian abilities to continue the aggression.
Ukiendelea kusoma hayo maelezo yaliyomo kwenye website yao, kuna masuala kama:
a) Aina za vikwazo vilivyowekwa na vitakavyowekwa.
b) Walengwa na wasio walengwa wa vikwazo (hapa kuna vikwazo dhidi ya sekta, taasisi pamoja na watu binafsi akiwemo Putin).
c) Maana ya vikwazo vilivyowekwa na namna vikwazo vinatekelezwa.
d) Masuala ya kisheria (uhalali ama legality ya vikwazo).
e) Namna za kudhibiti ama kukabiliana na ukiukwaji wa vikwazo.
Na mengine mengi!
Tukirudi katika lengo au malengo ya vikwazo kwa mujibu wa EU, masuala makubwa yanayozungumziwa ni mawili, ambayo ni: "to impose severe consequences" pamoja na "to effectively thwart Russian abilities to continue the aggression".
Kwa kuchunguza kwangu, sijaona mahali panaposema kwamba lengo ni "kuhakikisha uchumi wa Urusi unaanguka ndani ya wiki chache". Nilichokiona ni mpango mkakati ambao ni endelevu wenye lengo la kutoa adhabu kali yenye madhara makubwa na pia kuzuia kwa ufanisi uwezo wa Urusi kuendelea na uvamizi wake.
Tukirejea katika takwimu za kiuchumi ambazo nimezileta hapa, tayari madhara yameshaonekana katika mapato ya bidhaa muhimu zaidi ama bidhaa kubwa zaidi inayosimamia ama inayoendesha uchumi wa Urusi. Hapo nimezungumzia mafuta pekee, bado kuna sekta nyingine nyingi za kiuchumi ambazo zimeshapata madhara yatokanayo na vikwazo. Madhara ambayo wachangiaji wengine wameshaeleza vizuri kabisa.
Hivyo, siyo suala la kusubiri matokeo ama utendaji kazi wa vikwazo mpaka hapo baadaye bali tayari hivi sasa matokeo au madhara ya vikwazo yameshaanza kuonekana ingawa lengo la kuzuia kwa ufanisi uwezo wa Urusi kuendelea na uvamizi wake bado halijatimia.
Huo ndio mchango wangu kwa sasa. Nitachangia zaidi baadaye pale ambapo nitapata muda wa kufanya hivyo. Asante!
Huko duniani kwenye masoko ya mitaji kumekuwa na sintofahamu kubwa sana baada ya shirika la FITCH, linalohusika na CREDIT RATING kulishusha taifa la Marekani kiwango, na kusema kwamba siyo sehemu salama tena kufanya uwekezaji wa mitaji. Serikali ya Marekani imeng'aka na kusema kwamba hizo ni takwimu za uongo na zinalenga kuichafua Marekani.
Janet Yellen kalalama sana na kusema kwamba FITCH wametumia kikokotoo chenye hililfu na kusahau kwamba Marekani ina uchumi imara (A Resilient Economic System). Endapo, FITCH wametoa taarifa ya kweli, basi Marekani itaingia kwenye mtafaruku mkubwa na hata thamani ya hati-fungani zake ishuka, kwasababu mataifa mengi yataacha kuzinunua na kwenda kuwekeza kwingineko. Sababu kubwa ambazo FITCH wamezitoa ni hizi hapa:
1. Bad Governance over the past 20 years.
2. Rising Deficit (Kumbuka US inakusanya Trilioni 4 kwa mwaka, lakini inatumia zaidi ya Trilioni 4)
3. Debt Ceiling (Deni la Marekani ni kubwa na mpaka sasa hakuna makubaliano)
Naamini tulilizungumzia vizuri hili suala majuzi, mimi pamoja na Econometrician tukasema huu mchezo ambao Marekani anaucheza utakuja kumpasukia usoni. Janet Yellen amesema kile ambacho hata wewe ulikisema juzi, American Economic System is still resilient and robust. FITCH wameenda mbali na kusema kwamba ndani ya miaka mitatu ijayo uchumi wa Marekani utaingia kwenye mdororo mkubwa, na kuathiri utekelezwaji wa sera za kiuchumi (Fiscal Policies).
Hapa inamaanisha hivi:
Uchumi ukidorora, wawekezaji watauza madeni ya Marekani ambayo wanayashikilia.
Marekani itabidi ajifunge mkanda na kuanza kulipa riba za madeni yake (To avoid default)
Uchumi ukidorora inamanisha atapunguza matumizi kwenye ulinzi, afya na huduma jamii.
Kiuhalisia, picha imekaa vibaya mno. Wachumi wengi kama Dr Nouriel Roubin a.k.a Dr Doom aliyetabiri anguko la uchumi la mwaka 2008 akiwa kwenye kikao cha IMF lakini akachekwa na wachumi wenzake, alitoa utabiri mwingine mwezi wa February 2023 kuhusu mdororo wa uchumi (Recession) ambao FITCH nao wametabiri kupitia takwimu zao. Kasema hali itakuwa mbaya mno. Haya yote yanaweza kuwa kweli au siyo kweli, maana kitu ambacho nimejifunza ni kwamba uchumi ni kama kiumbe hai unaweza ukageuka muda wowote ule.
Mwisho kabisa, inasemekana mbali na deni la dola za kimarekani Trilioni 31, Marekani ina deni jingine ambalo halijaandikwa (Unfunded Liability) ambalo linafika kiasi cha dola za kimarekani Trilioni 128. Hili deni linatoka kwenye sekta ya Afya (Medicare), Mifuko ya hifadhi (Social Security) na Madawa (Medicare Drugs). Hivi unadhani, hali hii ilivyo, Marekani anaweza kuchomoka, ukizingatia uchumi wa dunia umeingia kwenye korongo ukisababishwa na UVIKO na UVAMIZI WA UKRAINE, ???
1. Kupandisha sana riba (Hiking Interest Rates) hadi kufika 5% na zaidi.
2. Uhaba wa bajeti ya Marekani (Rising Government Deficits)
3. Fedha ya Marekani kuwa ndiyo fedha ya akiba ya dunia (World's Reserve Currency)
4. Mashirika ya Marekani kuanguka na kusababisha matatizo.
Huko duniani kwenye masoko ya mitaji kumekuwa na sintofahamu kubwa sana baada ya shirika la FITCH, linalohusika na CREDIT RATING kulishusha taifa la Marekani kiwango, na kusema kwamba siyo sehemu salama tena kufanya uwekezaji wa mitaji. Serikali ya Marekani imeng'aka na kusema kwamba hizo ni takwimu za uongo na zinalenga kuichafua Marekani.
Janet Yellen kalalama sana na kusema kwamba FITCH wametumia kikokotoo chenye hililfu na kusahau kwamba Marekani ina uchumi imara (A Resilient Economic System). Endapo, FITCH wametoa taarifa ya kweli, basi Marekani itaingia kwenye mtafaruku mkubwa na hata thamani ya hati-fungani zake ishuka, kwasababu mataifa mengi yataacha kuzinunua na kwenda kuwekeza kwingineko. Sababu kubwa ambazo FITCH wamezitoa ni hizi hapa:
1. Bad Governance over the past 20 years.
2. Rising Deficit (Kumbuka US inakusanya Trilioni 4 kwa mwaka, lakini inatumia zaidi ya Trilioni 4)
3. Debt Ceiling (Deni la Marekani ni kubwa na mpaka sasa hakuna makubaliano)
Naamini tulilizungumzia vizuri hili suala majuzi, mimi pamoja na Econometrician tukasema huu mchezo ambao Marekani anaucheza utakuja kumpasukia usoni. Janet Yellen amesema kile ambacho hata wewe ulikisema juzi, American Economic System is still resilient and robust. FITCH wameenda mbali na kusema kwamba ndani ya miaka mitatu ijayo uchumi wa Marekani utaingia kwenye mdororo mkubwa, na kuathiri utekelezwaji wa sera za kiuchumi (Fiscal Policies).
Hapa inamaanisha hivi:
Uchumi ukidorora, wawekezaji watauza madeni ya Marekani ambayo wanayashikilia.
Marekani itabidi ajifunge mkanda na kuanza kulipa riba za madeni yake (To avoid default)
Uchumi ukidorora inamanisha atapunguza matumizi kwenye ulinzi, afya na huduma jamii.
Kiuhalisia, picha imekaa vibaya mno. Wachumi wengi kama Dr Nouriel Roubin a.k.a Dr Doom aliyetabiri anguko la uchumi la mwaka 2008 akiwa kwenye kikao cha IMF lakini akachekwa na wachumi wenzake, alitoa utabiri mwingine mwezi wa February 2023 kuhusu mdororo wa uchumi (Recession) ambao FITCH nao wametabiri kupitia takwimu zao. Kasema hali itakuwa mbaya mno. Haya yote yanaweza kuwa kweli au siyo kweli, maana kitu ambacho nimejifunza ni kwamba uchumi ni kama kiumbe hai unaweza ukageuka muda wowote ule.
Mwisho kabisa, inasemekana mbali na deni la dola za kimarekani Trilioni 31, Marekani ina deni jingine ambalo halijaandikwa (Unfunded Liability) ambalo linafika kiasi cha dola za kimarekani Trilioni 128. Hili deni linatoka kwenye sekta ya Afya (Medicare), Mifuko ya hifadhi (Social Security) na Madawa (Medicare Drugs). Hivi unadhani, hali hii ilivyo, Marekani anaweza kuchomoka, ukizingatia uchumi wa dunia umeingia kwenye korongo ukisababishwa na UVIKO na UVAMIZI WA UKRAINE, ???
1. Kupandisha sana riba (Hiking Interest Rates) hadi kufika 5% na zaidi.
2. Uhaba wa bajeti ya Marekani (Rising Government Deficits)
3. Fedha ya Marekani kuwa ndiyo fedha ya akiba ya dunia (World's Reserve Currency)
4. Mashirika ya Marekani kuanguka na kusababisha matatizo.
Nimepitia michango mbalimbali ya wachangiaji wengine katika mjadala huu hivyo kwa maoni yangu, nitajikita zaidi katika masuala ambayo hayajaguswa sana ili kuepusha marudio ya michango ya wengine.
Tuachane na hilo, tuzungumze kiuchumi zaidi!
Suala la kwanza ambayo nitalijadili ni usahihi na kuaminika kwa taarifa zilizopo (Data Integrity):
Kumekuwa na ugumu au changamoto katika upatikanaji wa takwimu sahihi zaidi za kiuchumi kuhusu Urusi hususani mara baada ya uvamizi wake nchini Ukraine.
Takwimu muhimu za kiuchumi kuhusiana na Urusi zilisitishwa kutolewa hadharani na Urusi yenyewe (serikali) mara tu baada ya uvamizi. Hivyo, makisio mbalimbali ya kiuchumi ambayo yamekuwa yakitolewa baada ya hapo na watafiti ama taasisi mbalimbali duniani kuhusiana na mwenendo wa uchumi wa Urusi yamekuwa yakitegemea data ama taarifa finyu moja kwa moja kutoka the Kremlin ama serikali ya Urusi yenyewe.
Mchumi mimi nimekusoma na nimekuelewa sana sanaaa tu. Ila nina mambo 3 tu:
Mosi, Suala zima la takwimu: Sasa naomba unisaidie zaidi kuelewa, INTERNATIONAL MONETARY FUND (IMF), tarehe 25 July walitoa takwimu zao ambazo zimerekebisha makadirio ya uchumi wa Urusi (Estimates) na kusema kwamba uchumi wa Urusi utakuwa kwa asilimia 1.5% kwa mwaka 2023 kutoka 0.7%.
Kumbuka, mwaka 2022 IMF walisema uchumi wa Urusi ungesinyaa (Contraction) kwa asilimia 12% kwa mwaka 2022, lakini kufika mwezi wa September wakarekebisha tena na kusema ungesinayaa kwa asilimia 2.1% tu. World Bank wamesema uchumi wa Urusi utakuwa kwa kasi chanya, japo kiwastani (Positive but modest growth) kwa asilimia 1.2% ifikapo mwaka 2024.
Lakini hebu tuzingatia takwimu basi, mtandao wa CIA unasema kwamba, mwaka 2021 kabla ya vita GDP (Purchasing Power Parity) ya Urusi ilikuwa ni USD Trilion 4, na baada ya vita wakasema ingeshuka hadi kufika USD Trilion 3.9. Ila katika kufunga mwaka 2022 IMF wakasema GDP (In Purchasing Power Parity) ya Urusi imefika USD Trilioni 5.51 ambayo ni kubwa kuliko Ujerumani ambayo ni USD Trilioni 5. Mtandao wa CIA, unasema hivi:
Hii ni mwaka 2021, na ila sasa WB na IMF wanasema mwaka 2022 imefikia USD 5.51 Trilion. Sasa nachoomba kufahamu ni hiki, umezungumzia, DATA INTEGRITY, ila hizi takwimu zimetolewa na IMF na WB, je tusizitegemee na kuziamini kwasababu zimetolewa na Urusi yenyewe, ???
Pili, nimesoma makala ya, The Wall Street Journal, la tarehe 2 AUGUST 2023, kwenye kichwa cha habari kisemacho hivi "The West Attacked Russia's Economy. The Result is Another Stalemate" waandishi ni Alan Cullison na Georgi Kantshev. Ndani ya hii makala amehojiwa mchumi nguli, Prof Nicholas Mulder ambaye amebobea katika vikwazo vya uchumi amesema haya yafuatayo:
Kwenye makala hiyohiyo, wanawanukuu wachumi wa The Carnegie Center ambao wanasema Urusi imepata faida ya ziada (Trade Surplus) mwaka 2022. Maneno yao ni haya hapa, naomba niyaweke tuyasome wote:
Hapa naomba nieleweshwe kiuchumi. Wachumi wanaposema, (A country has a trade-surplus in current account) huwa wanamaanisha nini kitalaamu, ???
Tatu, umesema lengo la vikwazo ni kuzuia uchumi wa nchi ya Urusi kuweza kuendesha vita vya uvamizi dhidi ya Ukraine. Katika maana nyingine wanachotaka ni kuufanya Uchumi wa Urusi uweze kudorora kwa muda mrefu. WB na IMF watoa takwimu zao za National Development Outlook, ambazo baadhi ya takwimu zake zipo hapo juu. Kiuchumi naomba nieleweshwe, kwasasa taifa la Urusi lipo sehemu gani kiuchumi kati ya hizi mbili:
Is Russian Economy facing a recession, ???
Is Russian Economy facing a Soft Landing, ???
At what point can we say, Russia is facing a recession or a soft-landing, ???
Vipi, mchumi umesoma taarifa ya Fitch niliyokuwekea hapa juzi kuhusu fedha ya Marekani na hali yake iliyopo. AU Fitch nao wamekosea, hawajachambua vizuri uchumi wa Marekani kama anavyosema, Janet Yellen, ???
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.