Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Huu mchezo pia umeingizwa kwenye kuibeba ccm ili ionekane inakubalika, matokeo yake ndio tunaona ccm isiyoweza kujenga hoja wala kushindana kisiasa zaidi ya kutegemea kupita bila kupingwa!
Tumuombe Mungu tu huyu incompetent person azidi kuwa mzima yawezekana ameletwa na Mungu ili atuondolee hili jini linaloitwa ccm
 
Mzee Mwanakijiji,
Magufuli ndo tatizo sasa nikwambie..

Ufufuaji wa shirika ulipaswa uendane na mafunzo kwa wafanyakazi, wakiwemo Wahudumu wa ndege, pamoja na kulipa mishahara mizuri...

Sasa hayo yote Rais kashikilia hataki yafanyike unataka Wafanyakazi - akiwemo na Waziri - waje na mwujiza upi???

Magu ndo tatizo la msingi nchi hii, endeleeni kuota!
 
Yeye si ndio kila kitu , wanafata maelekezo yake. Hivi ile route ya Mpanda aliyoamuru ianze imeshaanza?

Jack of all trade, master of everything.
Jack Of all trades, Master Of none🤣
 
Kwa vile ameweka hela nyingi sana humo labda ni muhimu kwa yeye kufuatilia hadi departure?
Kwa kuwa anajua kila kitu,kiongozi wa malaika huyu.Tanzania tuna mambo mengi ya kuonesha duniani hapa. inasemekana binadamu wa kwanza aliishi Tanzania, sasa mwanadamu wa kwanza kuongoza malaika anatarajiwa kutokea Tz.sasa sijui mambo mengine kama haya ya uendeshaji wa ATc tunakwama wapi
 
Mzee Mwanakijiji, Hebu kuwa serious kidogo,kweli hiyo changamoto unataka waziri aende kuipatia ufumbuzi.

Aisee,kweli uzee kwa wengine huwa shida.

Hebu kaitazame organization structure kisha rudi utuambie.

ATCL ukiona hivyo yawezakuwepo mengi yanafichika na hayasemwe kulinda vibarua vya watu.

Utampeleka punda mtoni lakini sio kumlazimisha anywe maji.

Rais Magufuli ametimiza sehemu yake na kuwaweka watendaji,kama wataliua tena hilo shirika watapa kitakachowastahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nauliza, lini au kwa shirika lipi la umma Watanzania tuliweza?


Talk is cheap.
Swali zuri, tutajiwe ili mashirika mengine yakaige mfano.
Tuache huu usani wa gawio, kwamba eti shirika linapanga foleni kwa mbwembwe kupeleka cheque ya gawio la mabilioni kwa Rais ili isemwe kuwa toka Uhuru halijawahi kutoa gawio bali awamu ta tano wameweza huku nyuma Tanesco wanataka kuwasitishia huduma kwa kushindwa kulipa bili ya mamilioni.
Usanii tupu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya mambo yanatushinda Watanzania (inawezekana Waafrika wote), ni usimamizi na uendeshaji endelevu...

Mfano mdogo tu wa mradi mwepesi uliotushinda ni usimamizi wa yale mabasi wanayoyaita yanaenda kasi...

Huwa najiuliza, kama kamradi kadogo tu kama hako na ndio kwanza kapo sijui phase 1, tunataabika kukaendesha, vipi miradi mikubwa kama SGR na safari za ndege?
 
Mzee Mwanakijiji, Acha kujitia Ujinga na Upofu...Akili za Kamwele ndio za Magu. hakuna jipya wala usisingizie lawama watu..,.

Magu na midege alikuwa anatafuta sifa tu, ukweli uwezo wa kuliendesha shirika na huduma zake ni mkurupuko tu wa kutafuta sifa.

Subiri hasara ya kuliendesha hilo Shirika uje ulielie hapa jamvini.. Unafiki ni mbaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JIWE ndio kila kitu hapo ATCL.

Hao wengine hapo ATCL ni pazia.

Ndio maana:

1. Manunuzi anafanya kwa mkono wake ( huku tukichekelea kama mabolizozo )

2. Anachukua ndege yoyote wakati wowote kumpeleka Chato ( Haijalishi kama ilikuwa na route kibiashara )

3. Anatoa maagizo kwa mdomo wake ya kupanga route na sometimes NAULI ( Refer: Mpanda Route na kubeba wajumbe wa CCM BURE kutoka Mwanza )

4. Ameua ushindani

5. Pesa kidogo wanayokusanya ATCL badala ya kuboresha huduma, wanampelekea yeye ( eti Gawio ) mbele ya makamera kibao. Ili ionekane anapata sana pesa kuliko waliomtangulia

6. Wakati yote hayo yakitokea, kwasababu MIJITU MYEUSI UNAFIKI kwetu DAMU DAMU tunatafuta mtu wa kumtupia LAWAMA.

Tena utatusikia tunasema kabisa 'Rais ana nia nzuri ila wasaidizi wake ndio wanamwangusha, hata kama maamuzi fyongo aliyafanya mwemyewe mbele ya TV.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu,nakupa mfano mmoja tu kukuonyesha ATCL ni dude la kuleta hasara na aibu..
Ona juzi Magufuli ameitisha Ndege ya ATCL Airbus inayochukua abiria 150+ imfate yeye pale Chato wakati anarejea Dar kutoka likizo..!!

Hawakupanda hata watu 20 mle ukichanganya na wahudumu wa Ndege..
Hapo amedisturb route ngapi za kubeba abiria wa ATCL??

Mind u.. na serikali ina Ndege zake ambazo zingeweza kumfata huko Chato.
Naomba nijibu.
 
Kwa ile income statement yao

Kila sh 1 ya faida mishahara na admin cost inachukua cent 67

Kila sh 1 ya faida direct costs zingine ni cent 78

Inamaa kwenye kila shilingi 1 wanayotengeza kutokana gharama za uendeshaji wana hasara ya cent 48 just to break even, atuja fikiria ata faida.

Wangelikuwa wafanya biashara wangekuwa wanaongea mambo restructuring kupunguza hizo gharama au wanaongelea income forecast zao kutokana na ndege walizopewa lini wanatarajia ku break even katika maelezo ya directors report to justify costs zao za sasa.

Ndio kwanza wanalalama ukubwa wa current liabilities at 177bn ambazo awajui wanazikamata vipi. Sijui wanatafuta route za ndege etc with nonsense.

Kuamini ATCL itafanikiwa chini ya management ya sasa wakati wamewezeshwa kwa nyanja zote ni sawa na kuombea majani yaote kwenye jangwa la sahara.

Hayo ya poor services ni kielelezo tosha ya uwezo wao ya kuwa kwamba ata customer services kwao shida let alone dealing with complicated finance of running an airline business.
 
Ingawa ushindani ni muhimu lakini swala la huduma mbovu imekuwa utamaduni. Mbona hata Rwanda air haina ushindani lakini service ni first class? Hii nchi huduma kwa mashirika ya umma ni tatizo zito.

Pia mijadala kama hii tuwe objective badala ya kujadili kishabiki sababu humpendi JPM, hivi huduma mbovu inaingiliana vipi na JPM? unapiga siasa hapa kesho ukipata huduma mbovu unamlalamikia tena JPM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wizara ya uchukuzi iondolewe ujenzi..

Wizara ya ujenzi inahitaji waziri bandidu ila wizara ya uchukuzi inahitaji waziri ambaye mind set yake imekaa kibiashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya mambo yanatushinda Watanzania (inawezekana Waafrika wote), ni usimamizi na uendeshaji endelevu...

Mfano mdogo tu wa mradi mwepesi uliotushinda ni usimamizi wa yale mabasi wanayoyaita yanaenda kasi...

Huwa najiuliza, kama kamradi kadogo tu kama hako na ndio kwanza kapo sijui phase 1, tunataabika kukaendesha, vipi miradi mikubwa kama SGR na safari za ndege?
Aisee ubarikiwe Kwa hili swali lako muruwaaa.
 
Back
Top Bottom