Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Duh! Nembo tu ndio tatizo..🙄🙄🙄
Mkuu hata uingereza wanatumia alama ya Simba 3 kama nembo Yao nchi nzima hata Cameroon nao wanatumia nembo ya Simba ni kama America wanamtumia eagle (yaani kuona mbali zaidi).
Mkuu umeona nchi gani wanatumia nembo ya TWIGA? Sasa kuna tofauti gani ya TWIGA na KINYONGA?
 
Mkuu hata uingereza wanatumia alama ya Simba 3 kama nembo Yao nchi nzima hata Cameroon nao wanatumia nembo ya Simba ni kama America wanamtumia eagle (yaani kuona mbali zaidi).
Mkuu umeona nchi gani wanatumia nembo ya TWIGA? Sasa kuna tofauti gani ya TWIGA na KINYONGA?
Mkuu una Imani kali Sana ila fahamu pia:

Twiga ni mnyama mwenye shingo ndefu hivyo hata yeye pia anaona mbali.

Pia ni mnyama mwenye kutembea kwa maringo akiwa mbugani na mwenye kupendeza sana hivyo anawakilisha ufahari, uzuri sio ulegevu au uvivu.

Hivyo nembo haiwezi kuwa tatizo kamwe.
 
Boss Mzee Mwanakijiji Una Hoja nzuri sana
Dawa ya yote .... ni kuweka ... Ushindani. ATCL sasa hivi hawana Ushindani, ndio maana wamelala, ni kama vile Tanesco.
ATCL wangekuwa na washindani au mshindani, wangepata akili, vile vile na Tanesco nao wangepata Mshindani na Washindani akili wangepata.

Pili, Labda tatizo ni Shirika kupangiwa cha kufanya, kupangiwa safari, kupangiwa ratiba, Angalia ile safari ya Mpanda, yaani mpaka aje Rais aseme, ndio wapeleke ndege. Yaani ATCL hawakuona wateja wa Katavi aka Mpanda???!!!

Mambo ni mengi na muda ni mdogo.



​

Hili ni swali ambalo linahitaji kujibiwa kwa usahihi, kwa haraka na kwa umakini. Ni kitu gani ambacho Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linahitaji kufanyiwa na Rais Magufuli ili liweze kutengeneza hadhi inayostahili shirika la kitaifa? Huku ndiko ninakokuita kubebeka. Hadi hivi sasa Magufuli amelipa pumzi ya uhai na kuliokoa kama mtu aliyeopolewa majini baada ya kuzama na watu wakajitahi kumpa CPR na hatimaye kuona anakohoa maji na kuanza kupumua tena. Magufuli alifanya hivyo lakini pia akaenda mbali zaidi; akalinyanyua na kulipa zana zote zinazohitajika ili liweze kuanza kujiendesha kama shirika la kisasa.

Bahati mbaya, bado kuna malalamiko na manung’uniko yanayohusiana na huduma (service). Kwa kampuni ya ndege huduma ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Huduma ya ndege inapimwa kwa ufanisi (efficiency) na usalama wake (safety). Shirika la ndege ambalo halina ufanisi au usalama watu wataliogopa, kulichukia na kulibeza. Na hatimaye linaweza kufa – na kwa kweli linastahili kufa. Mashirika yote ya ndege ambayo yameweza kufanikiwa baada ya muda mrefu yameweza kufanya hivyo kwa kuhakikisha mambo hayo mawili yako ya kiwango cha juu kabisa.

Sasa hivi hatujapata tatizo kubwa lenye kutishia usalama wa ndege zetu. Suala kubwa la sasa hivi ni la huduma. Hapa ndio hoja ilipo na Bw. Kamwele anahitaji kutoa jibu la usahihi, la haraka na makini: wanataka Magufuli alibebe shiriki hili vipi; kwa mbeleko ya sufu?
 
Mkuu,nakupa mfano mmoja tu kukuonyesha ATCL ni dude la kuleta hasara na aibu..
Ona juzi Magufuli ameitisha Ndege ya ATCL Airbus inayochukua abiria 150+ imfate yeye pale Chato wakati anarejea Dar kutoka likizo..!!
Hawakupanda hata watu 20 mle ukichanganya na wahudumu wa Ndege..
Hapo amedisturb route ngapi za kubeba abiria wa ATCL??
Mind u.. na serikali ina Ndege zake ambazo zingeweza jumfata huko Chato.
Naomba nijibu.

Akikujibu kimashiko najitoa JF,huyu ni mmoja wa Mpiga zumari wao wa mitandaoni,wameanza kusema wasaidizi ndio wanamuangusha mtu wao!!!
 
Ili Shirika letu litengamae na Lipate Faida lazima wawe Siriasi karika Mambo machache tu nayo ni :-
Mosi: Wapunguze Siasa kwenye Shirika, libaki kuwa huru

Pili: Wapunguze kuchelewsha Safari bila sababu ya msingi na ikitokea watoe Taarifa mapema kwa Wateja wao.
Tatu: WaajiriWatu wengine wenye Sifa stahiki kutoka Mataifa ya Nje , Mfano hapo kwa CEO, Wahasibu na Wahudumu wengine ili wawape wenyeji Changamoto

Mwisho : Nadhani waruhusu Makampuni mengine kama Fastjet na Precision Air ili wapate wapinzani wawape Changamoto naamini watajifunza mengi kutoka kwao na watakuwa Wabunifu kivyovyote vile!
 
MTAZAMO,
Hoja hizi hazitokani na kutompenda Magufuli bali ni kwa kuwa anaingilia utendaji wa shirika. Kinachotakiwa anatakiwa awape nafasi watendaji wa shirika wafanye kazi na vyombo vya udhibiti vifuatilie utendaji wao.
 
ATCL haitakuwa na ufanisi na huduma bora kama serikali itaendelea kuyawekea vikwazo mashirika ya ndege binafsi hasa yale ya hapa nchini. Na wakiendelea na hii Tabia naiona ATCL ikielekea kule ilikoenda ATC mara tu Magufuli akiondoka Madarakani
 
Back
Top Bottom