Swali la Ugomvi: Injinia Kamwelwe mnataka Rais Magufuli awabebeje ATCL?

Badilisheni Ile nembo ya TWIGA Kwenye hizo ndege ili MAMBO yaende sawa vinginevyo mtawatafuta WACHAWI bila kujua maana ya TWIGA....... sikuzote huyo mnyama anawakilisha ugoigoi,uzembe na ulofa
Twiga ni alama ya nchi mkuu, amekuwepo kabla wazazi wetu hawajazaliwa. Hizo ni imani za kishirikina, unaweza hata ukamuweka mende pale alipo twiga na kama unao ufanisi na ubunifu bado shirika likaendeshwa kwa faida.
 
Unaposema Magufuli kaipa pumzi ATCL kwani alitumia hela za mfukoni mwake au alitumia fedha za umma (na kodi zako pia)???? [emoji32][emoji22][emoji32][emoji22][emoji32][emoji22]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimgusa mjomba wa Mwanakijiji , jiwe utatafuta ugomvi na mwenye mjomba wake , haoni chochote kingine tena !
 

Uliona wapi mswahili akafanikisha jambo kama atukujifunza kwa makosa aliyofanya nyerere tufunzwe tena.Serikali haiwezifanya biashara ikafanikiwa.Shida watataka wapate maziwa mengi bila kulisha ng'ombe,hujuma yeyeto afanyayo mtumishi ni sababu ya maslai duni,umecheki kweli elimu bure.Mtumishi kama hana motisha ya kazi tija itoke wapi
 
Mzee Mwanakijiji

Hivi tunaweza kusema ATCL imefufuliwa ama imefikishwa idara ya wagonjwa mahututi yaani Intensive Care Unit na mgonjwa bado yu hoi taabani hajielewi anapumulia mashine, amepigwa nusu kaputi na kulishwa kwa mipira.

Tuwe wakweli ATCL haijafufuliwa bali imekimbizwa kwenye idara ya mahututi na hatujui hatima yake kama litapona kabisa au kutoka na ulemavu wa kila aina utakao sababisha kushindwa kujitegemea.
 
Usiseme "uwezo wao", sema uwezo wetu. Usiseme "customer service kwao shida", sema "customer service" kwetu shida.

Wewe si Mtanzania? Umefanya lipi la maana mpaka sasa?
 
Yaani Rais ndio asimamie hadi training?
 
Kwani hivyo vyama vyote vingine vilianzishwa na kina nani? Si hao hao waliokuwa CCM?

Hivyo vyama. Vingine vimefanya lipi la maana mpaka dakika hii?

Usianze kuharisha kijinga humu.
Swali bovu sana ! unaulizia vyama hivi hivi vilivyopigwa pini kwa mtutu wa bunduki ?
 
Usiseme "uwezo wao", sema uwezo wetu. Usiseme "customer service kwao shida", sema "customer service" kwetu shida.

Wewe si Mtanzania? Umefanya lipi la maana mpaka sasa?
Kwani mimi sehemu ya management ya ATCL mpaka niwe sehemu ya tatizo?

Uwezo wao to imply the management simple as that.
 
Ikiwa unafikiri tatizo lipo atcl pekee basi sina zaidi la kukufahamisha, ndiyo upeo wako ulipoishia.

Kumbuka tu, samaki mmoja akioza?...
Wote wameoza

Hila tatizo linabaki kwa uongozi husika popote kwenye tatizo la kitaasisi wao ndio wenye mamlaka ya maamuzi na kuweka mifumo ya kuhakikisha huduma bora inatoka muda wote, kiwango ambacho wateja wanakuja kukielewa kutokana na constitence na kutarajia kama sehemu ya ubora.

As the ‘Root Cause Analysis’ states it’s not about the individual employee who provided bad service in the work floor rather it’s the failure of system in place which can’t ensure all staff and process follow a set standard put in place.

Mimi na wewe atuhusiki na mipango ya operation ya ATCL or any goverment institute for that matter kwa ivyo popote penye tatizo ni wao (wahusika) na uendeshwaji wa shirika.
 
Hili shirika likifa Sasa Magufuli anaweza kujikuta anabebeshwa lawama anazostahili na asizostahili.
 
Mkuu swala la usalama hebu liache kwanza usije rusha watu roho bure............!!

Ila kuhusu hili zigo, watafanya kila kitu lakini halibebeki kirahisi kama vile unavyotaka kutuaminisha. Hata wale waliopewa taranta kwenye biblia, siyo wote walioweza kuzizalisha ....!!
 
Mwewe angefaa zaidi...
Ndiyo maana wenzetu wakenya wametumia nembo ya Simba Yangu enzi za ukoloni alkadhalika na waganda nao wametumia nembo ya cranes kama ishara ya kuona mbali(vision)
Labda kwa vile twiga ana shingo ndefu pia akaweza kuona mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…