Swali: Mbinguni Kuna sikukuu ya Christmas 25 December?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!

Msingi wa SWALI LANGU upo katika Sala Aliyotufumdisha Yesu sisi wanafunzi wake kusali Kwa hiyo, kwamba;

(Mathayo 6:10)
"Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama ilivyo Mbinguni "

Swali no 1.
Kusherehekea Christmas tarehe 25 December ni mapenzi ya Mungu aliye Mbinguni?

Swali no 2:
Ni mapenzi ya Mungu kusherehekea Christmas tarehe 25 December tarehe hiyo hiyo pakiwa na sherehe hizo hizo Mbinguni?

Na msingi wa SWALI hili ujibiwe kupitia Katiba yetu Wana wa Mungu iitwayo BIBLIA.

Ikiwa unapenda kuwa raia wa Mbinguni Ukiwa duniani, fuatisha Sala hii,

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, ULEVI USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AMIN

Karibuni 🙏
 
Salaam, Shalom!

Msingi wa SWALI LANGU upo katika Sala Aliyotufumdisha wanafunzi wake kusali Kwa hiyo kwamba,

(Mathayo 6:10)
"Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama ilivyo Mbinguni "

Swali no 2:
Ni mapenzi ya Mungu kusherehekea Christmas tarehe 25 December tarehe hiyo hiyo pakiwa na sherehe hizo hizo Mbinguni?

Na msingi wa SWALI hili ujibiwe kupitia Katiba yetu Wana wa Mungu iitwayo BIBLIA.

Karibuni 🙏
Thibitisha kuna Mungu, thibitisha kuna mbingu.

Katiba ya wana Mungu si Biblia, kuna watu wanaamini Mungu yupo lakini hawaamini Biblia.
 
U mmoja wa wanaoamini uwepo wa Mungu lakini hawaamini BIBLIA?
 
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Thibitisha kuna Mungu, thibitisha kuna mbingu.
Huwezi kujua pasi kuamini.

Na ikiwa huamini uwepo wa Mungu, Si Rahisi kujuthibitishia, huko ni kuvuka hatua muhimu.

Njia Rahisi ni kutafuta, ukimkosa njoo hatua inayofuata.
 
Ili nikuthibitishie uwepo wa Mungu,

Hatua ya kwanza ni kutaka kujua ikiwa Unaamini uwepo wake au la!

Do you believe?
Nikishaamini hakuna haja ya kuthibitisha.

Kuamini ni kukubali bila uthibitisho, sasa nikiamini uthibitisho wa nini?

Na nikishaamini, nishajiwekea bias ya kukubali hata uthibitisho wa uongo ili u fit kwenye imani yangu.

Sitaki kuamini.

Thibitisha kuna Mungu, thibitisha kuna mbingu.
 
Una point kubwa sana Ila jiulize

Ni nani aliyekusanya, kuichambua na kuipangilia biblia?....

Je, vitabu vilivyojumuishwa katika biblia ndivyo pekee vilikuwepo na je, kama sivyo pekee, hivyo vilivyobakia ni useless??.. Na kama sio useless wewe binafsi una access na hivyo vitabu

Kingine, una uhakika Roman Catholic Church inatumia Biblia pekee kufanya maamuzi yake??... Vipi kuhusu mapokeo ya kihistoria ambayo pengine kwenykwenye biblia hayakujumuishwa mfano, historia ya mama na baba wa Bikra Mariamu lakini pia historia yake ya kipekee hadi kuwa mwanamke mbarikiwa ambaye kupitia yeye agano jipya likafunguliwa..

Je, una elimu sahihi?....

Siipingi Biblia lakini Je, Biblia ni alfa na Omega wa taarifa, maarifa na mapokeo ya kihistoria ya ukristu duniani?...
 
Sasa ikiwa hutaki kuamini uwepo wa Mungu,

Usilazimishe nikuthibitishie uwepo wa Mungu Kwa Mimi niaminiye, niliye na HAKIKA juu ya uwepo wake.

Nakushauri mtafute katika huko kutoamini kwake, ukimkosa ndipo uje uniulize uthibitisho baada ya kuamini.
 
Salaam, Shalom!

Msingi wa SWALI LANGU upo katika Sala Aliyotufumdisha Yesu sisi wanafunzi wake kusali Kwa hiyo, kwamba;

(Mathayo 6:10)
"Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama ilivyo Mbinguni "

Swali no 2:
Ni mapenzi ya Mungu kusherehekea Christmas tarehe 25 December tarehe hiyo hiyo pakiwa na sherehe hizo hizo Mbinguni?

Na msingi wa SWALI hili ujibiwe kupitia Katiba yetu Wana wa Mungu iitwayo BIBLIA.

Karibuni 🙏
Labda na mimi nikuulize ni kalenda ipi na iliyo vumbiliwa nyakati zipi maana hii ya sasa mnayo tumia ni gregorian ya papa gregory moaka ya 1500s, sasa ni ipi inayo wadhihirishia kuwa siku ya sabato ni jumamosi ?na ndiyo siku iliyo tambuliwa na kutajwa na biblia.!? Unapo jibu ukumbuke kuwa mzunguko wa siku 7 za wiki ulivumbuliwa na nani na umeanza kutumiwa lini na kabla ya nyakati hizo usabato uliabudu siku gani?
 
Una point kubwa sana Ila jiulize

Ni nani aliyekusanya, kuichambua na kuipangilia biblia?....

Je, vitabu vilivyojumuishwa katika biblia ndivyo pekee vilikuwepo na je, kama sivyo pekee, hivyo vilivyobakia ni useless??.. Na kama sio useless wewe binafsi una access na hivyo vitabu

Kingine, una uhakika Roman Catholic Church inatumia Biblia pekee kufanya maamuzi yake??... Vipi kuhusu mapokeo ya kihistoria ambayo pengine kwenykwenye biblia hayakujumuishwa mfano, historia ya mama na baba wa Bikra Mariamu lakini pia historia yake ya kipekee hadi kuwa mwanamke mbarikiwa ambaye kupitia yeye agano jipya likafunguliwa..

Je, una elimu sahihi?....

Siipingi Biblia lakini Je, Biblia ni alfa na Omega wa taarifa, maarifa na mapokeo ya kihistoria ya ukristu duniani?...
NENO la Mungu limethibitishwa kuwa Kweli na halihitaji msaada wa mapokeo ya WANADAMU.

Na Kwa majibu Yako unajaribu kusema mapokeo kuhusu kusherehekea Christmas tarehe 25 December ni mapokeo ya WANADAMU ya ayostahili kupokelewa bila kuhojiwa na Wana wa Mungu?
 
Sasa ikiwa hutaki kuamini uwepo wa Mungu,

Usilazimishe nikuthibitishie uwepo wa Mungu Kwa Mimi niaminiye, niliye na HAKIKA juu ya uwepo wake.

Nakushauri mtafute katika huko kutoamini kwake, ukimkosa ndipo uje uniulize uthibitisho baada ya kuamini.
Kuthibitisha ni lazima pale tunapotaka kuhakiki ukweli.

Ila, una haki ya kuamini unavyotaka, ikiwa huweki madai kuwa unachoamini ni kitu cha ukweli.

Unaruhusiwa kuamini Mungu yupo, hiyo ni haki yako ya kikatiba na kibinadamu.

Ila, ukisema hiyo si imani yako tu, ni kweli Mungu yupo, hapo unahitajika kuthibitisha Mungu yupo.

Sasa wewe unasema unaamini tu Mungu yupo, lakini hujatoa madai kuwa Mungu yupo kweli?

Au unasema Mungu yupo kweli, si jambo la imani yako tu?
 
Narudia,

Imani juu ya uwepo wa Mungu inaanza ktk hatua ya kwanza,

Uhakika Inakuja hatua ya pili,

Hatua ya tatu ni kuthibitisha uwepo wa Mungu.

Sasa wewe unataka mavuno pasi kuanza na kupanda mbegu.

Fuata hatua hizo twende pamoja.
 
Back
Top Bottom