Swali: Mbinguni Kuna sikukuu ya Christmas 25 December?

Bwana yesu hakuzaliwa December
Alizaliwa kipindi cha baridi ambapo wafugaji huenda kuwanyoa kondoo manyoya yao.
Na ndipo walipotokewa na malaika kuweleza kuzaliwa kwa yesu
Alizaliwa may
Hii December ni sikukuu ya kirumi ya kupagani ambayo walikuwa wanamuabudu Mungu jua
Injili ilipowafikia wakaiendeleza wakisema ndiyo tarehe aliyozaliwa Mungu mpya.
 
Pepo anaekusumbua ni yule yule aliekuwa akiwasumbua wale askari wakati yesu yypo msalabani
Kama kweli wewe ni mwana waMungu shuka msalabani,mara otea nani amekupiga.
Huwa wanataka uthibitisho
MUNGU si wamaonyesho hayo,wala mashindano hayo
Yeye huwatokea wanaomtafuta,na wenye ham nae
YEye sio wa kila mtu,
Hata yesu hakuja kufia kila mtu
Isipokuwa wale aliopewa
Kwaio hata usijisumbue kupata ushahidi,kwa sababu si kwa ajili yako
Kama unaamini hayupo amini hivyo.
Endeleza maisha.
Mmoja kaama wewe alipokufa alimkuta lazaro ju ya kifua cha ibrahim akamuomba ibrahim amtume kwa ndugu zake duniani awaambie yanenwayo ni kweli.
Akajibiwa hata akienda hawatamwamini,maana huko duniani wapo wanaowaambia kila uchwao na hawaaamini.
 
Ni mapenzi ya Mungu Au ya WANADAMU kusherehekea Christmas tarehe 25 December?

Na Mbinguni sherehe hiyo huadhimishwa 25 December?
Katika maandiko yako huko nyuma uliwahi kusema kuwa huwa unaenda mbinguni kiroho na unaonana na malaika,watakatifu na yeye aliye keti katika kiti cha enzi.

Ulipoenda mbinguni,ulimuuliza Mungu kuwa mbinguni huwa wanasherehekea Christmas lini ?

Kwani mbinguni wamekuambia Yesu Kristo alizaliwa tarehe ngapi ? Mwezi gani ?
 
Rabbon..
Soma Yeremia 52:31

" Hata ikawa, katika mwaka wa thelathini na saba wa kuhamishwa kwake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evil-merodaki, mfalme wa Babeli, katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, akamwinua kichwa chake Yehoyakini, mfalme wa Yuda, akamtoa gerezani."
 
DR Mambo Jambo, hii inahusianaje na Krismasi? Ni matukio yamegongana tu.
 
DR Mambo Jambo, hii inahusianaje na Krismasi? Ni matukio yamegongana tu.
Yeremia 31:31-33

31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
 
Logical non sequitur fallacy. Whataboutism fallacy.

Thibitisha Mungu yupo. Thibitisha mbingu ipo.

Waliohusika na kuwepo kwangu ni wazazi wangu, Mungu hujathibitisha yupo.

Thibitisha Mtume Paulo alifika mbinguni.
 
Thibitisha Mungu yupo. Thibitisha mbingu ipo.

Acha longolongo.
 
Mfalme wa Babeli alimtoa gerezani mfalme wa Yuda tarehe hiyo,



Pia mwezi na tarehe uloweka havina mahusiano na Christmas, au unamaanisha Romans wamecoppy Babeli kuweka tarehe na siku hiyo isherehekewe miungu ya Babeli?
 
Tuendelee kumuombea Kiranga Ili Mungu YESU amtokee kama alivyofanya Kwa Paul Ili amthibitishie uwezo wake.
 
Mfalme wa Babeli alimtoa gerezani mfalme wa Yuda tarehe hiyo,



Pia mwezi na tarehe uloweka havina mahusiano na Christmas, au unamaanisha Romans wamecoppy Babeli kuweka tarehe na siku hiyo isherehekewe miungu ya Babeli?
Havina Uhusiano kabisa Ni kweli na Mimi nimeweka tu ili nikuze mjadala ila Kiukweli hakuna Uhusiano wowote..

Labda Pengine warumi walicopy.kutoka babeli
 
Sasa AGANO Hilo ni ujio wa Roho mtakatifu ndani ya MIOYO ya waamini!

Lina mahusiano yapo na tarehe 25 December?
 
Havina Uhusiano kabisa Ni kweli na Mimi nimeweka tu ili nikuze mjadala ila Kiukweli hakuna Uhusiano wowote..

Labda Pengine warumi walicopy.kutoka babeli
Na ndio Hasa msingi,

Watumishi wamefanikiwa kuingiza Kwa Siri sherehe ya miungu Yao ya 25 December isherehekewe makanisani Kwa ustadi mkubwa na watu hawastuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…