Kama unadhani sijaelewa si umjibu wewe uliyeelewa; Mwacheni ndugu rais afanye kazi yake.Hujaielewa hoja yake.
Ni hivi anashangaa mnaposema watekaji ni wanyarwanda lakini mbona mambo ya utekaji yanafanyika takribani nchi
nzima? akatowa mifano ya barabara zenye matatizo namimi nakubaliana naye 100%
Unatakiwa kukanusha maelezo yake kwa hoja sio kupindapinda.
Mwanakijiji kaleta mchango mzuri,
katika Hali kama hii watu wengi hujinufaisha Kwa kupitia mgongo wa tamko la rais, tayari wamejaa pale karagwe kununua ngombe za watu Kwa bei ya kutupa kicheko hadi magego ya mwisho! Pale kuna waliofutiwa vibali vya kuishi eti waombe upya wakati huo siku za kuishi zinahesabika. Katika Hali hii Wanaoandamwa hapa ni wenye kutoka Rwanda, mimi naonya tusijifanye vipofu kudhulum na kunyang'anya watu mali zao na haki zao, penye haki ya mtu serikali iilinde kuliko chochote. Tusijipofue macho kuonea wanyarwanda eti kwaajili ya matamshi ya kagame na JK! Hukumu ya dhambi ni mauti na itakuwa hapa hapa nduniani. Pia tupunguze kutukana wanyonge na wenyeshida Kwa kuwa tuko nyumbani na tumekula ndugu zetu walio nje wanaishi Kama wageni haram usa, uk etc na ndiyo watumia familia zetu nyingi school fees. Tukana ukikumbuka ndugu yako aliye nje ya Tanzania
ujasiri sio kufukuza vizee kule mpakani.Ujasiri ni kumtimua balozi wa Rwanda nchini na kufunga ubalozi wetu Kigali.
Kwanza tunaanza na hao wazee wako wahamiaji haramu. Message delivered, ujinga ukiendelea wacha balozi, tunafukuza Kagame mwenyewe. Hilo likumbuke.
Kama unadhani sijaelewa si umjibu wewe uliyeelewa; Mwacheni ndugu rais afanye kazi yake.
Swala sikumtatiza kikwete, lakini anasimamia sheria ipi inayochaguwa wahamiaji haramu?
Je ametambuwa uwepo wa sheria hii baada ya mzozo wake na kagame? alikuwa wapi hapo awali?
Je maafa yanayosababishwa na wanyarwanda kwa madai yenu ni zaid ya uhalibifu wa jamii yetu kwa madawa ya kulevya? Mbona hachukuwi hatua huku kunanini hasa?
Je, ufisadi wa mabilioni na ukosefu wa elimu na afya bora havioni huyo kikwete isipokuwa wanyarwanda?
Japokuwa mnalazimisha tuamini kwamba anasimamia sheria, nijambo la ajabu sana kuona sheria anayosimamia kikwete inafanya kazi kwa baadhi ya watu tu, wachina, wasomali na wahindi wao hii sheria ni kibogoyo/haitumiki.
Una mikogo wewe!
Una maana Kagame ameshaogopa?
Tusije sikia kauli za ''nilishauriwa vibaya''
Mkuu hizi argument hazitupeleki kokote, tulitakiwa tujiulize kama hoja alizotoa rais ni za kweli au si za kweli. Na kingine sijui kwa nini mnaamua kuchanganya mambo? Yeye amesema wahamiaji wote haramu waondoke ndani ya wiki mbili na kama mpaka sasa wanaoondoka ni hao kutoka Rwanda kumbe basi ni wazi Rwanda ina wahamiaji wengi haramu nchini Tanzania. Kama wengine kutoka nchi zingine wapo na hawajaanza kuondoka basi baada ya wiki mbili kuisha na chchote kisifanyike basi hapo mtakuwa na cha kuongea lakini kwa sasa wanaotii hilo agizo acheni watii na warudi kwao au wafuate taratibu za uhamiaji. Unaposema kwamba kwa nini ni kwa wahamiaji wa waliko Kagera na unajaribu kugusa vitu vingi vingi pamoja na madawa ya kulevya unajua kuna kesi ngapi za madawa ya kulevya ziko mahakamani? na isitoshe lazima kuna wakati na mahali utaanzia kufanya kitu huwezi kuanza kila mahali na muda usiojulikana, lazima kuwa na muda na mahali, labda nikuulize swali na wewe, ulitaka aanze na nini na angeanza lini?
Maamuzi ya hekima na busara pekee hutoa majibu sahihi kwa matatizo mabalimbali.
Maamuzi ya kidikiteta, lazima na visasi hasa huishia katika utata, majanga na hata vita visivo na sababu wala lazima
Sikuwahi kusikia nyerere kawafukuza waganda kagera hata siku moja, nakama ilifanyika mwenyetaarifa sahihi aziweke hapa.
Hata pale Nyerere alipofanikiwa kuwatiamikononi wanajeshi na dege lao kutoka Libya, Nyerere aliwarejesha kwao kwa utaratibu maalum (kumbuka mateka wa kivita na waliletwa kwa lengo moja tu wale waarabu kutumaliza)
Nasikitika sana sana kwetu watanzania kushupalia kitendo hiki kiovu, kibaya na kinacholihalibia sifa nzuri taifa letu.
Hili ni tatizo:-
-kikwete anapoelekeza nguvu zake kwa kundi maalumu la watu maalu pekee.
-Kikwete anapochukuwa hatua bila maandalizi wala ushikishwaji bora wa wahusika
-Kikwete bila kuzingatia kwamba huko kwa majirani zetu, pia wapo watanzania wengi wanaioshi bila vibali kama hawa.
Nadhani Kiongozi wanchi yampasa kuruhusu hekima zaid kuchukuwa nafasi yake zaidi ya chochote.
ni kawaida yenu mnapobanwa huwa mnasema 'mlininukuu vibaya'Nafikiri vyombo vya habari na mitandao vinapotosha agizo la JK. Agizo lilikuwa katika mambo mawili. Kwanza wale wote wenye silaha kinyume cha sharia wazisalimishe. Pili wahamiaji haramu ama waombe uraia au warejee kwao. Wote walipewa muda. Bahati mbaya sasa inafanywa kama walengwa ni Wanyarwanda! Kumbuka maeneo hayo ya kanda ya ziwa kuna wahamiaji harmu kutoka nchi zote tunazopakana nazo, wakiwemo Warundi, Wakongo, Wanyarwanda, Waganda, Wakenya na hata Wasomalia! Sasa haya ya Rwanda pekee yanatoka wapi kama si kutaka kukuza mgogoro?
ni kawaida yenu mnapobanwa huwa mnasema 'mlininukuu vibaya'
haya mambo ya kusindikiza mabasi hayakuwa Kagera tu maana nakumbuka kuna kipindi zilikuwa zikitolewa escot tena kali kati ya Sheluhi - Singida - Manyoni na Babati ambako sidhani kama kuna Wanyarwanda huko. Kusubject aina ya watu fulani katika suala lolote ni kitu hatari sana lakini mimi ninachokiona Watanzania wengi huwa wanajua kuwa nchi ni Dar es Salaam tu na ni wazi katika haya masuala ya kutoelewana na nchi jirani wakazi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kama Bagamoyo, Chalinze hamtaathirika sana kama sisi tulioko huku.Hivi mkuu wewe ni Mzee Mwanakijiji wa siku zote ambaye alikua anachambua mada vizuri na kwa busara kubwa au mtu anatumia jina lako?. Siku za karibuni umebadiluka sana! Kwenye hizo quote zako zote za bible,quran na katiba ya Tanzania kumeainishwa na kumefundisha watu wafuate taratibu na sheria zilizowekwa na mamlaka husika. Mbona hauja quote vipengele hivyo? Ulipenda watu waishi nchi si yao wakiwa si raia na wanyamaziwe?.Ulipenda watanzania walalamike kuhusu uhalifu wanaofanyiwa kila siku kwenye nchi yao. Ulipenda hali ya kusindikizwa na mapolisi kila watu wanapotaka kusafiri toka wilaya moja kwenda wilaya nyingine ndani ya nchi yao?. By the way wanaoondolewa kule si wanyarwanda peke yao ni raia wote wa kigeni ambao wanaishi isivyo halali.Mifano na quotes na refferences ulizotoa hazihusiani kabisa na linaloendelea kule. Pia hakuna nchi yeyote inayoruhusu mhamiaji kuishi akiwa hana passport,working permit au documents za kuhalalisha ukaaji wake. Kuhusu kuoana wala hakukatazwi ila asiye raia aombe uraia ili aishi ki halali.Ndio maana nikasema wewe ni yuleyule au tutegemee mwingine!?
Ni kweli kuna hali hii lakini hata ukimuuliza vizuri Kamanda Tossi (kama sikosei) aliyeshughulikia operesheni ya kusafisha haya mapori, waliobainika kuhusika na huu uhalifu hawakuwa wageni bali wenyeji tena kutoka mikoa mingine ya Tanzania na kwa kiasi fulani wakiwemo hao mnaowasema. Kawaulize vizuri watu wa maeneo hayo watakupa taarifa zaidi. Tusiwe subjective hivi maana tutaishi kutopata majibu na kuwasababishia matatizo zaidi wakazi wa maeneo haya kwa kisingizio cha 'wahamiaji haramu'.Tamko la JK kuhusu wahamiaji haramu ni sahihi kuzingatia maisha walioyokuwa wanaishi watu wa mikoa hiyo.Nimewahi kusafiri kwa basi hadi bukoba kutokea dar...Baada yta kufika Nyakanazi tukaambiwa sasa tunaingia kwenye eneo la msitu ambao ni hatari...kuna majambazi ambao wanateka na kufanya lolote wanalotaka....hawa majambazi ni watu kutoka rwanda na Burundi ambao wanamiliki silaha.Maisha ya wananchi wa maeneo yale yamekuwa ya hofu....Ni sahii JK kutoa order hiyo hata kama kusingekua na mabishano na kageme.
Hii ni Tanzania...ina sheria zake......kama unataka kuwa mtanzania fuata taratibu...ukikwepa taratibu...utakuwa accountable kwa matendo yako.
katika jambo lolote iwe la kufundisha au kusaidia liria taswira mbili, iwe la kuchukua hatua na la kiutu au tuseme la kidiplomasia na ndio maanaa utaona usa na wengineo katika kuondoa wahamiaji wanaangalia kama unafamili umekaa miaka mingapi, na mchango wako kiuchumi, na pia muda au wakati wa kuchukua hatua, na hata katika vita kuna kupigana na propaganda au hiyo diplomasia, sasa hapa tulipokosea ni nye diplomasiaFukuza fukuza inaonesha ujasiri na inawaonesha watutsi kama wewe kuwa tunaweza kuwashughulikia.
Na aendelee, kwani UN wamepewa ushauri mzuri kabisa, Kagame aendelee aone dunia itamfanua nini.
Kama anatafuta pakutokea, hapo ni wrong number.
Nna uhakika kuwa Kaagame ameshajuwa kuwa "his days are numbered" na iliyobaki anatafuta "scapegoat".
Kama umeisoma hotuba ya Kikwete aliyoitoa Addis Ababa utaona kuwa Kikwete aliongea maneno yanye maana na busara sana kwa mpenda amani yoypte duniani.