Maamuzi ya hekima na busara pekee hutoa majibu sahihi kwa matatizo mabalimbali.
Maamuzi ya kidikiteta, lazima na visasi hasa huishia katika utata, majanga na hata vita visivo na sababu wala lazima
Sikuwahi kusikia nyerere kawafukuza waganda kagera hata siku moja, nakama ilifanyika mwenyetaarifa sahihi aziweke hapa.
Hata pale Nyerere alipofanikiwa kuwatiamikononi wanajeshi na dege lao kutoka Libya, Nyerere aliwarejesha kwao kwa utaratibu maalum (kumbuka mateka wa kivita na waliletwa kwa lengo moja tu wale waarabu kutumaliza)
Nasikitika sana sana kwetu watanzania kushupalia kitendo hiki kiovu, kibaya na kinacholihalibia sifa nzuri taifa letu.
Hili ni tatizo:-
-kikwete anapoelekeza nguvu zake kwa kundi maalumu la watu maalu pekee.
-Kikwete anapochukuwa hatua bila maandalizi wala ushikishwaji bora wa wahusika
-Kikwete bila kuzingatia kwamba huko kwa majirani zetu, pia wapo watanzania wengi wanaioshi bila vibali kama hawa.
Nadhani Kiongozi wanchi yampasa kuruhusu hekima zaid kuchukuwa nafasi yake zaidi ya chochote.