Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Waache uharamia kwa wananchi wa Kagera....wanapora ardhi wanateka magari na kupora maliasili katika hifadhi...serikali ikiwavumilia mtasema legelege...ikiwashughulikia mnasema...sasa ifanyeje mridhike?
 
naona sababu imehama kutoka kwenye uhalifu na sasa imekuwa 'tumeelemewa'

huwezi kutetea blunders kwani mwisho wake ni kuumbuka.

Nasubiri kusikia ni wahamaji haramu kiasi gani wameitikia wito na wangapi wamefurushwa.Halafu napenda kusikia tukitangaziwa kuwa Kagera ya leo ni shwari,mabasi yatatembea bila askari.

NJIA YA MWONGO NI FUPI SANA!
 
meningitis,

..lakini hutuelezi ni utaratibu gani ulipaswa kutumika kushughulika na wahamiaji haramu.

..kwa upande wangu naamini wahamiaji haramu wanapaswa kuondolewa hata kama hawahatarishi hali ya usalama.

..kama umeisoma hotuba ya Kikwete amezungumzia wahamiaji haramu, wahalifu kwa maana ya majambazi, na wale waliovamia hifadhi zetu.

..kama Mtanzania unatakiwa utoe ushauri wa jinsi ya kurudisha hali ya amani ktk mkoa wa Kagera na Tanzania nzima. Usikae tu ukisubiri kulaumu, au ukiombea serikali yako isifanikiwe.

NB:

..Tueleze ni utaratibu gani ulipaswa kutumika ktk shughulika na TATIZO SUGU la wahamiaji haramu.
 
Last edited by a moderator:

Rahisi tu!
tufuate sheria na kanuni za uhamiaji tulizojiwekea,sio kwa kagera tu bali hata Upanga kwa wahindi.
Na tusisubiri mpaka Rais wa india atutukane ili tuwaondoe wahamiaji haramu wenye asili ya india.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu JokaKuu, tatizo sugu la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda si la kawaida sina shaka wanakuwa encouraged na some -ve forces nchini mwao wenye agenda ya siri ya kumanufacture Wanyamlenge Mkoani Kagera eventually, kuna baadhi ya watu wanangalia suala hili kijuu juu tu hawajui long term plan ya jamaa hawa; nilishasema mambo ya ukimbizi wa Wanyarwanda mkoani Kagera ni kiini macho tu wanacho tafuta kule ni kutaka kujitanua alafu baadae watugehuke kwa kutoa visingizio mbali mbali vya kutaka kujitenga na ku-annex aridhi kwa kutumia pretext yoyote ile under the sun! Plan ya softly softly ikishindikana basi wako tayari kumwaga damu kwa kutumia mtutu wa bunduki inapobidi mabo kama haya si tunayaona huko DRC(Kivu). Taifa letu lisipokuwa makini/macho matatizo ya Kivu na GOMA yatakuwa replicated katika mkoa wa Kagera muda si mrefu kutoka sasa na wanaonekana wako determined kweli kweli. Kuna Mnyarwanda ame-comment eti kwa nini wahamiaji haramu wanafukuzwa nchini wakati kuna pori huko Karagwe ambalo hajaendelezwa atuwezi ku-treat comment zake as if zilikuwa ni slip up ya ulimi neh, watakuwa wanazungumza mambo haya kwenye vikao vyao. Yaani a mtu mgeni anazungumza kana kwamba ni Waziri wa aridhi wa Tanzania? Mnyarwanda ana mamlaka gani ya ku-comment kuhusu matumizi ya aridhi nchini mwetu - basi tu wamejaa jeuri na kujitia ujuaji.
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu kuna mtu kasema hao si wahamiaji haramu ni masikini! Imagine.

Uganda na Kenya wanamakubaliano ya raia wao kuishi popote nashangaa Uganda inatimua tena wakimbizi wanaohitaji hifadhi na si wahamiaji haramu. Kagame ametimua Wakongo bila huruma. Sijui makubaliano hayo ni ya upuuzi wa aina gani

Halafu tunaambiwa Kagame ni Smart na wao wapo kwa maendeleo. Kama Rwanda kuna maendeleo chini ya Kagame, wanahitaji nini tena hadi wachukue uhamiaji haramu.
Tanzania ni kuzuri kwa mwenye akili ya kutambua vinginevyo hakuna mtu asingehama Rwanda

Hakuna suala la kuitaarifu serikali ya Rwanda kuhusu wakimbizi kwasababu hakukuwa na taarifa wakati wanakuja.

Eti watu wanataka takwimu za ujambazi, hivi kweli Mnyarwanda mwenye panga na grenade unaweza kumwalika katika sensa! Mnyarwanda!!!

Sasa tunajua kila nchi inawatimua, Kagame anayetaka makao makuu yahamishwe awaombee ukazi Nairobi. Kagame is stupid the least to say. Ndani ya EAC alitakiwa azungumzie suala la uhamaji na ukazi kwavile ana wananchi wengi EAC kuliko nchi nyingine.

Akaamua kuwafariji bwana zake wa Nairobi sasa wananchi wanavuka Rosmo usiku.
Nairobi haina msaada. Tunaambiwa smart guy
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji

Wakati wa mwalimu watu wengi walisaidiwa pamoja na jitihada za makusudi kabisa kuwawezesha waafrika kujitawala wenyewe. SA, Zimbabwe, Musumbiji na Angola walikuwa bado hawajawa huru. Sasa hivi kila nchi iko huru ooops uhuru wa bendera hawa economic migrants wasitusumbue, ni jukumu la serikali ya Tanzania sasa kuona resources za nchi hii zinawasaidia Watanzania kuondokana na umasikini uliokubuhu na tatizo la mlo moja kwa raia wake. Wageni wengi ni economic migrants na wanatumia mwanya wa huruma yetu kuwakandamiza Watanzania na kupora mali zao. Enough is enough kama USA, UK na western countries wanaona wana uwezo wa kuwasaidia wakimbizi hawa haramu wanaweza kuwabeba kwa ndege tu na kuwachukua. Hatuwezi kamwe kuwaendekeza watu ambao hawataki kuishi kwao kwa ustaarabu na baadaye kuja kuvuruga amani yetu.

Wote hawa wanatumia jina la mwalimu ili kujineemesha, Kenya wanataka kuchuma kutokana na kuendeleza utalii wa Tanzania kupitia kwao, na kichekesho kingine Rwanda ambao wanataka visa ziondolewa ....... these i d i o t s are living in the past, they think they can dictate what we should do.
 
Well said mkuu, hiki ndicho watu wengi wasichokiona.
Kwa kuongezea wahamiaji haramu hawataki kupewa hadhi za ukimbizi wakijua litawageuka siku moja.
Hawataki kuhamia mikoa mingine kama raia wa kujiandikisha wanataka wakae Kagera.

Tayari tatizo lipo kwasababu watu wa Kagera wameshahamishwa majumbani kwao kupisha wahamiaji haramu wa Rwanda kwa hoja ya huruma, umasikini na sisi hatuko hivyo bila kuangalia kuwa kuna raia wetu wanaathirika na tatizo hilo.
JokaKuu ameto hoja moja nzito sana, kwamba resource zetu hazitoshi na hivyo kuongeza watu bila kujua ni akina nani licha ya usalama ni tatizo katika huduma za jamii.

Kuwaacha wahamiaji haramu ni kukubali kuchukua mzigo usioujua una nini ndani. Mathalan, wanapopata majanga kama milipuko ya maradhi, au mauaji wakiwa nchini mwetu wanajulikana na Watanzania si wahamiaji haramu na serikali inabeba jukumu isilopaswa kulibeba kwa raia wasiojulikana na wa nchi gani.

DRC walikuwa na huruma wakawapa makazi Kivu, leo wanataka kivu ijitenge chini ya usimamizi wa Kagame.Hayo yametokea baada ya kuua wakongo milioni 3.

Kagame haoni tatizo la kuua kilicho mbele yake ni kuwatafutia watu wake nchi yaani eneo la Kivu na sasa anaitazama Kagera. Bado watu hawaoni tatizo hilo.
 
Last edited by a moderator:


Tofauti yenu (wewe na Mheshimiwa Rais) na MMj ni moja tu; MMj is objective and you are emotional.

My opinion is that, being objective is better than being emotional katika kuongoza nchi. Whether wale watu wako kiharamu au kihalali in Tanzania, inaonekana ni wazi kabisa wanafukuzwa sababu ya kauli mbovu za viongozi wa Rwanda. Hii ndo approach ya rais wetu na serikali....kweli? Hivi wakati wanondoka ninani atakuwepo kujua kuwa huyu yupo kihalali au hayupo kihalali, apo kumbuka kwamba tayari kwenye jamii raisi kashajenga muonekano kwamba hawa jamaa ni watu haramu?

Sitetei kauli za Kagame, wala sina urafiki na wanyarwanda endopowanataka kuchezea the integrity of this country. Swali ni kwamba, je kuna wasomali wangapi wanaishi hapa nchini kiharamu na kila siku wanapewa uraia mamia kwa mamia? Kuna wakimbizi kutoka burundi zaidi ya laki walipewa urai? Are these better than the Rwandan? Kama siyo kuwa emotional kwa mheshimiwa wetu ni nini? Mkwara ulikuwa unatosha tu.

Haka kanchi kananuka rushwa!!
 
There your are mkuu Nguruvi3 - mimi nikiona watu wanazungumza mambo ya Iddi Amin ambaye kusema kweli Tanzania ndio ilikuwa inamchokoza mara kwa mara tangu mwaka 1971 kisa wanataka OBOTE arudi Uganda kwa njia yoyote ile, walifikia hatua ya kuhiba ndege ya East Africa Airways mwaka 1972 ili wawapeleka wanajeshi wa OBOTE Uganda wakamvamie Amini, mara M7 na kundi lake kujaribu kumvamia tena Amin wakitokea Tanzania kupitia nyumbani kwao Ankole hawakufanikiwa wachachafya na majeshi ya Amini wakakimbilia tena mafichoni Tanzania, nyinyi mnajua kwa nini nchi nyingi za kiafrica zilikaa kimya wakati Amin alipotuvamia Kagera? Nikiona watu wanamulahumu Amini peke yake katika chochoko zilizo kuwa zinaendelea baina ya Nyerere na Amini huwa nashangaa sana, Amini hakuwahi kuzalisha wakimbizi nchini Tanzania na hakuna record yoyote ya kuonyesha Tanzania ilikuwa na Wakimbizi wa Uganda mpakani wakati wa enzi za Iddi Amini, kwanza Waganda ni hardworking wana aridhi kubwa yenye rutuba wangekuwa na sababu gani ya kukimbilia Tanzania kama walikuwa hawajishughulishi na siasa za kumpinga Iddi Amin huwezi kulinganisha enzi za Iddi Amini na enzi za Administration ya Kigali inayo zalisha wakimbizi wa kuchonga kwa lengo maalum. Wakimbizi wa Uganda walikuwa ni mafisa Wa jeshi wa OBOTE wa kabila la lake(lango) na karibu wote walikuwa wanaishi DSM na kambi nyingine sio mpakani - kwa hiyo issue ya Nyerere ku-deal na wakimbizi wa Uganda per se haikuwepo kabisa. Ninacho taka kusema hapa tusihingize mambo ya itikadi za vyama kwa kutafuta sababu za kutaka kumpakazia Mh.J.Kikwete ili aonekane amefanya jambo la kujidhalilisha kwa kumumshauri kwa nia nzuri tu Mh.Kagame! Wengi hapa wanajitia kumlahumu Kikwete kinafiki tu lakini deep down wanajua Mh.Kikwete alichukua a very bold step kumwambia ukweli Mh.Kagame unlike ma Rais wengine wa Kiafrica wanafiki ambao wanajua mgogoro wa KIVU/GOMA chanzo chake ni Kagame mwenyewe badala ya kumwambia ukweli Kagame wanakaa kimya wanamwacha yaje yamkute yaliyo wakumba wakina: Slobodan Milošević, Laurent Gbagbo na Charles Taylor - Marais wa kiafrica wanajua kabisa kwamba the Hague noose is closing in kwa mwezao, lakini walihamua kubaki tight lipped - ndio Wafrica tulivyo "WANAFIKI".Kwa akili za kawaida mtu ungetegemea Mh.Kagame angeuchukulia seriously ushauri wa Mh.Kikwete na kufanyia kazi, kwa nini nalisema hili: Wakati Mh.Kikwete alipokuwa ni Waziri wa mambo ya nchi za nje aliwahi kumtetea sana Mh.Kagame hasipelekwe Ufaransa kujibu mashtaka ya jinai yaliyo kuwa yanamkabiri kutokana na kifo cha marubani wawili wa kifaransa na wasaidizi wake waliokuwa wameajiriwa kwenye ndege ya Habyalimana iliyo tunguliwa, narudia kusema jitihada za Mh. Kikwete na wenzake ndizo zilifanya Serikali ya Ufaransa kulegeza kamba, bila hivyo Mh.Kagame angefungwa maisha au kuburuzwa kwenye Guillotine nchini Ufaransa kama angepatikana na hatia - in short walimu-save at the eleventh hour.Back 2 the main point, narudia kusema influx ya wakimbizi wa Kinyarwanda mkoani Kagera una lengo maalum - mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera najua ninacho zungumza hapa unlike watu wengine wanao lichukilia suala hili ki itikadi ya vyama, hawaoni kabisa tishio lililo dhahili kwa TAIFA letu kutokana na mipango ya siri ya mafashisti wa kabila la Kitutsi kuhusu mkoa wa Kagera - plan zao ziko kwenye hard copy siyo kwamba tunazungumza mambo ya kutunga hapa, hebu nenda pale wambie wakimbizi wa Kinyarwada kwamba watahamishiwa Mkuranga au Rufiji mkoa wa pwani uone kama kesho yake utumkuta mtu! Hapa nimeona watu wanalalamika eti sijuhi wanawake masikini na wanaume masikini kwa nini warudishwe makwao - wanacho sahau ni kwamba wale wanatumiwa na architects wa expansionism SCAM, wanawatumia Wanyarwanda masikini wanaswagwa tu na kuambiwa nyinyi nendeni huko Tanzania Mkoa wa Kagera zaeni kwa wingi ikiwezekana oaeni na wenyeji ili at the end of the day wapate kisingizio cha ku-bring system down from within population yao hiki-exceed magic number walio jiwekea wanao pull the strings ni wakubwa wao - plan hii imeandikwa kwenye machapishi yao sio utani!! Tukija kugutuka tatizo la KIVU/GOMA tunalikuta on our doorsteps. Mimi naona ajabu sana sijuhi kwa nini watu hawashangai why Rwandese - wakirudishwa makwao wanakaa kwa muda alafu wanarudi tena safari hii wana wakokota ndugu zao, shangazi zao, wajomba zao, marafiki and what have you - WHY?
 
Last edited by a moderator:

There your are mkuu Nguruvi3 - mimi nikiona watu wanazungumza mambo ya Iddi Amin ambaye kusema kweli Tanzania ndio ilikuwa inamchokoza mara kwa mara tangu mwaka 1971 kisa wanataka OBOTE arudi Uganda kwa njia yoyote ile, walifikia hatua ya kuhiba ndege ya East Africa Airways mwaka 1972 ili wawapeleka wanajeshi wa OBOTE Uganda wakamvamie Amini, mara M7 na kundi lake kujaribu kumvamia tena Amin wakitokea Tanzania kupitia nyumbani kwao Ankole hawakufanikiwa wachachafya na majeshi ya Amini wakakimbilia tena mafichoni Tanzania, nyinyi mnajua kwa nini nchi nyingi za kiafrica zilikaa kimya wakati Amin alipotuvamia Kagera?

Nikiona watu wanamulahumu Amini peke yake kutokana na chochoko zilizo kuwa zinaendelea baina ya Nyerere na Amini huwa nashangaa sana, Amini hakuwahi kuzalisha wakimbizi nchini Tanzania na hakuna record yoyote ya kuonyesha Tanzania ilikuwa na Wakimbizi wa Uganda mpakani wakati wa enzi za Iddi Amini, kwanza Waganda ni hardworking wana aridhi kubwa yenye rutuba wangekuwa na sababu gani ya kukimbilia Tanzania kama walikuwa hawajishughulishi na siasa za kumpinga Iddi Amin, huwezi kulinganisha enzi za Iddi Amini na enzi za Administration ya Kigali inayo zalisha wakimbizi wa kuchonga kwa lengo maalum. Wakimbizi wa Uganda walikuwa ni mafisa Wa jeshi wa OBOTE wa kabila la lake(lango) na karibu wote walikuwa wanaishi DSM na kambi nyingine sio mpakani - kwa hiyo issue ya Nyerere ku-deal na wakimbizi wa Uganda per se haikuwepo kabisa.

Ninacho taka kusema hapa tusihingize mambo ya itikadi za vyama kwa kutafuta sababu za kutaka kumpakazia Mh.J.Kikwete ili aonekane amefanya jambo la kujidhalilisha kwa kumumshauri kwa nia nzuri tu Mh.Kagame! Wengi hapa wanajitia kumlahumu Kikwete kinafiki tu lakini deep down wanajua Mh.Kikwete alichukua a very bold step kumwambia ukweli Mh.Kagame unlike ma Rais wengine wa Kiafrica wanafiki ambao walijua fika kwamba mgogoro wa KIVU/GOMA chanzo chake ni Kagame mwenyewe, sasa badala ya kumwambia ukweli Kagame wanakaa kimya wanamwacha yaje yamkute yaliyo wakumba wakina: Slobodan Milošević, Laurent Gbagbo na Charles Taylor - Marais wa kiafrica wanajua kabisa kwamba the Hague noose is closing in kwa mwezao (PK), lakini walihamua kubaki tight lipped - ndio Wafrica tulivyo "WANAFIKI".

Kwa akili za kawaida mtu ungetegemea Mh.Kagame angeuchukulia seriously ushauri wa Mh.Kikwete na kufanyia kazi, kwa nini nalisema hili: Wakati Mh.Kikwete alipokuwa Waziri wa mambo ya nchi za nje, aliwahi kumtetea sana Mh.Kagame hasipelekwe Ufaransa kujibu mashtaka ya jinai yaliyo kuwa yanamkabiri kutokana na kifo cha marubani wawili wa kifaransa na wasaidizi wake waliokuwa wameajiriwa kwenye ndege ya Habyalimana, ndege hiyo iliyo tunguliwa wakati inajitayarisha kutua Kigali!! Narudia kusema jitihada za Mh. Kikwete na wenzake ndizo zilifanya Serikali ya Ufaransa kulegeza kamba, bila hivyo Mh.Kagame angefungwa maisha au kuburuzwa kwenye Guillotine nchini Ufaransa kama angepatikana na hatia - in short wakina JK walimu-save at the eleventh hour, lakini Mh.Kagame anajifanya kasahau yote hayo - hivyo ndivyo ndugu zetu hawa walivyo kuwa wired na Mhumba "HAWANA SHUKURANI" anafikilia kumu-HIT sijua na ngumi, kitu kizito au cha ncha kali - chunga sana jamaa hawa hawana UTANI.

Back 2 the main point, narudia kusema influx ya wakimbizi wa Kinyarwanda mkoani Kagera una lengo maalum - mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Kagera najua ninacho zungumza hapa unlike watu wengine wanao lichukilia suala hili ki itikadi ya vyama, hawaoni kabisa tishio lililo dhahili kwa TAIFA letu kutokana na mipango ya siri ya mafashisti wa kabila la Kitutsi lenye lengo la kumega Mkoa wa Kagera - plan zao ziko kwenye hard copy siyo kwamba tunazungumza mambo ya kutunga hapa, hebu nenda pale wambie wakimbizi wa Kinyarwada kwamba watahamishiwa Mkuranga au Rufiji mkoa wa pwani uone kama kesho yake utumkuta mtu! Sioni kama vyombo vya DOLA vimewahi kulishtukia hilo la Wakimbizi wa Kinyarwanda kug'ag'ania kukaa Mkoa wa Kagera.

Hapa nimeona watu wanalalamika eti sijuhi wanawake masikini na wanaume masikini wa Kinyarwanda kwa nini warudishwe makwao - wanacho sahau ni kwamba wale wanatumiwa na architects wa expansionism SCAM, wanawatumia Wanyarwanda masikini wanaswagwa tu na kuambiwa nyinyi nendeni huko Tanzania Mkoa wa Kagera zaeni kwa wingi ikiwezekana oaneni na wenyeji ili at the end of the day wapate kisingizio cha ku-bring system down from within wakati population yao hiki-exceed magic number walio jiwekea, kumbuka wanao pull the strings ni wakubwa wao huko Kigali - plan hii imeandikwa kwenye machapishi yao sio utani!! Tukija kuzinduka kutoka uzingizini tunakuta tatizo la KIVU/GOMA liko on our doorsteps tukiwa tumechelewa - tuache utani nasema hivi time ya ku-nip in the bud tishio hili la dhahili is NOW not LATER.

Mimi naona ajabu sana! Sijuhi kwa nini watu hawashangai why Rwandese wakirudishwa makwao wanakaa kwa muda alafu wanarudi tena safari hii wana wakokota ndugu zao, shangazi zao, wajomba zao, marafiki and what have you - WHY? Jamani tujiadhali kabla.....
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa hakuna muda muafaka wa kufuata sheria za nchi. Umesema 'inaonekana'' kitu ambacho huna uhakika isipokuwa unadhani ndivyo. Kila mtu anaweza kuwa na maono yake na hilo ni haki yako. JokaKuu kaonyesha kuwa si mara ya kwanza zoezi hilo kufanyika. Mwaka 2003 lilifanyika pia.

Hata hivyo kauli za Kagame ni kiashirio kizuri kuwa hatua za haraka na madhubuti lazima zichukuliwe.
Umesema katika jamii rais ameshawajengea hali kuwa ni haramu. Ukweli ni kuwa ni wahamiaji haramu unless utueleze ni watu wa aina gani. Nimemuuliza mwenzako swali hili hana jibu zaidi ya matusi.

Kuhusu wasomali, tayari umeshasema wanapewa uraia na wakishaupata si haramu ni halali.
Wanyarwanda wangesaidiwa na Kagame kujenga hoja hiyo kupitia EAC, yeye akaona bora ni kuhamishia makao makuu ya EAC Nairobi. Leo Nairobi haiwatambui wala kuwajua na wala haipo tayari kuwapa hifadhi hata sentimita ya nchi yao.

Kuhusu wakimbizi waliotoka Burundi kupewa uraia, hiyo ni kuonyesha kuwa kuna ukarimu na hakuna shida ukufuata taratibu. Waburundi walikubali kuhamia mikoa mingine kuendeleza maisha.

Wanyarwanda hawataki wanachotaka ni kuishi bila kujulikana tena wakiwa karibu na Kigali, kuwafumbia macho ni kosa hata kuwarudisha ni kosa walitakiwa wapambane na mkono wa sheria.
 
Kitaturu hebu tueleze kitu gani unadhani wametendewa kinyume na haki za binadamu?
Pili, kitu gani unadhani hawakutendewa kwa mujibu wa sheria za nchi kama alivyozionyesha Mzee Mwanakijiji
 


Atauwachukue watusi wote walioko rwanda uwalete Tanzania, iwe kagera au mkuranga, pamoja na Kagame yule, hata siku moja hawataweza kuleta chokochoko wanazozileta Congo. The ethnic distribution in Tanzania is very complex than anywhere in the world, so our social system is quite different, difficult and complex, it does not allow one ethnic group to dominate over other. Na wakileta za kuleta watadhibitiwa tu, tena kirahisi. Sanasana walewahimiaji wanachokitafuta ni a place to live, to run away from their misable country, kuleta chokochoko za kutaka kujitenga hawawezi kufanikiwa na hawataweza kufanikiwa.

Hapa sinamaana kwamba wasidhibitiwe, kwani kudhibiti is part of the system and should be ongoing.
 
Nara,

..is our ethnic distribution more complex than Congo's?

..kama wameweza kui-destabilize Congo, what makes u believe kwamba they will not attempt, or hawataweza, kui-destabilize Tanzania??

..binafsi nadhani tuishinikize Rwanda idhibiti wananchi wake. hii nchi ina wakimbizi almost kila nchi ktk maziwa makuu.

..hili tatizo serikali inahangaika nalo tangu wakati wa Raisi Mkapa. Wahamiaji haramu wameondoshwa siyo mara lakini wanaendelea kurudi.

..What is going on in Rwanda?? Je, Rwanda ina-encourage raia wake kuingia Tanzania kama wahamiaji haramu??

cc Nguruvi3, Jasusi, Ogah
 
Last edited by a moderator:


Mkuu Koba......siwezi kukulaumu kwa kuwa kwa maandishi yako hayo inaonyesha huyafahamu vizuri mazingira ya wananchi wetu wa mikoa ya maziwa makuu na maeneo yaliyovamiwa na wahamiaji haramu........

......nilipokuwa kazini maeneo hayo......niliyashuhudia mengi ya kutisha............kwa kifupi.........silaha maeneo yale ziko nje nje.......unaweza kukuta hao unaodhani ni maskini lakini hiyo kasheshe wanayoweza kukuletea utajuta...maishani mwako....... hata hivyo nawapongeza Watanzania wenzetu kwa kuwavumilia wahamiaji haramu wale kwa muda wote huo......hata hivyo wale watu hawaaminiki hata kidogo....nilionywa wakati naishi kule!

NB: hili suala hatukuanza leo kulizungumzia....nakumbuka hii ilikuwa tangu tukiwa bcs, then EF, then Jambo Forum na sasa Jamii Forum....hili suala limeshasemwa sana...........
 
Rahisi tu!
tufuate sheria na kanuni za uhamiaji tulizojiwekea,sio kwa kagera tu bali hata Upanga kwa wahindi.
Na tusisubiri mpaka Rais wa india atutukane ili tuwaondoe wahamiaji haramu wenye asili ya india.

Zoezi la kuondoa wahamiaji haramu hatukuanza juzi.......soma hapa chini ikiwa ni baadhi ya mifani michache...acheni uzushi........


 

Mkuu Bukyanagandi.....wengi wa watu wanaojaribu kutetea uhamiaji haramu hapa JF nina imani kuwa hawayajui maeneo husika vilivyo......na hawana experience na maisha ya kule......ulichokisema hapo juu kina ukweli mwingi sana......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…