Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?


Phase #4 , wasipokuwa makini itakula kwao!!
 
ni kweli binadamu wote ni sawa, ila lazima wafuate taratibu na sheria na taratibu zilizopo, we mwenyewe huwezi kwenda kwa mtu ukaingia tu, lazima upige hodi ukaribishwe uoneshwe wapi ukae, huo ndo utaratibu, angalizo agizo halijasema wanyarwanda haramu, limesema wahamiaji haramu.
 
Nianzie hapo mwisho. Article hiyo ya EAC imeeleza ubaguzi kwa watu wanaoishi kihalali na siyo wahamiaji haramu. Kwahiyo kuinukuu inaonyesha jinsi gani Wanyarwanda wasioelewa maana ya EAC treaty.
Pili, hakuna makubaliano ya kuhamisha watu, mitaji na mali yaliyofikiwa katika EAC.
Kagame hajasema hilo jambo, tunachojua yeye alikuwa busy kuhamisha makao makuu ya EAC, Rwandese should blame their own stupid president apparently purported as smart guy! nay he is stupid.

Pili, angaliae hizo red, kuna mtu ana ng'iombe 200 na kipande cha ardhi. Anakiri kabisa kuwa yeye ni mhamiaji kwasababu alijua sisi ni EAC hakuna shida. Ikiwa Mtanzania aliyezaliwa Tanzania na kuhamia UK au US akiwa na miaka 59 haruhisiwi kumiliki ardhi, haki hii ya mhamiaji haramu anaipata wapi. Totally uninformed Rwandese.

Mwingine amekiri kuwa baada ya kushtukiwa akaomba hati za kuwa mkazi au raia. Yaani kwa miaka 59 hakuwahi kufikiria hivyo huku akitumia resource za nchi hii leo anataka kusamehewa kwasababu amekaa miaka 59. Hebu angalia hii.

Yupo anyedai kuwa jirani yake amechoma nyumba moto na kuchukua mali zake. Hii maana yake ni kuwa watu wa Kagera wameishi kwa dhiki na chuki lakini hawakuwa na la kufanya na sasa imepatikana nafasi wanaonyesha hisia zao.
Kama hali itaachwa ipo siku kutakuwa na mapambano kati ya wazawa na wahamiaji haramu na tutaelekea kuwa Goma.
Ndio maana tunasema upo uhalali wa kuwaondoa hawa kwasababu nyingi lakini muhimu ni wao kuwa wahamiaji haramu
.
 
Hakuna huruma kwa Wahamiaji Haramu nchini....waondoke tu.

Naandaa taarifa maalumu itakayoeleza ubaya na uzuri wa Wahamiaji Haramu wa Kinyarwanda. Nipo Murusagamba naenda Rusumo. Stay tuned
 
sio mwanakijiji ni mwanamishemishd, borntown anaejua vitu lakini anataka kuhamisha bongo za watu azipeleke marsi ambako maji yamepatikana juzi

bottom line, jiran mkorofo anaekaa uani kwako mzibie njia apite angani ful stop, Kagame ni JangalaAfria sio kama bib banda!
Id**s
 
Hakuna huruma kwa Wahamiaji Haramu nchini....waondoke tu.Naandaa taarifa maalumu itakayoeleza ubaya na uzuri wa Wahamiaji Haramu wa Kinyarwanda. Nipo Murusagamba naenda Rusumo. Stay tuned

Mkuu karibu sana, sisi hatuna tatizo na wahamiaji halali na tungependelea zaidi wahamiaji wenye mitaji ya kuwekeza nchini na kuleta ajila - lakini suala la Wanyarwanda naona liko a bit different - kwa nini wanahamia Mikoa ya mipakani kwa wingi wakati hakuna vita nchini mwao? Yaani inaonekana kana kwamba kuna ajenda maalumu ya kupenyeza Wanyarwanda na mifugo yao kwa wingi nchini mwetu, je hili ni jambo la kawaida kweli? - hapa wengi wao wamekili kwamba hawana kibali cha kuishi nchini lakini wanakuwa na ujasiri wa kuteka aridhi na kuhanza kulima na kujenga nyumba za kudumu with impunity! Wakiulizwa nyie vipi? Wanasema oh you know Rwandese have a lot in common na Wahangaza, Wahaya, Wanyambo na Waha nakubaliana nao kwa hoja hiyo lakini hilo haliwapi a blank cheque ya kuvunja sheria na kufanya watakalo mbona awahamii ANKOLE ambako nako tamaduni zao zina fanana na Wanyarwanda, as far as they are concern wanaona Tanzania kama ni shamba la bibi i.e hakuna anaye wafatilia kwa karibu kujua kulikoni?

Mimi sitachoka kutahadhalisha TAIFA letu kwamba uhamiaji wa kasi kubwa wa Wanyarwanda na mifugo yao nchini mwetu (in peace time) una an hidden Ajenda na wanakuwa encouraged na Serikali yao kwa lengo maalum, wengi wao wanakuja na pesa nyingi za kuonga Watanzania wasaliti wasio kuwa na uzalendo, wanaoga ili wapewa aridhi kubwa na vibali fake/halali, kitu cha kujiuliza hapa ni: Hivi Mnyarwanda masikini hela chungu nzima za kuonga wanazipata wapi kama sio kupewa na Serikali yao kwa lengo maalum.

Watu wanacho sahau ni kwamba hawa jamaa wanao julikana kwa jina la Banyamulenge ni Wanyarwanda walio hamia DRC mkoa wa KIVU mwaka 1924 baada ya vurugu nchini mwao, baadae mwaka 1958 yakatokea machafuko/mapinduzi tena nchini Rwanda yaliyo undoa madarakani utawala wa Kitutsi, watutsi wengi walikimbilia Kivu DRC na kungana na wenzao(Wanyamlenge) wengine walikimbilia Uganda na Mikoa ya Kagera/Kigoma. Wanyarwanda wa KIVU walipo zaliana vya kutosha na kuona idadi yao imekwisha kuwa substantial (the so called magic number) ndio wakanzisha vurugu za kutaka kujitenga wakitoa visingizio mbali mbali as if DRC haina makabila mengine zaidi ya Watusi, sasa zengwe hili ndilo linapikwa nchini mwetu na Viongozi wao, kwa bahati mbaya ni watu wachache wanao liona hilo, tukae tukijua MKOA wa Kagera utajikuta kwenye matatizo yanayo fanana na ya Mkoa wa KIVU (DRC) siku si nyingi kuanzia sasa, wanacho subiri ni idadi yao ikifikie (Magic Number) alafu watugehuzie KIBAO.
 


Hivi mkuu naomba nikuulize swali moja tu. Do you sincerely believe kwamba majambazi ndio yameitikia wito huo wa Kikwete yanarudi rwanda kwa hiari? Yameamua kuacha ujambazi!!!!Do you sincerely believe that?
 
Hivi mkuu naomba nikuulize swali moja tu. Do you sincerely believe kwamba majambazi ndio yameitikia wito huo wa Kikwete yanarudi rwanda kwa hiari? Yameamua kuacha ujambazi!!!!Do you sincerely believe that?
murutongore,

..I am not ruling that out mpaka tutakapopata taarifa za usalama toka mkoa wa Kagera and surrounding stating otherwise.

..Tanzania tumewahi kusumbuliwa sana na majambazi toka Somalia na Kenya, sasa why do u find it inconceivable kwamba kuna maharamia toka Rwanda, Congo, au hata Uganda?

..labda na mimi nikuulize. Why do u insist watu hawa waendelee kuishi huku kwetu wakati unaelewa kabisa kwamba wanafanya hivyo kinyume na sheria?
 

Jokakuu, i am not supporting illegal immigrant, wahamiaji haramu, what i'm saying is that kama kuna majambazi i'm 100% sure kuwa bado wako maporini wamejificha.

Pili, nadhani umesoma kwenye vyombo vya habari kuhusu manyanyaso wanayoyapata hao wananchi. Hivi nikuulize, lets say wewe una mke wa kinyarwanda, mna miaka 40 ya ndoa hata kama tuseme mke wako kwa kukosa elimu ya uraia, na ni mkulima ambae hajasoma hajui chochote. Yeye kazaliwa tanzania/tanganyika amekuwa akijua yeye ni mtanzania. Leo hii waje watu wa uhamiaji wanfungishe virago akuache wewe hapo bila kujua cha kufanya. In developed countries, of which we are not, watakuja watu wa uhamiaji watasikiliza kesi yako, watakupa fursa ya kuhalalisha uraia wako na kwa hiari yako kama hutaki uraia wa nchi husika watakupa muda tuseme miezi sita uuze mali zako halafu urudi huko wazazi wako walikotoka. Is this being done here? Don't you think that they(the government) are violating basic human right?

Kwa sababu kumekuwa na kutokuelewana baina ya Kagame na Kikwete? Na kutokuelewana ni kwenye ideology, its not a personal thing on the part of Kagame. Nothing personal kabisa.
 
murutongore,

..hivi si unajua kwamba ignorance of the law, is not an excuse to break the law??

..scenario uliyoitoa inasikitisha, lakini ukweli unabaki palepale kwamba cases like the one u mentioned are isolated, na sheria zetu za uhamiaji lazima zifuatwe.

..pia sitegemei zoezi kama hili liendeshwe perfectly bila kuwepo kwa matatizo ya hapa na pale.

..Tanzania tumekaa na wakimbizi wa Rwanda kwa miaka 40++. Hivi Rwanda hamuoni kwamba hilo ni jambo la aibu kwenu? Why dont u take care of our citizens badala yake mnalazimisha Tanzania ibebe mzigo wenu??

..Mwisho, hili zoezi limewahi kuendeshwa hata na Raisi Mkapa, je unataka kusema naye alikuwa na ideological problems with Kagame??

..Sasa kama ni ideological problem, basi itakuwa ni Kagame ndiye mwenye tatizo. In my opinion Kagame ana ideology kama ile ya Habyarimana na interahamwe, ambao walikuwa hawataki Wanyarwanda waliokuwa Uganda warudi nyumbani.
 
mzee mwanakijiji hapo kidogo busara zimekupungua......katiba ni nyaraka ya kisheria ungeomba ushauri wa kisheria katika kuitafsiri kwake kenye ibara hizo ndugu yangu....katiba ya Tanzania inapotaja mtu iko specifiki kwamba ni mtanzania na si vile unavyomaanisha...kwa tafsiri yako ni wazi wageni atapiga kura ktk uchaguzi mkuu miaka ijayo ikiwa ote tutakuwa na tafsiri hiyo
 
Muongo mkubwa saama wewe.Majambazi yapo kila mahali na kila siku, lakini kwa kanda ya ziwa Wanyarwanda wenye silaha nzito kama tunavyoona M23 waliingia na kuanza kuteka mali na kutisha watu kwa kupora ardhi kuua raia na kufanya Watanzania waishi ndani ya nchi yao kama wakimbizi badala ya wakimbizi aliomkimbia Kagame.

Pili, unaposema wanyarwanda wapewe fursa ya kesi huo ni ubabishaji na propaganda za kitoto sana.
Walipewa nafasi za ukimbizi wakakataa, wakapewa nafasi za kuishi sehemu nyingine Tanzania wakakataa wao wanataka Kagera tu kwa ajili ya empire ya kufikirika

Tatu, hakuna nchi duniani inayotoa uraia kwa hisani ya watoto au mke. Uraia ni suala la kisheria na linamgusa kila mmoja kivyake. Hawa wanyarwanda waliokuja miaka 40 iliyopita walikazani kununu mashamba na kuoa bila kuwa uraia gharama za upumvuva wao haziwezi kuwa excuse ya sheria. Hakuna nafasi ya kutumia pesa za umma kuendesha kesi za wapumbavu waisotaka kuishi kwa taratinbu na amani.

Nne, Hakuna taifa linalotoa nafasi ya kuuza mali. Kwanza kitendo cha kuwapa siku 14 za kuondoka ni hisani kubwa sana. Hawa walipaswa kukamatwa kupakiwa katika malori na kutupwa mpakani ikiwa ni huruma. Vinginevyo wameishi kiharamu nchini na sheria ilikuwa ni kuwaadhibu wakimaliza vifungo wanarudi na nguo tu.

Huwezi kutoa miezi minne kwa mtu aliyeua eti auze mali zake kama nyumba. Hiyo nyu,mba alijenga kwa kibali gani na nani alimpa haki miliki ya radhi. Hakuna sababu za kutoa nafasi kwa watu waliosababisha mateso kama hawa.

Tanzania imekuwa na huruma sana, hawa walipaswa kuongozwa kwenda Rusumo kwa mijeledi, mikanda ya jeshi na polisi. Ni wahalifu kama mhalifu mwingine na hawahitaji msamaha.

Hakuna Mtanzania anyenyanyasa Mnyarwanda, Mnyarwanda anaynaynyasawa na Kagame. Si tunasikia Rwanda imeendelea sasa nani anamnyanyasa mnyarwanda kwa kumwambi arudi kwao.

Hili la uhamiaji limewaumiza sana Rwanda, lakini limeniumuiza sana mimi Mtanzania kwasababu nilipenda wafikishwe mbele ya sheria wale vifungo na wakitoka hapo wapelekwe rusumo kwa miojeledi.

Wameua sana ndugu zetu eti kuna mpuuzi anataka wapewe nafasi za kuuza mali zilizopatikana kwa gharama za damu za Watanzania. huwezi kuua halafu ukahalialisha uuaji huo kwa kutumia nyumba!

Msako bado unaendelea, anayeishi knyume cha sheria pengine anaweza asipatae hata fursa waliyopata weznake kuvuka mpaka.

 
mkuu nikuulize tena,hivi sheria za uhamiaji ni dhidi ya wanyarwanda pekee au?usipromoshe mistari mirefu na kuficha uovu!are we dealing with wanyarwanda or illigeal immagrants?
 
mkuu nikuulize tena,hivi sheria za uhamiaji ni dhidi ya wanyarwanda pekee au?usipromoshe mistari mirefu na kuficha uovu!are we dealing with wanyarwanda or illigeal immagrants?
Tuna deal na immigrants.

Zoezi zima lililenga kuondoa wahamiaji haramu. Wameondolewa wa Burundi, Uganda, Zaire.
Katika hao asilimia zaidi ya 90 ni kutoka Rwanda.

Katika mataifa yote hakuna anayelalamika kuhusu wahamiaji haramu. In fact Uganda wamekataa Wanyarwanda.

Kinachonisukuma kusema ni Wanyarwanda ni kutokana na idadi yao waliopo hapa JF ambao wamekuwa wanarusha tuhuma kwa Tanzania kana kwamba ni tukio la uvunjaji wa haki za binadamu.

Ni kwa msingi huo utaona nimewajibu Wanyarwanda kwasababu wao ndio wanaonekana kulalamika pengine kwa kujua kuwa sehemu kubwa ya wahamiaji ni ndugu zao.

Tumewauliza ni haki gani za bindamu zimekiukwa kwa kuondoa wahamamiaji haramu, hakuna anayetoa jibu.

Utetezi wao ni kuwa wameoa na wana watoto. Ndio maana tunawauliza ni sheria za nchi gani zinazotoa uraia kwa kuangalia ndoa na watoto na wala si sheria?

Utetezi mwingine wa Wanyarwanda ni kuhusu kuondolewa na kuacha mali zao.
Tumewauliza hivi wakati wanakuja ni mahali gani wali declare mali zao. Hawana jibu.

Sasa wamekuja na uetetezi kuwa wahamiaji haramu walipaswa wasikilizwe katika mahakama.
Kwamba wahamiaji 21,000 waundiwe mahakama maalumu kwa gharama za Tanzania. Sijui ni taifa gani linalofanya upuuzi wa aina hiyo.

Mhamiaji haramu ni mhalifu wa sheria. Kitendo cha Tanzania kuwataka warudi kilikuwa cha huruma.
Hawa walipaswa washatakiwe kwasababu kuingia kwao kwa njia haramu ni tatizo la kiusalama, kijamii n.k.

Na kibaya zaidi hawa wapiga propaganda wa Rwanda wameligeuza suala hili kuwa la kufukuzwa kwa Watutsi wakati ambapo wapo Warundi, Wakongo na Waganda. Hii ni ''smear campaign;; kwa Tanzania ndio maana tunawapa majibu.

Labda na wewe utusaidie kuwa Tanzania ilikiuka sheria gani za kimataifa kuwarudisha wahamiaji haramu? Na utaratibu gani mzuri ambao unadhani ungetumika zaidi ya uliotumika ili kuhakikisha Rwanda wanaridhika?

Tusaidiane kuelimishana.
 
View attachment 106779

Haya rushasha na mukora1898...hii ndio tanzania mnayojivunia? subirini very soon mtakuwa kama wanaigeria halafu utakuja huku kutuomba passport ya kusafiria.

..if that is ur view about Tanzania and her ppl, kwanini hamuelemishi hawa ndugu zenu wasije huku?

..kila siku mnatuambia Rwanda ni Singapore ya Africa, sasa kwanini hambaki hukohuko mnakuja kutafuta nini Tanzania?
 
Ndugu yangu TZ haikatai wageni inawahitaji sana,lakini wale wanaofuata utaratibu wa nchi.Tanzania haina ugomvi na nchi ya Rwanda,tamko lililotolewa na Mh rais lilihusu wahamiaji haramu wote walioko TZ,hata uondoshwaji wa wahamiaji haramu wanaokamatwa huwa unafuata sheria za nchi hasa sheria ya uhamiaji Na 7 ya 1995,ambayo haina kipengele chochote kinacho ruhusu dhuluma,mateso,manyanyaso nk kwa wahamiaji haramu.Kama kuna mtumishi wa serikali ananyanyasa wahamiaji haramu anafanya hivyo kama mtu binafsi hajatumwa na serikali.NB Zoezi kubwa la kutoa uraia lililowahi kufanyika duniani kwa mara moja ni lile la serikali ya TZ kutoa uraia wa TZ(naturalization) kwa raia zaidi ya laki moja na nusu wa Burundi waliokuwa kwenye makambi ktk mikoa ya Rukwa na Tabora.
 
Ndugu yangu TZ haikatai wageni inawahitaji sana,lakini wale wanaofuata utaratibu wa nchi.Tanzania haina ugomvi na nchi ya Rwanda,tamko lililotolewa na Mh rais lilihusu wahamiaji haramu wote walioko TZ,hata uondoshwaji wa wahamiaji haramu wanaokamatwa huwa unafuata sheria za nchi hasa sheria ya uhamiaji Na 7 ya 1995,ambayo haina kipengele chochote kinacho ruhusu dhuluma,mateso,manyanyaso nk kwa wahamiaji haramu.Kama kuna mtumishi wa serikali ananyanyasa wahamiaji haramu anafanya hivyo kama mtu binafsi hajatumwa na serikali.NB Zoezi kubwa la kutoa uraia lililowahi kufanyika duniani kwa mara moja ni lile la serikali ya TZ kutoa uraia wa TZ(naturalization) kwa raia zaidi ya laki moja na nusu wa Burundi waliokuwa kwenye makambi ktk mikoa ya Rukwa na Tabora.
 
 
Nguruvi3 unadhani Kikwete alirejea au kurudia ushauri wake kwa PK katika mkutano wa leo?kama sivyo ni kwa nini?
 
Last edited by a moderator:

kumbe mkistuliwa mnastuka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…