Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?


Tatizo lenu ni kutokuelewa ujumbe unaotolewa halafu kutengeneza false conclusions.

Umeshawahi kumsikia Kikwete akisema anawaondoa wahamiaji toka Rwanda?

Maamuzi ya Rais ni secondary to safari yake ya kikazi mkoani Kagera na si maamuzi yanayowahusu wanyarwanda, yanawahusu wahamiaji haramu bila kujali walipotoka. Au hujui kwanini viongozi hufanya safari za kikazi?
 
Sikuwahi kusikia nyerere kawafukuza waganda kagera hata siku moja, nakama ilifanyika mwenyetaarifa sahihi aziweke hapa.

.

Hivi mnajua kwanini tulipigana?
Je kimyakimya manajua nini kiliendelea au?

Tuwe kweli Nyerer hakuwafukuza kwa kuwa aliwaitaji, By the way IDD Amin sio chizi Historia inapotoshwa akukurupuka tu kuja kuipiga Kagera, Idd amin akuja Ku-BOMB makambi ya waaasi amabyo tulikuwa Tunayafadhili na tulipigana ili kuimarisha HIMa/TUSI Empire Kumuweka Kagame madarakani na Kagame madarakani thats all.

Tusingeweza kuwafukuza kwa kuwa waliitajika kupigana dhidi ya IDD AMIN.
 

ha ha ha!jibu maswali yangu bana acha porojo.
Kwa hiyo maamuzi ya JK yanasubiri ziara ?kwani kabla ya kagera JK alizuru mkoa gani?......kumbukumbu zinaonesha ni Kigoooma ....sasa mbona hakutoa hilo agizo?
Hovyo kabisa...
 


Je inaweza sera hii kutumika pia kwa nchi zingine au hapana mkuu
 
Naona kuna watu wangeridhika zaidi kama ungeuliza mkapa aliwashughulikia vipi majangili wa kisomali pale loliondo
 
ha ha ha!jibu maswali yangu bana acha porojo.
Kwa hiyo maamuzi ya JK yanasubiri ziara ?kwani kabla ya kagera JK alizuru mkoa gani?......kumbukumbu zinaonesha ni Kigoooma ....sasa mbona hakutoa hilo agizo?
Hovyo kabisa...

Tatizo lako hujui jinsi serikali inavyofunction. Serikali sio duka la ubuyu. Rais hawezi kunyanuka tu na kusema kitu hadharani. Kitu kinaweza kuwa kinafanyiwa kazi muda mrefu kabla wewe hujakisikia kwenye jukwaa.

Kwani mara ngapi umesikia mtu ameteuliwa halafu unaambiwa uteuzi huo unaanza kazi tarehe ambayo imeshapita? Unajua maana yake ni nini? Well, hapo maana yake ni kwamba jambo hilo lilishafanyiwa kazi muda mrefu, ila taarifa ndio inatolewa later kwa wananchi.

Rais anaposema amewapa wiki mbili waondoke, hasemi tu toka usingizini. Kuna preparations zimeshafanyika muda mrefu.

by the way, wewe unaenjoy kuona wahamiaji haramu wapo nchini na silaha wakiwasumbua wenyeji?
 
Leo Mwanakijiji hoja yako imekua nyepesi sana na umeshindwa kutoa facts nzuri katika kujenga hoja yako...

Kimsingi mara baada ya vita vya Kagera kulikua na operations za chini chini za kuwabaini na kuwaondoa wahamiaji haramu na operatins hizi zilifanyika kwenye mikoa yote ya ukanda wa ziwa. Zilipewa majina tofauti sana ila maarufu ilikua kukamata wamiliki haramu na wasafirishaji haramu wa silaha.

Target ya kwanza ilikua ni kukamata mtu yoyote(hususan mganda) ambaye haeleweki eleweki katika ukanda ule na akileta ujuaji alikua anabambikiwa kuwa ni mchuuzi na mmiliki wa silaha za kivita kama bunduki.

Tuliokuwepo mkoa wa Mara na mikoa mingine ya kanda ya Ziwa enzi hizo mpaka miaka ya 80 tunajua ni nini kilikua kinafanyika japo ilikua ni chini chini mno. Wengi walikua wanakamatwa na kurudishwa makwao ila operations nyingi zilisimama baada ya mgogoro wa wahutu na watusi kupamba moto na wakimbizi kuanza kuruhusiwa kuishi nchini
 
Mzee Mwanakijiji tuwekane sawa kwanza
Je unaamini Kikwete amefanya hivyo kwasababu ya bifu lake na Kagame?
Je huu ndio msingi mkuu wa hoja yako?

I will be back.....
 
Last edited by a moderator:




Asante Mkuu wewe ni mtanzania mwenye busara na unaleta diginity katika taifa letu. Na sio wanasiasa ambao wana vuruga amani za wananchi. Asante sana. Endelea kuwapasha hao watu wanao dhani kuwa ukimbizi ni utendaji dhambi. Mtend dhambi ni yule mtu ambaye anashindwa kutetea haki ya mankind. Awe mkimbizi au mwananchi.

Tukifanya msako Dar au Bongo tutawapata watu karibu asilimia 25% ambao si watanzania na wako katika mashirika na makampuni mbambali. Kama tunataka ku contral immigrants basi tuingize ID Card kwa kila mtu kama wajerumani wanavyo fanya na kila mmoja ajiorozeshe katika ofisi ya mambo ya nchi za ndani. Nimekutana na watu kutoka katika nchi tofauti Bongo na wengi wao hawana hati za uhalali wa kuishi humu nchini kihalali. So what! Mimi sioni shida na sidhani kama mtanzania mwenye busara anaona hiyo ni shida. Matatizo yetu ya uchumi tutatue pengine na sie wote tuna jua wapi ila tunaogopa kuwashutumu hao wahujumu, kwani hawana mswalie mtume katika kutumia vyombo vya umma kutudhuru watu wanao dai haki zao.
 

unachokielezea ni theory ya jinsi ambavyo serikali inatakiwa kufanya kazi ambayo pia kwa bahati mbaya huijui barabara!

Serikali tuliyonayo haina preparations zozote juu ya hili,acha hadaa!

Kwa hiyo unataka kuniambia suala la wahamiaji haramu limeshajadiliwa kwenye hizo kamati zenu za chama?au limeshawahi kujadiliwa(recently) katika kamati ya bunge ya ulinzi/usalama na mambo ya nje?what preparations??
Nipo namanga(mpakani mwa kenya na Tanzania) hapa hakuna jipya zaidi ya kula nyama choma tu.
 
Jk inawezekana alitoa agizo hilo kwa nia nzuri kabisa kwa lengo la kuhakikisha wananchi wake wanaishi katika nchi yao kwa amani kabisa, tatizo ninalo liona mimi agizo la kuwafukuza wahamiaji haramu kalitoa wakati kuna hali ya kutoelewana kati yake na Kagame tena kwenye mpaka wa Rwanda Na Tanzania,angetoa agizo hilo kabla ya kuwepo kwa mvutano baina yao wala pasingekua na mtu wa kuhoji haya maswali.
Hilo ndilo linalipelekea watu wengi kuhisi ni kulipiza kisasi kwa kutukanwa na kutishiwa na Kagame,wengine wamefika mbali zaidi kwa kusema ni maandalizi ya vita.Hao wote ni mawazo yao tu na huwezi kumnyima mtu kuwaza tofauti na wewe.
Mzee Mwanankijiji siyo kayasema hayo kwa chuki dhidi ya JK,pengine ni jinsi swala zima hilo la wahamiaji haramu linavyopelekwa,hao wahamiaji haramu hawakuingia nchini jana wala juzi wengine wanaompaka wajukuu ambao mama zao ni dada zetu.
 
Mzee Mwanakijiji tuwekane sawa kwanza
Je unaamini Kikwete amefanya hivyo kwasababu ya bifu lake na Kagame?
Je huu ndio msingi mkuu wa hoja yako?

I will be back.....

Hayo maswali ulipaswa uyajibu wewe mkuu,yeye kaleta hoja na maswali yake badala ya kujibu na wewe unamuuliza.
 



Respect Mkuu! Nimejifunza mengi sana kwa siku hii ya leo kutoka kwako. You are really a man from Tanganyika and not a Tanzanian. Kwani nikikuhesabu wewe ni mtanzania nitakuvunjia heshima yako. Watanzania tumekuwa wanafki sana. Tumekuwa watu wa kujipendekeza pendekeza. Hatutaki kutumia ubongo wetu kujiuliza kwa nini mambo yanakuwa hivi? Sisi ni bendera fuata upepo. Hatuna nguvu za kuwapinga wahujumu. Roho zetu zimekufa hatuna means za kuweza kufight in a democratic way kwani tunajua hatuna future na ndiyo maana tunawaacha majambazi waendelee kutunyanyasa na kuwaonea watu ambao ni innocent.

Wewe ni mzalendo hasa! Gombea madaraka! Kura yangu ni yako. Watu kama nyinyi ndiyo tunao wahitaji katika taifa letu. Kwani mmejaa busara ambazo zinaweza zikaleta amani katika nchi hata kama wananchi wana matatizo.
 

We nawe kumbe hauna tofauti na Mwanakijiji, sasa chama kinaingiaje hapo?
 



Respect Mkuu! Nimejifunza mengi sana kwa siku hii ya leo kutoka kwako. You are really a man from Tanganyika and not a Tanzanian. Kwani nikikuhesabu wewe ni mtanzania nitakuvunjia heshima yako. Watanzania tumekuwa wanafki sana. Tumekuwa watu wa kujipendekeza pendekeza. Hatutaki kutumia ubongo wetu kujiuliza kwa nini mambo yanakuwa hivi? Sisi ni bendera fuata upepo. Hatuna nguvu za kuwapinga wahujumu. Roho zetu zimekufa hatuna means za kuweza kufight in a democratic way kwani tunajua hatuna future na ndiyo maana tunawaacha majambazi waendelee kutunyanyasa na kuwaonea watu ambao ni innocent.

Wewe ni mzalendo hasa! Gombea madaraka! Kura yangu ni yako. Watu kama nyinyi ndiyo tunao wahitaji katika taifa letu. Kwani mmejaa busara ambazo zinaweza zikaleta amani katika nchi hata kama wananchi wana matatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…