Wayne
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 659
- 204
I know the guy.......this is a leading question
Hey bro..whats up...vp iddi..achana naye huyo...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I know the guy.......this is a leading question
Mkuu pengine wewe ulikuwa bado kinda mwaka 1972 hadi 1978 ilipoanza vita rasmi na Idi Amin.
Nyerere alifanya kosa la kimsingi kutochukua hatua ya ku- contain the fith column.
Hata hivyo by mwaka 1978/79 somo lilikuwa limeshaeleweka baada ya Amin kuingia Kagera kama nyumbani kwake.
Mwalimu aliwakusanya kina Oyite Ojok na hata kina Museveni, waganda, wakapigane kwa ajili y ao wenyewe na kwa ajili ya Tanzania.
JK kafanya kweli, ni lazima adui ajulikane toka mwanzo kwa vile ameshajitanabahisha toka mapema, pa kupiga paeleweke mapema.
Kama mtu anafikiri kutukanwa na kutishiwa maisha kwa mkuu wa nchi na bado mtu ukachekelea kama huna akili nxuri, basi hata a
yekutukana atajua kuwa wewe ni zuzu.
Hey bro..whats up...vp iddi..achana naye huyo...
Swali hili linahitaji jibu; jibu lake linaweza kuwa rahisi au gumu. Lakini ni jibu linalotegemea ujuzi wa historia. Ni jibu linalojaribu kuangalia kama uamuzi wa serikali ya Tanzania kutekeleza sheria kwa upendeleo (selective justice) ni uamuzi sahihi au ni miongoni mwa maamuzi mabovu kabisa yaliyowahi kuchukuliwa na watawala wetu. Na pia ni swali ambalo linauliza kama kutoa adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la Kagame ni jambo sahihi. Lakini pia ni lazima tujiulize baada ya muda uliotolewa kwa wahamiaji wageni kuondoka nchini wale waliobakia wakianza kutendewa vibaya na wenyeji serikali itawachukulia hatua hawa wenyeji au itawaachia kwa sababu wale ni wageni wahamiaji? Quran na Biblia vinafundisha (na vinakubaliana kwa kiasi kikubwa) jinsi ya kuwatendea wageni wahamiaji katika nchi; na haihusishi kuwafukuza kwa nguvu! Katika Biblia kuna uhamiaji wa aina nyingi ambao wote una mafunzo kwa waamini; kuna uhamiaji wa Ibrahim (Abram) toka Uru wa Wakaldo Kulikua hakuna. Na kama walikuepo hawakutenda maovu na walitii amri za nchi na kuishi kwa amani.
jibu ni kwamba hakukua na wahamiaji haramu kipindi hicho,kama walikuwepo hawakufika hata kumi so hawangeweza kuwa tishio.wapinzani wa idd amini wengi walikuwa wamekimbilia Tanzania akiwamo obote,hao hawakuwa tishio kwa usalama.Swali hili linahitaji jibu; jibu lake linaweza kuwa rahisi au gumu. Lakini ni jibu linalotegemea ujuzi wa historia. Ni jibu linalojaribu kuangalia kama uamuzi wa serikali ya Tanzania kutekeleza sheria kwa upendeleo (selective justice) ni uamuzi sahihi au ni miongoni mwa maamuzi mabovu kabisa yaliyowahi kuchukuliwa na watawala wetu. Na pia ni swali ambalo linauliza kama kutoa adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la Kagame ni jambo sahihi. Lakini pia ni lazima tujiulize baada ya muda uliotolewa kwa wahamiaji wageni kuondoka nchini wale waliobakia wakianza kutendewa vibaya na wenyeji serikali itawachukulia hatua hawa wenyeji au itawaachia kwa sababu wale ni wageni wahamiaji?
Quran na Biblia vinafundisha (na vinakubaliana kwa kiasi kikubwa) jinsi ya kuwatendea wageni wahamiaji katika nchi; na haihusishi kuwafukuza kwa nguvu! Katika Biblia kuna uhamiaji wa aina nyingi ambao wote una mafunzo kwa waamini; kuna uhamiaji wa Ibrahim (Abram) toka Uru wa Wakaldoyo kwenda nchi ya ahadi; kuna uhamiaji wa Yusuph kwenda Misra (baada ya kuuzwa na nduguze) na uhamiaji wa kundi kubwa la Waisraeli Misri; kuna uhamiaji (katika Agano Jipya) wa Yesu Masihi kwenda Misri pia baada ya kutafutwa na Herodi auawe akiwa kichanga.
Katika Uislamu bila ya shaka somo kubwa kabisa la uhamaji (hijra) ni ule wa Mtume Mohammed kutoka Mecca kwenda Madina. Ni uhamiaji mkubwa na muhimu sana katika Uislamu kiasi kwamba mwaka wa kwanza katika Kalenda ya Uislamu unaanzia katika tukio hilo (Al Hijra) la mwaka 622 (AD). Ujio wa Mohammed Medina ulitenganisha matendo aliyotendewa na njama alizotendewa na watu wa Mecca hadi kumlazimisha yeye na waamini wa mwanzo kuondoka hapo kwenda Medina katika hali ya kificho na hatari tupu!
Dini zetu kubwa hizi mbili (hata ya Kiyahudi) zinatufundisha kuwatendea wageni vizuri; haijalishi kama walihamia kihalali au la. Tuweke utaratibu mzuri wa kuwashughulikia na kuwahalalisha au hata kuwarudisha makwao katika heshima inayotokana na utu wao. Tukumbuke kuwa Katiba yetu inasema (Ibara 12 hadi 13) kuwa:
Utaona kuwa Ibara hizo hazisemi "kila Mtanzania" au "Kila raia wa Tanzania" na wala hazisemi "Kila aishiye TAnzania"! Zinasema kuwa "Kila mtu" anazaliwa akiwa huru na ni wote ni sawa! Yaani, Mhaya wa Kagera na Mkurya wa Tarime wote ni sawa! Kwamba inasema "Kila mtu anastahili heshima na haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"; yaani Mndengereko na Mzaramo wana haki sawa kabisa ya kuthaminiwa utu wao kama ilivyo kwa Mnyarwanda na Mhabeshi! Yaani, hata kama wamevunja sheria ya uhamiaji - na inawezekana wengi wamefanya hivyo - hilo peke yake haliwafanyi wawe binadamu nusu au siyo watu kama wengine na hivyo hawalindwi na Katiba yetu! Katiba yetu inamlinda kila mtu aliyeko Tanzania!
Ndio maana hili swali linaendelea kusimama, Nyerere alishughulikiaje wahamiaji haramu kutoka Uganda wakati wa chokochoko? Kuna mtu anakumbuka au tuwasaidie hawa wa kizazi kipya somo la historia kidogo maana inaonekana watu wasiojua historia wanaenda kurudia makosa yake!
Tunaweza vipi kukubali serikali ichukue hatua za sheria kwa mfumo wa kibaguzi na udhalilishaji wa utu wa binadamu na bado tunajiita Watanzania?
Mungu atusaidia tusifurahie vitendo kama hivi kwa jina la 'uzalendo'!
MMM
Mpaka sasa iko tofauti ya tafsiri ktk tamko la JK; tafsiri moja kubwa na maarufu ni kuwafukuza "Wanyarandwa" na sio "Wageni waishio nchini isivyo halali".Ningemlaumu Rais Kikwete angewashupalia wahamiaji haramu wa Rwanda kwa kuwa tu ametukanwa kwani ningemwona hana uvumilivu.Tatizo ni pale wahamiaji haramu wanapofanya matukio ya kihalifu na kutumia nguvu dhidi ya wazawa kufaidi rasilimali haswa ardhi.Kama dalili ya mvua ni mawingu nadhani ni hatua sahihi japokuwa yaweza kuwa kwa njia isiyo na taswira nzuri.
Tatizo la Mwanakijiji ni kutokuijua Tanzania vizuri.
Yaani macho yake yameishia kuona kwamba wahamiaji haramu ni swala linalohusu chokochoko za kagame. Hujui kabisa kuwa Tanzania kuna sehemu huwezi kusafiri bila escort ya polisi kwa sababu ya wahamiaji haramu.
Hivi hao waganda unaowazungumzia walikuwa wanazuia watanzania kufanya movements zao nchini kwao?
Kumchukia kwako Kikwete kunakufanya kila analosema au kulifanya utafute jinsi ya kulipinga!
By the way, unapomlinganisha Nyerere na Kikwete unataka kujustify nini???
Chuki itakupeleka kubaya Mwanakijiji.
Mwanakijiji na unyarwanda wako pamoja na pasi ya Tanzania unayo2mia haukufanyi kudhihaki maamuzi ya nchi ye2
Ndugu Kobelo,
Ni kweli malalamiko ya wenyeji yalianza siku nyingi. Lakini kwa nini hatua hizo ziwe sasa? Kwani hiyo siku nyingi Rais na serikali yake walikuwa wapi? Kwani wakati wahamiaji hao wanahamia kienyeji, iwe ni kwa kutoroka makambi ya wakimbizi au kuvuka mpaka kienyeji serikali ilikuwa wapi?
Lina kuja hili la haki za hawa wahamiaji kikatiba. Katiba yetu imetamka wazi binadamu wote, watu wote kuzaliwa HURU na KUWA NA HAKI SAWA MBELE YA SHERIA. Ni kweli Wanapaswa kurejeshwa kwao kama wamekuwa humu kinyume na sheria zetu. Lakini siyo kwa kufukuzwa kienyeji. What is the meaning of diplomacy then? Ni mara ngapi hata wafungwa wanaporejeshwa makwao kunafanyika mawasiliano baina ya nchi husika, utaratibu wa kuwakabidhi na kuwapokea unafanyika kwa murua kabisa? Ni kweli kwamba Wafungwa wana hadhi kuliko hawa wageni?
Halafu kifuate hiki kipengele cha nasaba kati ya nchi jirani na wananchi waishio mipakani. Kwa waliowahi kuishi mipakani watakuwa mashahidi kuwa ni vigumu kuzingatia mpaka wa nchi. Ukienda maeneo hayo ni kawaida kuona mtoto anatoka asubuhi kwenda shule "Kenya" kwa sababu ni karibu na nyumbani kuliko ya "Tanzania" hata kama ni kwa kilomita 1. Kule ni kawaida mtu kukwambia naenda kwa mjomba ikawa anaenda "Kenya" au kukuta mtu anaaga naenda kisimani na ikawa anaenda kuchota maji Burundi. Mwisho wa siku, pamoja na malalamiko yote, siyo halali sana kuwafukuza tu kienyeji kwa sababu wengine ni Wajomba zao na Wahaya flani au ni mama mdogo wa rafiki yako wa pale mpakani na huenda mama mzazi wa Mtanzania flani! Na Kama wamekuwa "Wahamiaji Haramu" ghafla, nataka kukubaliana, kwa mantiki hiyo ya nasaba na kulinda utu, na mwana JF mmoja aliyewatambua hawa wageni kwa mtazamo wa "Wajomba zetu Haramu", "mama zetu haramu" au "Mkeo haramu" (Which is Mbaya)...Na kama wote ni wahalifu basi nasikitika kwani kuna wake za wenzetu siyo "Wananchi kabisa" na wengine wetu ni mapolisi wakuu (Law upholders)! What do you think. In the end hawa ni binadamu wa kawaida! Kuvunjika kwa sheria za uhamiaji hakuwatoi ubinadamu wao!. Jamani hata muhalifu pia ana haki zake.
Vyovyote inavyokuwa kitendo kile kilifanyika kwa jazba za kiongozi na kwa hasira ya matusi ya Rais wa jirani na si kwa kujali sana vilio vya wananchi. Na sitaki kuamini kuwa kwa vilio vya muda huo mrefu ndiyo Rais anavisikia juzi!
Mwisho nahitimisha kwa kusema ni vema tukawa mfano kwa wenzetu kwa vile tunavyotaka watufanyie sisi. Kama wote tungefanya hivyo sidhani kama kungekuwa na mahusiano mazuri na yeyote duniani. Imagine the world where ukipata wageni waliovunja sheria unawakusanya tu unakwenda nao mpakani kwao unawabwaga hapo na kuondoka! Kwamba na China ikusanye wale wauza unga "wetu" wote iwasafirishe mpaka bandarini iwaache kienyeji. Au Afrika ya Kusini ijibebee kina "Masogange wetu" wote ije iwamwage mpakani na kuondoka kimyakimya! Jamani kutakuwa kumebaki thamani ya ubinadamu duniani?......Ile ilikuwa hasira na haikuwa sawa. Siyo kitendo cha mfano wala hakifai kuigwa na si cha kupongezwa kwa namna yoyote hasa kufanywa na kiongozi tena mwenye washauri kibao.
Binafsi naona Mwanakijiji is right. And I do apologize, sincerely, if my understanding is contradictory to yours.
Unasema mwenyewe "Ni kweli malalamiko ya wenyeji yalianza siku nyingi."
Bila shaka tumepata sababu nzuri ya kuanza kuyashughulikia wakati huu. Ilikuwa ni lazima ifike muda fulani hatua zichukuliwe. Kama wanavyosema - sooner or later.
Wala haijasemwa wasije Tanzania. Wafuate taratibu zilizowekwa. Rwanda wapo Wa Tanzania wengi mpaka kwenye vyuo vayo wanategemewa. Hao wote wamefuata taratibu za kwenda huko.
Inaniuma sana kuwahangaisha jamaa zetu wamasai na wasukuma na mifugo. Wamefukuzwa Kilombero. Badala ya Wanyarwanda kuchunga mifugo yao Bongo, bora ndugu zetu waende huko. Mwisho wa siku mifugo hiyo inanifaisha uchumi wa Tanzania. Wanyarwanda hapa kwetu wanalisha tu, hatimaye wanaenda nayo kwao.
Apology not accepted.Ndugu Kobelo,
Ni kweli malalamiko ya wenyeji yalianza siku nyingi. Lakini kwa nini hatua hizo ziwe sasa? Kwani hiyo siku nyingi Rais na serikali yake walikuwa wapi? Kwani wakati wahamiaji hao wanahamia kienyeji, iwe ni kwa kutoroka makambi ya wakimbizi au kuvuka mpaka kienyeji serikali ilikuwa wapi?
Lina kuja hili la haki za hawa wahamiaji kikatiba. Katiba yetu imetamka wazi binadamu wote, watu wote kuzaliwa HURU na KUWA NA HAKI SAWA MBELE YA SHERIA. Ni kweli Wanapaswa kurejeshwa kwao kama wamekuwa humu kinyume na sheria zetu. Lakini siyo kwa kufukuzwa kienyeji. What is the meaning of diplomacy then? Ni mara ngapi hata wafungwa wanaporejeshwa makwao kunafanyika mawasiliano baina ya nchi husika, utaratibu wa kuwakabidhi na kuwapokea unafanyika kwa murua kabisa? Ni kweli kwamba Wafungwa wana hadhi kuliko hawa wageni?
Halafu kifuate hiki kipengele cha nasaba kati ya nchi jirani na wananchi waishio mipakani. Kwa waliowahi kuishi mipakani watakuwa mashahidi kuwa ni vigumu kuzingatia mpaka wa nchi. Ukienda maeneo hayo ni kawaida kuona mtoto anatoka asubuhi kwenda shule "Kenya" kwa sababu ni karibu na nyumbani kuliko ya "Tanzania" hata kama ni kwa kilomita 1. Kule ni kawaida mtu kukwambia naenda kwa mjomba ikawa anaenda "Kenya" au kukuta mtu anaaga naenda kisimani na ikawa anaenda kuchota maji Burundi. Mwisho wa siku, pamoja na malalamiko yote, siyo halali sana kuwafukuza tu kienyeji kwa sababu wengine ni Wajomba zao na Wahaya flani au ni mama mdogo wa rafiki yako wa pale mpakani na huenda mama mzazi wa Mtanzania flani! Na Kama wamekuwa "Wahamiaji Haramu" ghafla, nataka kukubaliana, kwa mantiki hiyo ya nasaba na kulinda utu, na mwana JF mmoja aliyewatambua hawa wageni kwa mtazamo wa "Wajomba zetu Haramu", "mama zetu haramu" au "Mkeo haramu" (Which is Mbaya)...Na kama wote ni wahalifu basi nasikitika kwani kuna wake za wenzetu siyo "Wananchi kabisa" na wengine wetu ni mapolisi wakuu (Law upholders)! What do you think. In the end hawa ni binadamu wa kawaida! Kuvunjika kwa sheria za uhamiaji hakuwatoi ubinadamu wao!. Jamani hata muhalifu pia ana haki zake.
Vyovyote inavyokuwa kitendo kile kilifanyika kwa jazba za kiongozi na kwa hasira ya matusi ya Rais wa jirani na si kwa kujali sana vilio vya wananchi. Na sitaki kuamini kuwa kwa vilio vya muda huo mrefu ndiyo Rais anavisikia juzi!
Mwisho nahitimisha kwa kusema ni vema tukawa mfano kwa wenzetu kwa vile tunavyotaka watufanyie sisi. Kama wote tungefanya hivyo sidhani kama kungekuwa na mahusiano mazuri na yeyote duniani. Imagine the world where ukipata wageni waliovunja sheria unawakusanya tu unakwenda nao mpakani kwao unawabwaga hapo na kuondoka! Kwamba na China ikusanye wale wauza unga "wetu" wote iwasafirishe mpaka bandarini iwaache kienyeji. Au Afrika ya Kusini ijibebee kina "Masogange wetu" wote ije iwamwage mpakani na kuondoka kimyakimya! Jamani kutakuwa kumebaki thamani ya ubinadamu duniani?......Ile ilikuwa hasira na haikuwa sawa. Siyo kitendo cha mfano wala hakifai kuigwa na si cha kupongezwa kwa namna yoyote hasa kufanywa na kiongozi tena mwenye washauri kibao.
Binafsi naona Mwanakijiji is right. And I do apologize, sincerely, if my understanding is contradictory to yours.
adolay,Maamuzi ya hekima na busara pekee hutoa majibu sahihi kwa matatizo mabalimbali.
Maamuzi ya kidikiteta, lazima na visasi hasa huishia katika utata, majanga na hata vita visivo na sababu wala lazima
Sikuwahi kusikia nyerere kawafukuza waganda kagera hata siku moja, nakama ilifanyika mwenyetaarifa sahihi aziweke hapa.
Hata pale Nyerere alipofanikiwa kuwatiamikononi wanajeshi na dege lao kutoka Libya, Nyerere aliwarejesha kwao kwa utaratibu maalum (kumbuka mateka wa kivita na waliletwa kwa lengo moja tu wale waarabu kutumaliza)
Nasikitika sana sana kwetu watanzania kushupalia kitendo hiki kiovu, kibaya na kinacholihalibia sifa nzuri taifa letu.
Hili ni tatizo:-
-kikwete anapoelekeza nguvu zake kwa kundi maalumu la watu maalu pekee.
-Kikwete anapochukuwa hatua bila maandalizi wala ushikishwaji bora wa wahusika
-Kikwete bila kuzingatia kwamba huko kwa majirani zetu, pia wapo watanzania wengi wanaioshi bila vibali kama hawa.
Nadhani Kiongozi wanchi yampasa kuruhusu hekima zaid kuchukuwa nafasi yake zaidi ya chochote.
baada ya siku 14 kuna msako utaanza,bila shaka utahusisha maeneo ya Upanga kwa wahindi na kinondoni kwa wakongo!Dar es salaam hakuna wahamiaji haramu ambao ni wahalifu pia ? arusha je? Au Mwanza hakuna wahamiaji haramu ? Kwanini agizo hili linahusu Kagera tu? Isn't that selective justice?
Dar es salaam hakuna wahamiaji haramu ambao ni wahalifu pia ? arusha je? Au Mwanza hakuna wahamiaji haramu ? Kwanini agizo hili linahusu Kagera tu? Isn't that selective justice?