Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Jasusi,

..hili zoezi liliwahi kuendeshwa mwaka 2000, 2003, na 2006.

..kuna mpaka research papers zimeandikwa kuhusu tatizo la wahamiaji haramu wa Rwanda nchini kwetu.

..kwanini watu hawa wanaendelea kurudi huku Tanzania? ina maana hawana taarifa kwamba haturuhusu wahamiaji haramu? je, serikali ya Rwanda ina-encourage raia wake wasiheshimu mipaka na sheria za uhamiaji za Tanzania??

cc murutongore, enviromental, Mzee Mwanakijiji, Ogah, adolay,

jokaKuu,'
Unachohitaji kujiuliza ni why now? Kama tatizo limekuwepo kwa miaka zaidi ya 13 kwa nini hatua zichukuliwe sasa wakati Kikwete ana beef na Kagame? We are not children. Na kwa nini ni Wanyarwanda tu ambao wameripotiwa kurudi kwao?
Do you see my point? Tunajua Kikwete ni mtu wa visasi na sasa analipiza kisasi chake kwa Kagame. I am not buying any of your arguments, people. I am ashamed to be a Tanzanian.
 
Mwanakijiji angeongeza kuwa ethnic cleansing anayoifanya Kikwete ni crime against humanity. Pia ku-destroy uchumi wa watu na kuwabakiza wakiwa masikini. Mhamiaji ana mifugi yake, ndo kila kitu, hana elimu, hajui bishara, hajui kulima, then unakuja unampa wiki mbili eti arudishe mifugo alikoitoa. Hajui kuwa hawa wafugaji hawajatoka kokote, ila wana asili tu ya Rwanda na Uganda, ila ni wa hapahapa. Unawafanya wauze ngome 1 kwa shs 20,00, ubinadamu huo? Hivi Kikwete si mwislamu?
Nimekutana na mzee mfugaji mmoja aliyekimbia na wigu la 1959. Sijui kama safari hii alipona au la. Kuna pande mbili za tatizo hili, upande mmoja tunadefine vipi mhamiaji haramu? Mfano wachungaji - nijuavyo huko mapalini hakuna vibandiko vya kueleza "Sasa unaingia Tanzania/Rwanda, au kawaida wafugaji wanafuata nyasi/maji determined na seasons. Upande wa pili ni ule wa wanaofaidika na operations hizi. Polisi, Afisa uhamiaji, Afisa mifugo - na wakubwa zao wanafaidika sana na ops hizi. Ukiambiwa wahamiaji wameondika na mifugo 5k - ujue 5k nyingine zimebaki nchini. Normal trading ng'ombe wa kawaida anapatikana kwa 80k huko maporini lakini katika kipindi hiki cha kusanya kusanya hata 20k wanapokea - ni unyama/unyayasaji.
 
Kuishi Tanzania hata miaka 50 hakuondoi ukweli kuwa mtu huyo ni mhamiaji haramu.

Ili kuondoa sintofahamu hiyo ndio maana kuna uraia wa kuzaliwa na uraia wa kupata.
Kwa miaka 40 kama mtu hakuchukua hatua za kuomba uraia na aliishi tu kwasababu amefika katika pori lislo na mwenyewe ni makosa.

Pili, baada ya vita ya Kagera sijui nyerere alipaswa kumfukuza nani! Hapa naomba ufafanuzi

Tatu, mbona hamkumbuki kuwa ni Tanzania hiyo imetoa urai wa watu zaidi ya 190,000 kwa mikupuo miwili achilia mbali wengine wanaopata kila siku?

Na hapa suala si wakimbizi, Tanzania haifukuzi wakimbizi.
Tumewshawahi kuwa na Wakimbizi milioni 2 kwa wakati mmoja.
Tunachoongelea hapa na ambacho umekitaja ni wahamiaji haramu

Lazima uelewe tofauti ya vitu hivyo viwili na ujitahidi sana kuvitenganisha.
Hakuna wakimbizi wa Rwanda kuna wahamiaji toka nchi jirani

Kwa vile kuna neno haramu basi lipo halali.
Sasa kinachobainisha halali na haramu ni sheria. Hawa hawakupewa fursa ya kukamatwa na kuburuzwa mahakamani hata kama wana watoto na wajukuu.

Wamepewa fursa ya kuondoka kwa amani na salama.
Matatizo ya madeni, mali n.k ni yao kwasababu hatujui walipokuja kwa njia haramu wallikuja na nini.

Kuna uwezekano walikuja na bunduki wakaua raia wa Tanzania kwenye mabasi na majumbani, leo eti wapewe muda wa kuondoka na mali zao! zipi walizo declare wakati wanakuja?
Zipi tunazojua walizipata kwa njia halali?!

Mkuu ahsante kwa kujaribu kuninyoosha hapa hio ndio maana ya mjadala.

Sasa mimi naishi nje kwa miaka mingi tu zaidi ya 20 na ninaishi kihalali tu ila sijachukua uraia wa nchi kati ya nilizokwishaishi, kwahio nafahamu tofauti ya wahamiaji halali na wale wahamiaji haramu. Naeleza hivyo kwasababu mimi ni mhamiaji halali.

Ila mkuu mwanakijiji ameleta hoja kwamba je zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu la sasa lina tofauti gani na wakati ule ambapo wahamiaji haramu na wakimbizi walitumia mwanya wa vita vya Kagera kuingia Tanzania na kupafanya nyumbani kwao.

Hawa wahamiaji haramu wapo nchi nzima na si wa kutoka Rwanda tu bali wapo Dar wakongo, wahindi, wachina wasomali na hata wanigeria.

Niliwahi kusema huko nyuma kwamba nimewahi kukutana na watanzania jina tu (yaani baadhi ni raia niliowataja hapo juu) lakini tayari wana pasi za kusafiria za Tanzania na pengine ndio wanaotumika kuvusha madawa ya kulenya kwenda sehemu mbalimbali duniani.

Halafu hapo kwenye RED ungefafanua kidogo, maana unajaribu kusema kwamba hao wahamiaji haramu si wale wanaojazana mpakani Rusumo tu bali wanaweza kuwepo hata Kigoma ama vipi?

Kwa ujumla suala la uhamiaji haramu ni suala zito na linahitaji mawazo yaliyotulia na kama idadi ya waliopo inajulikana basi hakuna neno maana wote watakuwa cleared ndani ya hizo wiki mbili.

Nchi nyingi duniani zinakabiliana na uhaliaji haramu kutoka USA, Mexico, Italy na hata Uingereza nao juzi wametoa mabango kabisa kuwaambia wahamiaji haramu kwamba warudi nyumbani au watakamatwa, lakini wanakuwa na mipango kabambe na inakuwemo katika ilani za uchaguzi katika kampeni za kisiasa.

Hiyo BLUE ya mwisho ni assumption yako juu ya nani anaweza kuwa mhusika wa uhalifu huo, lakini utekwaji wa Dr Ulimboka, mauaji ya marehemu Mwangosi, Ulipuaji mabomu kule Arusha mjini, na sasa kumwagiwa tindikali kwa raia wa kigeni tunaanza kusingizia wageni kweli?

Sasa sera ya CCM au CHADEMA kuhusu uhamiaji haramu zimesimama vipi au zinakuwa zinapikwa inapotokea kutokuelewana kwa viongozi wa mataifa haya tu?

Vinginevyo naelewa point yako kwamba wahamiaji haramu ndio target, lakini why now?
 
Jasusi,

..zoezi hili limekuwa likifanyika mara kwa mara.

..nimekwambia hata 2006 liliwahi kufanyika, wakati huo Lowassa akiwa ni Waziri Mkuu.

..kwani wewe ulitaka lifanyike lini ili ujiridhishe kwamba ni zoezi la kawaida la kuondosha wahamiaji haramu?

..kwa taarifa yako, wakati Rwanda wananungunika kwamba tunafukuza raia wao, na wao pia wako mbioni kufukuza wakimbizi toka Congo. sama hapa chini.

cc Koba, Nguruvi3, @enviromental, Ogah, Bukyanagandi, rushasha, FaizaFoxy, Mzee Mwanakijiji
[h=3]Rwanda to expel 320 Congolese refugees[/h]
Kigali, Rwanda (PANA) – The Rwandan authorities will from next week expel 320 Congolese refugees in the Busasamana camp in the north-west of the country for attempting to return home recently by passing through non-authorised routes at the border with the Democratic Republic of Congo (DRC), official sources said on Wednesday in Kigali.

The mayor of the district of Rubavu in the north-west, Cheick Hassan Bahame, confirmed that his country was preparing to expel those refugees, some of who live in shelters in the village located near the Congolese border.

"Half of them didn't want to be handed over to the UN High Commissioner for Refugees (UNHCR) in the camps ... Most of them insisted on returning home," said the Rwandan official.

He said that Rwanda waned to make sure that the return was done on strictly voluntary basis.

"But most (Congolese) refugees have broken the law by (deciding) to return home without the approval of the local administrative authorities," said Bahame, adding that people to be expelled would be handed over to UNHCR officials for repatriation.

Rwanda hosts some 20,000 Congolese refugees most of who are accommodated in camps spread over its territory, including Kigeme (south), Nyabiheke (north-east), Kiziba (west), Gihembe (north) and Nkamira (north-west).
-0- PANA TWA/TBM/IBA/MSA/MA 31July2013

31 july 2013 22:32:32

[TABLE="width: 645"]
[TR]
[TD="width: 645"]Rwanda has expelled 6,000 Congolese refugees
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 645"]
[TR]
[TD="width: 645"]afrol News, 10 September - The government of Rwanda is continuing to expel Congolese refugees against their will, the United Nations laments. According to new information, 6,000 refugees had already been sent back to areas controlled by the Rwanda-backed Congolese rebel group RCD-Goma.
- Continuing a practice which the United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR) has condemned, the Government of Rwanda has forced 6,000 refugees to return to the Democratic Republic of the Congo (DRC), Kris Janowski, a spokesman for the agency reported today.
Mr Janowski urged the Rwandan authorities to stop this practice. "The movement organised jointly by the government of Rwanda and the rebel group Congolese Rally for Democracy (RCD-Goma) has not been voluntary, with many refugees reporting pressure by Rwandan authorities for them to leave the camps," spokesman Janowski told the press in Geneva.
Last Thursday, High Commissioner Ruud Lubbers had written to Rwandan President Paul Kagame to express concern about the forced returns, calling for an end to the operation, which he termed "neither voluntary nor sustainable."
The number of people returning under pressure had however declined late last week following a visit to both camps by Rwanda's Minister of State for Local Government and a UNHCR official who told the refugees that they did not have to leave the country, according to reports by the UN.
UNHCR also had assured the refugees that the agency would continue to provide assistance to those who did not wish to return home, and that if they eventually did, they would also receive aid. This had caused the intimidated refugees to resist Rwandan repatriation pressure.
The assurances by the UN agency came in response to complaints that local officials had warned refugees that the current return operation was their last chance to return home with assistance. Some refugees had also said they had been threatened with forcible removal should they decline to leave. Such statements "clearly indicate that these return movements are being carried out under duress," Mr Lubbers noted last week.
Meanwhile, the refugees who have returned - mostly women and children - were being housed at a transit centre "in three old factory buildings without doors, windows or proper roofing," Mr Janowski complained.
UNHCR estimates that Rwanda is host to 35,800 refugees, mainly from the war-ravaged neighbour country; Congo Kinshasa.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Last edited by a moderator:
jokaKuu,'
Unachohitaji kujiuliza ni why now? Kama tatizo limekuwepo kwa miaka zaidi ya 13 kwa nini hatua zichukuliwe sasa wakati Kikwete ana beef na Kagame? We are not children. Na kwa nini ni Wanyarwanda tu ambao wameripotiwa kurudi kwao?
Do you see my point? Tunajua Kikwete ni mtu wa visasi na sasa analipiza kisasi chake kwa Kagame. I am not buying any of your arguments, people. I am ashamed to be a Tanzanian.

Mkuu Jasusi......ulitaka JK asubiri mpaka waelewane na PK ndio achukue hatua.....i.e kuwapa ultimatum wahamiaji haramu?........
.......halafu usiwe taken kirahisi sana na vyombo vya habari.....hata Wanyarwanda wenyewe wanasema vyombo vya habari mara nyingi vinapotosha.......nihivi wahamiaji haramu katika mkoa wa Kagera..(nina uasili kule Minziro)...na taarifa nilizopata hivi sasa hata wale Waganda wanaoishi isivyo kihalali walisha na wengine wanakatisha border hivi sasa.....

....tatizo hata lingekuwa miaka 70 (nini miaka 13)...one day somebody must act!.........Jenerali Ulimwengu alishashika uongozi nyeti serikalini.......lakini ilipofika wakati aliambiwa arekebishe makaratasi lah aanze......

...wewe na familia yako na mimi na familia yangu tunaishi nchi ya watu......je na uzee wetu huu na wajukuu tuishi miaka yote hii bila kuwa na makaratasi ya halali......tutamlaumu kiongozi yeyote atakayetoa amri tuondoke?........

...My experience na kushuhudia wahamiaji haramu si nzuri kwa kweli......kwa bahati nimeishi Rwanda, Uganda, Malawi, DRC, East Timor, South Africa, Caribbean, Ulaya, North America na sasa South America......nimeshuhudia wahamiaji haramu wanavyoshughulikiwa....hawa wahamiaji haramu walioko nchini kwetu mbona wamependelewa sana........
 
Wote mnaoshabikia Kikwete na kisasi chake kwa Kagame naomba mpitie tena thread number #229 . Angalieni zile picha za akina mama na watoto wanaorudishwa kwao halafu jiulizeni: is this who we are as Tanzanians? Is this the Tanzania we want?Na mpaka sasa sijapata jibu la mtu yeyote, awe Marcopolo, awe Faizafoxy, awe jokaKuu, vipi wale wasomali wanaochukua ardhi yetu? Vipi wahindi na wachina na wapakistan waliojazana Kariakoo mpaka nasikia hata madanguro ya Kichina yamefunguliwa jijini Dar? Vipi wale wanaoiba wanyama wetu mchana kweupe na kuwapandisha ndege kwenda Arabuni? Vipi hawa wanaotuibia madini? Vipi Wamalawi katika eneo la kusini magharibi? Wanarudi kwao pia. Vipi Wakenya wanaonunua mashamba kinyemela? Mbona tumeshupalia Wanyarwanda peke yao? Kama ni uhalifu polisi wetu wako wapi? Wako bize tu kufukuzana na Chadema na wameshindwa kulinda mipaka yetu? The questions are so numerous I do not know where to stop.
 
......Nchi nyingi duniani zinakabiliana na uhaliaji haramu kutoka USA, Mexico, Italy na hata Uingereza nao juzi wametoa mabango kabisa kuwaambia wahamiaji haramu kwamba warudi nyumbani au watakamatwa, lakini wanakuwa na mipango kabambe na inakuwemo katika ilani za uchaguzi katika kampeni za kisiasa....

Kila Serikali ina approach tofauti kushughulikia wahamiaji haramu.........nilichokiona kwenye nchi nyingi ambazo nimeishi kitu ambacho ni common....ni kuwa wahamiaji haramu hukamatwa na wanawekwa kizuizini.....wanashtakiwa...then deported....(with nothing....that belongs to them)......depending na availability ya Bajeti...au mazungumzo na serikali ya wanakotoka wahamiaji hao.......

hatuwezi kusubiri mpaka uchaguzio eti iwekwe kwenye ilani ya uchanguzi....wakati hili ni suala la kufuata sheria na taratibu tulizojiwekea tena kikatiba.....na zinajulikana hata kimataifa.....

......Sasa sera ya CCM au CHADEMA kuhusu uhamiaji haramu zimesimama vipi au zinakuwa zinapikwa inapotokea kutokuelewana kwa viongozi wa mataifa haya tu?

Vinginevyo naelewa point yako kwamba wahamiaji haramu ndio target, lakini why now?

....again at some point.....something had to be done by somebody....and in this case unfortunately under circumstances surrounding relationship between our JK & PK.......sorry to our neighbours!........
 
Nyerere hao wote angewapa uraia na mashamba ya kulima,unafukuza hao maskini,watoto wao na mbuzi zao for the name of uhamiaji haramu huku ukweli tunajua hii ni revenge kwa kagame and has nothing to do with uhamiaji...fumbo mfumbie mjinga!!
 
Wote mnaoshabikia Kikwete na kisasi chake kwa Kagame naomba mpitie tena thread number #229 . Angalieni zile picha za akina mama na watoto wanaorudishwa kwao halafu jiulizeni: is this who we are as Tanzanians? Is this the Tanzania we want?Na mpaka sasa sijapata jibu la mtu yeyote, awe Marcopolo, awe Faizafoxy, awe jokaKuu, vipi wale wasomali wanaochukua ardhi yetu? Vipi wahindi na wachina na wapakistan waliojazana Kariakoo mpaka nasika hata madanguro ya Kichina yamefunguliwa jijini Dar? Vipi wale wanaoiba wanyama wetu mchana kweupe na kuwapandisha ndege kwenda Arabuni? Vipi hawa wanaotuibia madini? Vipi Wamalawi katika eneo la kusini magharibi? Wanarudi kwao pia. Vipi Wakenya wanaonunua mashamba kinyemela? Mbona tumeshupalia Wanyarwanda peke yao? Kama ni uhalifu polisi wetu wako wapi? Wako bize tu kufukuzana na Chadema na wameshindwa kulinda mipaka yetu? The questions are so numerous I do not know where to stop.
Hii operation has nothing to do with UHAMIAJI HARAMU or anything close to that,ni operation fukuza RWANDESE thats it!!!
 
Wote mnaoshabikia Kikwete na kisasi chake kwa Kagame naomba mpitie tena thread number #229 . Angalieni zile picha za akina mama na watoto wanaorudishwa kwao halafu jiulizeni: is this who we are as Tanzanians? Is this the Tanzania we want?Na mpaka sasa sijapata jibu la mtu yeyote, awe Marcopolo, awe Faizafoxy, awe jokaKuu, vipi wale wasomali wanaochukua ardhi yetu? Vipi wahindi na wachina na wapakistan waliojazana Kariakoo mpaka nasika hata madanguro ya Kichina yamefunguliwa jijini Dar? Vipi wale wanaoiba wanyama wetu mchana kweupe na kuwapandisha ndege kwenda Arabuni? Vipi hawa wanaotuibia madini? Vipi Wamalawi katika eneo la kusini magharibi? Wanarudi kwao pia. Vipi Wakenya wanaonunua mashamba kinyemela? Mbona tumeshupalia Wanyarwanda peke yao? Kama ni uhalifu polisi wetu wako wapi? Wako bize tu kufukuzana na Chadema na wameshindwa kulinda mipaka yetu? The questions are so numerous I do not know where to stop.

.......Mkuu you are quite right....ninapoangalia picha ile ninahuzunika sana.........I'm looking at them just like ndugu zangu......infact ni ndugu zetu.......unfortunately tumejiwekea sheria ili zitulinde.....sasa how our authorities act to protect our sheria its another case.......jambo ambalo tunalipigia kelele kila siku hapa JF........

....binafsi na watu wengi sana hapa JF tumepiga kelele sana issue ya Wasomali......kwani yalinikuta nikiwa mbugani.....isingekuwa mbinu za medani nilizopitia kule JKT.......Ogah asingekuwepo hapa anaandika......Wasomali wanachukua passport zetu kama njugu......Wahindi, Wa-Nigeria, Wakenya hali kadhalika..........na uchafu wanaofanya huko wanakoenda in the name of our country its beyond explanation......ni aibu....
 
Mkuu Jasusi .....again it is unfortunate hivi vitendo vya kihalifu (watu kuporwa mali na kuwa raped wanaposafiri) vinakuwa associated na wakimbizi/wahamiaji haramu.......kwa sababu si mara zote inaweza kuwa ni kweli......ninapoandika hapa ninazungumzia baadhi ya personal experience...nilizowahi kumbana nazo.........kuna kipindi nikiwa safarini (mwanzoni mwa miaka ya 2000) kuelekea Biharamulo...mambo niliyokutana nayo...inahuzunisha kwa kweli.......tulikuta wananchi wamepigwa, wamevuliwa nguo, wengine raped na kuporwa mali zao......karibu na sehemu inaitwa mlima wa Simba.............I WILL NEVER FORGET THAT EXPERIENCE.....

......tulipokuwa tunakaribia........kwanza tulitaka kugeuza kwani tulifikiri ndio kundi la majambazi na kwamba inaweza kuwa ni mtego......wale watu walipiga sana kelele na kuinua mikono yao......tukapata ufahamu kuwa wanaomba msaada.......tuka-take risk ya kuwafuata...kwani ingewezekana kweli ulikuwa ni mtego.........utafikiri wale wananchi...anyway...to cut a story short......wanachi wale straight walituambia kuwa ni majambazi kutoka Rwanda........kilichonishangaza.......wakati nakaribia Biharamulo kuna Kambi ya Jeshi letu........

Nina experience mbaya za safari zangu ndani ya Tanzania........hiyo ilikuwa ni mojawapo tu......nyinine ilikuwa (Arusha, Moshi, Morogoro, Tabora) namshukuru sana Mwenyezi Mungu kuniweka hai hadi leo hii..... ndani ya Rwanda na Uganda pia nilishakutana na visa.......
 
JAMBO USILO LIJUA NI SAWA NA USIKU WA KIZA KINENE...!!!! Hili jambo pana kuliko unavyoliona @ Mwanakijiji na kitu kingine labda leo nikiseme humu kwa wengine kunikashfu na kunishambulia na kuniona mwendawazimu "lakini time will tell" nalo ni"JK ni the Mwalimu in a moedern day tofauti yao huyu atarekebisha yalio mshinda Nyerere na atafanya mambo kwa namna inayokinzana na muono wa watu juu alivyo fanya Nyerere kwa mafanikio makubwa kwa nchi hii"

Swali hili linahitaji jibu; jibu lake linaweza kuwa rahisi au gumu. Lakini ni jibu linalotegemea ujuzi wa historia. Ni jibu linalojaribu kuangalia kama uamuzi wa serikali ya Tanzania kutekeleza sheria kwa upendeleo (selective justice) ni uamuzi sahihi au ni miongoni mwa maamuzi mabovu kabisa yaliyowahi kuchukuliwa na watawala wetu. Na pia ni swali ambalo linauliza kama kutoa adhabu ya jumla (collective punishment) kwa kosa la Kagame ni jambo sahihi. Lakini pia ni lazima tujiulize baada ya muda uliotolewa kwa wahamiaji wageni kuondoka nchini wale waliobakia wakianza kutendewa vibaya na wenyeji serikali itawachukulia hatua hawa wenyeji au itawaachia kwa sababu wale ni wageni wahamiaji?

Quran na Biblia vinafundisha (na vinakubaliana kwa kiasi kikubwa) jinsi ya kuwatendea wageni wahamiaji katika nchi; na haihusishi kuwafukuza kwa nguvu! Katika Biblia kuna uhamiaji wa aina nyingi ambao wote una mafunzo kwa waamini; kuna uhamiaji wa Ibrahim (Abram) toka Uru wa Wakaldoyo kwenda nchi ya ahadi; kuna uhamiaji wa Yusuph kwenda Misra (baada ya kuuzwa na nduguze) na uhamiaji wa kundi kubwa la Waisraeli Misri; kuna uhamiaji (katika Agano Jipya) wa Yesu Masihi kwenda Misri pia baada ya kutafutwa na Herodi auawe akiwa kichanga.

Katika Uislamu bila ya shaka somo kubwa kabisa la uhamaji (hijra) ni ule wa Mtume Mohammed kutoka Mecca kwenda Madina. Ni uhamiaji mkubwa na muhimu sana katika Uislamu kiasi kwamba mwaka wa kwanza katika Kalenda ya Uislamu unaanzia katika tukio hilo (Al Hijra) la mwaka 622 (AD). Ujio wa Mohammed Medina ulitenganisha matendo aliyotendewa na njama alizotendewa na watu wa Mecca hadi kumlazimisha yeye na waamini wa mwanzo kuondoka hapo kwenda Medina katika hali ya kificho na hatari tupu!

Dini zetu kubwa hizi mbili (hata ya Kiyahudi) zinatufundisha kuwatendea wageni vizuri; haijalishi kama walihamia kihalali au la. Tuweke utaratibu mzuri wa kuwashughulikia na kuwahalalisha au hata kuwarudisha makwao katika heshima inayotokana na utu wao. Tukumbuke kuwa Katiba yetu inasema (Ibara 12 hadi 13) kuwa:

Utaona kuwa Ibara hizo hazisemi "kila Mtanzania" au "Kila raia wa Tanzania" na wala hazisemi "Kila aishiye TAnzania"! Zinasema kuwa "Kila mtu" anazaliwa akiwa huru na ni wote ni sawa! Yaani, Mhaya wa Kagera na Mkurya wa Tarime wote ni sawa! Kwamba inasema "Kila mtu anastahili heshima na haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"; yaani Mndengereko na Mzaramo wana haki sawa kabisa ya kuthaminiwa utu wao kama ilivyo kwa Mnyarwanda na Mhabeshi! Yaani, hata kama wamevunja sheria ya uhamiaji - na inawezekana wengi wamefanya hivyo - hilo peke yake haliwafanyi wawe binadamu nusu au siyo watu kama wengine na hivyo hawalindwi na Katiba yetu! Katiba yetu inamlinda kila mtu aliyeko Tanzania!

Ndio maana hili swali linaendelea kusimama, Nyerere alishughulikiaje wahamiaji haramu kutoka Uganda wakati wa chokochoko? Kuna mtu anakumbuka au tuwasaidie hawa wa kizazi kipya somo la historia kidogo maana inaonekana watu wasiojua historia wanaenda kurudia makosa yake!

Tunaweza vipi kukubali serikali ichukue hatua za sheria kwa mfumo wa kibaguzi na udhalilishaji wa utu wa binadamu na bado tunajiita Watanzania?

Mungu atusaidia tusifurahie vitendo kama hivi kwa jina la 'uzalendo'!

MMM
 
I think if u are leaving without proper docs,then they have a right to deport u away

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wanatucheka sana na kujisifu mno eti wameendelea kuliko sisi na ubabe juu. Alafu kuna mijitu inajifanya inahuruma ya kugawa uraia. Hao ni watu wa Skeleton Kagame ahangaike nao yeye mwenyewe Au awape wakenya aliowapa dili la kutumia badari yao.
HAKUNA NCHI DUNIANI UNAWEZA KUINGIA BILA KUULIZWA, HUKU UNASWAGA NG'OMBE ISIPOKUWA TANZANIA.
Hakuna nchi katika Africa iliogawa uraia kwa wakimbizi wengi kama TANZANIA.
FAIDA TUNAYO IPATA LEO NI KUTUKANIWA RAIS WETU.

Nakupa 100% mkuu
 
Utangulizi:

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu, ila post ya mwanakijiji imenifnya niibuke:
Kwanza kabisa nimpe pole Mh: Rais JK kwa mambo yote yanayomsibu, ikiwemo watu kukurupuka na kuanza kulaumu bila kutafuta ukweli wa nini Rais alikisema mkoani Kagera.

Katika hotuba yake, Rais JK aliagiza hivi:

  1. wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, wazisalimishe
  2. wahamiaji haramu (a) KUONDOKA au (b) KUHALALISHA ukazi wao.

Rais alitoa wiki mbili kwa hao wote, na baada ya muda huo, operesheni ndo ianze
Mambo ambayo Raisi hakusema, cha ajabu ndiyo mwanakijiji kaibuka nayo:

  1. Rais JK hakutaja ni wahamiaji kutoka nchi gani – Hakutaja Wanyarwanda
  2. Rais hakuitaja Rwanda wala Kagame wakati akihutubia, na kutoa agizo hilo huko mkoani Kagera

Kwa mtu ambaye hajaishi mikoa ya Kagera, Kigoma na baadhi ya visiwa ndani ya Ziwa Victoria, anaweza asijue ni kwa kiasi gani wahamiaji haramu na majmbazi ni tatizo. Matatizo wanayokuja nayo ni kama yafuatayo:

  1. Mifugo mingi ambayo inaingia kwenye mashamba ya wenyeji
  2. Silaha za kivita – kuna wakati gari haliwezi kutoka Biharamulo kwenda Muleba bila kusindikizwa na Polisi
  3. Ujambazi wa kudumu – wakifanya ujambazi wanakimbilia nyumbani kwao zaidi Rwanda na Burundi. Hapa niseme wanashirikiana na wenyeji, na hata polisi wanatuhumiwa.
Historia ya Operesheni hizi:
Kwa kifupi tangu miaka ya 1995 alipoingia madarakani Mzee Mkapa, mpaka 2010, hakuna mwaka umepita bila operesheni dhidi ya either Wahamiaji haramu, au Majambazi.
Operesheni kubwa zaidi, zimefanyika wakati wa Kamanda Vincent Tossi.
Tangu aondoke, hazijafanyika operesheni kubwa kama za enzi zake, lakini ikumbukwe pia mikoa ya pembezoni, haiwi well covered na media.
Na kwa wale ambao wanafuatilia mambo, hususani mkoa wa Kagera, kwenye miaka ya 2005- mpaka sasa, hakuna kiongozi wa kitaifa ataenda Kagera asiambiwe kuhusu wahamiaji haramu!. Mara zote ambazo Rais Jk ameenda Kagera swala la wahamiaji haramu ameligusia.
Kwa nini hii ya sasa hivi imeonekana ya tofauti:

  1. Imecoincide na issue ya JK Vs Kagame
  2. Imekuwa covered sana na vyombo vya nje – hasa BBC na Wanyarwanda wametake advantage
  3. Vyombo vyote ndani na nje vinaripoti wanyarwanda wanaoondoka – lakini ukweli Warundi na Wakongo wanaondoka.
Ukweli ni kwamba watanzania tusikubali kupotoshwa, hizi operesheni sio za leo na wala haziwalengi Wanyarwanda. Watu kama mzee mwanakijiji hasitake kuunganisha hii issue na Kagame ili kutetea wahamiaji haramu, kwa kweli ni unafiki wa hali ya juu.
Hapa Chini nitakupa mtiririko wa udhibiti wa wahamiaji haramu mkoani Kagera kabla ya issue ya juzi juzi kati Rais Kagame na Rais Kikwete

  1. Tarehe 23 January 2013, ilifanyika operesheni ya kuwafukuza wafungaji walioingia mkoani Kagera kinyume cha sheria ‘ Rejea taarifa ya habari ya ITV ya tarehe 23 January 2013 Wananchi wa kijiji cha Kasuro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Rwanda wameendesha operesheni ya kuwaondoa nchini wahamiaji haramu wenye makundi makubwa ya mifugo Wananchi wa Ngara waendesha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu [video] | Habari
Cha kutisha operesheni ya tarehe 23 Janaury 2013, ilifanywa na wananchi wenyewe, baada ya kuchoka na makundi ya ngombe kutoka nchi za jirani kuvamia mashamab ya wenyeji – Kumbuka ngombe wanaaoingia mkoani kagera wanatoka (Rwanda, Uganda na Burundi)

  1. Hotuba ya Rais JK ya tarehe 30 January 2008
Akiongelea wahamiaji haramu mkoani Kagera Rais alisema hivii ……Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. www.tanzania.go.tz/.../080131%20Hotuba%20kwa%20wananc hi.h

  1. TIMUA TIMUA YA WAHAMIAJI HARAMU YAANZA BUGANGO NA KAKUNYU 9 May 2013 Blogu ya Bugango: An Award Winning Blog: TIMUA TIMUA YA WAHAMIAJI HARAMU YAANZA BUGANGO NA KAKUNYU
Timua timua ya wahamiaji haramu iliyoanza katika kata ya Kakunyu wiki iliyopita imezua kitimtimu kwa wakazi wa Kata hii ambapo makundi ya wahamiaji haramu wameonekana wakikimbia makazi yao kufuatia msako mkali wa kuwatimua unaondelea katika vijiji vya Bugango na Kakunyu.

  1. IDARA ya Uhamiaji Mkoani Mwanza imeendelea kuwanasa Wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa njia za panya baada ya hivi karibuni kuwakamata vijana watatu raia wa Burundi. UHAMIAJI MKOA WA MWANZA YANASA WATATU. - Mon site SPIP
  2. RC aagiza wahamiaji haramu wakamatwe : Tarehe 2 January 2012 RC aagiza wahamiaji haramu wakamatwe

  1. KAGERA YAHITAJI MAMILIONI KULINDA MIPAKA YA NCHI – 29 August 2012 KAGERA YAHITAJI MAMILIONI KULINDA MIPAKA YA NCHI - Kagera Yetu

  1. RC Kagera atangaza kiama cha wahamiaji haramu 6 June 2012 BUKOBA PAMOJA BLOG: RC Kagera atangaza kiama cha wahamiaji haramu

  1. Rais Jakaya Kikwete ametangaza vita dhidi ya majambazi mkoani Kagera na nchi nzima Tarehe 30 January 2008: Raia Mwema - Majambazi wako serikalini
 
Utangulizi:

Nimekuwa kimya kwa muda mrefu, ila post ya mwanakijiji imenifnya niibuke:
Kwanza kabisa nimpe pole Mh: Rais JK kwa mambo yote yanayomsibu, ikiwemo watu kukurupuka na kuanza kulaumu bila kutafuta ukweli wa nini Rais alikisema mkoani Kagera.

Katika hotuba yake, Rais JK aliagiza hivi:

  1. wanaomiliki silaha kinyume cha sheria, wazisalimishe
  2. wahamiaji haramu (a) KUONDOKA au (b) KUHALALISHA ukazi wao.

Rais alitoa wiki mbili kwa hao wote, na baada ya muda huo, operesheni ndo ianze
Mambo ambayo Raisi hakusema, cha ajabu ndiyo mwanakijiji kaibuka nayo:

  1. Rais JK hakutaja ni wahamiaji kutoka nchi gani – Hakutaja Wanyarwanda
  2. Rais hakuitaja Rwanda wala Kagame wakati akihutubia, na kutoa agizo hilo huko mkoani Kagera

Kwa mtu ambaye hajaishi mikoa ya Kagera, Kigoma na baadhi ya visiwa ndani ya Ziwa Victoria, anaweza asijue ni kwa kiasi gani wahamiaji haramu na majmbazi ni tatizo. Matatizo wanayokuja nayo ni kama yafuatayo:

  1. Mifugo mingi ambayo inaingia kwenye mashamba ya wenyeji
  2. Silaha za kivita – kuna wakati gari haliwezi kutoka Biharamulo kwenda Muleba bila kusindikizwa na Polisi
  3. Ujambazi wa kudumu – wakifanya ujambazi wanakimbilia nyumbani kwao zaidi Rwanda na Burundi. Hapa niseme wanashirikiana na wenyeji, na hata polisi wanatuhumiwa.
Historia ya Operesheni hizi:
Kwa kifupi tangu miaka ya 1995 alipoingia madarakani Mzee Mkapa, mpaka 2010, hakuna mwaka umepita bila operesheni dhidi ya either Wahamiaji haramu, au Majambazi.
Operesheni kubwa zaidi, zimefanyika wakati wa Kamanda Vincent Tossi.
Tangu aondoke, hazijafanyika operesheni kubwa kama za enzi zake, lakini ikumbukwe pia mikoa ya pembezoni, haiwi well covered na media.
Na kwa wale ambao wanafuatilia mambo, hususani mkoa wa Kagera, kwenye miaka ya 2005- mpaka sasa, hakuna kiongozi wa kitaifa ataenda Kagera asiambiwe kuhusu wahamiaji haramu!. Mara zote ambazo Rais Jk ameenda Kagera swala la wahamiaji haramu ameligusia.
Kwa nini hii ya sasa hivi imeonekana ya tofauti:

  1. Imecoincide na issue ya JK Vs Kagame
  2. Imekuwa covered sana na vyombo vya nje – hasa BBC na Wanyarwanda wametake advantage
  3. Vyombo vyote ndani na nje vinaripoti wanyarwanda wanaoondoka – lakini ukweli Warundi na Wakongo wanaondoka.
Ukweli ni kwamba watanzania tusikubali kupotoshwa, hizi operesheni sio za leo na wala haziwalengi Wanyarwanda. Watu kama mzee mwanakijiji hasitake kuunganisha hii issue na Kagame ili kutetea wahamiaji haramu, kwa kweli ni unafiki wa hali ya juu.
Hapa Chini nitakupa mtiririko wa udhibiti wa wahamiaji haramu mkoani Kagera kabla ya issue ya juzi juzi kati Rais Kagame na Rais Kikwete

  1. Tarehe 23 January 2013, ilifanyika operesheni ya kuwafukuza wafungaji walioingia mkoani Kagera kinyume cha sheria ‘ Rejea taarifa ya habari ya ITV ya tarehe 23 January 2013 Wananchi wa kijiji cha Kasuro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Rwanda wameendesha operesheni ya kuwaondoa nchini wahamiaji haramu wenye makundi makubwa ya mifugo Wananchi wa Ngara waendesha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu [video] | Habari
Cha kutisha operesheni ya tarehe 23 Janaury 2013, ilifanywa na wananchi wenyewe, baada ya kuchoka na makundi ya ngombe kutoka nchi za jirani kuvamia mashamab ya wenyeji – Kumbuka ngombe wanaaoingia mkoani kagera wanatoka (Rwanda, Uganda na Burundi)

  1. Hotuba ya Rais JK ya tarehe 30 January 2008
Akiongelea wahamiaji haramu mkoani Kagera Rais alisema hivii ……Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. www.tanzania.go.tz/.../080131%20Hotuba%20kwa%20wananc hi.h

  1. TIMUA TIMUA YA WAHAMIAJI HARAMU YAANZA BUGANGO NA KAKUNYU 9 May 2013 Blogu ya Bugango: An Award Winning Blog: TIMUA TIMUA YA WAHAMIAJI HARAMU YAANZA BUGANGO NA KAKUNYU
Timua timua ya wahamiaji haramu iliyoanza katika kata ya Kakunyu wiki iliyopita imezua kitimtimu kwa wakazi wa Kata hii ambapo makundi ya wahamiaji haramu wameonekana wakikimbia makazi yao kufuatia msako mkali wa kuwatimua unaondelea katika vijiji vya Bugango na Kakunyu.

  1. IDARA ya Uhamiaji Mkoani Mwanza imeendelea kuwanasa Wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa njia za panya baada ya hivi karibuni kuwakamata vijana watatu raia wa Burundi. UHAMIAJI MKOA WA MWANZA YANASA WATATU. - Mon site SPIP
  2. RC aagiza wahamiaji haramu wakamatwe : Tarehe 2 January 2012 RC aagiza wahamiaji haramu wakamatwe

  1. KAGERA YAHITAJI MAMILIONI KULINDA MIPAKA YA NCHI – 29 August 2012 KAGERA YAHITAJI MAMILIONI KULINDA MIPAKA YA NCHI - Kagera Yetu

  1. RC Kagera atangaza kiama cha wahamiaji haramu 6 June 2012 BUKOBA PAMOJA BLOG: RC Kagera atangaza kiama cha wahamiaji haramu

  1. Rais Jakaya Kikwete ametangaza vita dhidi ya majambazi mkoani Kagera na nchi nzima Tarehe 30 January 2008: Raia Mwema - Majambazi wako serikalini
 
Mkuu ahsante kwa kujaribu kuninyoosha hapa hio ndio maana ya mjadala.

Sasa mimi naishi nje kwa miaka mingi tu zaidi ya 20 na ninaishi kihalali tu ila sijachukua uraia wa nchi kati ya nilizokwishaishi, kwahio nafahamu tofauti ya wahamiaji halali na wale wahamiaji haramu. Naeleza hivyo kwasababu mimi ni mhamiaji halali.

Ila mkuu mwanakijiji ameleta hoja kwamba je zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu la sasa lina tofauti gani na wakati ule ambapo wahamiaji haramu na wakimbizi walitumia mwanya wa vita vya Kagera kuingia Tanzania na kupafanya nyumbani kwao.

Hawa wahamiaji haramu wapo nchi nzima na si wa kutoka Rwanda tu bali wapo Dar wakongo, wahindi, wachina wasomali na hata wanigeria.

Niliwahi kusema huko nyuma kwamba nimewahi kukutana na watanzania jina tu (yaani baadhi ni raia niliowataja hapo juu) lakini tayari wana pasi za kusafiria za Tanzania na pengine ndio wanaotumika kuvusha madawa ya kulenya kwenda sehemu mbalimbali duniani.

Halafu hapo kwenye RED ungefafanua kidogo, maana unajaribu kusema kwamba hao wahamiaji haramu si wale wanaojazana mpakani Rusumo tu bali wanaweza kuwepo hata Kigoma ama vipi?

Kwa ujumla suala la uhamiaji haramu ni suala zito na linahitaji mawazo yaliyotulia na kama idadi ya waliopo inajulikana basi hakuna neno maana wote watakuwa cleared ndani ya hizo wiki mbili.

Nchi nyingi duniani zinakabiliana na uhaliaji haramu kutoka USA, Mexico, Italy na hata Uingereza nao juzi wametoa mabango kabisa kuwaambia wahamiaji haramu kwamba warudi nyumbani au watakamatwa, lakini wanakuwa na mipango kabambe na inakuwemo katika ilani za uchaguzi katika kampeni za kisiasa.

Hiyo BLUE ya mwisho ni assumption yako juu ya nani anaweza kuwa mhusika wa uhalifu huo, lakini utekwaji wa Dr Ulimboka, mauaji ya marehemu Mwangosi, Ulipuaji mabomu kule Arusha mjini, na sasa kumwagiwa tindikali kwa raia wa kigeni tunaanza kusingizia wageni kweli?

Sasa sera ya CCM au CHADEMA kuhusu uhamiaji haramu zimesimama vipi au zinakuwa zinapikwa inapotokea kutokuelewana kwa viongozi wa mataifa haya tu?

Vinginevyo naelewa point yako kwamba wahamiaji haramu ndio target, lakini why now?

Hili suala la wahamiaji haramu linanikera sana. As far as I know, there is no wahamiaji haramu in Kagera. If they are then they are a few who probably came after 2010. Ask me why?

In 2009, the Government of Tanzania had a program funded by UNHCR which set a goal of giving all foreigners in that region resident permits. ALL and I mean ALL were given resident permits. Now as per the laws of any country, once you are a resident then you wewe sio mhamiaji haramu. I tell you if you go to Dar Es Salaam at the Immigration Headquarters, all these people who are crossing coming into Rwanda, you will find their files there as residents. Sasa hao wahamiaji haramu wanatoka wapi? This is a personal vendetta by your president because he wants to flex his muscles but he is doing it the wrong way. Anyways, we know that this is wrong because all of these people wote wanaokuja wanasema walikuwa wananyang'anywa hizo resident permits zinachanwa halafu wanaambiwa eti ondokeni. Very sad indeed.
 
Back
Top Bottom