Kuishi Tanzania hata miaka 50 hakuondoi ukweli kuwa mtu huyo ni mhamiaji haramu.
Ili kuondoa sintofahamu hiyo ndio maana kuna uraia wa kuzaliwa na uraia wa kupata.
Kwa miaka 40 kama mtu hakuchukua hatua za kuomba uraia na aliishi tu kwasababu amefika katika pori lislo na mwenyewe ni makosa.
Pili, baada ya vita ya Kagera sijui nyerere alipaswa kumfukuza nani! Hapa naomba ufafanuzi
Tatu, mbona hamkumbuki kuwa ni Tanzania hiyo imetoa urai wa watu zaidi ya 190,000 kwa mikupuo miwili achilia mbali wengine wanaopata kila siku?
Na hapa suala si wakimbizi, Tanzania haifukuzi wakimbizi.
Tumewshawahi kuwa na Wakimbizi milioni 2 kwa wakati mmoja.
Tunachoongelea hapa na ambacho umekitaja ni wahamiaji haramu
Lazima uelewe tofauti ya vitu hivyo viwili na ujitahidi sana kuvitenganisha.
Hakuna wakimbizi wa Rwanda kuna wahamiaji toka nchi jirani
Kwa vile kuna neno haramu basi lipo halali.
Sasa kinachobainisha halali na haramu ni sheria. Hawa hawakupewa fursa ya kukamatwa na kuburuzwa mahakamani hata kama wana watoto na wajukuu.
Wamepewa fursa ya kuondoka kwa amani na salama.
Matatizo ya madeni, mali n.k ni yao kwasababu hatujui walipokuja kwa njia haramu wallikuja na nini.
Kuna uwezekano walikuja na bunduki wakaua raia wa Tanzania kwenye mabasi na majumbani, leo eti wapewe muda wa kuondoka na mali zao! zipi walizo declare wakati wanakuja?
Zipi tunazojua walizipata kwa njia halali?!
Mkuu ahsante kwa kujaribu kuninyoosha hapa hio ndio maana ya mjadala.
Sasa mimi naishi nje kwa miaka mingi tu zaidi ya 20 na ninaishi kihalali tu ila sijachukua uraia wa nchi kati ya nilizokwishaishi, kwahio nafahamu tofauti ya wahamiaji halali na wale wahamiaji haramu. Naeleza hivyo kwasababu mimi ni mhamiaji halali.
Ila mkuu mwanakijiji ameleta hoja kwamba je zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu la sasa lina tofauti gani na wakati ule ambapo wahamiaji haramu na wakimbizi walitumia mwanya wa vita vya Kagera kuingia Tanzania na kupafanya nyumbani kwao.
Hawa wahamiaji haramu wapo nchi nzima na si wa kutoka Rwanda tu bali wapo Dar wakongo, wahindi, wachina wasomali na hata wanigeria.
Niliwahi kusema huko nyuma kwamba nimewahi kukutana na watanzania jina tu (yaani baadhi ni raia niliowataja hapo juu) lakini tayari wana pasi za kusafiria za Tanzania na pengine ndio wanaotumika kuvusha madawa ya kulenya kwenda sehemu mbalimbali duniani.
Halafu hapo kwenye
RED ungefafanua kidogo, maana unajaribu kusema kwamba hao wahamiaji haramu si wale wanaojazana mpakani Rusumo tu bali wanaweza kuwepo hata Kigoma ama vipi?
Kwa ujumla suala la uhamiaji haramu ni suala zito na linahitaji mawazo yaliyotulia na kama idadi ya waliopo inajulikana basi hakuna neno maana wote watakuwa cleared ndani ya hizo wiki mbili.
Nchi nyingi duniani zinakabiliana na uhaliaji haramu kutoka USA, Mexico, Italy na hata Uingereza nao juzi wametoa mabango kabisa kuwaambia wahamiaji haramu kwamba warudi nyumbani au watakamatwa, lakini wanakuwa na mipango kabambe na inakuwemo katika ilani za uchaguzi katika kampeni za kisiasa.
Hiyo
BLUE ya mwisho ni assumption yako juu ya nani anaweza kuwa mhusika wa uhalifu huo, lakini utekwaji wa Dr Ulimboka, mauaji ya marehemu Mwangosi, Ulipuaji mabomu kule Arusha mjini, na sasa kumwagiwa tindikali kwa raia wa kigeni tunaanza kusingizia wageni kweli?
Sasa sera ya CCM au CHADEMA kuhusu uhamiaji haramu zimesimama vipi au zinakuwa zinapikwa inapotokea kutokuelewana kwa viongozi wa mataifa haya tu?
Vinginevyo naelewa point yako kwamba wahamiaji haramu ndio target, lakini why now?