Tetesi: System mpya ya malipo yote ya Serikali kupitia Mabenki

Tetesi: System mpya ya malipo yote ya Serikali kupitia Mabenki

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Habari za chini ya kapeti ule usemi wa mzee wa kazi Rais Magufuli kuwa anawaandalia majizi kifo cha mwisho ndani ya Serikali sasa umekuwa kweli.

Habari za kuaminika kutoka ndani inasemekana Serikali imeyapa mabank makubwa matatu hapa nchini kufanya kazi ya agent wa Serikali ktk kukusanya malipo yote ya Serikali tangu ngazi ya wilaya,miji,mikoa na taasisi zote za Serikali.

Wale wahasibu walikuwa wakiandika virisiti fake nakuibia Serikali sasa watafute kazi nyingine maana sasa malipo yote sasa yatafanyika bank na serikali itakuwa iki issue receipt tu. Yani hakuna vidirisha uchwara kuibia wananchi ktk ofisi za serikali wala hakuna pesa ya serikali kupotea kama ilivyo sasa.

Vile system itafanya itakuwa kama vile TRA inavyokusanya mapato yake kwa sasa ambapo kibank inaitwa tax banking ambapo tra wame link system yao ya malipo na sytem ya bank ambapo mtu akienda bank kulipa anaenda na receipt yenye ref number ambapo sio rahisi kubadilisha figure ie kama unalipa tzs 40,000/= bas teller anapo ingiza ref amount iliopo kwenye receipt ndio inatokea no edit labda nilipe 20,000/= no system haitokubali lipa full. Pia eti uku unajaza milion kule uweke laki tano payement inagoma yani hakuna kupindisha malipo wala kupotezea kulipa deni la serikali. Makusanyo yote mwisho wasiku yanaenda bank kuu na serikali ndio inagawa pesa kwa matumizi yani nikiama kwa majizi.

Aina hii ya system ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la mafisadi ambapo hawato kuwa na uwezo wakuandika low est nakujilipa ama kufanya udanganyifu.

Jambo lingine wapo wahasibu walikuwa wakikaa na pesa za malipo na baadae kwenda deposit bank ktk hili wengi walikuwa wakijikopesha na baadae kurudisha this time hakuna hiyo room pesa yote inakusanywa bank n mwisho wewe unacheck system yako kama imeingia yani punde mteja aki deposit ukiingia kwenye mtandao serikali unakuta malipo. Kiukweli hii niatuwa muhimu sana kufikia uchumi wa kati na kama ilivyokwisha wahi kusemwa huyu rais ataleta mapinduzi ya kweli kiuchumi.

Inshort tutegeme vifo vingi vya presha maana no eazy money..
Shime Mh Rais.
 
naona walafi wa madaraka wamejifungia magogoni wanatumbua kodi zetu..
magogoni nayo wameifanya ni ya chama baada ya lile jeshi lao..
jizi kubwa ni lile lililojikabizisha kapu la hazina yeye na mpwa wake..
*matumizi wanaidhinisha wenyewe, wamekua bunge
*CAG ni wao wenyewe, hawakaguliwi..
kanda ya ziwa.
 
nona walafi wa madaraka wamejifungia magogoni wanatumbua kodi zetu..
magogoni nayo wameifanya ni ya chama baada ya lile jeshi lao..
jizi kubwa ni lile lililojikabizisha kapu la hazina yeye na mpwa wake..
*matumizi wanaidhinisha wenyewe, wamekua bunge
*CAG ni wao wenyewe, hawakaguliwi..
kanda ya ziwa.

CAG anakaguliwa
 
escrow ilipigwa na singa singa ambaye ana degree ya wizi kutoka chuo bora duniani akishauriwa na chenge havard lawyer ha ha ha huku majaji wakiwa wasaidizi...

Timu ya Ushindi ile, kila shuti bao
 
Timu ya Ushindi ile, kila shuti bao

ha ha ha wafanyakazi wa halmashauri vidampa tu hawana jeuri ya upigaji wa levo zile..

malipo ya benk tu wanatishika.. huku kina singa walizipiga kutoka bot kabisaaa ha ha ha
 
Back
Top Bottom