Kwenye baadhi ya ma-group ya hizi mambo ambayo yanakutanisha Wadau; siku majina yanatolewa, watu walishangaa kweli kweli na kuhoji what's going on! Kwenye moja ya ma-group haya, mmoja wa Mwana-Group, ambae nae nimemuona kwenye list ya washindi, akatetea kweli kweli na kudai hiyo ilikuwa ni hatua ya awali tu!Ujanijibu kama nilivokuuliza , pia majina wakati wa uteuzi hakuna alietilia maanani maana hakuna alietegemea watashinda
Anyway, I was kinda busy kwahiyo sikuweza kuchangia wala kufuatilia mjadala ule, kwahiyo sishangai haya yanayolalamikiwa leo!
All in all, nadhani hizi hazikuwa tuzo za msanii maarufu bali tuzo za msanii bora!
Suala la kuhoji ni namna gani mshindi alipatikana! Tuzo kama hizi zina namna mbalimbali za kupata mshindi! Namna ya kwanza ni kura za mashabiki kwa 100%! Kwa mfumo kama huo, there's no way hao watoto wangeweza kuingia hata kwenye 3 bora manake mtu kama Wema anaweza kushinda mfululizo hata bila kucheza filamu yoyote!!!
Namna ya pili ni ya Watalaamu peke yake na namna ya tatu ni Kura za Mashabiki + Majaji ambao most likely wanakuwa ni wataalamu wa sanaa husika. Huu ndio mfumo bora kuliko wa kura za mashabiki kwa sababu, ukitumia kura za mashabiki peke yake, ndo pale unakuta Ali Kiba anamshinda Christian Bella, na Diamond Platnumz anamgaragaza Wiz Kid!!!
Na linapokuja suala la Kura za Majaji + Kura za Mashabiki; napo itategemea ni kura za nani zimepewa % kubwa! In most cases, Kura za Majaji ndizo hupewa percentage kubwa, sometimes hata 70%.
Sasa kama hali ndiyo hiyo, usishangae kuona hao madogo wakawa wameshinda kwa sababu hapo sio suala la wewe ni maarufu kiasi gani au una wafuasi wengi kiasi gani; manake hata kama utapigiwa kura za NDIYO na Watanzania wote 55 Million, hiyo itakuwa ni only 30% ya sehemu ya kura zako!!
this's not about who you're but it's all about what you delivered katika kipindi husika! Filamu husika inaweza isiwe maarufu kwa mashabiki lakini wataalamu (Majaji) wakaona ustadi wa waigizaji!