Doyi
JF-Expert Member
- Dec 4, 2011
- 1,845
- 2,347
Uongozi wa kampuni ya loliondo mnahitaj kuwafanyia semina elekez watumishi wenu kitengo cha mizigo
Ipo hivi-:
Tulipanda garI kutoka mwanza kuelekea arusha na tulipokaribia kufika Babati zikiwa zimebaki kama km 35 kuingia Babati mjini tukaanza kuona moshi ndani ya gari na kusikia harufu kama ya kitu kinaungua,abiria tukapiga kelele kwamba kuna hali ya hatari lakin hamkusimama kwa wakat had pale kelele zilipokuwa nyingi ndio mkasimama,abiria wakaomba gari ikaguliwe mkasema hamna kitu hyo harufu eti ni breki oil na huo moshi ni reflection ya mwanga na ukungu wa hali ya hewa,tumezozana hapo nje ya gar mnatulaumu et tumeleta taharuki wakat hamna kitu na kutunanga na kutubagaza kwa kufanya "utoto"....mkaamua kwamba turud ndani ya gari tuendelee na safari ,
Baadhi ya abiria wakaingia ndani ya gari ila wengine wakagoma kwa kuwa walidai kusikia bado kitu kinaungua na wakaomba konda akague mzigo mmoja baada ya mwingine kujua kulikoni
Kwa shingo upande na huku mkiendelea kututupia maneno makali mkafungua boot na kuanza kukagua mizigo
Laaahaulaaa....mlibeba vitu kama kemikal ambazo hata nyie wenyewe hamjui ni kemikali gan ila zilipata mtikisiko wa mda mrefu na kutengeneza msuguano hatimae kutengeneza moto...na mlipofungua ndio moto ukazidi na mizigo hyo ikatolewa nje na kuendelea kuungulia nje,kwa kweli nimewadharau sana yaani kweli abiria tunatoa hali ya tahadhari mnatuona sie watoto hatujui harufu ya breki au tairi...bahat mbaya mizigo mwingine wa dagaa nao ulianza kushika moto...najiuliza tusingeshituka moto ukashika tenk la mafuta ingekuwaje mda huu???
Sisi kama abiria tunawashauri kitengo cha mizigo pale mwanza muwape mafunzo ya nini hawatakiwi kuchukua na ikibidi muwe mnakagua mizigo gan mnabeba,mtakuja kuuwa watu kwa tamaa za hao wachache na kuharibu brand ya kampuni yenu nzuri.naomba niishie hapo ila uongozi kama mkiona hili tangazo fanyieni kazi hayo mapungufu