Taa ya kuongozea magari Kinondoni Biafra inakaribia kuanguka, kodi kubwa tunazolipa zitumike vizuri!
Wakuu,
Hizi ni taa zipo Kinondoni Biafra, Dar. Moja imejishikilia vizuri wakati nyingine inakaribia kuanguka. Naamini kufanyiwa maboresho sasa ni bora na itakuwa gharama nafuu kuliko kusubiri ianguke iharibike zaidi.
Kodi zetu ndio zinawezesha ukarabati huo kufanyika na kama ikiachwa ikaanguka na kuharibika zaidi ni kodi zetu hizi hizi ndio zitatumika kununu mpya. Mamlaka husika wajibikeni kwenye hili, gharama za maisha zimepanda sana kuacha kodi za wananchi zipotee kizembe hivi.