DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Kibaya zaidi katika eneo hilo hakuna traffic maalum ambaye anakaa kama mbadala ili kuongoza magari labda inapotokea hali imekuwa mbaya zaidi ndipo anajitokeza askari wa kawaida kutoa msaada kuongoza magari, tofauti na hivyo muda mwingi unawakuta kondakta wa daladala ndio wanashuka kwenye magari yao na kuanza kutoa msaada hili magari yaweze kutembea.
Wito wangu wa mamlaka husika, taa hizo kama zimeharibika zifanyiwe matengenezo, ambavyo kutofanya hivyo kwa kipindi kirefu ni kukosa uwajibikaji stahiki hali ambayo inahatarisha usalama wa Watumiaji wa barabara katika kipindi ambacho usalama wa barabarani umekuwa ukisisitwa zaidi na mamlaka.
Kama mamlaka husika haziwezi kuchukua hatua za kuhakikisha mataa hayo yanafanya kazi muda wote basi katika eneo hilo waweke Traffic ambaye atatekeleza majukumu ya kuongoza magari muda wote kama ambavyo tumekuwa tukiona kwenye baadhi ya maeneo ili kuepusha msongamano wa magari ambao ni kero.