Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Matumizi ya zebra kwa waendao kwa miguu maeneo yenye taa, yanaongozwa na taa za barabarani. Na hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 65(7)(b) na 65 (8).
Jukumu la kuheshimu taa za barabarani ni la watumiaji wote wa barabara na sio magari tu. Hivyo basi, kwa mujibu wa kifungu cha 65 (7)(b) muenda kwa miguu hatakiwi kuingia barabarani baada ya kuwa magari yameruhusiwa na taa au askari kuendelea na safari. Kufanya hivyo ni kosa la kutokutii alama na maelekezo kwa huyu muenda kwa miguu.
Maana yake ni kwamba taa zikisharihusu magari yaende kwa kuwaka kijani, dereva hatakiwi tena kusimama kwenye zebra kupisha mtu aliyesimama kando mwa barabara akitaka kuvuka, mwenda kwa miguu husika inabidi asubiri taa yake. Hii ndio sheria hata pale askari anapoongoza magari. Gari hazitasimama kwenye zebra hadi askari asimamishe hizo gari na kuruhusu waenda kwa miguu.
Dereva anachokatazwa kufanya kwenye makutano yanayoongozwa na taa yakiwa na zebra
Dereva hatakiwi kuondoka hata kama taa yake (kijani) imemruhusu kuendelea na safari, hadi mwenda kwa miguu aliyekuwa akivuka wakati huo amemaliza kuvuka.
Kwa maana ya kwamba upande wa dereva iliwaka taa nyekundu na upande wa mwenda kwa miguu iliwaka ya kijani kumruhusu apite. Sasa wakati mwenda kwa miguu anapita taa yake ya kijani ikazima ikawaka nyekundu wakati upande wa dereva ikawaka kijani. Wakati huu mwenda kwa miguu bado hajamaliza kuvuka.
Katika mazingira haya dereva unatakiwa na sheria kusubiri huyu amalize kuvuka kabla hujaondoa gari. Na hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 65 (9) cha sheria ya usalama barabarani Tanzania.
Hivyo kwa eneo kama fire ukitokea Muhimbili kukunja kushoto kwenda mjini, iwapo itawaka taa ya kijani kuruhusu magari muenda kwa miguu hatakiwi kuvuka hadi taa yake ya kijani imewaka kumruhusu avuke kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Kwa pale Fire toka upande wa fire kwenda kariakoo au upande wa kariakoo kwenda jengo la fire lilipo.
Hali ni tofauti na makutano ya barabara ya Bibi Titi na Morogoro eneo la akiba. Pale kuna taa za waenda kwa miguu na taa za magari. Iwapo taa za magari zimewaka dereva anayepinda kushoto kutokea DIT kuelekea posta anatakiwa pia kuangalia taa za waenda kwa miguu kwenye ile filter. Ikiwaka NYEKUNDU lazima asimame hata kama kwenye main road ile ya BRT taa bado za kijani. Kusimama huku kunafanywa ili kuruhusu waenda kwa miguu wavuke.
Maeneo mengine ni yale yenye filter light. Kama ilivyokuwa pale TAZARA zamani. Kwamba ukitokea gongo la mboto kupinda kushoto kwenda buguruni. Pale kulikuwa na taa ya mshale (ndio hiyo nimeiita filter light) ambayo ndiyo inakuruhusu kupinda kushoto. Kwa hiyo kama gari za kutoka Tazara kwenda mjini zimesimamishwa, wewe unayepinda kwenda buguruni huruhusiwi kufanya hivyo hadi filter light yako imewaka green kukuashiria kupinda kushoto. Hii taa ipo pia eneo la NAMANGA kupinda kulia kuelekea Msasani.
Kwa maeneo yasiyo na hii taa, basi dereva ataendelea kupinda kushoto au kulia iwapo taa kubwa ya mviringo iliyopo main road imewaka Kijani. Kwani tayari taa za upande mwingine zitakuwa zimezuia gari kuelekea upande unaotaka kwenda. Hiki ndicho kinachofanyika TAZARA kwa sasa. Zikiruhusiwa gari za kwenda mjini na zile za kupinda kushoto kwenda buguruni zinakwenda.
Ni imani yangu makala hii imesaidia kukujuza matumizi ya zebra eneo la makutano yanayoongozwa na taa.
Kwa hisani ya RSA Tanzania