Taa zikisharuhusu magari yaende, dereva hatakiwi tena kusimama kwenye zebra. Mtembea kwa miguu asubiri taa yake

Nje ya kidogo ya mada

Kuna wale madereva ambao wakiona tu taa ya kijani imewaka wanaanza kupiga honi.. wanakera
Ile ni sawa Kwani Kuna waenda Kwa miguu wengine wanaunga msururu bila kujali muda wao umekwisha!! Taa ni muda maalumu, sema sekunde 30, ukiendelea kuruhusu watu wapite muda wako utakwisha, lazima uwasimamishe Kwa honi,
 
Kuna watembea kwa miguu huwa wanavuka barabara kwenye zebra kwa maringo kama twiga
Wengi wanasema Magufuli aliwaruhusu wavuke kwa raha zao, ili wasiendelee kunyanyaswa na wenye magari.
Wengine wanasema kuwa ni Laisi wa Wanyonge ndio alievumbua mistari ya kuvukia Wanyonge

 
Hii hata DSM ipo, hii inaitwa obstruction, Madereva wengi ni wazembe, ndio inalazimu askari wengi kujiweka katikati ya barabara kusaidia
 
Uko sawa sawia.....
 
Elimu hii inatakiwa itolewe sana kwa watembea kwa miguu, hasa wanaotumia hizi barabara mpya mfano hii ya Mwenge-Morocco, Mwenge-Ubungo maana kuna zebra nyingi sana ambazo zinaongozwa na taa. Sasa watembeaji wengi hawajui kama wakifika pale wanatakiwa wafuate taa zinasemaje, badala yake huwa wanavuka tu labda kwa kukimbia wakishindana na wenye magari kitu ambacho ni hatari. Mwaka jana mwishoni nilishuhudia mtu akigongwa pale kwenye taa za Mwenge ITV ambapo alivuka wakati taa zimeruhusu magari, nikaona kuna umuhimu mkubwa sana wa kutoa elimu ya usalama barabarani hasa kwa watembea kwa miguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…