Mchalinze
JF-Expert Member
- Jun 7, 2025
- 266
- 735
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa barabara za katikati ya mji (Posta Mpya/Sanamu la Askari). Kuna changamoto kubwa ya kimfumo (design fault) kwenye taa za kuongozea watembea kwa miguu katika eneo la Sanamu la Askari.
Shida iko wapi?
Taa za kuongozea watembea kwa miguu kwenye kile kivuko zimeelekezwa upande wa watembea kwa miguu pekee (zinaangalia pembezoni mwa barabara au upande watu wanakovukia). Matokeo yake:
Dereva anayekuja na gari haoni taa hiyo: Dereva akiwa barabarani hana uwezo wa kuona kama taa imemruhusu mtembea kwa miguu kuvuka au la, kwa sababu hana mwonekano (angle) wa taa hizo.
Mgongano wa haki ya njia: Mtembea kwa miguu anapoona taa imemruhusu (kijani), anaanza kuvuka akiamini yuko salama. Lakini madereva wanaendelea kupita kwa sababu hawajui kama watu wameruhusiwa au la.
Hali hii inasababisha madereva kutokusimama hata wakati taa zikiwa kijani kwa watembea kwa miguu jambo linalohatarisha maisha ya raia na wageni wengi wanaovuka hapo kila siku.
Wito kwa Mamlaka (TARURA / TANROADS / Jeshi la Polisi Usalama Barabarani): Zirekebishwe taa hizo au ziongezwe taa za madereva (repeater signals) zinazoonyesha wazi kuwa kivuko cha Zebra kimeruhusu watembea kwa miguu ili madereva wasimame.
Kuwekwe alama za wazi au taa za kuwasaidia madereva kujua wanakaribia kivuko kinachotumia taa.
Ni vizuri kero hii ikafanyiwa kazi mapema kabla hajasababishwa ajali au maafa katika eneo hilo lenye mzunguko mkubwa wa watu.