Travellar jr
Member
- Sep 17, 2023
- 34
- 69
Wakuu habari za muda huu 🤝
Kuna namna fulani threads za hapa JF zinavyokuwa na mambo ya taasisi mbalimbali zinazolipa vizuri Tanzania, ukizisoma unajikuta unasema, “Dah, Mungu siku moja na mimi anione.”
Aisee kuna baadhi ya threads ukikaa ukasoma experiences za watu, career journeys zao na taasisi walizowahi kufanya kazi au kujitolea, unaweza kuacha ndala kabisa.
Basi leo nimeamua kufufua thread yangu kwa design yangu mwenyewe.
Mimi ni mwanafunzi wa UDOM, nasoma Bachelor of Arts in Economics (specialization in Environmental and Natural Resources), na sasa naelekea kuingia mwaka wangu wa mwisho wa masomo.
Ninaomba sana ndugu zangu humu ndani wenye experience katika sekta mbalimbali, hasa Dodoma, kama kuna taasisi nzuri zinazopokea watu kwa kujitolea, internship, volunteer work au hata opportunities za kujifunza, mnishike mkono kwa experience zenu. 🙏
Hata field nilipambana kupata sehemu nzuri lakini sikubahatika aisee. 🥲Nakumbuka nilijaribu kupeleka barua NEMC, EWURA na sehemu nyingine, lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia.
Sasa leo nimekaa zangu maghetoni kwangu huku Dodoma, sina hata kazi ya kusaidia fundi 😂, nikasema ngoja niingie JF kwanza nikapate muongozo wa mabrother zangu.
Kitu kingine kinachonifanya nipende sana threads hizi ni kuona watu wakitoa experiences zao za career. Kuna raha fulani unapata unapomsoma mtu akisema alianza kama volunteer/intern, akapitia taasisi fulani, akapata experience, mpaka kufika sehemu nzuri. Inatia moyo sana hasa kwa sisi ambao bado tupo chuoni.
Kwa hiyo naomba pia mabrother na masister waliosoma au wanaofanya kazi kwenye maeneo kama:
- Economics
- Taxation
- Accounting
- Finance
- Procurement
- HR
- Environmental Economics
- Renewable Energy Engineering
- Energy sector
- Banking
- Government institutions
- NGOs na development organizations
mtupe experience zenu.
Taasisi mlizowahi kujitolea, internship mlizofanya, namna mlivyopata nafasi, skills mlizojifunza, challenges mlizokutana nazo na hata mambo ambayo mngependa mtu angewaambia mlipokuwa bado chuoni.
Na hata kama unaona una connection au nafasi fulani nzuri, usisite kutushika mkono.
Internship, volunteer opportunity, attachment, research project au hata mwaliko wa “njoo tu uje uone mazingira ya kazi” tunapokea kwa moyo wote. 😂😂
Lengo la thread hii si mimi peke yangu. Natamani iwe sehemu ambayo sisi wadogo zenu tunapata mwanga, connections na matumaini kabla hatujaingia rasmi kwenye soko la ajira.
Na msione aibu kujisifia kidogo pia 😂. Kama umeanzia chini, ukaenda volunteer, ukapata internship, ukapata connection, ukafika kwenye taasisi nzuri—tupatie story yako.
Hasa ukute mtu wa taaluma yako amepitia njia kama unayotaka kupitia, unaweza kupata direction kubwa sana.
Mabrother na masister, tushikeni mikono kidogo.
Tupo chuoni, lakini maisha baada ya chuo yanaanza kututazama sasa hivi. 😂
Ahsanteni sana waheshimiwa. Karibuni kwenye thread. 🤝