Taarifa: Aina mpya ya utapeli mjini

Taarifa: Aina mpya ya utapeli mjini

Nadhani hata humu ni mahala sahihi pakutolea taarifa hii:

Kumekua na wimbi la utapeli unaofanyika na watu wanaojipambanua kua wanahusika na kampuni ya usambazaji wa mayai ya kisasa, watu hawa uwaambia wateja watume fedha nusu kwa kiasi cha idadi ya tray za mayai wanazotaka then nusu iliyobaki watawalipa watakapo fikisha mzigo sehemu husika hivyo mtu akituma hiyo fedha basi imekua ameshatapeliwa.

Namba anayotumia kufanya utapeli ni 0786869108 mtu huyu anasema yupo kisiju na mbeya.

Hivyo vyombo husika tunaomba mshuulikie swala hili kikamilifu
Umesahau kuweka namba za waliotapeliwa ili vyombo husika viweze kupata ushahidi wa utapeli
 
Kuna mtu aliniletea hoja ya biashara ya maharage kwa bei karibia nusu ya bei halisi nikamwambia leta hata tani 100 nitalipa yakifika. Basi akaanza danadana mwisho ananiambia nimtumie pesa kwani sehemu imetangulia. Nikamjibu asubiri ikifika namlipa. Hadi leo (more than 5 years) bado nasubiri mzigo ufike nilipe. Kifupi usilipe pesa kizembe kwa yeyote hata kama unamfahamu utalizwa
 
Binadamu wa ajabu sana


Mtu anakupigia simu yupo mbeya anauza mayai ya jumla na wewe upo kigoma unaomba utumiwe mayai na hela unatuma duh

Mi nadhan tumpongeze aliyewatapel maana mazuzu hawaishi hapa Tanzania
😄😄😄😄😄
 
Utapeli gani sasa hapa...huo ni ujinga wa huyo mtumaji hela
 
Niungane nawe, unatapeliwaje kijingajinga, mtu mzima unatumaje hela ya mayai wakati ukitembea mjini station za wauza mayai wa jumla kibao, labda kama yeye alikuwa na nia ya kutapeli akatapeliwa.

Maana kafanya mawasiliano na walio Kisiju na walio Mbeya.

Everyday is Saturday... 😎
Nadhani mkuu umenena vema lengo lake ni kutapeli kumbe mtego umewekwa tayari kumkiza hiyo advance payment yake
 
Back
Top Bottom