DOKEZO Taarifa Binafsi zinakusanywa na "Kampuni za Mikopo Mtandaoni" ni Hatarishi kwa Faragha ya Mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umetufungua macho sasa


tunatokaje ikiwa tushaingia kwenye mfumo🤔
 
Ukishaona jambo linalalamikiwa ila lipo tu na serikali haifanyi lolote ujue mwenye jambo huenda ni sehemu ya wanaopelekewa malalamiko. Unachotakiwa kufanya, USIKOPE HUKO.
 
TAARIFA YA HABARI - AZAM TV 20/03/2024

KUHUSU MIKOPO YA MTANDAONI

video hapa hichi👎
Your browser is not able to display this video.
 
TAHADHARI KUHUSU APP YEYOTE INAYOTOA MKOPO KWA MUDA YA SIKU 7. Serekali haikubali mikopo kama haya.

Tunawezakujadiliana mengi kuhusu aplikesheni hizi lakini ukweli ni kwamba watanzania wanahitaji hela na wanakopa sana. Hiyo kitu haitaisha. Lakini ngoja nitoe elimu yangu kidogo.

Nataka kutoa elimu kidogo kwa wale wanaosema hawalipi deni zao. Mimi ni mtafiti na nimesoma na kufanya utafiti kuhusu mikopo ya kidijitali.

Ni kweli kwamba siku hizi kuna aplikeshini za wachina, na wana riba kubwa na hawatoi huduma nzuri. Lakini kuna baadhi ya aplikesheni na huduma zinazoaminika na wanatoa huduma safi. Hawatumi sms kwa contacts yako kamą ukichelewa kulipa

Inabidi tujifunze kutenganisha kati ya huduma nzuri na hawa kama PesaX/CashX/MkopoWako/TwigaLoans.

Mkopo inayoanzia na siku 28 n.k zinafaa kidogo lakini hakikisha ume elewa riba na ada za ucheleweshaji.

Watu wa tanzania hawana elimu kuhusu kile kinachotoke wasiporejesha mkopo. Wanafikiri wapo smart na hakuna kitakachofanyika, ila hizi app zinachukua NIDA yako na kuripoti taarifa hizo kwenye credit bureau. Credit bureau ni shirika inayosanya data kuhusu ulipaji wa madeni kutoka mikopo ya kidijitali na benki zote.

Ofisi hizi za credit bureau zina jukumu la kukupa alama kulingana na tabia yako ya kukopa, ili kujua kama unaaminika au la.

Sasa hasara za kukopa zitakapo ongezeka sana, hizi makampuni wataanza kupata taarifa kutoka kwa credit bureau ili kabla ya kukupa mkopo waangalie kama unamadeni.

Siku za hivi karibuni, kila mtu ambaye amecheza na mikopo hii na kukimbia bila kulipa atawekwa kwenye orodha na hataweza kukopa tena.

Kwa hivyo jihadhari, usichukue mkopo kwa kujifurahisha na ulipe mkopo wako kwa wakati au hata ukichelewesha, hakikisha umeurudisha.
 
Nilienda kuuliza utaratibu wa kukopa simu sehemu nikaambiwa,sharti lwa kwanza nisiwe na mkopo sehemu yoyote,iwe bank,kampuni nyingine za mikopo ya simu,wala mikopo online,nikaondoka.

Nilipokwenda ktk simu za samsung sikukutana na shart hilo,wale wa awali niliwashangaa lakini nikatafakari labda ndio namna bora wameona ni salama kujihakikishia malipo ya simu yao,lakini nikaona mbona wanakosa wateja kwa mashart ya kijinga,kweli kuna watu wana mikopo chefu chefu kwenye hivyo vitaasisi vya kiosk,lakini vipi kwa watu wenye mikopk rasmj kutoka ktk taasisi zinazoeleweka na hawana historia mbaya ya kutorejesha???

JUkumu a mkopeshaji ni kuhakikisha kwa namna yoyote anatoa mkopo akiwa na uhakika 100% utarejeshwa bila msuguano na mkopeshwaji sio ategemee huruma ya mkopaji,
Utaghairi kumkopesha sababu hana historia nzuri,nayeye ataangalia wapi kuna kampuni inayoweza kumpa kwa hali hiyo hiyo bila tatizo.
 
ALAFU HATA UKIWASHALIPA WANASUMBUA ETI KOPA TENA. YAANI KITENDO CHA KUA NA NAMB ZAKO NI MAKOSA MAKUBWA. WANASUMBUA HADI NDGU ETI KOPA USTAWI LOAN, SIJUI BOBA CASH 🤣🤣🤣
 
Kwahiyo ukikopa app ndio inakuomba access kwenye hivyo vitu?? Je ukikataa kutoa permission?? Wao watapata vipi taarifa zako??
 
Bila wapinzani kuliongelea hili jambo, watawala hawawezi kushituka.
 
Uliwaza mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…