SoC04 Taarifa Binafsi zinazokusanywa na Makampuni ya mikopo Ya Online ni hatarishi kwa Faragha ya Mtu

SoC04 Taarifa Binafsi zinazokusanywa na Makampuni ya mikopo Ya Online ni hatarishi kwa Faragha ya Mtu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Otman Moood

Member
Joined
Jul 12, 2022
Posts
27
Reaction score
12
Siku hizi kumekuwa na Kampuni nyingi za Mikopo Online kama
Branch, PesaX, Twiga Loan, Mloan, Cash X. Bongopesa

Na watu bila kuwa makini mtakuja jikuta mnaingia matatizoni kutoka na taarifa zinazokusanywa na Kampuni hizi.

Nimejaribu kadhaa na hakuna ya afadhali, unakuta inakusanya taarifa hizi:-
  • SMS - yan wanaweza kusoma sms zote zilizoingia katika namba yako uliyosajilia, hii ikujumuisha sms za miamala, mapenz, siri za familia na kadharika je unahisi upo salama?
  • CONTACTS - wanaweza kuona majina na namba zote ulizosave kwenye simu yako unahisi watu wako watakuwa salama?
  • CAMERA - hii wanaweza kurekodi au kupiga picha bila wewe kujua na hapa ndo linapokuja swala zima la connections kuvuja
  • STORAGE - wanaweza ku-access picha, video, na files zote zilizoseviwa kwenye simu yako, je unahisi wataacha kushare na wwngine siri zako?
  • APPS - wanaweza kuona app zote kwenye simu na kuzifikia, hii ikijumlisha WhatsApp, IG, app za kutunz afaragha zako n.k
  • TAARIFA BINAFSI - kama Vyeti, elimu, kazi, mahala pa kuishi, urefu, picha zako, unadhan utakuwa salama mtu kuwa na taarifa zako zote..
Ikatokea mfanyakaz akatoka hapo tayar anajua siri za wengi, na ni rahisi kuzitumia kuscam watu mitandaoni
Watanzania tuweni makini na maamuzi yetu, hizi ndo huchangia watu kudhalilika mitandaoni, na kutoa siri za watu kama history za bank, miamala, chati za siri na faragha za watu, je unahisi utakuwa salama wewe na uwapendao?.

Mamlaka ishughulikie hawa watu wanapata wapi dhamana ya kukusanya taarifa za watu kama Sensa ya Kidigitali?

Mdau weka screen ya App ya Mikopo tuone taarifa wanazokusanya kwenye Simu yako.

1.png
2.png
3.png
 
Upvote 2
Back
Top Bottom