Taarifa fupi juu ya kwanini SIMBA walizuiwa kuingia uwanjani -Lupaso

Mambo ya wachawi wa pangani waliomtuma hersi saidi.

Washindwe na walegee.
 
Kama hii ndiyo taarifa fupi, Ndefu itakuwaje?

Rage ajengewe sanamu
 
Unajua umeonesha wapi ujinga wako zaidi? Uliposema unasisitiza hatuwezi kuwa na mpira unaoendeshwa kishirikina alafu hapo hapo unasifia simba kwenda kutegua mabomu kitendo ambacho kimsingi ni ushirikina
 
Saa tatu MNYAMA anaibuka kimya kimya LUPASO , Yanga inapewa info SSC imefika…. ; wakasisitiza wasiruhusiwe.
Mbongo kila tukio lazima aitungie stori halafu atajifanya za ndani kabisa. Watu wamewaona Simba wamefika uwanja wa Mkapa saa moja na dakika 20 na kuondoka saa tatu baada ya kuzuiliwa, wewe unatudanganya eti saa tatu Simba ndio wamefika Lupaso.
 
Uwongo wako unaanzia hapo kwenye 51mba kufika eneo la nje ya uwanja saa 3 usiku..!!!
 
Acha story za kijiweni! Sababu ya simba kwenda kufanya mazoezi usiku na bila taarifa ilikuwa ni moja tu! Wazuiliwe kuingia, ili wapate kisingizio cha kususia mechi baada ya kufanya tathmini ya kina na kugundua wangeangushiwa kichapo cha mbwa mwizi.

Sidhani kama kuna sababu nyingine yenye mashiko zaidi ya hii.
 
Nonsense
 
Hii timu inaendeshwa kihuni sana. Wamesahau wamefungwa mechi nne mfululizo na hao wachezaji wao ambao wangekosekana ile juzi! Yaani wakubali tu hata hiyo mechi ikirudiwa kutokana na utoto wao wa kususia, na pia kulindwa na Bodi ya ligi; bado watafungwa tu.
 
Mbona umejivua heshima ww mzee jamani...hata sheria za mpira huzijui au? SIMBA imefika saa moja uwanjani na kanuni zinamtaka au zinamfeva mgeni kufanya mazoeizi muda ule atakaocheza mechi..
Mbona utopolo unawatopoa kabisa akili zenu...
Kuna ushahid wa kila namna Simba kufika pale saa moja...na kuondoka saa tatu
Nyie ndo mliogopa kupigwa kipigo cha mbwa koko..mkafanya ya kufanya ili simba isuse.....kama sio kuvundika majanaba uwanjani...mkajua leo wakija hawa wataondoa vi mzizi..
Uwiiiiiiiiiiiii
 
Sasa kulikuwa kuna ugumu gani wa kutoa taarifa kwa wenyeni wenu, na kuchagua kwenda kimya kimya?
Na sababu ya kuzuiliwa kufanya hayo mazoezi siku ya mwisho ndiyo yasababishe msusie mechi iliyotangazwa kwa zaidi ya mwezi!

Nyinyi semeni tu mliogopa kichapo.
 
Ww hatupelekeshwi aiseee...kama mlikua mna uhakika wa kufunga why muanze kuhara mapema?? Aisee mna bahati sana ilikua ni kilio jangwani jmos..
Kwaheri
 
Kutofuata kanuni na sheria Tanzania ni jambo la kawaida, Si kwenye mpira tu bali hadi kwenye siasa.
Haya ya Yanga na Simba ni matokeo ya tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…