Taarifa kutoka hospitali aliyopo Wastara kuhusu matibabu yake

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260

Siku ya February 10, 2018 imetolewa taarifa na Masoud Kaftany ambaye ni Afisa Habari, Uenezi , Mahusiano katika chama cha Waigizaji Kinondoni, kuhusu Muigizaji Wastara Juma taarifa hiyo inasema Wastara ameshafanyiwa Vipimo (Operation ) na anaendelea kupatiwa Matibabu.

Muigizaji Wastara ambaye yupo katika Hospitali ya Saifee (Mumbai ) Nchini India anaendelea vizuri na siku hiyo ya jana alitembelewa hospitalini na Muigizaji wa Bongomovie REGINA KAOLE ambaye yupo Mumbai nchini India kwa shughuli zake za kikazi.

Wanatasnia na wadau wa filam nchini wanaombwa kuzidi kumuombea Muigizaji huyo Wastara ili apone Haraka na kurejea nchini salama.



Chanzo: Millard Ayo.
 
Nauliza Tu Hizi Picha Zote Ni Kutoka Hospital Alikofanyiwa Upasuaji???

Mbona Naona Nyingine Kasuka Na Nyingine Kavaa Wigi Na Room Pia Zikotofauti Au Mimi Sioni Vizuri???

Na Kulikuwa Na Umuhimu Gani Wa Kuweka Picha Ambazo Haziendani Na Content Ya Post Au Ndio Ule Usanii Bado Tunaendelea Nao???

Ila Namtakia Kila La Kheri Na Mungu Amuongoze Ili Apone Aweze Kurudi Nyumbani Akiwa Mzima Na Buheri Wa Afya
 
aiseee kumbe umeona ..hahaa ana wiving then kasuka ..hii Kali aisee..kwahiyo amelazwa huku anasuka huko huko hospital
 
Halafu leo amelala wakati jana nilimuona kwa da'Mange akiwa amekaa, ha ha ha. Mange kawaambukizeni chuki zake zilizojaa wivu na husda.
 
Hiyo picha anayoonekana amekalia viti vya plastic itakuwa ya Tanzania. Hospitali za India hawana viti vya plastic!
 
Sasa wabongo kwa kujifanya wajuaji ooohhhh sijui Cannula imekaaje .

Achen mbwembwe zenu bana , hamna MTU anayeweza kutumia ugonjwa wake kujistarehesha.

KILIO CHA MTU MZIMA HUWA KINA UCHUNGU BANA !!.

Mliniboa sana nyote mlokalia kumponda mwanadada huyu.
 
Nadhani anahamishwa hamishwa hospital na saloon mbali mbali kwa ajili ya kubadilisha mtindo wa nywele
 
Yaani ukipewa Msaada unageuka kuwa mtumwa maana itakulazimu kuwahakikishia Raia kuwa ule Msaada unatumika kama ilivyopangwa.

Ndo maana Wastara anaangaika hivi, mara picha atume, mara ajirekodi tu-clip kidogo atume,
Sasa anapofanya yote hayo lazima ajiweke fresh katika suala zima la cosmetics huwezi kukurupuka maana wabongo mngeanza maneno yenu "ooohh hata kama kuumwa ndo uwe rough hivyo"

Afu watu hawajui kitu kimoja, unapoenda kutibiwa nje au hata hapa nchini lkn upo kibinafsi au Upo grade kama inavyojulikana Basi unaishi kama Mfalme unakuwa kama Upo home tu because you pay for all services.

Hii ndo Inaitwa operation monickbird....... Yaani uongo uenezwa kwa kasi mpaka watu uamini ni kweli kama Mange Kimambi alivyofanya kwa Wastara.
 
Hizi hospital zetu shida tupu!

Hiyo picha ya kwanza mbona anafanyiws matibabu huku akiwa amevaa suruali na kachumba ni km kadogo km choo, ila pia hicho kiti alichokaliwa ni kweli Hiyo ni hospital iliyopo India??

Na huyu jamaa anaemfungua/funga mguu ni mhindi kweli, mbona km mweusi??


Km bi hivyo basi Bora hata angetibiwa akiwa Tanzania!
 
Wabongo watu waajabu sana !! msaada hawakumpa wao lkn sasa MTU anataka kujua mpaka Matibabu anayopewa.
 
nilijuwa uongozi wa hospitali umetoa taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…