Uchaguzi 2020 Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua

Sasa unataka waingie na simu wapige picha waanze kutuma matokeo wakati sio kazi yao unaona kabisa ndio wanakuwaga chanzo cha migogoro.. BiG UP NEC na wachunguzwe hata saa za mkononi zinakua na camera wasiingie nazo watatuletea shida
 
Acha kuweweseka, awamu hii hakuna wizi wa kura
 
Sasa simu kituoni za kazi gani? Sio lazima kupinga kila kitu. Kama uchaguzi mnashinda mtashinda na kama mnashindwa mtashindwa hata mkiingia na computer [emoji985] maana wananchi ndio wanaamua. Msilazimishe kuonekana kwamba mnaonewa kwenye kila jambo. Wakati kiukweli inaonekana upinzani maji yapo kidevuni.
 
Wamelenga kuiba kura

Sheria zinazoongezwa hizi katikati ya mechi hazina nia njema.

Sasa hivi ni muda wa mechi taratibu, kanuni na sheria mpya si muda wake.

Sheria, kanuni na taratibu mpya mpya zote hizi hazikubaliki. Sote wenye nia njema ya kuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki tuungane kukemea na kuyakataa haya kwa nguvu zetu zote.

Aluta continua!
 

Kama simu hazina madhara kwa nini tushindanie suala la simu?

Ninyi simu zinawakera nini?

Sheria inayozuia simu iko wapi au ndiyo hizi mpya mpya kila mkiamka mna jipya?
 

Hatuaimini tume maana ni moja ya taasisi zinazotumika kuharibu uchaguzi na wizi wa kura.
 
Utetezi dhaifu, kila wakala awe na matokeo kutoka kwenye fomu gani za matokeo? Mnataka kuleta matokeo ya wizi?
 
Hoja Hafifu kabisa..
Mawakala tayari wameaminika na Vyama vyao na sidhani kama kuna uhitaji wa kua na simu kwenye vituo na sidhani kama sheria inaelekeza kufanya hivyo.
 
Brother hebu nielimishe kidogo. Kama kuna document imeandikwa "CCM ni chama tawala." Wewe ukatumia simu yako kuipiga picha na mimi ninatumia simu yangu kupiga picha document HIYOHIYO unataka kusema kuna uwezekano wa picha moja itaonyesha CCM Ni chama tawala na nyingine inaweza kuonyesha CHADEMA ni chama tawala? Au unataka kusema je? Nitwange shule kidogo nieleweke ndugu yangu!
 
Mkuu penda kufikirisha ubongo otherwise kichwa kinaweza kuwa mzigo usiyo na maana kwa miguu,NEC inasema mawakala siyo lazima kupewa nakala za matokeo na wakati huohuo inakataza simu kuhifadhi matokeo,Si ndo upuuz huu
 
Penye dhambi ni mahala palipo na giza na usiri mkubwa. Wanazuia simu ili wapate mwanya wa kuchezea matokeo.
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ Juakalee matokea hutangazwa na tume tu sio mpiga kuraa..na safari hii hata fomu za matokeo hawatapewa maana ni za tume sio wakala..πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›..hizo ni kanuni za TUME yetu kwa uchaguzi huu tuu. Hapa CCM tusiposhinda walahhaa tutakuwa wajinga..
 
Sasa unataka waingie na simu wapige picha waanze kutuma matokeo wakati sio kazi yao unaona kabisa ndio wanakuwaga chanzo cha migogoro.. BiG UP NEC na wachunguzwe hata saa za mkononi zinakua na camera wasiingie nazo watatuletea shida
Mgogoro unatoka wapi wakati matokeo yanahesabiwa na kurekodiwa na mawakala wote. Tume isisahau tumeonyeshwa uchaguzi huru na wa wazi kabisa (mbashara) na chaguzi za ndani za vyama CCM na Chadema , huu usiri wa TUME faida yake nini? . Chaguzi za ndani za vyama zimeonywashwa mbashara nyie mnaficha nini? Mnajitafutia lawama isiyo na sababu. Njia pekee ya TUME kujivua lawama ni kuweka mambo hadharani . HATUJASIKIA MGOMBEA HATA MMOJA AKIMLAUMU MSIMAMIZI WA UCHAGUZI katika chaguzi za ndani za vyama , lawama zote zimenda kwa WAJUMBE. TUME jivueni lawama , Lawama ziende kwa wapiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…