Taarifa kwa Umma kuhusu Ajira za Walimu

MRISHO KOMBO

Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
31
Reaction score
2
Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki nazo.

Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.

Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu,

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

23 Machi, 2015

 
Aaàaaaàah.....sasa mwezi wanne ndio wanatoa majina au.

mm jana nilipata habari ya kuchekesha kwa gvment yetu. Eti wameshaa fanya kila kitu hadi allocation ila wanasubiria pesa. Sasa najiuliza hiyo bajeti ni ya mwaka jana au ya mwaka huu. Pesa ilishaaa tengwa nini shida tena.

Ma chichiemu nòouma. ila wao ndio wameshikilia makali ndio maaana hatuwezi kuwafanya lolote. Ila bana humu ndani kuna watu wanajua hadi waliko pangwa na tareh za kuripoti.

chrzea bongoòoo nini veve?

believe me or not.
 

Ni figure tu zile sio pesa ambazo tayari zilikuwepo coz bajeti ni makadirio ya mapato na matumizi hivyo inawezekana pesa zilizotengwa kwa wizara husika hazijapelekwa zote ukizingatia bajeti ya nchi inAtegemea wahisani kwa asilimia kadhaa,

kwa maaa hiyo inawezekana kuna tatizo la pesa na ilisemekana baadhi ya wahisani waligoma kutoa pesa na nasikia hivi karibuni ndo wameridhia kutoa huenda mara baada ya kupata hizo pesa wakaajiri.
 
MRISHO KOMBO,

Tangazo lako umelichakachua mkuu, kwenye website ya MOEVT lisomeka kuwa limetolewa trh 23 march!!
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jambo tata.
Nimejaribu kuwasiliana na wabunge tofauti nikiwashinikiza wauleze swali kwa TAMISEMI, but wote wamekua na majibu ambayo sikutegemea!
 
mkuu majina huwa yanatolewa website ya MOEVT halafu TAMISEMI wao huwa watoa taarifa tu! Ndivyo ninavyofahamu ila huyo nae aliyeleta tangazo apelekwe milembe!

Mkuu you ar wrong, ilikua kipindi cha nyuma ila kuanzia mwaka juz wizara ya elimu imejitoa , ajira ni jukumu la Tamisemi...
 
Hili ni jambo tata.
Nimejaribu kuwasiliana na wabunge tofauti nikiwashinikiza wauleze swali kwa TAMISEMI, but wote wamekua na majibu ambayo sikutegemea!
Jibu lake hili hapa chini

nyamwenga said:
mkuu wabunge wote wanawaza kama watarudi mjengoni awamu ijayo au la! Bunge hili wabunge huwa wanastress sana wala usitegemee swali km hilo!

Na kutokana na stress zao hawawezi wakakujibu kwa ufasaha,

weng wanawaza kutoa kafala tu mtaani.
 
Kusema ukweli hali ya serikali yetu ni Mbaya. Nasikia shule Mbili mkoani Tabora, Kazima na Tabora boys, zimefungwa kwa ukosefu wa chakula!

According to Ester Bulaya, mkoani Mara, wazabuni wa chakula wanaidai Serikali zaidi ya Two bilioni na wanatishia kugoma. Kwa hali hii, walimu bado mnadhani tutaajiriwa?

Tukawafundishe akina nani wakati shule zimefungwa? Pesa ya kujikimu itatoka wapi? Mishahara? Au tutakua tunajitolea? Nachelea kusema kuwa Mungu kapanga kuwaaibisha CCM na serikali yake.
Ukweli Mchungu.
 
Last edited by a moderator:
Ndo tuamue kuiondoa madarakani tumechoka kuongozwa na wasiyojitambua
 
Hatar sana, watu wamesoma kwa ela za kuungaunga, tena wengine vyuo vya private had wazaz kuingia madeni wakiamini ipo siku vijana wataajiriwa alafu leo watu wanagawana mabilioni hatimaye shule zinafungwa, ajira hazipatkani pamoja na uhaba wa walimu, mafunzo kwa vitendo(BTP) yanaondolewa kwa sababu tu watu wanajinufaisha wao!!!
 
mwendo wa kujitolea tu ukisubili hizi ajira ni kuongeza stress tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…