Taarifa kwa umma: Ufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kamera 40 kufungwa Kariakoo kwa Tsh milioni 514

Waweke BoQ hapa tuone
 
Ufafanuzi upi mzuri?

We kwa akili zako huoni kuna walakini kwenye taarifa yao? Wamesema wanafunga Camera ngapi? Za aina gani?

Huyo mdakuzi alijaribu kuelezea kitu kwa juju juu tu. ilipaswa hawa waje kusema wanafunga Camera ngapi? kwa gharama ipi kwa kila Camera?
 
Ni jambo la uzuri kutoa taarifa kama hii kwenye hafla ya kutia saini kisha watu wenu wa uhusiano watoe taarifa kama hii kwenye vyombo vyote vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii.

Ndugu mkurugenzi, tambua kuwa watanzania wa sasa si wale wa mwaka 1961 tulipopata uhuru maana watu wachache waliweza kuwa ndo waamuzi wa kila kitu na hakukuwepo na ukosoaji wenye mantiki, ukosoaji wa sasa ni wa mstari kwa mstari na neno kwa neno.

Pia tambua kuwa watanzania hawahawa wa Leo na khasa hapa JamiiForums ni wasomi, wataalam na wengine ni wabobezi wa masuala haya khasa usalama kama wa kutumia hizo CCTV, kufanya tathmini, kuzifunga na mengine yahusianayo.

Hivyo mfanyapo mambo yenu ya kubuni miradi kama hiyo ambayo yahusu umma ni lazima muwe tayari kukosolewa kwa namna yoyote ile kwani fedha zinotumika ni za watanzania ambao wamelipa kodi.

AHSANTE.
 
Haya ukitazama hapa kwenye bandiko lao


Kosa la Jamiiforums liko wapi

Nashauri Jamiiforums watoe tamko kwa kukashifiwa wakati kosa si lao
 
Sijaona sehemu ambapo inaonesha taarifa iliyotolewa humu jamii forum kama Ina kosa.mkurugenzi naona kama anarudia tu kutuhabarisha
 
Ukweli hawa wakapimwe mkojo kabisa wanashida kichwani, kumbe wana account yao Jamiiforums!!!

 
Taarifa hii rasmi ya ufafanuzi imetosha, na kupitia andiko la aliyeleta uzi wengi tumefahamu kuhusiana na ufungwaji huo wa kamera ambayo ni taarifa njema ya kupongezwa Mkurugenzi wa Jiji na watendaji wake.
Wakafungue tu kesi, Jamiiforums itashinda kesi asubuhi kwakuwa taarifa ya jiji imejieleza
 
Kafungue kesi mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…