Taarifa kwa umma: Ufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kamera 40 kufungwa Kariakoo kwa Tsh milioni 514

Taarifa kwa umma: Ufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kamera 40 kufungwa Kariakoo kwa Tsh milioni 514

Sijaona sehemu ambapo inaonesha taarifa iliyotolewa humu jamii forum kama Ina kosa.mkurugenzi naona kama anarudia tu kutuhabarisha
Vitisho tu vya kijinga kutaka kuwa intimidate Jamii Forums!

Taarifa hiyo nilipost mimi Lord denning tena kwa kuweka Taarifa iliyotumwa na ITV.

Waliosema Camera 40 ni ITV na ndo mana tukawa tunahoji hapa.

Wangewauliza ITV wamepata wapi taarifa ya Camera 40 na sio Jamii Forums.

Taarifa ya ITV iliyosema Camera 40 zinafungwa kwa Mil. 514 hii hapa chini👇
Screenshot_20250218_171059_Facebook.jpg
 
Hii inanikumbusha sakata la Billionea Saidi Lugumi na machine hewa za alama za vidole,sijui kwa nini.
 
Kafungue kesi mahakamani.
Wewe huna akili hadi unapost vitu bila kufikiria?

Waliosema Camera 40 kwa Mil. 514 ni ITV au Jamii Forums? Kwa nini wawatishe Jamii Forums?

Jamii Forums tumepost kuhoji usahihi wa gharama kutokana na taarifa iliyorushwa na ITV!

Sasa wao wanatakiwa waseme wanafunga Camera za namna gani zenyw gharama ipi kwa kila Camera? Sio kuwatisha Jamii Forums ambao ni jukwaa huru.

Screenshot_20250218_171059_Facebook.jpg
 
Ni sawa kwa hiyo bei especially mkifunga mifumo genuine na quality kama mfumo wa Fiber wa Camera za Axis...ila tukija kukuta ni Camera za elfu sabini Sabini za Dahua au HIK vision za MP 2 au 4 hapo hamtakua na wakuwatetea.
Tupe BoQ
 
Duh! Hapa sasa Mbwa kala mbwa. Jiwe lililokataliwa limekuwa jiwe kuu!
Wamejidhihirisha kuwa ni wajinga kabisa
  1. Wao wenyewe wana account humu
  2. Bandiko kwenye site yao inasema hivyo
  3. Wanasema wananchi wacsome taarifa kwenye vyanzo vya kuaminika wakati tangazo lao wameposti humu wasipopaamini tena kwa account yao, je swali kama Jamiiforums haiaminiki wamekujaje kuweka tangazo lao humu? Je kwanini waishupalie Jamiiforums wakati hata website yao imeandika kitu hichohicho?
 
Taa za Barabarani hakuna lakini mnakimbilia kufunga camera.

Huku Temeke Mabarabara mengi ni Giza tupu.
 
KUNA njia Moja ya KWENDA Sudan tokea Uganda
Dah jamaa wameweka macamera kama yote sasa zile km 80phr 50phr pitiliza

UNAENDA mwendo MREFU unafurahia hakuna polisi leooo

Hahaha unakutana na defender kadha zimekaaa kama zinakusubiria unapunguza mwendo wanakusimamisha

Weka PEMBEN unajuankosa lakoo sijui

Unapoonyeshwa picha ya speed ya gari yakoo aisee Toka sikuhio nilianza kuendesha kwa adabu

Ikanikumbusha jnb south Africa nao Wana haya mambo n shidaaaaaaa

Ukikataa kuendesha WANAKWAMBIA unadharau ofisi Sina hamu

Traffick wafundishwee pia jinsi ya kukamata wahalifu WA speed HAPO kariakoo

Tukutane kwa prophet suguye tupojee udongo WA baraka
By
Pdidyjr2025
 
Panya road na wahalifu wengine matumbo yameanza kuunguruma.
Tunataka Dar na nchi yote mwananchi waweze kutembea popote masaa 24 bila hofu ya majambazi
 
Kwahio huo mtiririko wote wa gharama zote na nyinginezo mpaka za kununua labda maandazi na tissue za mtayarishaji kujifuta jasho..., Je zitaleta matokeo gani ? Camera 40, 400 au elfu nne (4000) ?

Sababu kama outcome ni camera arobaini bado sidhani kama hio ni value for money..., Sababu ukinipikia chakula kilichoungua huwezi kuniambia eti chote akikuungua ni sahani chache tu, au ukiniletea chapati kwa gharama ya elfu kumi wakati naweza kununua ya Tshs 300/ sitajali kwamba kuna nyingine zipo jikoni kama ningehitaji ningepewa...
 
Tunawashukuru kwa Taarifa hii.

Halikadhalika, sasa Watanzania na Wananchi tunawafahamu; wachochezi na vibaraka wao, wapotoshaji na vibaraka wao, ambao walienda mbali na hata kudai mapinduzi na uasi wa kijeshi nchini-kitu ambacho sio tu kinahatarisha usalama wa Taifa letu, bali pia yawezekana kabisa, kwamba wamevunja sheria kadhaa Nchini na miongozo mingine ya JamiiForums.

Merci.
 
Huyo mpotoshaji ni wakukamatwa na kufikishwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wazee wengine wanaoutuhadaa sisi vijana wa kesho.
 
Tunawashukuru kwa Taarifa hii.

Halikadhalika, sasa Watanzania na Wananchi tunawafahamu; wachochezi na vibaraka wao, wapotoshaji na vibaraka wao, ambao walienda mbali na hata kudai mapinduzi na uasi wa kijeshi nchini-kitu ambacho sio tu kinahatarisha usalama wa Taifa letu, bali pia yawezekana kabisa, kwamba wamevunja sheria kadhaa Nchini na miongozo mingine ya JamiiForums.

Merci.
Unashukuru wa taarifa ipi we nzi wa kijani? Kuna ufafanuzi gani hapo zaidi ya kuendelea kujichanganya na kuji implicate?

Hii taarifa ilitumwa na JAMII FORUMS?

Hivi huko CCM mmejaa wapuuzi sana eeh?

Screenshot_20250218_171059_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom