Taarifa maalumu, 'operation' imesitishwa, nuru imeonekana na 'the State' wamesema apewe muda

Taarifa maalumu, 'operation' imesitishwa, nuru imeonekana na 'the State' wamesema apewe muda

Namba 11 Mama kakiuka kwa kuendelea kukopa na kuongeza Deni la Taifa!!Mumemtuma Ndugai aseme !!! Mmechukia jamaa kazinguliwa uspika!!nadhani operation Will be executed next stage itaendelea na mpo jikoni mnajipanga kwa sasa!!see you soon comrade!!
That is rubbish,unaweza nitajia Nchi ambayo haikopi? Kwenye Nchi zilizo na hali mbaya ya deni la Taifa,umewahi kuiona Tzn ikitajwa mahala?

Hiyo mnayoita miradi ya kimkakati mtajengea vidole na miguu yenu?
 
19. Marais waliopita wachunguzwe kwa mali walizonazo sasa na zile kabla ya kuwa marais, wakibainika walijilimbikizia mali wanyongwe
20. Wakurugenzi wapigwe chini na wilaya ziwe chini ya mkuu wa wilaya
21. Viongozi wote serikalini wawe na mikataba ili wakishndwa kazi wanyongwe
22. Dini za kuletewa zote zifutwe na kupigwa marufuku hapa nchini
23. Wanawake omba omba wakamatwe na kufungwa pia kuomba hela mwanamme liwe kosa la jinai
 
19. Marais waliopita wachunguzwe kwa mali walizonazo sasa na zile kabla ya kuwa marais, wakibainika walijilimbikizia mali wanyongwe
20. Wakurugenzi wapigwe chini na wilaya ziwe chini ya mkuu wa wilaya
21. Viongozi wote serikalini wawe na mikataba ili wakishndwa kazi wanyongwe
22. Dini za kuletewa zote zifutwe na kupigwa marufuku hapa nchini
23. Wanawake omba omba wakamatwe na kufungwa pia kuomba hela mwanamme liwe kosa la jinai
Bora tuhamie Ukraine kuliko kuacha kuomba hela, hela ya mwanaume ni tamu, ina baraka...tutaomba tu
 
Nimekusoma mkuu

Changamoto ya kwanza ni katiba. Rais anapata madaraka yake kwenye katiba ambapo 'theState', pamoja na kuwa na capacity, wako well trained kujua mipaka yao, kwamba lazima katiba na sheria ziheshimiwe.

Ikiwa sisi tutaona ni sawa kuvunja katiba na kuyapoka madaraka ya rais, basi nasi hatutakuwa tofauti na hao tutakaokuwa tunataka kuwapoka madaraka. Lazima kila mtu afanye kazi kwenye misingi ya utawala wa sheria.

Ajenda kuu na ya mwanzo kwa sasa, hasa kuanzia kipindi kile cha awamu ya nne na yaliyotokea awamu ya tano, ni uundwaji wa katiba mpya. Sasa imekuwa lazima na pressure imekuwa kubwa sana hata pale 'stpeters'.

Kwa miaka mingi 'stpeters' pale kumekuwa na nguvu kubwa kwenye kulinda wakubwa. Lakini sasa kwa madhaifu ya nyuma na matatizo ya hapa karibuni, wapo wanaoona umuhimu wa kuwa na taasisi zitakazofuata msingi ya sheria na haki.

Kumbuka 'stpeters' na 'theState' sio taasisi moja. Hawa 'theState' wao wametoa muda mpaka mwakani kwa mchakato wa katiba kuanza. Nachelea kusema kama 'aliyepewa muda' hataanza hili inaweza kuwa 'too late' kwake.

Sasa kule 'stpeters' bado kuna wale conservatives ambao wanataka mambo yaende hivihivi na wanaamini wanazo means za kuhakikisha inabaki hivi. Wapo ambao wanashughulikiwa kimyakimya na muda mchache hawatakuwepo tena. Watakaobaki wakiendelea wanaweza kufanya too late ya 'aliyepewa muda' isiwe beyond mwakani.

Traditionally, kwenye miradi huko na utendaji kuliachiwa wanasiasa. Maslahi ya kiuchumi yaliachwa sana kwa watendaji serikalini. Mabadiliko ya kuweza kuwa na 'economic intelligence' kwenye taasisi ya pale 'stpeters' yatakuja mfumo wote utakapobadilishwa.

Yaani hii itakuwa transformation kubwa sana kuona focus isiwe tu kwenye ulinzi na usalama bali iende pia kwenye uchumi na biashara. Hapa bado kuna jukumu kubwa sana ila najua wapo watu kadhaa pale 'stpeters' wamekuwa wakipikwa kwa takribani miaka 12 sasa. Mmoja wao akipewa kuongoza ile idara basi anaweza kuleta tija.

Mpaka wakati huu hakujakuwa na vitendo vya kulipiza kisasi. Watu wamebadilishwa na wengi wamepewa nafasi nyingine, tena zenye heshima kabisa, ili wapate nafasi ya kujitafakari na kujipanga. Ila utashi wa kisiasa utaamua nani abaki na nani aendelee.

Man thumbs up eeeh
 
Hao bashiru, Pole Pole walichangia kubaka democrasia yetu Tena bashiru akakengeuka kabisa na kusahau misimamo yake akiwa chuoni, na Kuna siku alijiropokea wao Wana Dola kwanini washindwe kupata ushindi asilimia zote, huwezi kuwatoa hao wawili.
Na huyo makonda sabaya na wengineo walioharibu washtakiwe regardless walitumwa au walikuwa wanajipendekeza kwa mteuaji

Wasulubiwe hao
 
Mkuu 'theState' ina wajibu juu ya taifa tu. Haina 'feelings' towards or against any individual. We are only loyal to the nation.

Pia taasisi hii tangu kuasisiwa kwake haijihusishi na vitendo vya mauaji au kuleta maumivu kwa watu.
Lakini mkuu kama mpo (royal) kwa ajili ya taifa inakuwaje mambo mengi yamefanyika/yanafanyika ya kifisadi na mnashindwa kuchukua maamuzi? Au ndani yenu kuna baadhi yenu mpo kwa ajili ya masirahi binafsi?
 
Lakini mkuu kama mpo (royal) kwa ajili ya taifa inakuwaje mambo mengi yamefanyika/yanafanyika ya kifisadi na mnashindwa kuchukua maamuzi? Au ndani yenu kuna baadhi yenu mpo kwa ajili ya masirahi binafsi?
Wanakuwa wazalendo pale maslahi yao yanapoguswa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Msitishe Madame President, Tanzania iko imara na Hayati John P. Magufuli alifariki kifo Cha kawaida na kila mtu anajua na sio ule utabiri wako feki.

Pengine sababu kuu ni ukaidi wake wa namna ya kupambana na COvid-19 na kisha akaji- expose kupita kiasi ili Hali alikuwa katika kundi hatarishi. Hili lilionekana dhahiri na hata lilionekana wazi linaweza muathiri kama ilivyotokea kwa Mkurunzinza.

You're nobody...wewe ni kama wasaliti wengine walioko kwenye serikali wenye access ya information muhimu ambao wanavujisha kabla hazijatangazwa.
Mkuu! mama huko america kasema yupo tayari KUHUSU KATIBA hata kama itagharimu uraisi Wake !je tutarajie katiba kuandikwa kabla ya 2025!!
 
Lakini mkuu kama mpo (royal) kwa ajili ya taifa inakuwaje mambo mengi yamefanyika/yanafanyika ya kifisadi na mnashindwa kuchukua maamuzi? Au ndani yenu kuna baadhi yenu mpo kwa ajili ya masirahi binafsi?
Soma post namba 129.
 
Imeamuliwa 'next stage' isitishwe. Baadhi ya maombi ya unyenyekevu ya 'theState':

1. Sheria zifuatwe na zile zisizofaa zibadilishwe.
2. Mwakani kuwe na mwendelezo wa kuandika katiba ambapo bunge liundwe na lisilazimike kuingiza wabunge waliopo sasa isipokuwa wale wenye tija.
3. Wabunge wasiokuwa halali waondolewe kutoka bungeni.
4. Ikiwezekana yale majimbo na kata ambayo ilionekana kabisa kulikuwa na upotoshaji wa matokeo basi uchaguzi urudiwe. Uchaguzi wa serikali za mitaa usubirie mpaka katiba mpya.
5. Stahiki za wafanyakazi wa umma na wastaafu zilipwe. Fao la kujitoa lirejeshwe kwa wale waliopoteza ajira.
6. Fungua milango ya nchi ili biashara na mitaji ikaribie na ku-unlock uchumi. Wawekezaji wakaribishwe kwa sera na sheria wezeshi.
7. Wananchi kule kimara walipwe fidia na kwingineko ambapo watu waliumizwa.
8. Ofisi ya DPP na mwanasheria mkuu ifumuliwe na watu watendewe haki.
9. Watendaji wote 'walio-dance the tune' na kuvunja sheria huku wakiumiza watu waondolewe.
10. Miradi ya SGR na Stiegler's iendelezwe pamoja na ile ya barabara lakini upembuzi ufanyike ili ikiwepo isiyo na tija iachwe.
11. Kuna tatizo kubwa sana deni la taifa.. angalau punguza sasa kukopa na weka mazingira ili uvutie wawekezaji na hasa wale wa ndani ambao wameficha matrilioni ardhini na nje ya nchi.
12. Uchunguzi huru ufanyike kwa yale matukio yote ya utekaji, mauaji na mashambulizi dhidi ya binadamu.
13. Ondoa elimu bure kwasababu inajenga taifa lenye 'irresponsible' minds. Angalia namna ya kubadilisha mfumo wa elimu ili uendane na nyakati tulizonazo.
14. Fanya maridhiano na wapinzani na taasisi zilizotengwa ili kuleta umoja wa kitaifa.
15. Serikali iendelee kubaki Dodoma na ikiwezekana ikulu ya Dar es salaam pajengwe kituo maalum cha utalii.
16. Chama bado kina misingi mizuri, imarisha kwa kuteua watu wenye maono na uzalendo kwa nchi.
17. Sisi hatutakuja kukuingilia, teua na unda timu kwa kadri unavyoona inafaa.. watendee watu haki nasi tutaendelea kukuunga mkono.

18. Mpaka sasa umetuonesha mwanga mwema nasi kwakuwa tunaipenda nchi tumesitisha 'mipango' yetu ili utimize majukumu yako na kusimamia haki.

Tulishauri, hakusikiliza na sasa hayupo. Nimepewa ujumbe, nimeufikisha.

Hizo zilikuwa ni ndoto za alinacha! Nani angekubali hiyo!
 
Jambo unalopaswa kujua ni kwamba 'hatma' ipo kwenye ule ujumbe wa rais ambaye hajawahi kugombea ila fursa ya 'neema' inaachiliwa kufanya remedy.

Hakuna maono ambayo hayapo subject to changes. Ikiwa tu zile condition zilizopelekea maono zitabadilika basi maono pia yaweza kubadilika.

Madam president kaonesha tofauti na hapa anapatiwa nafasi ya kufanya namna inayobadilisha maono.

Asipofanya ile dhamira ya awali inakuwa na uhalali kuendelea.
Mkuu
Vipi Hadi sasa
Unaonaje malengo yenu yanatekelezwa!!?
 
 
Mwakani kuwe na mwendelezo wa kuandika katiba
Naona hatua kwa hatua
Wabunge wasiokuwa halali waondolewe kutoka bungeni.
Hoja zote zinajibiwa.
Stahiki za wafanyakazi wa umma na wastaafu
Limeonekana pia.
Fungua milango ya nchi ili biashara na mitaji ikaribie na ku-unlock uchumi.
Royal tour?

Watendaji wote 'walio-dance the tune' na kuvunja sheria huku wakiumiza watu waondolewe.
Tumeona hili
Fanya maridhiano na wapinzani na taasisi zilizotengwa ili kuleta umoja wa kitaifa.
Ni dhahiri bila chenga.
 
Namba 2 na namba 3 tayari imetekelezwa jana [emoji736]
 
Kama wewe ni mwana usalama, basi hii nchi tuko uchi kila sehemu

Kama mnafanya tukio kubwa kama hili na mnakuja kujisifu mitandaoni, sishangai kigogo akijua kila kinachofanyika ikulu

kama hii nchi ina wana usalama wengi kama wewe, narudia kusema tuko uchi na na tumeweka roho na rasilimali zetu mikononi mwa wajinga sana.

Mkuu, ndio maana nchi yetu iko hivi uionavyo na matatizo yake ni makubwa kutokana na watu wa namna hii.
Usitegemee kama nchi tukaweza pambana kiuchumi duniani na hata kucheza rafu kama wengine wafanyavyo ikiwa tutaendelea kuwa na watu kama hawa. Kwa Putin hawa ni kupigwa “nerve agent” tu kwa usalama wa Nchi.
 
Back
Top Bottom