Nimekusoma mkuu
Changamoto ya kwanza ni katiba. Rais anapata madaraka yake kwenye katiba ambapo 'theState', pamoja na kuwa na capacity, wako well trained kujua mipaka yao, kwamba lazima katiba na sheria ziheshimiwe.
Ikiwa sisi tutaona ni sawa kuvunja katiba na kuyapoka madaraka ya rais, basi nasi hatutakuwa tofauti na hao tutakaokuwa tunataka kuwapoka madaraka. Lazima kila mtu afanye kazi kwenye misingi ya utawala wa sheria.
Ajenda kuu na ya mwanzo kwa sasa, hasa kuanzia kipindi kile cha awamu ya nne na yaliyotokea awamu ya tano, ni uundwaji wa katiba mpya. Sasa imekuwa lazima na pressure imekuwa kubwa sana hata pale 'stpeters'.
Kwa miaka mingi 'stpeters' pale kumekuwa na nguvu kubwa kwenye kulinda wakubwa. Lakini sasa kwa madhaifu ya nyuma na matatizo ya hapa karibuni, wapo wanaoona umuhimu wa kuwa na taasisi zitakazofuata msingi ya sheria na haki.
Kumbuka 'stpeters' na 'theState' sio taasisi moja. Hawa 'theState' wao wametoa muda mpaka mwakani kwa mchakato wa katiba kuanza. Nachelea kusema kama 'aliyepewa muda' hataanza hili inaweza kuwa 'too late' kwake.
Sasa kule 'stpeters' bado kuna wale conservatives ambao wanataka mambo yaende hivihivi na wanaamini wanazo means za kuhakikisha inabaki hivi. Wapo ambao wanashughulikiwa kimyakimya na muda mchache hawatakuwepo tena. Watakaobaki wakiendelea wanaweza kufanya too late ya 'aliyepewa muda' isiwe beyond mwakani.
Traditionally, kwenye miradi huko na utendaji kuliachiwa wanasiasa. Maslahi ya kiuchumi yaliachwa sana kwa watendaji serikalini. Mabadiliko ya kuweza kuwa na 'economic intelligence' kwenye taasisi ya pale 'stpeters' yatakuja mfumo wote utakapobadilishwa.
Yaani hii itakuwa transformation kubwa sana kuona focus isiwe tu kwenye ulinzi na usalama bali iende pia kwenye uchumi na biashara. Hapa bado kuna jukumu kubwa sana ila najua wapo watu kadhaa pale 'stpeters' wamekuwa wakipikwa kwa takribani miaka 12 sasa. Mmoja wao akipewa kuongoza ile idara basi anaweza kuleta tija.
Mpaka wakati huu hakujakuwa na vitendo vya kulipiza kisasi. Watu wamebadilishwa na wengi wamepewa nafasi nyingine, tena zenye heshima kabisa, ili wapate nafasi ya kujitafakari na kujipanga. Ila utashi wa kisiasa utaamua nani abaki na nani aendelee.