Neuro
JF-Expert Member
- May 13, 2017
- 1,551
- 1,721
Ulianzishwa kwa lengo hilo chifu au hujui. Ila baadae Mkapa akaja kuidiversify. Ila ilikuwa mainly kwa waajiriwa. Kwasababu, bima tuliyonayo ni social insurance, kwamba unaitaji kuwa endelevu na anayeumwa anatibiwa na asiyeumwa. Mfuko ulikuja kupata shida baada ya watanzania kutokujua kuwa bima siyo tiba bali ni kinga. Unawekeza leo ili matatizo yakifika uweze kuitumia, chakushangaza mzazi anawwza kukaa na watoto miaka mpaka miaka siku akija kukata bima ujue mtoto kapewa rufaa kwenda hospitali ya kanda au ya taifa. Kimbembe ni kuwa consultation charges za hospitali ya kanda kama Bugando ni 50,000/= so yule mtoto atatumia pesa yake ya mwanzo aliyewekeza huku akija kutumia na 1-2M more maana watoto waliojiunga wengi walikuwa na matatizo ya usonji, moyo nakadharika. Hivyo ukisema mfuko wa toto afya card uwazishwe wenyewe kama wenyewe bila kutegemea pesa za mfuko wa makato ya walioajiriwa utakuwa negative maana hamna mtu aliyewekeza bali wote wapo on time kutumia. That to say, huku kwa waajiriwa kuna wagonjwa wa dialysis ambaye mgonjwa mmoja wa dialysis anatumia 150M per year na mwingine wa anticancer anatumia 50M per year. Automatically mfuko mwingine utabidi uufinance mwingine mwisho wa siku yote huishia kucollapse. Watu wengi pia hawajui pia kuwa wanasiasa walikuwa wanaitumia hiyo bima kupiga kampeni hasa wabunge. Mbaya zaidi, serikari haitoi ruzuku kwashirika, kila kitu na operation cost unajitegemea. Mwishowe, the secured funds zinanegate na kuwa running at losses maana ndani ya humohumo kuna watoa huduma wanafanya ubadhirifu ili wapate mapato mengi nakuna wanachama wanafanya ubadhirifu kujipatia faida. Ndio maana losses haziishi. Actually NHIF ya Kenya imeshindwa mpaka ikabidi uigawanye mfuko mmoja kuwa mitatu na kustick kwenye kucoordinate watoa huduma na sio kufanya utendaji kama hapo awali. Ruto ameshindwa kabisaa. Maana watu hujua bima ni tiba ilihali ni kinga.Huu mfuko inaonekana ni maalum kwaajili ya waajiriwa tu.
Sisi maskini acha tufe tu.